Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

Bongo ni kuzuri ila uwe na pesa
Unaweza kuwa na pesa ndio.

Lakini miundombinu mibovu na huduma mbovu bado zitakuwa na kikwazo kwako.

Ndio maana kuna watu wana pesa sana hapa bongo, lakini kuna baadhi ya huduma wanalazimika kwenda nje ya nchi kuzifuata.

Hata kama una pesa, Bado Bongo ni ngumu.

Kuna magonjwa ukiugua hapa nchini, lazima uende nje ya nchi.

Kuna teknolojia na utaalamu ambao ukiuhitaji lazima utoke nje ya nchi.
 
Unafurahi kuzaliwa na kuishi Tanzania?

Umewahi kusikia watu wakisema hawapendi nchi walizozaliwa?

Leo katika kipindi cha Amka na BBC kuna taarifa nimesikia kuhusu wahamiaji kutoka nchi za Nicaragua na Honduras

Wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wanafunga safari wakipitia nchi ya Mexico na kujaribu kuvuka mpaka kuingia Marekani kwa madai ya kutafuta maisha bora

Hata kwetu kuna watu wamekuwa wakiondoka na kwenda nchi nyingine
Watanzania wengi wapo Afrika Kusini mpaka tumeona miezi ya nyuma walivyofurushwa na kurudi nyumbani tena kwa msaada wa serikali wengine wakiwa na muonekano wa kutia shaka

Watanzania wengi pia wapo Ulaya kujitafutia kipato
Wengine wanatamani kurudi nyumbani lakini wenyewe wanadai nyumbani Tanzania pamekuwa pachungu sana na hawavutiwi tena licha ya kua wana pakumbuka

Nina rafiki yangu yupo USA anasema anatamani kurudi bongo hasa mitaa aliyokulia ila havutiwi tena

Nimegundua
Nchi nyingi ambazo wananchi wake wanazikimbia zina mazingira magumu ya kuishi

Nitaongelea hapa Tanzania kwetu

Tunaweza kukubaliana kwamba nchi hii ni ngumu na haivutii kuishi, labda uwe na kiwango fulani cha maisha la sivyo ni shida sana

Umewahi kwenda kwenye hospitali za umma? Msongamano mazingira yasiyo rafikiI mean uchafu umeshuhudia?

Usafiri wa umma daladala alooo!

Watu wanajazwa kuliko hata uwezo wa daladala
Humo ndani ni kukanyagana

Mtu anaenda kazini alfajiri kuwahi foleni anarudi anadandia gari kama vile nyani wanavyodandia miti unapanda daladala unaogopa kugusa hata lile bomba mana lina majasho ya kila namna

Msongamano harufu za kila aina zisizovutia unaweza kupata depression

Masoko jamani! Masokoni ukienda huko kipindi cha mvua uvae gumboots, la sivyo unarudi kama umetoka kulima mpunga
Umewahi kwenda Soko la Mabibo kipindi cha mvua?

Machinga wamezagaa mabarabarani member kwa miguu anaposhana na magari pkpk bajaji uso kwa uso vipaza sauti, sumu za mende, kunguni.
Yaani unatembea unahisi kuchanganyikiwa

Hayo ni machache kati ya yale mengine mengi

Hivi, muda huu unavutiwa na kuishi Tanzania?

Umezaliwa Tanzania 🇹🇿 na unatamani kuondoka?
Ni nini sababu yako?

ShesRise_1 ✋️
Hao waliokwenda nchi za Ulaya,wanawanawisha na kuwaogesha vibibi vya kizungu na vibabu vya kizungu
 
Natamani kuzurula duniani ila naipenda nchi yangu. Na napenda kuishi hapa kuliko mahali pengine popote duniani.
Unaipenda nchi yako kwa sababu hujawahi kutoka na kuona nchi zingine zilivyo.

Ukitoka na kuona nchi nyingine zilivyo na mifumo yao ilivyo, hutoipenda tena hii bongo yenye maisha ya kuunga unga.

Masoud Kipanya alifika Europe, akoana mifumo ya wenzetu ilivyo, akabaki anajiuliza hawa wenzetu wanafanyaje fanyaje. Yani kila kila kitu kina run smoothly. Hakuna longolongo.

Lakini kwa ambao hawajatoka, wanaweza kuridhika na kuona kwamba Maisha ya Tanzania ni bora sana. Na wakabaki kuyapenda, Kumbe hawana exposure.
 
👏👏
 
Unaweza kuwa na pesa ndio.

Lakini miundombinu mibovu na huduma mbovu bado zitakuwa na kikwazo kwako.

Ndio maana kuna watu wana pesa sana hapa bongo, lakini kuna baadhi ya huduma wanalazimika kwenda nje ya nchi kuzifuata.

Hata kama una pesa, Bado Bongo ni ngumu.

Kuna magonjwa ukiugua hapa nchini, lazima uende nje ya nchi.

Kuna teknolojia na utaalamu ambao ukiuhitaji lazima utoke nje ya nchi.
Bado Bongo ni kuzuri, ata huko unakotaka kukimbilia changamoto zipo, ilimradi wewe ni mwanadamu, changamoto ni sehemu ya maisha yako
 
Back
Top Bottom