Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

Hongera sana tumetofautiana
Nadhani hii kasumba inatokana na makuzi. Kwa mara ya kwanza kutoka nje ya TZ nipale nilipokwenda kusoma nchi za watu. Nchi hiyo watu hujivunia utaifa wao. Pili nilipoongeza ujuzi nilikanyaga nchi ambayo ubaguzi kwa watu wote hata ukiwa Mwingereza unaonekana ni dogo tu isipokuwa mmarekani. Na sisi tulikuwa tunaulizwa, ni Mmarekani mweusi ili uheshimike. Ila ungangari wetu tulikuwa tunakubali kuitwa nyani potelea mbali. Hadi leo nikiwa nje, nikirudi Airport nafurahi kurudi nyumbani. Titi la mama tamu hata likiwa la mbwa,waswahili walituasa
 
Mkuu nakuelewa sana titi la mama tamu eeh

Hakuna anaechukia nyumbani hayupoo tunazungumzia mazingira hayavutii kuishi
 
Unafurahi kuzaliwa na kuishi Tanzania?

Umewahi kusikia watu wakisema hawapendi nchi walizozaliwa?

Leo katika kipindi cha Amka na BBC kuna taarifa nimesikia kuhusu wahamiaji kutoka nchi za Nicaragua na Honduras

Wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wanafunga safari wakipitia nchi ya Mexico na kujaribu kuvuka mpaka kuingia Marekani kwa madai ya kutafuta maisha bora

Hata kwetu kuna watu wamekuwa wakiondoka na kwenda nchi nyingine
Watanzania wengi wapo Afrika Kusini mpaka tumeona miezi ya nyuma walivyofurushwa na kurudi nyumbani tena kwa msaada wa serikali wengine wakiwa na muonekano wa kutia shaka

Watanzania wengi pia wapo Ulaya kujitafutia kipato
Wengine wanatamani kurudi nyumbani lakini wenyewe wanadai nyumbani Tanzania pamekuwa pachungu sana na hawavutiwi tena licha ya kua wana pakumbuka

Nina rafiki yangu yupo USA anasema anatamani kurudi bongo hasa mitaa aliyokulia ila havutiwi tena

Nimegundua
Nchi nyingi ambazo wananchi wake wanazikimbia zina mazingira magumu ya kuishi

Nitaongelea hapa Tanzania kwetu

Tunaweza kukubaliana kwamba nchi hii ni ngumu na haivutii kuishi, labda uwe na kiwango fulani cha maisha la sivyo ni shida sana

Umewahi kwenda kwenye hospitali za umma? Msongamano mazingira yasiyo rafikiI mean uchafu umeshuhudia?

Usafiri wa umma daladala alooo!

Watu wanajazwa kuliko hata uwezo wa daladala
Humo ndani ni kukanyagana

Mtu anaenda kazini alfajiri kuwahi foleni anarudi anadandia gari kama vile nyani wanavyodandia miti unapanda daladala unaogopa kugusa hata lile bomba mana lina majasho ya kila namna

Msongamano harufu za kila aina zisizovutia unaweza kupata depression

Masoko jamani! Masokoni ukienda huko kipindi cha mvua uvae gumboots, la sivyo unarudi kama umetoka kulima mpunga
Umewahi kwenda Soko la Mabibo kipindi cha mvua?

Machinga wamezagaa ma barabarani watembea kwa miguu unapishana na magari pkpk bajaji uso kwa uso vipaza sauti, sumu za mende, kunguni.
Yaani unatembea unahisi kuchanganyikiwa

Hayo ni machache kati ya yale mengine mengi

Hivi, muda huu unavutiwa na kuishi Tanzania?

Umezaliwa Tanzania 🇹🇿 na unatamani kuondoka?
Ni nini sababu yako?

