Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,167
- 11,757
Tatizo lako Field Marshall kwako wewe kila kitu ni black or white. Hii inakuzuia kuona shades of grey. Mtu aidha anamtetea Masha au anamshutumu kwa ufisadi. Mimi siko kote huko. Mimi sijawahi kudai kuwa Masha ni fisadi au la. Simjui, sijaona utendaji wake kwa hiyo sina haki ya kumhukumu. Wewe mwenzangu katika jitihada zako za kumkingia kifua ndiyo unaingiza vipimo kama umeneja wa amusement park marekani kama kipimo tosha cha kumfanya huyu awe kiongozi Tanzania. Hapo naona haututendei haki hata kama sisi ni nchi masikini! Ingekuwa hiyo ndiyo experience pekee aliyokuwa nayo Masha hata mimi ningepata wasiwasi na uweza wake! Katika juhudi zako hizo hizo unatoa madai ambayo si ya kweli kuhusu elimu marekani. Sasa kama Masha ndiye aliyekwambia kuwa alikataliwa kusoma sheria marekani kwa sababu yeye ni mgeni ingawa uwezo wa kipesa na kiakili alikuwa nao, hii nayo itatufanya sisi tusiomjua tuanze kumtilia shaka. Unasema aliombwa na World bank kufanya kazi akakataa. Hii nayo ninaitilia wasiwasi maana mpaka World Bank waku'head hunt' wewe ni mkali sana na hauwezi kwenda kukaabila mshahara kwenye ofisi ya Warioba. Sasa yote haya hakuyasema Masha bali ni wewe uliyetuletea. Ndiyo maana nilikushauri kuwa haya mambo personal yasiyo na maana katika mada usiyalete hapa. Hivi si kumtetea Masha dhidi ya shutuma za ufisadi ambazo wengine wamezileta. Nakubaliana nawe kuwa hakuna uthibitisho uliotolewa kuhusu shutuma hizo isipokuwa wa mazingira. Hatuwezi kumnyonga mtu kwa ushahidi kama huo ingawa mimi ni Tomasi inapokuja kwenye ushahidi wa kwenye mtandao. Naomba ujaribu kunielewa na si kuniweka mahali ambako sipo. Shukurani!