ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 23,089
- 52,849
- Thread starter
- #101
Sina tatizo na hiloHao waliokwenda nchi za Ulaya,wanawanawisha na kuwaogesha vibibi vya kizungu na vibabu vya kizungu
Kwani hiyo sio kazi?
Sina tatizo na hiloHao waliokwenda nchi za Ulaya,wanawanawisha na kuwaogesha vibibi vya kizungu na vibabu vya kizungu
Asante sana.Hongera vishu
Hongera sana mkuuMimi niliamua kutoka nchi niliyozaliwa kwa bahati (sisemi bahati mbaya, bahati tu) na kwenda nchi niliyotaka kuishi.
Hello welcome back jukwaani twin 😍Hello Twin, ukweli mchungu ni kwamba Bongo hata ukiwa na pesa bado utaishi maisha ya kubahatisha tu kwa sababu nchi nzima haina basic standards.
Yani unakuwa kama mfalme kwenye kisiwa cha takataka, ndani kwako ni kuzuri, lakini ukifungua tu geti unakutana na fujo, vumbi, foleni za kijinga, na miundombinu iliyochoka. Unanunua gari la kifahari halafu linaharibika suspension ndani ya mwaka mmoja kwa sababu ya mashimo barabarani, unalipa kodi kubwa halafu bado unachimba kisima chako mwenyewe, unafunga solar na majenereta, na unaajiri walinzi binafsi kwa sababu huduma za umma zimefeli.
Mbaya zaidi, hata kwenye huduma za afya au usalama, pesa yako haikupi uhakika wa kupona ukipata dharura usiku kwa sababu hakuna mfumo wa dharura unaoeleweka, unaishia kufa kizembe tu ukiwa na mamilioni yako benki.
Ndiyo maana wanaopata nafasi wanaenda nchi zilizoendelea si kwa sababu kule kuna pesa za bure, bali kule mfumo tayari umeshatengeneza quality of life, kwa hiyo hata ukiwa na kipato cha kawaida unaishi kwa heshima na amani ya akili kuliko tajiri wa huku anayetumia nguvu nyingi kujilinda na mazingira mabovu.
Kila la kheri mkuuMi mwenyewe sio mtanzania.Mimi ni MTANGANYIKA ila kama mambo yangu yakikaa sawa japo na uzèe wangu wa miaka 41 lazima niondoke na nitafia huko na nitarudishwa majivu, na sio Utani.
Mtu hawezi kujivunia sehemu ambayo anaona haimpi thamani na wala haimsaidii kusonga mbele. So far vijana wengi wana mtazamo huo, hata hivyo kila taifa sahivi ni jau. Ni mataifa machache yametulia. Kuna wakati huwa najiuliza nini kilitokea nikazaliwa huku 🤗Unafurahi kuzaliwa na kuishi Tanzania?
Umewahi kusikia watu wakisema hawapendi nchi walizozaliwa?
Leo katika kipindi cha Amka na BBC kuna taarifa nimesikia kuhusu wahamiaji kutoka nchi za Nicaragua na Honduras
Wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wanafunga safari wakipitia nchi ya Mexico na kujaribu kuvuka mpaka kuingia Marekani kwa madai ya kutafuta maisha bora
Hata kwetu kuna watu wamekuwa wakiondoka na kwenda nchi nyingine
Watanzania wengi wapo Afrika Kusini mpaka tumeona miezi ya nyuma walivyofurushwa na kurudi nyumbani tena kwa msaada wa serikali wengine wakiwa na muonekano wa kutia shaka
Watanzania wengi pia wapo Ulaya kujitafutia kipato
Wengine wanatamani kurudi nyumbani lakini wenyewe wanadai nyumbani Tanzania pamekuwa pachungu sana na hawavutiwi tena licha ya kua wana pakumbuka
Nina rafiki yangu yupo USA anasema anatamani kurudi bongo hasa mitaa aliyokulia ila havutiwi tena
Nimegundua
Nchi nyingi ambazo wananchi wake wanazikimbia zina mazingira magumu ya kuishi
Nitaongelea hapa Tanzania kwetu
Tunaweza kukubaliana kwamba nchi hii ni ngumu na haivutii kuishi, labda uwe na kiwango fulani cha maisha la sivyo ni shida sana
Umewahi kwenda kwenye hospitali za umma? Msongamano mazingira yasiyo rafikiI mean uchafu umeshuhudia?
Usafiri wa umma daladala alooo!
