Msavila,
Usinitishe na maneno ya choooni mkuu, mimi ninamtetea Masha kuwa sio fisadi kwa sababu hapa sijaona ushahidi, kama unamjua Masha kuliko mimi na una ushahidi kuwa ni fisadi weka ushaidi wako hapa which is not an ishu hapa unless una lako jambo,
Yes nimesema ninamjua Masha, tena kwa karibu sana mkuu kuliko hata nilivyokwisha sema, na ninarudia kuwa baada ya kuzisoma kwa makini hizi post za hii topic nitaongea naye kwa kirefu sana, baaada ya huu mjadala kuisha,
Ngoja nirudie, nimeishi na Masha na wadogo zake pia John na Mugisa, akiwa Georgetown nimekwenda mara nyingi sana pale alipokuwa akiishi na mkuu wangu Joe Kusaga, mpaka alipomaliza na kurudi NY, na kufanya kazi Playland, kabla ya kurudi bongo kufanya kazi kwenye Warioba Law Firm, Oxygen, Kamati ya rais ya marekebisho ya katiba ya muungano, IMMA, ujumbe wa baraza la vijana ccm Mwanza, kugombea ubunge na kuwa waziri mdogo, mpaka waziri kamili, na kama ulikuwepo kule kwenye sherehe ya Mama migiro then uliona kuwa nilimualika pale na akaja, sasa usinipe lecters za kitoto, peleka hizo lectures zako kwenye kumtoa mwali sio hapa, toka nimfahamu sijawahi kuona anything cha kumfanya awe fisadi au mtu yoyote kwenye familia yake ndio maana ninamtetea kwa nguvu zangu zote, na ninamuamini kuwa ni kiongozi safi na proud to be my friend, na ninaamini kuwa atakuwa na great political future,
Now take it or leave it, lakini usiniletee ishu za nje ya mada, weka ushahidi kuwa Masha ni fisadi, kama huna endelea na mazungumzo baada ya habari, off course I love it kwamba mjadala unaendelea maana in the process kila mwenye akili anjionea ukweli na uongo ulipo, kama huiwezi hiii topic kaa pembeni waachie wanaoiweza mkuu, lakini take your lectures huko porini usiniletee mkuu.
Na siendi kokote ninataka huu mjadala uendelee mkuu, ni kwa faid ya Masha, na yeye na familia yake wanajua kuwa hata siku moja siwezi kujiweka kwenye anything cha kumharibia yeye wala anybody kwenye familia yake, sasa usinifundishe what I know tayari, yaani namna ya kumtetea rafiki yangu.
Ahsante Mkuu.