Minister belittles link with JK's son

Minister belittles link with JK's son

Masha amesema ameacha shughuli za IMMA, je bado anapata malipo yoyote kutokana na share zake kule?

Mkuu MMJ,

Nona lako so far ndio swali la msingi, Kama Masha, bado anapata malipo huko kutokana na share zake huko kama anazo bado, basi havunji sheria yoyote ya taifa letu, hasa baada ya kuvunjwa kwa Azimio La Arusha, ndio maana kina Kapuya wanamiliki mgodi, ni sawa kisheria zatu za jamhuri.

Kwa wale wengine I am sorry, siwezi kujibu maswali ambayo yako nje ya mada, kama kuna wanaotaka anzisheni topic mpya ku-cover maswali yenu, mimi ninajibu yale tu yanayohusikana:-

1. Masha, kutokuwa fisadi kutokana na ushahidi usiokuwepo so far.

2. IMMA, sio kampuni ya kifisadi, kwa sababu ushahidi hakuna.

3. Kwamba kumuajiri Ridhiwani, ulikuwa ni strickly uamuzi wa IMMA, na sio bunge wala serikali, hata kama hakuwa na elimu kabisa.

Ninamtetea Masha, tena bila ya wasi wasi kwenye haya matatu, na si kweli kabisa kuwa eti Masha ndiye mmiliki wa IMMA, that is pure nonesense, na siwezi kupoteza muda na this kind of questions, mmiliki mkubwa wa IMMA ni Mujulusi, sio Masha.

Naona taarifa ya habari imeisha sasa tunaendeea tu na mazungumzo baada ya habari, inakubalika!
 
Kama ameacha alikuwa na haja gani kwenda kuongea na press kuhusu hiyo kampuni na mwajiriwa wake Ridhiwani au hawa watu wamechanganyikiwa?

hapo sasa, ndio maana mie jana nikamwambia kaka FMES amwambie rafiki yake, awe makini, Tanzania ya leo si ile ya zamani!!

kingine, dunia nzima kampuni kubwa nchini kama TOL shares zake haziwezi kuanguka kwa zaidi ya asilimia 50 na kusiwe na uchunguzi rasmi, utakaopelekea watu kutingishwa kwa pilato na labda kufungwa au kuwajibika kwa jinsi flani!! wote tunajua nini kilimtokea kenneth "ken boy" ray wa ENRON ingawa alikuwa mtu wa karibu na Bush.........hapa kuna kitu, na mh Masha itabidi aite press conference nyingine kujieleza kwa kina, ama sivyo ndio hivyo tena label ya "six letters word" itakuwa yake!!.
 
Masha amesema ameacha shughuli za IMMA, je bado anapata malipo yoyote kutokana na share zake kule?

Kupata malipo toka kwenye shares zake atakuwa anapata wala hilo sio tatizo. Ni sawa tu na angenunua shares za kiwanda cha beer.

Yeye anabanwa na sheria za conflict of interest ambazo hata kwenye Azimio la Zanzibar zipo, tatizo ni kwamba hakuna anayefuatilia wale wanaokiuka hizo sheria.

Kwenye hili naona Masha hakutakiwa kabisa kuongelea mambo ya IMMA, hasa kuitisha mkutano specifically kwa ajili hiyo, labda angeulizwa kama mengineyo. Lakini kwa TZ, viongozi wetu wanaona wapo juu ya sheria.

Inaelekea EPA inaweza kumtafuna Masha, wacha tuendelee kusubiri report.
 
hivi Bongo kuna equivalent ya SEC(securities and exchanges commission)?? na bungeni kuna commerce committe!!?? samahani, maana nimesahau kidogo lakini ningependa kufahanishwa na kuona jinsi gani agency hizo zimefanya kazi zao ktk hili.
 
Kupata malipo toka kwenye shares zake atakuwa anapata wala hilo sio tatizo. Ni sawa tu na angenunua shares za kiwanda cha beer.

