TUTATOKAJE HAPA TULIPOFIKA?

TUTATOKAJE HAPA TULIPOFIKA?

Jeep wrangler

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
1,847
Reaction score
3,460
Tanzania ni nchi masikini lakini tangu kuasisiwa kwake imekuwa ni nchi bora kwa umoja na mshikamano.

Kwa umasikini wao siku zote wamekuwa wakishikamana kwa upendo.

Wakiombana chumvi hadi chakula kwa upendo mwingi.

Wameshirikiana kwenye misiba na sherehe

Dini zao hazikuwafanya wachukiane wala kubaguana.

Itikadi zao hazikufanikiwa kuwagawa wala kuwatenga.

Wamekuwa ni wema na wakarimu kwa wageni.

Walipokea wakimbizi kwa upendo wa dhati wa mioyo yao na kuwathamini.

Waliwapokea na kuwahifadhi wapigania Uhuru toka mataifa mbalimbali kwa mfano Afrika ya Kusini, Msumbiji nk.

Upendo huu umedumu miongo kadhaa, yaani watu ni masikini lakini wamejaa umoja na ushirukiano na furaha tele.

Miaka ya hivi karibuni, furaha, upendo na umoja wetu umeingia dosari kubwa sana.

Ushirikiano katika shida na raha umepungua na uliopo umekuwa wa mashaka.

Mbali na kutoshirikiana. Kumeingia wimbi la kushangilia misiba ya wengine.

Narudia, kumeingia kirusi cha kutakiana vifo, afapo mtu ni fura ha ya wengine.

Hiki ni kiwango cha juu sana cha upotofu, uharibifu na kuchukiana baina yetu.

Nani ametufikisha hapa?

Nini kimetokea?

Tutatokaje kwenye mkwamo na hali hii ya kutisha?

Nani hasa wa kulaumiwa?


Kila mtu ana majibu yake lakini jibu langu ni hili; ULAFI WA MADARAKA NA UFISADI ndio umetufikisha hapa.


1. Enzi za uongozi wa Mwl. Nyerere haya mambo hasi niliyoyataja hayakuwepo au yalikuwepo kwa kiwango kidogo sana.

2. Mwalimu Nyerere kama mfano hakuwahi kuwa mbinafsi, mlafi na fisadi, hii ilimsaidia kuwa jasiri kukemea walafi na mafisadi bila woga wala nafsi kumsuta.

3. Mwinyi, huyu aliongoza kama kaka mkubwa chini ya usimamizi wa baba yaani Mwl Nyerere, hivyo pamoja na madhaifu yake lakini kwa kiwango kikubwa alidhibitiwa sana ( japa wakubwa wanajua nisemalo)

3. Enzi ya Mkapa, hapa ndipo baadhi ya mmomonyoko wa mila na desturi za umoja na upendo wetu kama taifa ulianza kutikiswa kwa rushwa kubwa kubwa kutajwa, matabaka ya walicho nacho na wasicho nacho kuanza kujitokeza kwa kiwango cha juu san.

4. Enzi za JK, hapa sasa ndipo kuta zianza kuonyesha nyufu kubwa.
Likaanza kutumika hata neno geni na msamiati mpya (Unanijua mimi ni nani). Hii ilikuwa sasa ilikuwa ni level ya juu kabisa ya kupotoka kutoka kwenye misingi ya upendo, kuhurumiana na kuahirikiana.

Wenye watu wao kqenye kitu ninaitwa system ndio walianza kutesa na kuitafuna nchi kama mchwa mjane.

Wakazaliwa mafisadi makubwa makubwa na mazito mazito na yakapewa majina (Vigogo)
Hapo kuna nini tena!?

Uvundo huu ukawa mzito , na taratibu upendo na umoja vikaanza kuwa vya mashaka sio tu kwa raia bali hata kwa vigogo na vimiti wenyewe.

Katika awamu zingine nina haja ya kusema neno?

Nyie wenyewe si mnaona yanayoendelea?

Mnaiona level ya ulafi na rushwa, na ufisadi vikishamiri na kuvishwa suti za thamani?

Msinawaona wala rushwa walivyo majasiri kama simba?

Je hamuona wanavyogawana keki ya taifa kwa ngazi za koo zao na hata familia?

Je si mnaona kiasi ambacho hata damu ya mtu kumwagwa ni sawa na mtu kunawa mikono ili ale chakula?
Si ninyi wenyewe mnaona hata hoja tu ya maneno matupu inapigwa risasi kama vile mtu anaua mnyama tu?

Upuuzi huu, ufedhuli huu, umwamba huu wa kishamba na ulimbukeni umetufikisha pabaya mnoo.

Tumegeuka kituko kwa mataifa.

Tumeonekana watu wasio na akili wala utu kwa kiwango cha juu.

Ile heahima ya kukigamba na kujitambulisha " mimi ni Mtanzani" kwishaaa kabisa.

Ujitambiliahe kuwa Mtanzania utemewe mate? Uchekwe???

Kizuri au kibaya sasa tunaumia wote, wenye chama dola wanaumia yaani viongozi, vigogo kwasa wanaumia kwani raia wanawaombea vifo na wakifa nchi inafurahi...hii inawatase na wameanza kutoa milio..

Wanachamaw wao nao hawako salama wanakiona cha moto, wakihoji wanakiona cha moto, wanasifia mambo kinafiki lakini deep down wana mizigo mizito kama ya dhami.

Wapinzani, hwa wamegeuka mawindo na chakula cha waliopoka furaha ya nchi hii, wanauawa kama nzi mchana kweupe.

Wasio na vyama nao hawako salama.

Kwa ujimla hakuna mqenye furaha ya kqeli kwani kila mty hajui keaho yake ipoje.

Je hali hii itaendelea mpaka lini?


PAULO ANASEMA HIVI:
Warumi 13:12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia,

DAUDI NAYE ANENA HIVI:
Zaburi 30:5B . Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.

WATANZANIA WENZANGU
1. Tuna hali ngumu sana lakini ninawahakikishia hii biashara ya damu mwisho wake umekaribi

2. Nina uhakika hawa wanaofanya biashara za damu za wati muda si mrefu tutawajua kwa majina, kwa sasa wanafurahia ujira wa kumwaga damu lakini aibu yao inakuja

3. Wanaofashili biashara ya damu nao siku zao sio nnyingi sana tutawajua waziwazi.

4. Chuki, visasi na uonevu nao havitadumu .

Tuwe imara saa ya Tanzania mpya inakuja.

Saa ya nderemo na vifijo i karibu, tuingoje kwa saburi, tusife moja wala tudiruhusu mikono yetu kushiriki uovu wao.

Daudi aliwahi kusema;

Zaburi 73:3 Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.

Usifike wakkati ukaitamani furaha ya watu wabaya

Usifike wakati ukatamani laiti ungezaliiwa na kigogo au kiongozi flani mwenye pesa lakini muovu

TUISUBIRIE ASUBUHI YA FURAHA

TUISUBIRIE TANZANIA YA HAKI

TUISUBIRIE TANZANIA YA KUTUKUKA...HUKU NASI TUKIWEKA MCHANGO KATIKA KUIFANYA ITOKEE.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom