Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

Ungepata nafasi ya kuchagua nchi unayopenda uzaliwe kati ya Marekani na Tanzania?

Au unapewa nafasi, mke wako ambaye ni mjazito achague nchi ya kumzaa mtoto wako kati ya Marekani na Tanzania?

Ungechagua nchi ipi?
Hapa utajibiwa kinafiki. Wanaokula keki ya nchi wenyewe watoto wao wanawapeleka huko wakapate mikoba.
 
Hello Twin, ukweli mchungu ni kwamba Bongo hata ukiwa na pesa bado utaishi maisha ya kubahatisha tu kwa sababu nchi nzima haina basic standards.

Yani unakuwa kama mfalme kwenye kisiwa cha takataka, ndani kwako ni kuzuri, lakini ukifungua tu geti unakutana na fujo, vumbi, foleni za kijinga, na miundombinu iliyochoka. Unanunua gari la kifahari halafu linaharibika suspension ndani ya mwaka mmoja kwa sababu ya mashimo barabarani, unalipa kodi kubwa halafu bado unachimba kisima chako mwenyewe, unafunga solar na majenereta, na unaajiri walinzi binafsi kwa sababu huduma za umma zimefeli.

Mbaya zaidi, hata kwenye huduma za afya au usalama, pesa yako haikupi uhakika wa kupona ukipata dharura usiku kwa sababu hakuna mfumo wa dharura unaoeleweka, unaishia kufa kizembe tu ukiwa na mamilioni yako benki.

Ndiyo maana wanaopata nafasi wanaenda nchi zilizoendelea si kwa sababu kule kuna pesa za bure, bali kule mfumo tayari umeshatengeneza quality of life, kwa hiyo hata ukiwa na kipato cha kawaida unaishi kwa heshima na amani ya akili kuliko tajiri wa huku anayetumia nguvu nyingi kujilinda na mazingira mabovu.
Mimi nilikuwa naona uvivu kuandika haya yote maana hata unaemwandikia haelewi unazungumza nini. Tz hata uwe na hela ni pa hovyo tu. Achilia mbali mazingira hata kisiasa unaweza kuwa bilionea lakini ukakimbizwa mchakamchaka na akina Makonda au Chalamila bila sababu yoyote ya maana.
 
Wala hatujajipata 😂 Mi napenda ku temper na mifumo kwahiyo bongo kunanifaa sana.

But i highly recommend watu wakipata nafasi waondoke, Kaka yangu aliondoka akiwa na miaka 35, now ana 38 you won’t believe ni kiasi gani amejiboresha, People in bongo are working hard in a wrong country (huu msemo niliusikia humu)

wagai gai ndio tubaki. Mimi nina chances za kuondoka, jiulize kwanini bado nipo 🤣
Hapa panawafaa sana nyie wapigaji wa mifumo. Kuna cousin aliondoka 5 yrs ago. Miaka miwili ya kwanza alikuwa anatamani amalize shule arudi. Sasa hivi ana kazi na maisha yake akija hapa mwezi tu anaona mwaka anagombana na kila mtu. Hataki kuishi tena Tz. Baba yake alikuwa anamsisitiza asirudi.
 
Ha ha ha. Watu wanajiaminisha uongo hadi unakuwa ukweli. Life expectancy ya Mtanzania haijawahi kuwa juu zaidi ya ilivyo sasa hivi. Meaning zamani wengi walikuwa wanakufa na umri mdogo ila tukiona wazee wachache wametoboa miaka 100 tunahitimisha.
See!
 
Hapa panawafaa sana nyie wapigaji wa mifumo. Kuna cousin aliondoka 5 yrs ago. Miaka miwili ya kwanza alikuwa anatamani amalize shule arudi. Sasa hivi ana kazi na maisha yake akija hapa mwezi tu anaona mwaka anagombana na kila mtu. Hataki kuishi tena Tz. Baba yake alikuwa anamsisitiza asirudi.
Walahi bongo jau, Kuna hitaji uwe mbabaifu sana, Kama umenyooka it’s not worthy it.

Unajua sehemu ambayo kuna mifumo na rules, We know exactly what to expect unapoamka asubuhi, au unapoenda/unapokuwepo mahali.

Huku sasa: Umeamka uwahi kazini , unafika kituoni mwendokasi haifanyi kazi, blah blah Huwezi kupangilia mambo, unapangiwa mambo na mifumo mibovu.