ShesRise_1 ✋️
Binafsi kwakweli nina furaha mno Mwenyezi Mungu kunipa zawadi ya uhai na kufanya nizaliwe Tanzania, na kwahivyo sina sababu kufahamu sana ya wengine, but mimi na familia yangu kwakweli nainjoy sana kuishi Tanzania 🙏
 
Nasema hivi, mimi napenda kuishi Tanzania, Bongo siyo bahati mbaya.

Ubovu wa miundombinu, ubaya wa huduma hospitalini na mashuleni siyo issue kwangu.

Hizo ni changamoto kama changamoto nyingine zilizopo sehemu nyingine

Mpaka hapo umeelewa?
Labda hata kama Ulaya na Marekani kama maji ya bomba bado ni changamoto na watu bado wanachota maji kwa ndoo na madumu visimani kama sisi bado nina uhakika changamoto ya wanawake/mabinti kuwa ombaomba hadi vocha na nauli kwa vijana iko bongo tu, sio kama sehemu nyingine.
 
Duh umemaliza mkuu hili nalo neno,,unaweza nunua gari kali lakini miundombinu hovyo hutoenjoy hiyo gari,, ukiumwa uende India,unalipa Bill ya maji lakini maji yenyewe mashaka,umeme hivohivo unakatika zaidi ya malaya an hovyo sana,na wakati huo Kodi unalipa 🙄.
Kabisa hua najiuliza watu wana RR,ferrari ila sijawahi ona zikipita mbezi,kimara
 
Labda hata Ulaya na Marekani hata maji ya bomba bado ni changamoto na watu bado wanachota maji kwa ndoo na madumu na visimani kama sisi ila nina uhakika changamoto ya wanawake/mabinti kuwa ombaomba hadi vocha na nauli kwa vijana iko bongo tu, sio kama sehemu nyingine.
Maisha ni changamoto

Niwe mkweli tu, mimi utamu wa titi la mtu mzima nililonyonya ukubwani ndio naukumbuka, utamu wa titi la mama sikumbuki kabisa😁
Eeeh usiniambie Yoda 😅
Hongera sana kunyonya na utu uzima huo
 
Binafsi kwakweli nina furaha mno Mwenyezi Mungu kunipa zawadi ya uhai na kufanya nizaliwe Tanzania, na kwahivyo sina sababu kufahamu sana ya wengine, but mimi na familia yangu kwakweli nainjoy sana kuishi Tanzania 🙏
Hongera sana
 
Hapana ila mpo ila wachache
Na nyie ndio wanasema mmejipata 😊
Wala hatujajipata 😂 Mi napenda ku temper na mifumo kwahiyo bongo kunanifaa sana.

But i highly recommend watu wakipata nafasi waondoke, Kaka yangu aliondoka akiwa na miaka 35, now ana 38 you won’t believe ni kiasi gani amejiboresha, People in bongo are working hard in a wrong country (huu msemo niliusikia humu)

wagai gai ndio tubaki. Mimi nina chances za kuondoka, jiulize kwanini bado nipo 🤣
 
Wala hatujajipata 😂 Mi napenda ku temper na mifumo kwahiyo bongo kunanifaa sana.
Hii nayo ni maajabu 😅😇
But i highly recommend watu wakipata nafasi waondoke, Kaka yangu aliondoka akiwa na miaka 35, now ana 38 you won’t believe ni kiasi gani amejiboresha, People in bongo are working hard in a wrong country (huu msemo niliusikia humu)
People in Bongo work extremely hard, but the rewards don't match the effort they put in
wagai gai ndio tubaki. Mimi nina chances za kuondoka, jiulize kwanini bado nipo 🤣
Hongera hii ndio dhana halisi ya binadamu tumetofautiana namna ya kuyachukulia mambo
 
Acha kukariri wewe, kula chakula bora utapunguza maradhi mengi, acha kugonga mademu wa buku tatu utapunguza kutumia madawa ya kizungu kama vile AZUMA.

Kabla ya kuja mkoloni wazee wetu waliishi miaka mingi tena zaidi hii tunayoishi sasa.
Mkuu, with all due respect; Fact check hilo.
 
Back
Top Bottom