Yeye anabanwa na sheria za conflict of interest ambazo hata kwenye Azimio la Zanzibar zipo, tatizo ni kwamba hakuna anayefuatilia wale wanaokiuka hizo sheria.

Kwenye hili naona Masha hakutakiwa kabisa kuongelea mambo ya IMMA, hasa kuitisha mkutano specifically kwa ajili hiyo, labda angeulizwa kama mengineyo. Lakini kwa TZ, viongozi wetu wanaona wapo juu ya sheria.

Inaelekea EPA inaweza kumtafuna Masha, wacha tuendelee kusubiri report.

Kawaida waandishi wanaangalia ni habari ipi italipa, kwa hiyo usitegemee kuongea na waandishi ukitegemea kwamba unachowazia kwamba ndio ajenda kuu ndicho kitakachotoka gazetini. Ni kinyume chake. Ukiweza kutokujibu maswali, ni vizuri zaidi wakati mwngine.
 
hivi Bongo kuna equivalent ya SEC(securities and exchanges commission)?? na bungeni kuna commerce committe!!?? samahani, maana nimesahau kidogo lakini ningependa kufahanishwa na kuona jinsi gani agency hizo zimefanya kazi zao ktk hili.

YournameisMINE,

Tanzania katika utendaji wame copy kila kitu toka UK, hivyo nina uhakika hizo kamati zote zipo. Bungeni kuna kamati ya fedha na mipango.

DSE pia nina imani wana kamati zote zinazotakiwa, tatizo la Tanzania ni utendaji wa wahusika. Hata sheria zetu naona sio mbaya, kilicho kibaya ni jinsi zinavyotekelezwa.
 
hivi Bongo kuna equivalent ya SEC(securities and exchanges commission)?? na bungeni kuna commerce committe!!?? samahani, maana nimesahau kidogo lakini ningependa kufahanishwa na kuona jinsi gani agency hizo zimefanya kazi zao ktk hili.


Nilizungumza kwenye reply yangu ya awali. Kuwa na DSE wakati hatuna government institute inayo provide check and balance ni sawa na kuwaibia wananchi mchana wa jua kali.

Nikawaambia watu ya kwamba soma the Lexus and Olive tree. Stock exchanges zipo mpaka Mongolia, republic of central africa, tatizo ambalo wote tunalikumba ni rules and regulation za kuwabana wauzaji kwenye soko hilo huria.

Kama mtu alisababisha share ikaenda kwenye tank for more than 50% na haija recover since then, swali linakuja kwa nini huyo mtu hajafungwa kwenye 24hrs security Jail?
 
Nilizungumza kwenye reply yangu ya awali. Kuwa na DSE wakati hatuna government institute inayo provide check and balance ni sawa na kuwaibia wananchi mchana wa jua kali.

Nikawaambia watu ya kwamba soma the Lexus and Olive tree. Stock exchanges zipo mpaka Mongolia, republic of central africa, tatizo ambalo wote tunalikumba ni rules and regulation za kuwabana wauzaji kwenye soko hilo huria.

Kama mtu alisababisha share ikaenda kwenye tank for more than 50% na haija recover since then, swali linakuja kwa nini huyo mtu hajafungwa kwenye 24hrs security Jail?

.....exactly!!!! niliiona ile post yako ya mwanzo, nilikuwa najaribu kupigia mstari points zako na kuiweka wazi ishu ya kuwa na agency ya kudili na masuala kama haya!!!.

mfano.....Feds leo hii wametangaza kuwatingisha Countrywide kortini kwa mitkasi kama hiyo shady, ambayo imepelekea watu kupata shida ktk mortgages na kupoteza nyumba zao!!!!
je serikali yetu ilifanya nini kwa TOL??
 