Kuna mtu alisema hata watoto Tz wote wamepatikana kwa bahati mbaya 🤣
 
mi naona hata ukiwa na hela tanzania hutaenjoy . kuna mifumo mibovu sana . yani hata kama una hela ukiona umaskini unaokuzunguka au namna watu anavyoteseka kwa kiukosa huduma muhimu unajikuta tu moyo unasinyaa na furaha ya utajiri wako inanywea.
Uko sahihi, Mimi huwa najiuliza Kwanini mpaka leo 2026 watu wanabebeshwa magunia na mizigo mizito mgongoni (Kuli) Traditional kuli, huku ni kuua watu migongo aiseee, kuna machine chungu tele za kurahisisha kazi.

Kuna mambo ukiyaangalia moyo unashuka chini.
 
Unafurahi kuzaliwa na kuishi Tanzania?

Umewahi kusikia watu wakisema hawapendi nchi walizozaliwa?

Leo katika kipindi cha Amka na BBC kuna taarifa nimesikia kuhusu wahamiaji kutoka nchi za Nicaragua na Honduras

Wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wanafunga safari wakipitia nchi ya Mexico na kujaribu kuvuka mpaka kuingia Marekani kwa madai ya kutafuta maisha bora

Hata kwetu kuna watu wamekuwa wakiondoka na kwenda nchi nyingine
Watanzania wengi wapo Afrika Kusini mpaka tumeona miezi ya nyuma walivyofurushwa na kurudi nyumbani tena kwa msaada wa serikali wengine wakiwa na muonekano wa kutia shaka

Watanzania wengi pia wapo Ulaya kujitafutia kipato
Wengine wanatamani kurudi nyumbani lakini wenyewe wanadai nyumbani Tanzania pamekuwa pachungu sana na hawavutiwi tena licha ya kua wana pakumbuka

Nina rafiki yangu yupo USA anasema anatamani kurudi bongo hasa mitaa aliyokulia ila havutiwi tena

Nimegundua
Nchi nyingi ambazo wananchi wake wanazikimbia zina mazingira magumu ya kuishi

Nitaongelea hapa Tanzania kwetu

Tunaweza kukubaliana kwamba nchi hii ni ngumu na haivutii kuishi, labda uwe na kiwango fulani cha maisha la sivyo ni shida sana

Umewahi kwenda kwenye hospitali za umma? Msongamano mazingira yasiyo rafikiI mean uchafu umeshuhudia?

Usafiri wa umma daladala alooo!

Watu wanajazwa kuliko hata uwezo wa daladala
Humo ndani ni kukanyagana

Mtu anaenda kazini alfajiri kuwahi foleni anarudi anadandia gari kama vile nyani wanavyodandia miti unapanda daladala unaogopa kugusa hata lile bomba mana lina majasho ya kila namna

Msongamano harufu za kila aina zisizovutia unaweza kupata depression

Masoko jamani! Masokoni ukienda huko kipindi cha mvua uvae gumboots, la sivyo unarudi kama umetoka kulima mpunga
Umewahi kwenda Soko la Mabibo kipindi cha mvua?

Machinga wamezagaa ma barabarani watembea kwa miguu unapishana na magari pkpk bajaji uso kwa uso vipaza sauti, sumu za mende, kunguni.
Yaani unatembea unahisi kuchanganyikiwa

Hayo ni machache kati ya yale mengine mengi

Hivi, muda huu unavutiwa na kuishi Tanzania?

Umezaliwa Tanzania 🇹🇿 na unatamani kuondoka?
Ni nini sababu yako?

ShesRise_1 ✋️

Kwa dunia na kwa Afrika Tanzania ina kiwango kidogo sana cha wananchi wake kukimbia nchi kiharamu na kwenda nchi zengine kutafuta maisha bora.
 
Marais wa Africa wenyewe muda mwingi wapo Ulaya. Africa wanarudi kupoteza muda, kudanganya maboya na kuzikwa tu. Hao ni marais wenye kila kitu at their disposal, vp wananchi?

Africa ni shithole kama MwaTrump alivyosema. Ingewezekana kila mtu angeondoka au kila mtu atabaki kama ikipiga hatua. Until then, bongo bahati mbaya.
 
Masoud akahitimisha kua anaipenda Europe kuliko Tanzania sio??

Kwani kuna mtu hajui jinsi hizo nchi zilivyo mkuu?? Na kuna sababu mbalimbali za mtu kuipenda sehemu fulani sio lazima iwe huduma za kijamii na mifumo mizuri.

Hata walio huko nao wana changamoto nyingine pamoja na ubora walionao kwenye baadhi ya mambo. Kwahiyo hilo ni jambo mtambuka.

Pamoja na hayo bado naipenda Tanzania.

