Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

izi nchi sio za kuzaliwa
Hizi nchi ni makaburini mkuu, ukisikia jehanum ndio huku sasa. Vitu basics kabisa kwa binadamu vimetushinda tunaishi kama kuku wa kienyeji tu. Hata ukiwa na pesa bado sulubu utazipata tu, ndio maana mzee wa Msoga kajitafutia ajira aweze kua anazunguka mamtoni akirudi bongo anasalimia kidogo wajukuu anaanza zake. Mamaetu nae kajitengenezea njia akimaliza muda wake atakua anapumzika Dubai, Oman au Qatar. Nani anataka mashida banaa kila mtu anapenda raha ukichoka unamuita "Alexa" anarahisisha, mambo ya maji ya mandoo kichwani huo ni ujima.
 
Hizi nchi ni makaburini mkuu, ukisikia jehanum ndio huku sasa. Vitu basics kabisa kwa binadamu vimetushinda tunaishi kama kuku wa kienyeji tu. Hata ukiwa na pesa bado sulubu utazipa tu, ndio maana mzee wa Msoga kajitafutia ajira aweze kua anazunguka mamtoni akirudi bongo anasalimia kidogo wajukuu anaanza zake. Mamaetu nae kajitengenezea njia akimaliza muda wake atakua anapumzika Dubai, Oman au Qatar. Nani anataka mashida banaa kila mtu anapenda raha ukichoka unamuita "Alexa" anarahisisha, mambo ya maji ya mandoo kichwani huo ni ujima.
hapa ni namna tu ya kutoka bongo wallah sitakuja kanyaga tena hapa
 
Kama hupendi ubora, inamaanisha unapenda uduni, huduma mbovu na miundombinu duni?
Kila pahala pana ubora wake na uduni wake, inategemeana na mtu mwenyewe anapenda mambo gani maishani mwake.

Hatufanani wajameni, kwanini hamuelewi hilo.
 
Wabongo wenyewe waliotoka South Africa juzi juzi tu hapa. Wanakwambia maisha ya South Africa ni mazuri sema shida ni magenge ya uhalifu tu. Na ile chuki ya wazulu dhidi ya raia wa kigeni (Xenophobia).

Lakini Wabongo wenzetu walikuwa hawataki kuondoka South Africa.

Kwenye miundombinu, Wanakwambia South Africa kama Ulaya.

Wamerudi hapa bongo, wengine hawajui hata wanaanzia wapi.

Mmoja kafika Mwananyamala hiyo kakuta hela alizokuwa anatuma ili nyumba ijengwe zimepigwa. Hakuna nyumba, hakuna hela. Kaona isiwe kesi wakagawana majengo ya serikali na wazazi wake. Yeye jela, wazazi futi sita underground.

Maisha ya bongo sio mchezo aseeh!
 
Kila pahala pana ubora wake na uduni wake, inategemeana na mtu mwenyewe anapenda mambo gani maishani mwake.

Hatufanani wajameni, kwanini hamuelewi hilo.

Kwamba wewe unafurahia huduma mbovu, maji na umeme kuwa changamoto miaka 60 baada ya uhuru huku mkiomba misaada ya madawati na vyoo kwa wahisani? Kama hii sio epitome ya ujinga ni nini?
 
wazungu wenyewe wanaitaman Africa

Wazungu gani hao wanaotamani Afrika? Wanatamani kutembelea au kuishi?

Unajua nchi karibu zote za Ulaya na America kuingia Africa ni visa on arrival? Nini kinachowashinda kuhamia kama wanaitamani sana?

Isingekuwa kikwazo cha visa Afrika nzima ingekua Ulaya. Ona wamatumbi wanavyokufa kama sisimizi pale Mediterranean Sea wakijaribu kuzamia Ulaya. A real tragedy. Umewahi sikia wazungu wanazamia bara la giza?