.....exactly!!!! niliiona ile post yako ya mwanzo, nilikuwa najaribu kupigia mstari points zako na kuiweka wazi ishu ya kuwa na agency ya kudili na masuala kama haya!!!.

mfano.....Feds leo hii wametangaza kuwatingisha Countrywide kortini kwa mitkasi kama hiyo shady, ambayo imepelekea watu kupata shida ktk mortagages na kupoteza nyumba zao!!!!
je serikali yetu ilifanya nini kwa TOL??

YournameisMINE,

Si umeona watu wamechota pesa BOT na kila mtu anajua na tunawajua lakini
hata kuwakamata tu tunaona usanii kibao. Sheria zote za kuwakamata zipo, ila TZ yetu imejaa usanii. Ni usanii ule ule uliomwachia Ditopile huku sheria zote za kuua zipo safi kabisa.

Tatizo sio sheria wala kukosekana agencies, tatizo ni hao waliopewa majukumu ya kusimamia hizo sheria. Sheria zetu zina macho, zinaangalia mhusika ni nani, kama sio mmoja wao basi zinakata, kama ni mwenzao, hapo usanii unaanza kufanya kazi.

Report ya Richmond tumeiona, wanasubiri nini kutuonyesha report ya EPA?

Tuombe mungu tu, maana kuna siku watu watachukia, yatatokea yale ya Kenya. Sisi itakuwa sio ukabila tena basi ufisadi. Watu watapita mitaani wanasafisha nyumba za mafisadi.
 
Ditto kweli ni mjasiriamali wa kuuza asali kwa sasa baada ya kuua dereva wa daladala!

Haya yanaweza tu kutokea Tanzania!
 
Mimi nashindwa kuelewa kwanini watu wanmasafisha Masha na kumuuona mtu clean! Hivi uhusiano wao na Deep Green ambayo IMMA ndo waliorithi ilipofilisiwa, na kuwa ni moja ya kampuni iliyochota mabilioni EPA, hamtaki kuona hilo kuwa lina harufu ya ufisadi jamani! Au mpaka Mwakyembe asome ndo mkubali.

Meremeta, Tangold, Deep Green zinao uhusiano mzuri wa kibiashara na IMMA advocates ambacho ndo kigezo cha kuuona mkono wa wahusika katika IMMA kuwa na ufisadi.

napenda kusadiki kuwa, uhusiano wa Ridhiwani na IMMA, kuchaguliwa kwa Masha ktk uwaziri, wakili wa IMMA kuwa jaji hautokani tu na utendaji mzuri bali fadhila ambayo ndo kigezo cha kuwa waziri awamu ya 4 Tanzania. Plus, IMMA advocates hawatajinasua na Deep Green, na Deep Green haitajinasua ktk ufisadi..

Msiomjua Ridhiwani kwa tambo zake na uwezo mdogo wa kielimu ndio mtahoji hapa forum.
Kwa ufupi...Masha will soon be on the list of shame and is directly involved whenever you mention of Deep Green and Tangold.
 
Ditto kweli ni mjasiriamali wa kuuza asali kwa sasa baada ya kuua dereva wa daladala!

Haya yanaweza tu kutokea Tanzania!

Mzalendohalisi,

Si ajabu wamempa na pesa toka BOT au TIB kimya kimya, ya Tanzania hayaeleweki kabisa. Ukishangaa ya Musa, utaona ya Firauni.

Yaani sijui haya madudu yataenda mpaka lini?

Baadaye Ditopile ataanza kutukana watu akijifanya mjasiriamali hodari, kumbe kachota sehemu.
 
Nakulilia Tanzania,
Mkuu nimekusikia sana isipokuwa nadhani hapa tunachanganya vitu viwili bila kutoa uhakika wa kile kinachotangulia. Kwanza kumbuka tunazungumzia Tanzania na sheria za Tanzania sio unavyofikiria ama kutaka wewe ama mtu mwingine yeyote. Hata mimi hapa sipendezewi na yote yanayotokea lakini nafungwa kamba na sheria kwani TZ hakuna kitu conflict of interest.. labda kwa wake zetu tu.
Ikiwa Masha ni mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo ya mawakili IMMA na mwajiri wa Ridhwan, na kisha ni Waziri ktk wizara ya Mambo ya ndani, basi anayo kila haki kisheria kutetea/kujibu tuhuma zozote zile zinazohusiana na kampuni yake ama wizara yake kwani kabeba/bebeshwa kofia zote kisheria.
Mkuu, ni Azimio la Zanzibar linalompa uwezo wa kuendesha biashara achana kabisa na swala la kununua shares. Hivyo Masha anaweza kuwa Waziri na pia CEO wa kampuni ama makampuni yake mwenyewe binafsi na ktk kitengo chochote kile hata kama kiwe kinahusiana na wizara yake. Nadhani anaweza pia hata kufungua ofisi hiyo ndani ya wizara yake -Ruksa, Mkapa aliweza fungua Ikulu itakuwa wizarani?...Hakuna kipengele chochote cha sheria kinachomkataza kiongozi kutofanya hivyo....til then.
Ndio maana viongozi wetu wengi wamefungua makampuni yanayoihusiana na kazi zake kiserikali kama waziri na ndio maana hata mtu kama Lowassa aliweza kuingilia maamuzi ya tender ambayo haikuwa kazi yake ila tu kwa maslahi ya kampuni yake - Richmond. Kumbuka hata kule Bungeni pamoja na kuwa haikuwa kazi yake kukana matatizo ya mkataba wa Richmond lakini mara kibao aliweza kuingilia kati na kusema hakuna matatizo akiongezea kuwa ndege yetu inapoaa!

Kwa hiyo mkuu hadi hapo mtakapo nambia kuwa Masha hana mamlaka kisheria ndani ya IMMA labda naweza kubaliana nanyi kwani tuhuma za Ridhwan zinahusiana na kampuni yake - IMMA.
 
Mzee Mkandara, nimeipokea changamoto yako.. sheria ipo. Angalia sheria yenyewe ibara 6, vipengele vya d, e, f, g, h,
 
Saa ingine wala haina haja ya Bunge kupitisha sheria ambazo hazifuatwi! Ni kupoteza tu mda wa wabunge kuwalipa posho!

Hebu niambiani..je sheria inasemaje juu yu mtu kuua? Na je leo hii Ditto sii mjasiriamali na anauza asali pamoja na kuua mtu?

Sasa hizi sheria zinaaply kwa nani???
 
Mimi nashindwa kuelewa kwanini watu wanmasafisha Masha na kumuuona mtu clean! hamtaki kuona hilo kuwa lina harufu ya ufisadi jamani! Au mpaka Mwakyembe asome ndo mkubali.

Mkuu hatuwezi kuhukumu viongozi wetu mahodari na wachapakazi safi kwa ajili ya harufu, nafikiri ni very low IQ kujaribu hata kuiweka hapa kesi ya harufu!

napenda kusadiki kuwa, uhusiano wa Ridhiwani na IMMA, kuchaguliwa kwa Masha ktk uwaziri, wakili wa IMMA kuwa jaji hautokani tu na utendaji mzuri bali fadhila ambayo ndo kigezo cha kuwa waziri awamu ya 4 Tanzania.

Then mkuu na wewe nenda utoe fadhila, ili upewe nafasi sidhani kama hi nayo inahitaji brainer, wale waliomsaidia rais wakati wa uchaguzi ni haki yao kupewa nafasi, maana angekosa wangekosa pia, kma kina Keenja, alipokosa Sumaye nao wameenda na maji, ndio siasa za kisasa mkuu, Karl Rove na Rice walimsaidia Bush, alipopata urais wakaula, mkuu hiyo ni political fatc kila nchi duniani, kwa hiyo hakuna cha ajabu kama your theory ya vyeo bongo ni kweli, maana ni kweli dunai nzima!

