Ni kweli, ICC wako nchini

Ni kweli, ICC wako nchini

Ishu ya Tesha labda huijui kwa undan.

Zile vurugu zingeenda siku ya pili. Hii nchi ingetawaliwa na Jeshi.
Jesh ndio maana siku ya 1 lilikaa kimya. Likisubiri kinuke zaidi.

Jeshini kuna mpasuko.
Tenda zile na Ulaji ambao Magu alikuwa anawapa kwa kupitia Miradi mbalimbali ya serikali sikuhizi hamna .wana njaa kali. Na weng wanamchukia Mama.
Kama ulikuwa hujui basi ndio ujue hilo.

Cha pili. NRNE imepokelewa kwa maana tofauti.
Lissu hakuwa na maana watu wafanye fujo.
Mm mwenyewe sikutoka kupiga kura na najua weng hawakutoka.

NRNE ni kususia uchaguzi maana hata tungeenda kura zetu zisingethaminiwa.
Ila sio kufanya vurugu.
..ndio madhara ya kupokea taarifa za kijiweni km ndio taarifa rasmi, ukizoea kula takataka huwezi tena kuona tofauti ya chakula safi na kichafu.
 
Na si jeshini tu kaka hata Wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama wanamwitikia ndio mdomoni Ila kimya kimya wana lamumiana hasa CDF kuwekwa mtu kati siku ya Uchaguzi na kundi la wahuni
Ina wezekana CDF kuwekwa chini ya usngalizi na twiss ?
 
Exactly. Mazingira wanayoyaset.

Kama ICC wakifungua mashtaka.
Basi Hii kesi Samia wala vyombo vyake vya Usalama hawaguswi.

Kuna kichaka wanajifichia nazo.
Ili kuwa na uhalifu dhidi ya Binadamu kwanza inabidi uue Raia wasio na hatia kwa makusudi.

Ila Vyombo vya Dola wanaweza kurespond kuwa wamepiga risasi watu ambao walikuwa wanachoma moto sheli, na kuharibu mali za Umma na kuwa kuna jaribio la mapinduzi.
Kwa respond hii. Hakuna kesi icc wanapewa hao mabwela.

Ile ya Kenya. Pamoja na tume kutoa report kuwa watu 1,100+ wameuliwa. Tena nusu wameuliwa na Polisi.
Ila kesi ilifutwa kwa kukosa ushahidi na Raisi hakuguswa kabisa.
Kuna sheria yyte kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa 🇹🇿 inayoruhusu kuua watu wasio na siraha
 
Aliyetoa order shoot to Kill ni IGP.

Achana na chanzo.
Tuongelee namna tukio lilivyofanyika.

Polisi walikuwa wanapiga risas hata watu walioko nyumban.
Ila ushahidi wake ili shauri lifunguliwe kuna ugumu.

Waandamanaji wangekuwa wako barabarani na polisi wakawafyatulia Risasi na wakawaua. Hii ingekuwa kesi ya kujibu.

Polisi wao watasema walikuwa wanapira risasi Raia ambao wamechoma miundo mbinu ya umma. Na kufanya fujo.
Hii inakuwaje Kesi ya Kujibu?.
Wakat wao walikuwa wanafanya wajibu wao wa kulinda mali za nchi?.
Sijui umeelewa ugumu wa hii kesi ulivyo?.

Narudia tena. ICC Inashtak watu waliofanya uhalifu dhidi ya binadamu.
Hii ya kuua watu wanaosadikika kuharibu miundo mbinu haiwez kuwatia hatiani Mapolisi wala Kiongozi wao.
Aliyetoa order Yuko Hapa niliwaonya watu wakapuuza

 
Kuna sheria yyte kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa 🇹🇿 inayoruhusu kuua watu wasio na siraha
Najua nguvu inayotumika lazima ilingane na tishio lililopo.
Na Sheria inakataza kusababisha kifo cha mtu isipokuwa tu pale ambapo ni lazima kabisa ili kulinda maisha ya wengine au kuzuia jeraha baya sana.

