FUNGUAMDOMO
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 34,269
- 51,992
Hamia Burundi mzee.Kwa kweli nikipata upenyo mie huyooo nasepa nisiwe mnafiki aisee
Bwana mwgulu alishatoa maagizo
Hamia Burundi mzee.Kwa kweli nikipata upenyo mie huyooo nasepa nisiwe mnafiki aisee
Wapi ambapo ni pazuri bila pesa ?Bongo ni kuzuri ila uwe na pesa
Sure thingB ukiwa na pesa Tanzania utaishi kama mfalme
Paaingekuwa na Watz wanaokwenda Ulaya na Marekani na kisha kurudi tena Tanzania kuendelea na maisha yao.Ukitoka na kuona nchi nyingine zilivyo na mifumo yao ilivyo, hutoipenda tena hii bongo yenye maisha ya kuunga unga.
Shukran sana mkuu kama majibu yangu hajakurishisha ni kama mimi pia sijaridhishwa na maoni yako ni kama hatujaridhishanaMajibu Yako hayajaniridhisha Bado.
Niambie ni mambo mangapi nyumbani kwenu hayapo sawa??? Je! Uliona solution ni kukimbia kwenu??? Kuhama ukoo??? Au kujiita jina la kitajiri???
Ukinijibu hapa angalau nitakuelewa.
Mimi Huwa siendi kwenye masoko machafu, alafu pia Huwa nawashawishi na watu wengine wasiende hiyo sehemu. Nakushauri tumia kalamu kufanya hivyo.
Naamini ujumbe wako utafika.
SawaHaya yapo karibia kwenye miji yote mikubwa duniani.
Tembea uone.
Wewe una degree? Unasubiri kazi za Public Service Recruitment Secretariat??Au sio huihui
Kwani kwa hapa Tanzania kama huna elimu unaweza kufanya kazi kwa makaratasi?
Labda uwe CCM 🤣🤣
Siku hizi kuna bodaboda wenye degree we huoni tatizo hapo?
Hakuna anaetetea ujinga, lakini ni lazima tukubali kwamba nchi yetu Kuna vitu inafeli na inakwama lakini Je! Kwa kuwa nchi yetu inakwama ndio tuikimbie???Hoja hujibiwa kwa hoja hakuna anaependa wepesi
Hakuna watoto hapa baadhi yetu kusema tunatamani kwenda njee ya Tanzania hakuna aliesema anaenda kuokota hela
Acheni kutetea ujinga
Hapana mkuu, siwezi kubaki na majibu yangu yanaweza kuwa siyo sahihi.Shukran sana mkuu kama majibu yangu hajakurishisha ni kama mimi pia sijaridhishwa na maoni yako ni kama hatujaridhishana
Basi kila mtu abaki na mtazamo wake asante sana kwa maoni yako na karibu tena
Mie sina degree vip wewe unayo?Wewe una degree? Unasubiri kazi za Public Service Recruitment Secretariat??
Mkuu situliiHakuna anaetetea ujinga, lakini ni lazima tukubali kwamba nchi yetu Kuna vitu inafeli na inakwama lakini Je! Kwa kuwa nchi yetu inakwama ndio tuikimbie???
Hakuna solution kwenye kukimbia tatizo, dawa yake ni kukabiliana nalo.
Tulia mkuu baki hapa nchini analyse hayo matatizo and come up with solution.
Naweza kufanya yote hayoHapana mkuu, siwezi kubaki na majibu yangu yanaweza kuwa siyo sahihi.
Naomba unijibu wewe umeshakimbia kwenu kwasababu ya matatizo yaliyopo??? Au ulibadili JINA la ukoo kwasababu ukoo wenu unachangamoto??? Au unaweza ukakipa JINA la kitajiri ili kuficha umaskini wa nyumbani kwenu???
Mkuu am not in that league.Kila mtu anapenda wepesi unadhani maviongozi yenu yasingependa wepesi mbona nchi ingekua mbali sana hii, jidanganye tu utakufa waje watoto wako, vitukuu hata vilembwe bado watalikuta hili li nchi lako liko hivyo hivyo sioni likiendelea kutoka hapo. Acha watu waondoke wakapambanie familia zao hio nchi bila kua kwenye circlr ya ma ccm, jijue utakufa maskini na watoto watarithi kuendesha boda boda.
