Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

Unaipenda nchi yako kwa sababu hujawahi kutoka na kuona nchi zingine zilivyo.

Ukitoka na kuona nchi nyingine zilivyo na mifumo yao ilivyo, hutoipenda tena hii bongo yenye maisha ya kuunga unga.

Masoud Kipanya alifika Europe, akoana mifumo ya wenzetu ilivyo, akabaki anajiuliza hawa wenzetu wanafanyaje fanyaje. Yani kila kila kitu kina run smoothly. Hakuna longolongo.

Lakini kwa ambao hawajatoka, wanaweza kuridhika na kuona kwamba Maisha ya Tanzania ni bora sana. Na wakabaki kuyapenda, Kumbe hawana exposure.
Masoud akahitimisha kua anaipenda Europe kuliko Tanzania sio??

Kwani kuna mtu hajui jinsi hizo nchi zilivyo mkuu?? Na kuna sababu mbalimbali za mtu kuipenda sehemu fulani sio lazima iwe huduma za kijamii na mifumo mizuri.

Hata walio huko nao wana changamoto nyingine pamoja na ubora walionao kwenye baadhi ya mambo. Kwahiyo hilo ni jambo mtambuka.

Pamoja na hayo bado naipenda Tanzania.
 
Bado Bongo ni kuzuri, ata huko unakotaka kukimbilia changamoto zipo, ilimradi wewe ni mwanadamu, changamoto ni sehemu ya maisha yako
Changamoto za first world countries sio sawa na changamoto za huku ushenzini third world countries.

Huku unalipa bills halafu bado huduma unazopata ni mbovu. Pesa za umma zinaliwa na mafisadi.

First world countries, huduma ni quality. Bills unazolipa unaona kabisa zinaboresha huduma.

Huku Afrika, The poor pay taxes for the rich to grow.

Halafu wakubwa wanakwepa kodi.

Sasa huu si ujinga!!
 
Hello Twin, ukweli mchungu ni kwamba Bongo hata ukiwa na pesa bado utaishi maisha ya kubahatisha tu kwa sababu nchi nzima haina basic standards.

Yani unakuwa kama mfalme kwenye kisiwa cha takataka, ndani kwako ni kuzuri, lakini ukifungua tu geti unakutana na fujo, vumbi, foleni za kijinga, na miundombinu iliyochoka. Unanunua gari la kifahari halafu linaharibika suspension ndani ya mwaka mmoja kwa sababu ya mashimo barabarani, unalipa kodi kubwa halafu bado unachimba kisima chako mwenyewe, unafunga solar na majenereta, na unaajiri walinzi binafsi kwa sababu huduma za umma zimefeli.

Mbaya zaidi, hata kwenye huduma za afya au usalama, pesa yako haikupi uhakika wa kupona ukipata dharura usiku kwa sababu hakuna mfumo wa dharura unaoeleweka, unaishia kufa kizembe tu ukiwa na mamilioni yako benki.

Ndiyo maana wanaopata nafasi wanaenda nchi zilizoendelea si kwa sababu kule kuna pesa za bure, bali kule mfumo tayari umeshatengeneza quality of life, kwa hiyo hata ukiwa na kipato cha kawaida unaishi kwa heshima na amani ya akili kuliko tajiri wa huku anayetumia nguvu nyingi kujilinda na mazingira mabovu.
 
Hakika.
 
Bado Bongo ni kuzuri, ata huko unakotaka kukimbilia changamoto zipo, ilimradi wewe ni mwanadamu, changamoto ni sehemu ya maisha yako
Changamoto za wenzetu huko nje ni kama baridi kali, upweke n.k ambazo ni matokeo ya mifumo inayofanya kazi au hali ya hewa. Lakini changamoto za Bongo nyingi ni za kujitakia ambazo zilitakiwa ziwe zimeshatatuliwa karne iliyopita.

Mtu haupaswi kuhatarisha maisha yako kwa kukosa huduma ya dharura hospitalini, kuvuka mitaro ya maji machafu katikati ya jiji, au kukaa kwenye foleni masaa matatu kwa sababu tu mipango miji imefeli. Kwa hiyo, hatukimbii changamoto za ubinadamu, tunakimbia mazingira yanayofanya mambo ya msingi yawe anasa!
 