Nishakiri huko juu kuwa Polisi wamezingua. Hakukuwa na haja ya kupiga risasi za moto.

lakini pia. Kwasababu wao ndio walikuwa eneo la tukio wanaweza kujitetea kuwa wafanya fujo walikuwa na nia mbaya zaid na wasingewazuia kwa namna ile madhara yangekuwa makubwa.
 
Aliyetoa order Yuko Hapa niliwaonya watu wakapuuza


Dah. Kumbe na hili uliliona na ukatoa onyo mapema.
Salute kwako kaka.
 
Kuna jambo ambalo nchi za ulimwengu wa tatu linasahau

Hawa ICC wanaweza wasitusaidie chochote

Nowadays imekuwa jokes

Ukiangalia mauaji yaliyofanyika 29/10/2025 kama alivyo comment Nyani Ngabu sehemu kwamba kwa Ushahidi uliowazi vile wao wanachelewa nini kufanya maamuzi

Tunajua ICC uchukua muda kufanya uchunguzi kwa kina na inaweza tumia hata Miaka 3 au 5 Mpaka mtu anatiwa hatian, suala la Kijiuliza hapa je kwanini waje kimya kimya ?

Kwa maslahi ya nani ? Kwanini isiwekwe wazi? (uhakika ni kweli hata IGP kapata wito kuongea na wajumbe Ila wamezungumza nini ndo bado tuna dig kuona)

Kuna elimu watanzania mnabidi muipate.
ICC haipo kwa ajili ya haki, ipo kwa maslahi ya Marekani na washirika wake. Kama tungekuwa very independent na hatuwategemei kwa baadhi ya mambo, ishu ingeshaitwa kati

Hii nchi bado ni koloni la marekani na washirika wake km ilivyo nchi nyingi za Africa. Wanatumia makosa ya Samia km leverage ya kuchota mali Tanzania,

Hapo ndo Maana Hana hata uwoga wowote ule juu ya ICC

pamoja alokuwaga msaidizi kumu implicate na kutoa maushahidi lakin bado wana sita kuchukua maamuzi, hata kesi kutajwa au kuorodheshwa bado,

Tunajua walipokea kesi Yenye page 84 kwa ajili ya Tanzania Ila sasa ni kama hawana muda na kesi hii


Samia ni muoga wa watanzania na CCM zaidi ya ICC kama hamjajua hili ,

ICC anajua tu pale kwanza yanaweza kutengenezwa mazingira akapewa mtu Tofauti kesi (Reffer Kenya 2007, Kibaki hakuguswa Ila walopelekwa ni Rutto na Kenyatta ambao wala hawakuwa madarakani)

Hivo ICC ya sasa hivi imejaa siasa sana na meno yake yamefubaa



Cha kufanya Watanzania bora kuja na mbinu ambayo ntaiweka Baadae ambayo Samia anaiogopa kama ukoma,

Kujitoa muhanga ndo soln now

Kuishia kushktaki kwa UsA na Ulaya ambazo Baadae tunaona zinaendelea kushirikiana na Tanzania ya Uongozi ule ule kutimiza miradi yao na plans ni udwanzi

IGP kakutana na nani na wapi ? Kwa Usalama wa JF siandiki hapa

Britanicca
We nae bogus tu, ICC huiacha nchi husika ifanye uchunguzi,isipofanya wao huingia mzigoni,hiyo huchukua miaka,wewe miezi 13 unataka watu wawajibishwe wakati tz yenyewe inafanya uchunguzi
 
Kuna elimu watanzania mnabidi muipate.
ICC haipo kwa ajili ya haki, ipo kwa maslahi ya Marekani na washirika wake. Kama tungekuwa very independent na hatuwategemei kwa baadhi ya mambo, ishu ingeshaitwa kati
Ina maana hufahamu Marekani haijawahi kuwa mwanachama wa ICC.

Isitoshe Utawala wa Trump unaendesha kampeni kubwa za kuifuta hiyo Mahakama.