Afrika nitajiri ina rasilimali za kutosha sema tuna viongozi wabovu na wenye tamaa
ndio maana wazungu wakafanya afrika colon lao kwaajili ya kuchota mali na kiwekeza kwao
tungekuwa na viongozi bora kama gadafi sidhani kama tungetamani kuzaliwa nje ya afrika
Mkono mtupu haulambwi mkuu, nipo kwenye mchakato mwakani nichonge barabara ya kama km9 ili niweze kufika shambani kwangu muda wote.1. Mkuu unataka tutoe pesa zetu mfukoni tuchonge barabara?
Kodi tunazolipa zinakwenda wapi? Kuna mantiki gani ya kuongeza tozo kila uchao?
2. Umesema usafi ni bonge la fursa, ila shida ni mtaji
Sasa hapo huoni kwamba tayari kukosa mtaji kunaweza kuwa ni matokeo ya mazingira magumu ya kiuchumi?
Kwa nini watu wengi wakose mitaji? Hilo si suala la uchumi?
Au pengine kuna wenye mitaji lakini wanabanwa, huoni hapo kuna tatizo? Tutapenda vipi kuishi sehemu ya namna hii?
Okay, Sasa nakuomba ukiwepo hapa nnchini bhasi tuungane kutafuta solution ya matatizo yetu.3. Hatuwezi kukimbia wote kwenda ughaibuni
Ughaibuni si kwa kila mtu
Ndiyo maana bado tupo hapa na tunaendelea kulalamika licha ya kutofurahishwa na mazingira tuliyopo period!
Mkuu ardhi ni rasilimali, sio lazima itumike hapo hapo. Itatumika wakati sahihi ukifika.4. Kwa mfano wa shamba lenu, lakini huu mfano hauakisi uhalisia hata kidogo
Kwa nini milioni 400 ikae tu bila kuzungushwa?
Kama shamba halina matumizi yanayoingiza pesa.si lingekuwa limeuzwa ili hiyo hela izae nyingine?
Mkuu labda hujazunguka hii nchi.5. Uongoooo ukweli ni kwamba
Viongozi wetu wanauza rasilimali kwa sababu ya ufisadi hakuna kingine Mapori na maeneo mengine wayagawe watu waone kama hawatayatumia kuzalisha na kujiletea maendeleo
Sasa fursa zimejaa tele, tukitaka kuitoa CCM bhasi ni.lazima wote tuamue kuutafuta utajiri.6. Upo sahihi CCM inaogopa matajiri
Na ndiyo maana haitaki kuona Mtanzania yeyote akipiga hatua
Wanajua ni rahisi kwao kutawala na kuendesha watu maskini
Ndiyo maana hakuna juhudi za pamoja za kuhakikisha Watanzania wengi wanapiga hatua na walau wanaishi kwa kipato cha kati
Ni rahisi kumuongoza mtu mwenye njaa kwa sababu hata uwezo wake wa kufikiri na kufanya maamuzi unaweza kuathirika
CCM wanalijua hilo
Wanatembea beat njaa haimpendezi mtu
Wengi wa wanaotaka kukimbia huwa hawana uwezo wa kutatua changamoto ndio maana wanachagua shortcut ya kukimbia.Tulia mkuu baki hapa nchini analyse hayo matatizo and come up with solution.
Mkuu umesema kwamba watu wenye akili timamu hawasubiri kufanyiwa vitu vyenye maslahi kwaoMkono mtupu haulambwi mkuu, nipo kwenye mchakato mwakani nichonge barabara ya kama km9 ili niweze kufika shambani kwangu muda wote.
Wenye akili timamu hawasubiri kufanyiwa vitu vyenye maslahi kwao.
Hilo shamba lipo jirani kabisa na mradi mkubwa wa serikali, Yaani kama angekuwa Magufuli nafikiri lami ingepita shambani kwangu kabisa lakini ndio hivyo siwezi kusubiri serikali.
Kwa hiyo umekariri mpaka Leo lack of capital???
Toka NDANI ya Hilo box umejifungia, onesha uwezo wako alafu utaona jinsi fedha zinavyokufuata.
Binafsi capital kwangu sio shida kabisa ila shida ni Mimi, Mimi sipendi kushika hela za watu, sipendi niulizwe maswali Kila muda, hivyo niliamua kutochukua fedha ya mtu yeyote.
Lakini kama unaweza kutolea maelezo na kutunza fedha za watu, nakwambia onesha kitu gani unaweza alafu utaona jinsi Hela zinavyokuja kwako.
Shortly I can say this. Hii user ID ni heshima kwa Mzee wangu mmoja alishatangulia mbele za Haki, yeye alisoma Urusi alishanipa connection za kwenda Urusi nyingi lakini mimi ndio nilizingua, mwishoni aliamua kuniamini nikiwa na miaka 24 alitaka kunikabidhi kampuni yake ya ujenzi ikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 300 tena ikiwa imeshika tenda ya zaidi ya milioni 500 bahati mbaya sana alifariki kwa ajali.