Masoud akahitimisha kua anaipenda Europe kuliko Tanzania sio??
Huwezi kuupenda umaskini.

Hata kama hakusema kwamba anaipenda Europe.

Huwezi kufika sehemu iliyobora halafu ukapenda sehemu mbovu.

Hii ni nature ya kila binadamu.

Hakuna asiyependa pazuri bwana.
Kwani kuna mtu hajui jinsi hizo nchi zilivyo mkuu?? Na kuna sababu mbalimbali za mtu kuipenda sehemu fulani sio lazima iwe huduma za kijamii na mifumo mizuri.

Hata walio huko nao wana changamoto nyingine pamoja na ubora walionao kwenye baadhi ya mambo. Kwahiyo hilo ni jambo mtambuka.

Pamoja na hayo bado naipenda Tanzania.
Honestly speaking,

Sasa hivi ukapewa uraia wa kudumu wa kwenda Marekani kuishi, utakataa?

Kwa sababu unaipenda Tanzania.

Be honest.

Utakataa?
 
Huwezi kuupenda umaskini.

Hata kama hakusema kwamba anaipenda Europe.

Huwezi kufika sehemu iliyobora halafu ukapenda sehemu mbovu.

Hii ni nature ya kila binadamu.

Hakuna asiyependa pazuri bwana.

Honestly speaking,

Sasa hivi ukapewa uraia wa kudumu wa kwenda Marekani kuishi, utakataa?

Kwa sababu unaipenda Tanzania.

Be honest.

Utakataa?
Uraia wa kudumu hapana, ila nafasi ya kuitembelea sawa na nitaitembelea tu pamoja na nchi kadhaa za Ulaya.

Pamoja na kupenda vizuri lakini hilo tu halihitimishi mtu kutoipenda nchi yake.
 
Changamoto za wenzetu huko nje ni kama baridi kali, upweke n.k ambazo ni matokeo ya mifumo inayofanya kazi au hali ya hewa. Lakini changamoto za Bongo nyingi ni za kujitakia ambazo zilitakiwa ziwe zimeshatatuliwa karne iliyopita.

Mtu haupaswi kuhatarisha maisha yako kwa kukosa huduma ya dharura hospitalini, kuvuka mitaro ya maji machafu katikati ya jiji, au kukaa kwenye foleni masaa matatu kwa sababu tu mipango miji imefeli. Kwa hiyo, hatukimbii changamoto za ubinadamu, tunakimbia mazingira yanayofanya mambo ya msingi yawe anasa!
Mkuu umekuwa brain washed, babu zako na watu kabla yao, waliishi hapa Tanzania na wali enjoy nature na hakukuwa na hizo modern infrastructure au huduma za kipigaji za hospitali.

Kwanza unapaswa kujua kwamba huduma za afya za kibepari ni za kipigaji, madawa mengi ya kizungu hayajatengenezwa kutibu, bali kupooza maradhi.

Wewe unaonekana umeingia kwenye mifumo ya mabepari, unataka ufanye shopping kwenye supermarket ya beberu na uache kununua nyaya za mangi hapo jirani yako.

Uende ukaishi kwenye maisha ya upweke ili hali hapa Bongo tunaishi vizuri tu kijamaa na ndugu na jamaa

Mifumo ya maisha ya Bongo ni mizuri na inahakisi uanadamu
 
Hello Twin, ukweli mchungu ni kwamba Bongo hata ukiwa na pesa bado utaishi maisha ya kubahatisha tu kwa sababu nchi nzima haina basic standards.

Yani unakuwa kama mfalme kwenye kisiwa cha takataka, ndani kwako ni kuzuri, lakini ukifungua tu geti unakutana na fujo, vumbi, foleni za kijinga, na miundombinu iliyochoka. Unanunua gari la kifahari halafu linaharibika suspension ndani ya mwaka mmoja kwa sababu ya mashimo barabarani, unalipa kodi kubwa halafu bado unachimba kisima chako mwenyewe, unafunga solar na majenereta, na unaajiri walinzi binafsi kwa sababu huduma za umma zimefeli.