Msiomjua Ridhiwani kwa tambo zake na uwezo mdogo wa kielimu ndio mtahoji hapa forum.

Kuajiriwa kwake IMMA ni simply uamuzi wa IMMA, na sio wananchi wala bunge, hata kama hajui kuandika jina lake, by the way alipokuwa rais wa wananfunzi huko chuo alipewa na IMMA, kwa sababu baba yake alikuwa rais, au alichaguliwa na wananfunzi kwa kuwekewa bunduki vichwani, maana kwa maneno yako inaonekana jamaa hafai kabisa, sasa ilikuwaje wanafunzi wenye akili timamu wakamchagua kumpa hiyo nafasi?

Kwa ufupi...Masha will soon be on the list of shame and is directly involved whenever you mention of Deep Green and Tangold.
kuwa lina harufu ya ufisadi jamani!

Mwisho tizama jinsi unayojichanganya mwenyewe! Chuki, fitina, na majungu, kumbe hata kwenda kusoma na kuishi nje ya bongo, haisadiii tabia zetu original hatuwezi kuziacha, it is a shame!

Masha, is doing great sasa tumsaidie kijana mwenzetu atuongoze kwa umakini, maana the kid ni potential future president, wakuu hawa kina Masha ndio viongozi wetu wapya, kina Kingunge hawarudi tena, sasa kuwapiga vita bila sababu haisadii, tusaidie wazalendo wenzetu hawa, kijana angeweza akabaki USA na ku-practice law tena angekuwa baaaaaaaabu kubwa, lakini unajua uzalendo tena kwa hiyo tuwasaidie ndugu zangu kina Masha waendelee.

Ahsante Wakuu.
 
Mzee nadhani uko very correct hapa; tusikosoe ili kuwaangusha (isipokuwa when it is absolutely necessary) kama jamaa yetu wa NY yatakavyomkuta sasa - Spiltzer. Tunapowakosoa hawa viongozi vijana tufanye hivyo ili kuwasaidia.

Hata hivyo tusiwaache kuwakosoa kwa sababu ni potential leaders; to me that is the very good reason for us to keep our eyes on them. Tuliwafumbia macho kina Mkapa, kina Kikwete, na sasa tunajua tulipofikia. WE can not take that chance.

Kama unaamini Masha ni potential President unanipa sababu kubwa zaidi ya kufahamu wakati mabadilishano ya fedha kati ya Tangold na Deep Green upande mmoja na Immma upande mwingine Bw. Lawrence Masha alikuwa wapi; alijua nini; na alifanya nini? Je hadi leo hii bado analipwa na IMMMA? Je kama Waziri wa Mambo ya Ndani, yuko tayari kuamuru uchunguzi ufanyike kuhusu Tangold, Meremeta, na Deep Green? Je, ikitolewa hoja ya kufanya uchunguzi huo yuko tayari kuiunga mkono?

Now, I really want to know about him, maana kwa mzee kama wewe kumanoint huyu kijana kama "future President" i'm taking it very serious, na kwa vile motto yangu ni kuwa hapendwi mtu, haogopwi mtu, haonewi mtu, na hapendelewi mtu, nadhani Masha is a fair game!
 
Mwanakijiji,

Unafikiri ilitokea kwa bahati mbaya Bwana Masha kuwepo kwenye Deep Green (yenye uhusiano na IMMA) na Ridhiwani kuwemo IMMA na Bi Karume kwepo IMMA wakati wote baba zao ni Ma rais wa nchi?

Once is happenstance, twice is a coincidence, thrice is enemy's action ( of this nation).

Kutokea watu watatu...Waziri (masha) Presidents wawili = Watu watatu wana ushirikiano wa kisiasa na vilevile wa kibiashara ina maana moja tu nayo unaijua.
 
FD, kuna ndugu zetu hawataki tuliangalie hilo... kwa sababu tukilikodolea kwa karibu inaitwa "fitna, na chuki"...
 
Back
Top Bottom