Always R.I.P F.J.T uliniamini zaidi hata ya mzazi wangu.
Okay, Sasa nakuomba ukiwepo hapa nnchini bhasi tuungane kutafuta solution ya matatizo yetu.
Usicomplain na unapoliona tatizo andika kwa namna ya kuliaddress tatizo na mwisho toa njia mbadala au ushauri wa namna ungeona inafaa lifanyike.
Mkuu ardhi ni rasilimali, sio lazima itumike hapo hapo. Itatumika wakati sahihi ukifika.
Wewe kama unaona hiyo fedha ni nyingi bhasi uelewe kwamba hata sio nyingi. Shamba la ekari 400 haliwezi kuuzwa kizembe hivyo eti kwasababu tuu halitembelewi.
Mkuu labda hujazunguka hii nchi.
Kuna vijiji nimeenda Mimi ardhi unapewa Bure kabisa, ukienda mkoa wa Rukwa Kuna vijiji ekari inauzwa kwa elfu 20.
Kuna wasukuma wanajikatia maeneo huko vijijini ni hatari. Nimeshuhudia mtu binafsi anamiliki ekari 3000 na zote amepanda miti tena serikali ndio ilimpa Mbegu Bure kabisa.
Nimeshuhudia msukuma mmoja anamiliki ekari 200 na aliuza ekari 60 kwa milioni 60.
Sasa kwa mifano hiyo shida hapo ni viongozi wetu au shida ni akili zetu za kupenda kukaa mijini na kulalamika???
UNATAKA serikali ikugawie ardhi,Je! Unaweza kuilipia hiyo ardhi??? Hizo Kodi tunakatwa kwenye MITA imekua ni manung'uniko je kuilipia ardhi mtaweza???
Sasa fursa zimejaa tele, tukitaka kuitoa CCM bhasi ni.lazima wote tuamue kuutafuta utajiri.
Kuna siku nilishawahi kuandika humu tena ni kwenye Uzi wako nikasema kuliko kupiga kelele na kuandamana ni Bora tuingie mashambani, migodini na kwenye Kila aina ya fursa tukazifanyie kazi na endapo Kuna kiongozi atakuja kutusumbua huku bhasi huyo awe ni halali yetu, Yaani wewe kufa nae tuu kama alivyofanya ndugu yangu wa maana sana MOHAMED MWAMWINDI
Ni kweli na upo sahihi kabisa.Wengi wa wanaotaka kukimbia huwa hawana uwezo wa kutatua changamoto ndio maana wanachagua shortcut ya kukimbia.
Mkuu umesema kwamba watu wenye akili timamu hawasubiri kufanyiwa vitu vyenye maslahi kwao
Unatumia maneno ya dharau then siwezi kuendelea na mjadala kwa mtindo huu
Kitu nimegundua ni kama hujui wajibu wa serikali kwa wana nchi wake
Au kama unajua umeamua kupuuza
Asante kwa maoni nimeshaona hatutafika tamati narejea maneno yangu ya awali kwamba kila mtu abaki na mtazamo wake
Ndio hua nakimbia mjadala kama naona ni mjadala usio na mwishoSio kweli unless unataka kukimbia mjadala.
Ni sahihi kabisa kusema kama UNAAKILI timamu huwezi kusubiri serikali ikufanyie jambo lenye maslahi kwako.
Mfano umepata eneo Lina dhahabu huko porini utasubiri serikali ikupelekee barabara???
Mfano umepata soko la uhakika la parachichi utasubiri serikali ipeleke miundombinu shambani kwako ndio ukafanye kilimo???
Sasa nasema kwamba ikiwa utasubiri serikali ifanye hayo kwa maslahi Yako bhasi wewe utakua haupo timamu kwa mtazamo wangu.
Umeuliza kuhusu wajibu wa serikali, wajibu wa serikali ni kukusanya Kodi na kufanya maendeleo kwa wananchi kupitia Kodi zao. Sasa je! Kama serikali inachelewesha maendeleo wewe utaendelea kusubiri???
Kuna comment Yako Moja nimeona unalaumu kwamba serikali haitoi ajira ndio maana watu wanadegree lakini ni bodaboda.
Naomba nikuulize swali hivi mtu anakwenda shule ili aajiriwe au anakwenda shule ili kujifunza mbinu za kupambana na hali ya maisha???
Hivi elimu ndio njia ya kuondoa umaskini au ni nyenzo ya kuondoa umaskini???
Naomba unijibu haya maswali kwanza.