Kama hupendi ubora, inamaanisha unapenda uduni, huduma mbovu na miundombinu duni?
 
Marais wa Africa wenyewe muda mwingi wapo Ulaya. Africa wanarudi kupoteza muda, kudanganya maboya na kuzikwa tu. Hao ni marais wenye kila kitu at their disposal, vp wananchi?

Africa ni shithole kama MwaTrump alivyosema. Ingewezekana kila mtu angeondoka au kila mtu atabaki kama ikipiga hatua. Until then, bongo bahati mbaya.
Mie leo nimebaki ku like yote mmeongea wadau🔥🔥
 
Nimegundua kuna watu bado wako tayari kutawaliwa na wazungu.

Kwa mentality yako, tukiweka opinion poll, wewe utakubali kurudi utumwani, ukafanye kazi ya kumenya vitunguu na kubeba ma-box ya wazungu kuliko kutatua changamoto zako huko kwenu umatumbini.

Mkuu, acha kuwapa utukufu wazungu, jitahidi usome world history, ujue civilizations zilizofanya mambo makubwa kabla yao wazungu ambao sehemu kubwa ni wezi na waporaji.

Tuliza fuvu Mkuu, watu weusi kutoka Afrika wamefanya mambo makubwa sana kwenye hii dunia kabla ya hao wazungu wababaishaji.

Hayo mambo makubwa yapo wapi au yaliishia wapi?

Africa yote ilikuwa mbali kimaendeleo wakati wa ukoloni kuliko sasa. Leo hii waafrika wakienda Ulaya na mizungu kuja Africa, in 5yrs wamatumbi wote watakua wanapambana kuzamia Africa. The bitter truth.
 
Marais wa Africa wenyewe muda mwingi wapo Ulaya. Africa wanarudi kupoteza muda, kudanganya maboya na kuzikwa tu. Hao ni marais wenye kila kitu at their disposal, vp wananchi?

Africa ni shithole kama MwaTrump alivyosema. Ingewezekana kila mtu angeondoka au kila mtu atabaki kama ikipiga hatua. Until then, bongo bahati mbaya.
Kuna yule Rais wa Cameroon Paul Biya anaishigi Switzerland, huwa anarudi Cameroon kutembelea tu
 
Kuna yule Rais wa Cameroon Paul Biya anaishigi Switzerland, huwa anarudi Cameroon kutembelea tu

Bora yule kaweka wazi, hawa wengine wote ni same thing. Hakuna rais wa Africa asiye na residence Ulaya au wakijitahidi sana SA (kwa mizungu as well). Hadi kings wa huko North Africa kama Morocco wanaishi muda mwingi France. Na wakiumwa wanakimbia kutibiwa Ulaya. Africa ni makaburini wanarudi kuzikwa tu.
 
Wala hatujajipata 😂 Mi napenda ku temper na mifumo kwahiyo bongo kunanifaa sana.

But i highly recommend watu wakipata nafasi waondoke, Kaka yangu aliondoka akiwa na miaka 35, now ana 38 you won’t believe ni kiasi gani amejiboresha, People in bongo are working hard in a wrong country (huu msemo niliusikia humu)

wagai gai ndio tubaki. Mimi nina chances za kuondoka, jiulize kwanini bado nipo 🤣
Walinisema kikongwe nshachelewa jamani ahhh naenda na mimi states
Never been happy in this country
 
Nadhani hii kasumba inatokana na makuzi. Kwa mara ya kwanza kutoka nje ya TZ nipale nilipokwenda kusoma nchi za watu. Nchi hiyo watu hujivunia utaifa wao. Pili nilipoongeza ujuzi nilikanyaga nchi ambayo ubaguzi kwa watu wote hata ukiwa Mwingereza unaonekana ni dogo tu isipokuwa mmarekani. Na sisi tulikuwa tunaulizwa, ni Mmarekani mweusi ili uheshimike. Ila ungangari wetu tulikuwa tunakubali kuitwa nyani potelea mbali. Hadi leo nikiwa nje, nikirudi Airport nafurahi kurudi nyumbani. Titi la mama tamu hata likiwa la mbwa,waswahili walituasa
Jipe moyo tu, hayo maviongozi yako ndio yanayoongoza kupachukia huko nyumbani na yanakwiba haswaa pesa za umma ili yaje yaishi mamtoni yenyewe na familia zao. Wewe huko mpenda nchi mpaka leo umeme wa kuunga unga, maji safi ya bomba hamna, barabara mbovu, madawa feki ya India n.k. endelea kulipenda titi la mama 😀 😀 😀 😀
 
Back
Top Bottom