Wamatumbi tuache kujilisha upepo. Mbele ni mbele na Afrika bado ni bara la giza. Nchi inayopewa misaada ya madawati na vyoo na bado hawawezi kuvitunza unailinganisha vp na nchi zinazoongelea kufika nje ya milky way galaxy!
 
Afrika nitajiri ina rasilimali za kutosha sema tuna viongozi wabovu na wenye tamaa
ndio maana wazungu wakafanya afrika colon lao kwaajili ya kuchota mali na kiwekeza kwao
tungekuwa na viongozi bora kama gadafi sidhani kama tungetamani kuzaliwa nje ya afrika
 
Unafurahi kuzaliwa na kuishi Tanzania?

Umewahi kusikia watu wakisema hawapendi nchi walizozaliwa?

Leo katika kipindi cha Amka na BBC kuna taarifa nimesikia kuhusu wahamiaji kutoka nchi za Nicaragua na Honduras

Wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wanafunga safari wakipitia nchi ya Mexico na kujaribu kuvuka mpaka kuingia Marekani kwa madai ya kutafuta maisha bora

Hata kwetu kuna watu wamekuwa wakiondoka na kwenda nchi nyingine
Watanzania wengi wapo Afrika Kusini mpaka tumeona miezi ya nyuma walivyofurushwa na kurudi nyumbani tena kwa msaada wa serikali wengine wakiwa na muonekano wa kutia shaka

Watanzania wengi pia wapo Ulaya kujitafutia kipato
Wengine wanatamani kurudi nyumbani lakini wenyewe wanadai nyumbani Tanzania pamekuwa pachungu sana na hawavutiwi tena licha ya kua wana pakumbuka

Nina rafiki yangu yupo USA anasema anatamani kurudi bongo hasa mitaa aliyokulia ila havutiwi tena

Nimegundua
Nchi nyingi ambazo wananchi wake wanazikimbia zina mazingira magumu ya kuishi

Nitaongelea hapa Tanzania kwetu

Tunaweza kukubaliana kwamba nchi hii ni ngumu na haivutii kuishi, labda uwe na kiwango fulani cha maisha la sivyo ni shida sana

Umewahi kwenda kwenye hospitali za umma? Msongamano mazingira yasiyo rafikiI mean uchafu umeshuhudia?

Usafiri wa umma daladala alooo!

Watu wanajazwa kuliko hata uwezo wa daladala
Humo ndani ni kukanyagana

Mtu anaenda kazini alfajiri kuwahi foleni anarudi anadandia gari kama vile nyani wanavyodandia miti unapanda daladala unaogopa kugusa hata lile bomba mana lina majasho ya kila namna

Msongamano harufu za kila aina zisizovutia unaweza kupata depression

Masoko jamani! Masokoni ukienda huko kipindi cha mvua uvae gumboots, la sivyo unarudi kama umetoka kulima mpunga
Umewahi kwenda Soko la Mabibo kipindi cha mvua?

Machinga wamezagaa ma barabarani watembea kwa miguu unapishana na magari pkpk bajaji uso kwa uso vipaza sauti, sumu za mende, kunguni.
Yaani unatembea unahisi kuchanganyikiwa

Hayo ni machache kati ya yale mengine mengi

Hivi, muda huu unavutiwa na kuishi Tanzania?

Umezaliwa Tanzania 🇹🇿 na unatamani kuondoka?
Ni nini sababu yako?

ShesRise_1 ✋️
Mkuu salama? Like always I like you.

Kuhusu maada ya Leo, naomba niandike kwa herufi kubwa NAPENDA KUZALIWA TANZANIA, NA SIKU ZOTE NAFURAHIA KUISHI TANZANIA. NDANI YA MOYO WANGU TANZANIA NI YA PEKEE SANA.

Sijatembea sana kuzunguka nchi za watu lakini nimeizunguka Tanzania karibia yote, nimeishi mikoa zaidi ya 20 hapa Tanzania, nimetembea wilaya zaidi ya 60 pia katika kutembea nimeishi na jamii tofauti sana, niseme tuu ukweli wangu Tanzania ni nzuri sana, Tanzania inafursa za Kila aina na mwisho Tanzania inapendeza sana ukiiangalia kwa jicho la uzuri.