Sasa hayo maslahi ya Marekani yanalindwaje na ICC,Wakati hata majaji na waendesha mashtaka wa ICC wamewekewa vikwazo na Marekani.
 
Nilichelewa sana kumuelewa Hamza , ila baada ya October 29 nikagundua Hamza hakuwa na makosa watu walimlazimisha kufika hatua aliyofika pengine wakaja kuzaliwa akina Hamza wengine baadae.
 
..juzi mtoto Angel amefariki chanzo ni jinai iliyotendeka oct. 2025 chini ya samia, kuna maelfu ya case km ya mtoto Angel..ushahidi upo, sasa unaulizaje jinai ya samia km huijui..kutochukuliwa hatua kwa jinai ya ruto hakufanyi samia asichukuliwe hatua km alitenda jinai, makosa yanatofautiana, muda, madhara, chanzo nk jiulize maandamano chanzo chake ni nini? hao unaita wachochezi wanachochea nini, wewe unateka watu, unaua, unahonga media zisiripoti mauwaji na ukandamizaji unaofanya, unaiba mali za umma yote haya unataka watu wasiseme? wakisema unawaita wachochezi..WHY? dola ndio yenye silaha iliua watu, mambo ya uchochezi hayana base, kupigia kelele maovu na kuambia watu kukataa uovu kwa kuandamana si uchochezi..maandamano ni haki ya raia kikatiba, huwezi kuita maandamano ya kukataa uovu

Yanapotokea machafuko tambua jambo moja, kuna kitu kinaitwa kukutwa katikati ya ambush au kuwepo kwenye line of fire, siyo huyo binti Tu wapo wengi waliingia kwenye ambush wakati vyombo vinajaribu kurudisha utulivu Kwa maslahi ya wengi ambao hata hawajui chochote na wala hawakuwa sehemu ya hizo harakati...

Nimwambia hapo juu, hao ICC kimedani wanaweza kuja kufanya uchunguzi na viongozi wenu akina Mange, Maria nk wakajaa nyavuni, (hujui yaliyokuwa nyuma ya pazia),

Unazungumzia waandamaji waliotoka hapo ubungo karibu na kanisa la Gwaji boy tarehe 29 wakafika daraja la kijazi na kujigawa wengine wakienda mwenge na wengine wakichukua uelekeo wa buguruni, wale wabuguruni wakisema live wanakwenda Segerea, airport, bandarini kutia moto storage tanks nk...hawa ndio unataka vyombo vya usalama viwasindikize na wale wengine wakielekea mbweni kupitia goba njiani wakitia moto vituo vya mafuta ulitaka Askari wasindize hawa watu au sio???..

Kabla ya tarehe 29 hukumsikia Mange, Kapt Tesha, Maria wakiimba kufanya mapinduzi??? Unajua kazi ya jeshi na vyombo vya usalama kazi yao kunapokuwa na tishio la mapinduzi?.

Unajua kwamba kazi ya vyombo vya usalama ni pamoja na kulinda maslahi ya wengi na sio wanaharakati, wanasiasa na wafuasi wa CDM???..
Unafahamu kama maandamano Kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania huwa yanataratibu zake na lazima kuwe na mawasiliano na vyombo vya usalama??? Unafikiri kwanini yale maandamano yalifanyika tarehe 29 ambayo kisheria ilikuwa ni siku ya uchaguzi??

Sauti ya Mtanzania,
Safarini Khost - Afghanistan.
 
Kuna elimu watanzania mnabidi muipate.
ICC haipo kwa ajili ya haki, ipo kwa maslahi ya Marekani na washirika wake. Kama tungekuwa very independent na hatuwategemei kwa baadhi ya mambo, ishu ingeshaitwa kati
Halafu unasema "kuna elimu watanzania mnabidi muipate", elimu ambayo imekuwezesha wewe kutojuwa kwamba huyo Marekani wala hata siyo mwanachama wa mahakama hiyo, na ndiye mkereketwa mkubwa wa kutaka ifutwe! Halafu unakuja hapa na kujigamba watu kutokuwa na elimu. Unataka wawe na elimu ya namna gani.

