Salama mkuu
Shukran sana 🙏🙏
🙏🙏🤝
Asante sana kwa maoni yako mkuu.
Umesema unaipenda Tanzania
Naomba nikwambie kila mmoja wetu hapa anaipenda Tanzania tena sana
Ndiyo maana kila siku tunaandika hapa jukwaani tukidai mabadiliko
Kama unaipenda kwanini useme bongo bahati mbaya🤔🤔🤔🤪 tena ukatupia na wimbo wa Young D ambaye yeye mwenyewe alishapakimbia hapa nyumbani???
Kinachochukiwa si Tanzania kama nchi wala jina lake
Tunachokichukia na kutofurahishwa nacho ni mazingira yaliyopo
Mazingira ya hovyo mwanadamu kuishi karne ya 21
Mkuu haya mazingira magumu ndio changamoto zenyewe na Kila changamoto inafursa ndani yake.
Binafsi naona hizi changamoto tunaweza kuzitatua sisi wenyewe. Mfano uchafu katika masoko tunaweza kuondoa hiyo changamoto kwa kuweka masoko ya mtandao au tukagomea kwenda kununua bidhaa katika masoko machafu.
Mimi nikienda mahali nikakuta mazingira ya uchafu huwa sifumbii macho, nakuchana tuu, Sasa je! Hili la uchafu nalo tunataka Serikali ndio ipige kelele???
Kipindi Cha Magufuli kulikua na utaratibu wa kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi. Kwakweli ilikua ni changamoto sana kupata huduma katika hiyo siku, vijana wa halmashauri walikua wanasumbua sana endapo wataikuta biashara Yako imefunguliwa wakati wa kufanya usafi, Lakini mimi binafsi nilikua nafungua ofisi na nafanya biashara vizuri kabisa. Siku waliyonikamata niliwapa jibu jepesi tuu kwamba MIMI SIHITAJI KUAMBIWA NIFANYE USAFI MAANA BIASHARA YANGU INAHITAJI USAFI.
Pia nilikua nasumbuliwa sana na ushuru wa taka na kusafisha mitaro, lakini ilifikia kipindi nikawaambia ukweli kwamba siwezi kutoa tena Hela yangu kuwapa ninyi mpaka nije kuwaona mkisafisha mitaro pia gari la taka likipita walau mara mbili kwa wiki, kwa msimamo wangu huu tulipekeshana mpaka kwa mtendaji kata baadae polisi mwishowe ilibidi waniache tuu.
Kuna mahali kuna mashamba watu wanalima parachichi za kutosha lakini barabara ni changamoto, walichoamua ni kutafuta bulldozer na kuchonga barabara Yao. Hizi changamoto zingine inabidi sisi wenyewe ndio tuzitatue sio kila kitu ni lazima serikali. Ninachotaka kusema ni kwamba muda mwingine tuzitumie changamoto kama fursa pia kwetu wenyewe.
Mfano mwingine ni huo wa usafiri hapo Dar kwangu Mimi naona ni bonge la fursa lakini kwasasa shida ni mtaji tuu, pia walio na mitaji wanaangalia sehemu watakayopata Hela pasipo kuumia, kitu ambacho sio kweli hakuna mafanikio yasiyo na maumivu. We have to pay the price.
Uzuri ni kwamba baadhi ya kero umezitaja mwenyewe na umesema hukuambiwa bali wewe mwenyewe umeshuhudia
Hayo uliyoyasema na mengine mengi ndiyo yanayofanya baadhi yetu tusivutiwe kuishi Tanzania
Au walio njee ya Tanzania wasitamani kurudi
Lakini haimaanishi kwamba hatuipendi nchi yetu tunaipenda sana
Mkuu unataka nani aje kubadilisha haya???
Tukikimbia wote na kwenda ughaibuni ndio tutakua tumemaliza tatizo???