Watu wanajazwa kuliko hata uwezo wa daladala
Humo ndani ni kukanyagana
Mtu anaenda kazini alfajiri kuwahi foleni anarudi anadandia gari kama vile nyani wanavyodandia miti unapanda daladala unaogopa kugusa hata lile bomba mana lina majasho ya kila namna
Msongamano harufu za kila aina zisizovutia unaweza kupata depression
Masoko jamani! Masokoni ukienda huko kipindi cha mvua uvae gumboots, la sivyo unarudi kama umetoka kulima mpunga
Umewahi kwenda Soko la Mabibo kipindi cha mvua?
Machinga wamezagaa ma barabarani watembea kwa miguu unapishana na magari pkpk bajaji uso kwa uso vipaza sauti, sumu za mende, kunguni.
Yaani unatembea unahisi kuchanganyikiwa
Hayo ni machache kati ya yale mengine mengi
Hivi, muda huu unavutiwa na kuishi Tanzania?
Umezaliwa Tanzania 🇹🇿 na unatamani kuondoka?
Ni nini sababu yako?
ShesRise_1 ✋️
AlooooBongo nyoso japo watoto wa kombo wanaishi kama peponi
Japo naipenda nchi yangu na nitaishi maisha yangu yote hapa hapa ila usijidanganye kubadilisha mfumo mchafu uliopo sio rahisi.Binafsi zamani nilikuwa na mawazo kama yako.
Nilitamani kuhamia USA 🇺🇸 ila Nikaja kugundua every one was born for a reason, wewe kuzaliwa Africa kuna sababu, sababu nyingi na nzuri mno..
Sikufichi ukihamia nje, unaweza kuona raha mwanzoni ila trust me home is where the heart belongs.
Kama unaona Tz ni chafu do something to make it a better place.
Wacha kuwa delusional, be the change you wish to see in the world
😄 🤣 😂 😆Una lakini wewe 😅😅
Sasa maisha yanafaa nini bila kuwa na marafiki, ndugu na jamaa. Hapa mjini mnaweza kuwa na grp lenu la marafiki, mnachagua weekend moja kila mwezi mnakaa pamoja, kula na kunywa pamoja, kuongea ujinga na mengine yote, mkimaliza ukoenda home akili iko refreshed kama mtoto(nasema hivi coz nina grp la watu kumi, familia tano), tukikutana unatamani dunia isimame kwa mda coz mnafurahi hadi basi.Uko sahihi kwa mtazamo huo, ikiwa kipaumbele chako cha juu zaidi kuliko vingine ni maisha ya ujamaa na socialization za undugu na urafiki zaidi kuliko miundombinu bora, uhuru binafsi, utawala bora, wingi wa fursa, teknolojia, innovations, ufanisi, meritocracy na mambo mengi ya aina hiyo yaliyo zaidi na yanayowezekana zaidi kwa sasa jamii za Magharibi, Japan, Singapore na Korea Kusini basi hakika bongo ni sehemu nzuri.
Okay 👍Sasa unasubiri nini, nyie ndo mnakuja kujitoa muhanga ndugu zenu ili tu mkimbile nje..
👍Binafsi zamani nilikuwa na mawazo kama yako.
Nilitamani kuhamia USA 🇺🇸 ila Nikaja kugundua every one was born for a reason, wewe kuzaliwa Africa kuna sababu, sababu nyingi na nzuri mno..
Sikufichi ukihamia nje, unaweza kuona raha mwanzoni ila trust me home is where the heart belongs.
Kama unaona Tz ni chafu do something to make it a better place.
Wacha kuwa delusional, be the change you wish to see in the world
Hakuna kilichotokea zaidi ya wazazi wako walifanya meeting huku mkuu😅Mtu hawezi kujivunia sehemu ambayo anaona haimpi thamani na wala haimsaidii kusonga mbele. So far vijana wengi wana mtazamo huo, hata hivyo kila taifa sahivi ni jau. Ni mataifa machache yametulia. Kuna wakati huwa najiuliza nini kilitokea nikazaliwa huku 🤗
Late Ali Mufuruki alisema unaweza kuwa na mamilioni lakini ukapata ajali hapo Msata ukafa kwa kukosa huduma ya kwanza. Kama huna pesa unaweza ukafikiri ukiwa na pesa ndio kila kitu.Bongo ni kuzuri ila uwe na pesa
Linachapa dada ake uwiiii 😅😄 🤣 😂 😆
Wewe hili jua la kazi na utu tusonge mbele bila kazi halikupigi eeenh???