Wachochezi wa hiyo mahakama ya kipumbavu ni hao wazungu wa Ulaya, siyo Marekani.

Na hii haina maana kwamba Marekani ni watetezi wa haki zaidi ya kutetea maslahi yao wenyewe.
 
Ina maana hufahamu Marekani haijawahi kuwa mwanachama wa ICC.

Isitoshe Utawala wa Trump unaendesha kampeni kubwa za kuifuta hiyo Mahakama.

Sasa hayo maslahi ya Marekani yanalindwaje na ICC,Wakati hata majaji na waendesha mashtaka wa ICC wamewekewa vikwazo na Marekani.
Hawatofanikiwa, Trump sidhani kama anaendelea muhula mwingine, Netanyahu mwenyewe yupo hoi...
 
Yanapotokea machafuko tambua jambo moja, kuna kitu kinaitwa kukutwa katikati ya ambush au kuwepo kwenye line of fire, siyo huyo binti Tu wapo wengi waliingia kwenye ambush wakati vyombo vinajaribu kurudisha utulivu Kwa maslahi ya wengi ambao hata hawajui chochote na wala hawakuwa sehemu ya hizo harakati...

Nimwambia hapo juu, hao ICC kimedani wanaweza kuja kufanya uchunguzi na viongozi wenu akina Mange, Maria nk wakajaa nyavuni, (hujui yaliyokuwa nyuma ya pazia),

Unazungumzia waandamaji waliotoka hapo ubungo karibu na kanisa la Gwaji boy tarehe 29 wakafika daraja la kijazi na kujigawa wengine wakienda mwenge na wengine wakichukua uelekeo wa buguruni, wale wabuguruni wakisema live wanakwenda Segerea, airport, bandarini kutia moto storage tanks nk...hawa ndio unataka vyombo vya usalama viwasindikize na wale wengine wakielekea mbweni kupitia goba njiani wakitia moto vituo vya mafuta ulitaka Askari wasindize hawa watu au sio???..

Kabla ya tarehe 29 hukumsikia Mange, Kapt Tesha, Maria wakiimba kufanya mapinduzi??? Unajua kazi ya jeshi na vyombo vya usalama kazi yao kunapokuwa na tishio la mapinduzi?.

Unajua kwamba kazi ya vyombo vya usalama ni pamoja na kulinda maslahi ya wengi na sio wanaharakati, wanasiasa na wafuasi wa CDM???..
Unafahamu kama maandamano Kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania huwa yanataratibu zake na lazima kuwe na mawasiliano na vyombo vya usalama??? Unafikiri kwanini yale maandamano yalifanyika tarehe 29 ambayo kisheria ilikuwa ni siku ya uchaguzi??

Sauti ya Mtanzania,
Safarini Khost - Afghanistan.
Matukio ya utekaji yalikithiri.. mbaya zaidi serikali ilikuwa kimya..

2025 kulikuwa na matukio mengi sana ya utekaji na mauaji ya kinyama...

Hii JF ilifungiwa muda mrefu kisa tu watu kutoa maoni yao, kila anayesema anatafutwa...

Kupora uchaguzi, kukamata wapinzani, polisi kutumia mabavu...

Ufisadi ndipo usiseme... Gwajima alizungumza kuhusu suala la utekaji kukithiri tayari akaanza kutafutwa akamatwe badala ya watawala kufanyia kazi wao wakaona wamshikishe adabu na kufunga kanisa lake.... ujinga ulioje? Maana yake serikali ilijidhihirisha inatetea utekaji na mauaji...

Wananchi wakatoka kwa hasira kuona hawasikilizwi, watu wamepiga kelele sana kuhusu matendo ovu ya watawala lakini badala yake ndipo kama wakawa wanazidisha matendo ya kishetani kwa kiburi, dharau na ubabe...

Unategemea raia wangefanya nini? Wangeipongeza serikali?
 
Back
Top Bottom