Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

Yeah ndio maana wapo watu vijijini hamna hata umeme wana furaha kuliko baadhi ya watu Masaki. Lakini bado huko kijijini na mazingira yake ni sehemu ya hovyo tu na unaweza kung'atwa na nyoka ukafa kwa kukosa dawa ya 15000 wakati una 100m.
Mkuu,
Nilienda kijiji kimoja huko Dodoma, wakati naenda nikakutana na panda wanapeleka mama mjamzito kujifungua, niliumia sana.

Kiukweli bongo ni basi tu.
 
Mkuu, mwisho wa siku ni yule anayeishi pale, je ana furaha au ana enjoy.

Mimi nadhani kila mtu anajua nini kinachompa furaha, wapo watu wanakaa Masaki wanaacha nyumba zao wanaenda kuishi na Mchepuko Tandale
Ni kwa sababu hawawezi kuileta michepuko yao Masaki, japo ni kweli pia kuna baadhi ya watu wanapendelea zaidi kuishi mazingira ya hovyo ya msongamano, kelele, huduma mbovu, uchafu, uswahili n.k
 
Nimefuatilia comment zako tangu huko juu, lakini sielewi unachokitetea mkuu.

Unatetea miundombinu mibovu? Huduma mbovu hospitalini, mashuleni au nini hasa?
Nasema hivi, mimi napenda kuishi Tanzania, Bongo siyo bahati mbaya.

Ubovu wa miundombinu, ubaya wa huduma hospitalini na mashuleni siyo issue kwangu.

Hizo ni changamoto kama changamoto nyingine zilizopo sehemu nyingine

Mpaka hapo umeelewa?
 
Nasema hivi, mimi napenda kuishi Tanzania, Bongo siyo bahati mbaya.

Ubovu wa miundombinu, ubaya wa huduma hospitalini na mashuleni siyo issue kwangu.

Hizo ni changamoto kama changamoto nyingine zilizopo sehemu nyingine

Mpaka hapo umeelewa?
Nimeelewa kwamba unajifariji kwenye
Hamna nimevutiwa na hilo
 
Nimeongelea wabongo kwa ujumla, lakini inawezekana wewe ni outlier, ngoja nisikuchukulie poa. Tunakuombea uingie Toronto, New York, LA, Paris au London utupe mrejesho wa high paced life ya huko ukiwa umetokea jamii slow slow 😁.
Nitakuaje Yoda 😅😅
 
Tulikua na msemo wetu mabaharia " Bora uzaliwe mbwa/paka ulaya utaishi vizuri kuliko hata kuzaliwa binadamu bongo". Bongo/Africa , mashida ni mengi sana hata ukiwa na pesa ni bure tu. Ndio maana watu wenye pesa zao na marais uwa wanahakikisha wananunua mijumba na kuweka pesa zao ulaya na marekani na wakitaka kuenjoy maisha wanaenda huko. Baada ya wazungu kuwabana siku hizi wananunua mijumba Dubai kwa ajili ya kukimbia mashida ya Africa.
 
Back
Top Bottom