Mbaya zaidi, hata kwenye huduma za afya au usalama, pesa yako haikupi uhakika wa kupona ukipata dharura usiku kwa sababu hakuna mfumo wa dharura unaoeleweka, unaishia kufa kizembe tu ukiwa na mamilioni yako benki.

Ndiyo maana wanaopata nafasi wanaenda nchi zilizoendelea si kwa sababu kule kuna pesa za bure, bali kule mfumo tayari umeshatengeneza quality of life, kwa hiyo hata ukiwa na kipato cha kawaida unaishi kwa heshima na amani ya akili kuliko tajiri wa huku anayetumia nguvu nyingi kujilinda na mazingira mabovu.
Duh umemaliza mkuu hili nalo neno,,unaweza nunua gari kali lakini miundombinu hovyo hutoenjoy hiyo gari,, ukiumwa uende India,unalipa Bill ya maji lakini maji yenyewe mashaka,umeme hivohivo unakatika zaidi ya malaya an hovyo sana,na wakati huo Kodi unalipa 🙄.
 
Mimi binafsi nikiwa na pesa Tanzania itakuwa sehemu mzuri sana ya kuishi,,lakini hivi kapuku ni hovyo sana. Tanzania mtu mwenye pesa naamini anaenjoy sana maisha kuliko mwenye pesa wa kiwango sawa wa ulaya,,huku huduma za jamii duni sana,kama ulivosema,, wanao enjoy maisha ya Tanzania ni waliojipata tu,, mafisadi na watoto wao, wafanyabiashara wakubwa,na watu wa tabaka la kati wenye kipato cha uhakika daily..NB ukiwa na pesa Tanzania utaishi kama mfalme.
Hakikisha unakuwa CCM na unachangia mbio za mwenge.
 
Uraia wa kudumu hapana, ila nafasi ya kuitembelea sawa na nitaitembelea tu pamoja na nchi kadhaa za Ulaya.

Pamoja na kupenda vizuri lakini hilo tu halihitimishi mtu kutoipenda nchi yake.
Ungepata nafasi ya kuchagua nchi unayopenda uzaliwe kati ya Marekani na Tanzania?

Au unapewa nafasi, mke wako ambaye ni mjazito achague nchi ya kumzaa mtoto wako kati ya Marekani na Tanzania?

Ungechagua nchi ipi?
 
Mkuu umekuwa brain washed, babu zako na watu kabla yao, waliishi hapa Tanzania na wali enjoy nature na hakukuwa na hizo modern infrastructure au huduma za kipigaji za hospitali.

Kwanza unapaswa kujua kwamba huduma za afya za kibepari ni za kipigaji, madawa mengi ya zungu hayajatengenezwa kutibu, bali kupooza maradhi.

Wewe unaonekana umeingia kwenye mifumo ya mabepari, unataka ufanye shopping kwenye supermarket ya beberu na uache kununua nyaya za mangi hapo jirani yako.

Uende ukaishi kwenye maisha ya upweke ili hali hapa Bongo tunaishi vizuri tu kijamaa na ndugu na jamaa

Mifumo ya maisha ya Bongo ni mizuri na inahakisi uanadamu
Unajifariji na umaskini kwa kisingizio cha asili. Babu zetu hawakuwa na hizo huduma, ndiyo maana life expectancy yao ilikuwa fupi, vifo vya mama na mtoto vilikuwa vingi, na magonjwa madogo kama malaria au kipindupindu yalikuwa yanafyeka vijiji vizima. Dunia imebadilika, hata wewe uliyeandika hayo yote unatumia smartphone na mtandao uliotengenezwa na hao hao mabepari badala ya kupiga ngoma kuwasiliana na wenzako!

Labda nikuulize kama huduma za afya za kisasa ni za kipigaji, mbona viongozi na matajiri wa Bongo wakiumwa tu kidogo wanakimbilia huko huko kwa mabepari India, Ulaya, au Marekani kutibiwa na hawabaki kunywa mitishamba?

Acha kujaribu kuhalalisha mazingira magumu ya maisha kwa sababu tu umeshaizoea shida na unaogopa kudai viwango bora vinavyomstahili binadamu wa karne ya 21!
 
Back
Top Bottom