Nakubaliana nawewe mtoa maada kuhusu baadhi ya kero, mfano

1. Barabara ni mbovu sana katika baadhi ya wilaya hapa nchini. Kuna mwaka nilishawahi kwenda Manyara, wilaya sijui ni kata inaitwa Hydom aisee nilitamani safari iishie njiani maana barabara ni mbovu sana, matope na utelezi.

2. Kuna vijiji hakuna kabisa huduma za afya na kama zipo bhasi ni za viwango duni sana. Nilishawahi kuwa katika Kijiji Fulani nikazidiwa kwenda zahanati nakuta umeme hakuna na dokta hawezi kufanya kazi gizani, nikachukua boda kwenda hospital ya kata, napo nilifika nikamkuta mtu wa mapokezi tuu, nikaandikisha alafu nikapewa dawa ya kuzuia kutapika kwa sababu dokta hakuwepo 😡😡😡💔 na elfu 20 ikaishia kuandikisha na kupewa dawa ya kuzuia kutapika tuu. Ilikua mida mibovu sana around saa6 usiku ikanilazimu kwenda km 20 ili kuifuata hospital ya misheni ndio nikalazwa huko😡😡😡💔. Nilitumia gharama kubwa sana kwa tatizo la kawaida kabisa. Hivyo Kuna umuhimu wa Serikali kuboresha huduma za afya hasa hasa vijijini.

3. Kero za usafiri mijini, hili suala ndilo Huwa linanifanya napakimbia daslam, kwakweli Hilo Jiji foleni zimezidi, hiyo kitu inarudisha sana nyuma uchumi wa watu binafsi na hasa vijana ambao hawana option za ziada.

4. Kuhusu kero za uchafu masokoni, hizi ni sisi wananchi ndio tunasababisha. Binafsi huwa sinunui kitu mahali pachafu, nitakupa mfano wa Mbeya wale ndugu zangu ni wachafu sana Yaani hawajali kabisa mazingira ya usafi hivyo hata Mimi niliamua kutafuta mazingira yangu ya usafi ili niishi kwa amani.

5. Ukosefu wa elimu, hii ni changamoto kubwa sana katika nchi yetu. Ukienda vijijini unaweza ukatoa machozi, watu wanaishi katika mazingira magumu na mabaya sana lakini sio kwamba hayo mazingira hayafai kuishi watu, Bali watu wamekosa uelewa wa kurahisisha mazingira yao yawe Bora kwa wao kuishi. Unakuta mtu anang'ombe zaidi ya 30 lakini anakaa nyumba ya hovyo sana, watu wanalima alizeti lakini wanakula mboga bila mafuta😡😡😡💔. Hapa naungana na sera ya late E.N.L ELIMU,ELIMU,ELIMU. Serikali ijielekeze katika kuwasaidia watu kujikomboa, tuachane na hii elimu ya mkoloni ambayo inamaliza rasilimali za familia na kuleta umaskini.

6. Mazingira wezeshi kwa vijana wanaoamua kufanya shughuli za kujiinua kiuchumi. Nimeishi sehemu nyingi nimekutana na vijana wengi na kuwasikiliza, wengi wao wanafanya kazi kwa bidii sana lakini matunda ni madogo au hayapo kabisa kwasababu ya kukosa mazingira wezeshi. Mazingira wezeshi inahusisha kwenye mifumo ya kikodi, elimu ya kuendeleza miradi Yao na pia madalali wanaua sana mitaji ya vijana hasa pale wanapotaka kuingia katika masoko makubwa hasa Dar es salaam. Pia serikali ilitakiwa itoe misamaha ya kikodi kwa makampuni ya vijana wa kitanzania kama ambavyo inatoa kwa makampuni ya nje.

7. Kutekana, kuuana, kutishiana maisha na siasa za kipumbavu ndio zinaipa taswira mbaya nchi yetu. Hope Kuna siku tutatoka kwenye hili ombwe.

