FUNGUAMDOMO
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 34,269
- 51,992
Upo tayari kuitwa chawa au muuaji?Sio kweli unless unataka kukimbia mjadala.
Ni sahihi kabisa kusema kama UNAAKILI timamu huwezi kusubiri serikali ikufanyie jambo lenye maslahi kwako.
Mfano umepata eneo Lina dhahabu huko porini utasubiri serikali ikupelekee barabara???
Mfano umepata soko la uhakika la parachichi utasubiri serikali ipeleke miundombinu shambani kwako ndio ukafanye kilimo???
Sasa nasema kwamba ikiwa utasubiri serikali ifanye hayo kwa maslahi Yako bhasi wewe utakua haupo timamu kwa mtazamo wangu.
Umeuliza kuhusu wajibu wa serikali, wajibu wa serikali ni kukusanya Kodi na kufanya maendeleo kwa wananchi kupitia Kodi zao. Sasa je! Kama serikali inachelewesha maendeleo wewe utaendelea kusubiri???
Kuna comment Yako Moja nimeona unalaumu kwamba serikali haitoi ajira ndio maana watu wanadegree lakini ni bodaboda.
Naomba nikuulize swali hivi mtu anakwenda shule ili aajiriwe au anakwenda shule ili kujifunza mbinu za kupambana na hali ya maisha???
Hivi elimu ndio njia ya kuondoa umaskini au ni nyenzo ya kuondoa umaskini???
Naomba unijibu haya maswali kwanza.
Humu jf usipoiponda serikali unageuka adui.