Akili ya namna hii nimeiona hata kwenye familia yetu, Kuna shamba lilikua porini sana lakini Mimi nilishawahi kwenda na nikakaa miezi mitatu lakini Kuna siku akatokea mteja akalitaka kwa milioni 400, binafsi nilikataa shamba kuuzwa lakini wanandugu wengine wakataka liuzwe eti kwasababu lipo mbali alafu pia hakuna mtu anaweza kuliangalia kwa ukaribu😓😓😡💔. Nikawauliza swali nani kati yenu alishawahi kwenda kukaa kule shamba hata wiki moja tuu??? Hakuna alietoa jibu nikawaambia Mimi nimeshakaa miezi mitatu hivyo hiyo sababu yenu haina mashiko na pia Haina msingi wowote. Shamba lipo mpaka kesho kutwa.
Kutokana na huo mfano ndio maana viongozi wetu wanauza rasilimali zote kwasababu wanaona wananchi wake wako busy kulaumu na wengine wanawaza kukimbia nchi, hivyo na wenyewe wanaona ni Bora wachukue chochote kitu.
Halafu pia mimi naona kama kuna kukosa elimu au uelewa wa masuala Fulani Fulani, hao diaspora wengi wanaishia kwenye masuala ya ubalozini tuu pia wanafikiri kila jambo linafanyiwa maamuzi kwa siasa au Kila tatizo linatatuliwa kwa siasa tuu.
Ngoja niwaibie Siri hapa, sisi watu weusi tumejaa upumbavu, ujinga na ubinafsi.
Hao waarabu na wahindi ndio wanawapa hela wanasiasa wetu ili wakabadilishe sera na kuweka sera zinazowabeba wao wenyewe tuu.
Kitu ambacho wengi wenu hamkifahamu ni hiki. CCM inawaogopa sana matajiri na siku watanzania watakapoamua kutafuta fedha kwa nguvu zote ndio siku ambayo CCM itatoka madarakani kwa njia yoyote ile au CCM itarudi kuwa chama cha siasa, nje na hapo tutasubiri sana na kulalamika sana.
Kuhusu kuongea na kupaza sauti kudai mabadiliko yanayoendana na kasi ya dunia wewe mwenyewe unaona kinachotoke
Pale tu ukijaribu kutoa maoni au kupinga jambo fulani unakutana na kesi za hapa na pale
Hapa nafikiri umemezwa na demokrasia ya uongo uongo, HAKUNA MABADILIKO YATAKUJA KWA KUONGEA ONGEA AU KUPAZA SAUTI.
Shuleni, kazini, nyumbani na hata sehemu yoyote wanayoishi watu wanajitambua ni kwamba hakuna kitu kinaitwa demokrasia hivyo Mimi sisapoti hayo masuala ya kupaza sauti au kukaa kupiga kelele humu mitandaoni. Kama nikiona jambo halipo sawa kwa upande wangu namtafuta muhusika namuelewesha tusipoelewana bhasi mwenye nguvu atapishwa tuu.
Tanzania ni nzuri kuitaja mdomoni
Tanzania ni nzuri kwa kutembelea ngorongoro na serengeti
Lakini ukirudi kwenye maisha halisi na makazi ya watu na huduma za kijami Tanzania haivutii kuishi na mtu aliestarabika
Tanzania ni nzuri sana endapo watanzania wote tutawajibika kuijenga nchi yetu. Nilitoa mifano ya barabara kwasababu kwa Sheria za nchi yetu mtu binafsi hauruhusiwi kuchonga barabara ndio maana nikasema serikali iwajibike kwenye kuchonga barabara, lakini hata hivyo inawezekana kwa mtu binafsi kuchonga barabara pia. Baba yangu Mimi alishawahi kuchonga barabara japokuwa ilileta mgogoro na TANROAD lakini kulikua hakuna namna hatuwezi kusubiri TANROAD waje kwa wakati wanaoujua wao.
Tuache kulalamika, tuache kuwaza kukimbia changamoto alafu tutafute namna ya kuzitatua hizi changamoto zetu.