Haya ni baadhi tuu ya kero ninazoziona hapa nnchini kwetu lakini nchi yetu Bado ni nzuri sana kwa kuishi.
 
Kwamba wewe unafurahia huduma mbovu, maji na umeme kuwa changamoto miaka 60 baada ya uhuru huku mkiomba misaada ya madawati na vyoo kwa wahisani? Kama hii sio epitome ya ujinga ni nini?
Aliesema anafurahia huduma mbovu ni nani?? Mbona mnahamisha mjadala.
Issue ni kuipenda nchi yako au kutamani ungekua majuu.

Nimechagua kuipenda, na sababu za kuipenda nchi fulani sio hizo tu za huduma, kuna mengi nyuma ya hayo.

Hujawahi kusikia mtu anaenda nje kunamshinda na kwa hiari yake anarudi bongo akidai mazingira ya huko yamemshinda.

Na hizo nchi sio kua haziendeki, zinaendeka kwanini msiende??
 
Mkuu salama? Like always I like you.
Salama mkuu
Shukran sana 🙏🙏
Kuhusu maada ya Leo, naomba niandike kwa herufi kubwa NAPENDA KUZALIWA TANZANIA, NA SIKU ZOTE NAFURAHIA KUISHI TANZANIA. NDANI YA MOYO WANGU TANZANIA NI YA PEKEE SANA.

Sijatembea sana kuzunguka nchi za watu lakini nimeizunguka Tanzania karibia yote, nimeishi mikoa zaidi ya 20 hapa Tanzania, nimetembea wilaya zaidi ya 60 pia katika kutembea nimeishi na jamii tofauti sana, niseme tuu ukweli wangu Tanzania ni nzuri sana, Tanzania inafursa za Kila aina na mwisho Tanzania inapendeza sana ukiiangalia kwa jicho la uzuri.

Nakubaliana nawewe mtoa maada kuhusu baadhi ya kero, mfano

1. Barabara ni mbovu sana katika baadhi ya wilaya hapa nchini. Kuna mwaka nilishawahi kwenda Manyara, wilaya sijui ni kata inaitwa Hydom aisee nilitamani safari iishie njiani maana barabara ni mbovu sana, matope na utelezi.

2. Kuna vijiji hakuna kabisa huduma za afya na kama zipo bhasi ni za viwango duni sana. Nilishawahi kuwa katika Kijiji Fulani nikazidiwa kwenda zahanati nakuta umeme hakuna na dokta hawezi kufanya kazi gizani, nikachukua boda kwenda hospital ya kata, napo nilifika nikamkuta mtu wa mapokezi tuu, nikaandikisha alafu nikapewa dawa ya kuzuia kutapika kwa sababu dokta hakuwepo 😡😡😡💔 na elfu 20 ikaishia kuandikisha na kupewa dawa ya kuzuia kutapika tuu. Ilikua mida mibovu sana around saa6 usiku ikanilazimu kwenda km 20 ili kuifuata hospital ya misheni ndio nikalazwa huko😡😡😡💔. Nilitumia gharama kubwa sana kwa tatizo la kawaida kabisa. Hivyo Kuna umuhimu wa Serikali kuboresha huduma za afya hasa hasa vijijini.

3. Kero za usafiri mijini, hili suala ndilo Huwa linanifanya napakimbia daslam, kwakweli Hilo Jiji foleni zimezidi, hiyo kitu inarudisha sana nyuma uchumi wa watu binafsi na hasa vijana ambao hawana option za ziada.

4. Kuhusu kero za uchafu masokoni, hizi ni sisi wananchi ndio tunasababisha. Binafsi huwa sinunui kitu mahali pachafu, nitakupa mfano wa Mbeya wale ndugu zangu ni wachafu sana Yaani hawajali kabisa mazingira ya usafi hivyo hata Mimi niliamua kutafuta mazingira yangu ya usafi ili niishi kwa amani.

5. Ukosefu wa elimu, hii ni changamoto kubwa sana katika nchi yetu. Ukienda vijijini unaweza ukatoa machozi, watu wanaishi katika mazingira magumu na mabaya sana lakini sio kwamba hayo mazingira hayafai kuishi watu, Bali watu wamekosa uelewa wa kurahisisha mazingira yao yawe Bora kwa wao kuishi. Unakuta mtu anang'ombe zaidi ya 30 lakini anakaa nyumba ya hovyo sana, watu wanalima alizeti lakini wanakula mboga bila mafuta😡😡😡💔. Hapa naungana na sera ya late E.N.L ELIMU,ELIMU,ELIMU. Serikali ijielekeze katika kuwasaidia watu kujikomboa, tuachane na hii elimu ya mkoloni ambayo inamaliza rasilimali za familia na kuleta umaskini.

6. Mazingira wezeshi kwa vijana wanaoamua kufanya shughuli za kujiinua kiuchumi. Nimeishi sehemu nyingi nimekutana na vijana wengi na kuwasikiliza, wengi wao wanafanya kazi kwa bidii sana lakini matunda ni madogo au hayapo kabisa kwasababu ya kukosa mazingira wezeshi. Mazingira wezeshi inahusisha kwenye mifumo ya kikodi, elimu ya kuendeleza miradi Yao na pia madalali wanaua sana mitaji ya vijana hasa pale wanapotaka kuingia katika masoko makubwa hasa Dar es salaam. Pia serikali ilitakiwa itoe misamaha ya kikodi kwa makampuni ya vijana wa kitanzania kama ambavyo inatoa kwa makampuni ya nje.

7. Kutekana, kuuana, kutishiana maisha na siasa za kipumbavu ndio zinaipa taswira mbaya nchi yetu. Hope Kuna siku tutatoka kwenye hili ombwe.

Haya ni baadhi tuu ya kero ninazoziona hapa nnchini kwetu lakini nchi yetu Bado ni nzuri sana kwa kuishi.
Asante sana kwa maoni yako mkuu.

Umesema unaipenda Tanzania
Naomba nikwambie kila mmoja wetu hapa anaipenda Tanzania tena sana
Ndiyo maana kila siku tunaandika hapa jukwaani tukidai mabadiliko

Kinachochukiwa si Tanzania kama nchi wala jina lake
Tunachokichukia na kutofurahishwa nacho ni mazingira yaliyopo
Mazingira ya hovyo mwanadamu kuishi karne ya 21

Uzuri ni kwamba baadhi ya kero umezitaja mwenyewe na umesema hukuambiwa bali wewe mwenyewe umeshuhudia

Hayo uliyoyasema na mengine mengi ndiyo yanayofanya baadhi yetu tusivutiwe kuishi Tanzania
Au walio njee ya Tanzania wasitamani kurudi
Lakini haimaanishi kwamba hatuipendi nchi yetu tunaipenda sana

Kuhusu kuongea na kupaza sauti kudai mabadiliko yanayoendana na kasi ya dunia wewe mwenyewe unaona kinachotoke
Pale tu ukijaribu kutoa maoni au kupinga jambo fulani unakutana na kesi za hapa na pale

Tanzania ni nzuri kuitaja mdomoni
Tanzania ni nzuri kwa kutembelea ngorongoro na serengeti

Lakini ukirudi kwenye maisha halisi na makazi ya watu na huduma za kijami Tanzania haivutii kuishi na mtu aliestarabika
 
Kila mtu yupo huru kuishi apendapo,
Home is where the heart is,home is the feeling not a place,ukiona mambo hayaendi hapo ulipo,move you are not a tree,

Nawasilisha wabeba box wenzangu.
Kwa mtazamo wangu, kauli hii ina ukweli. Nyumbani ni pale unapohisi amani, unapokubalika na unapoweza kuwa wewe mwenyewe. Wakati mwingine hisia hiyo unaipata mbali kabisa na mahali ulipozaliwa.
 
Back
Top Bottom