Wakuu niende moja kwa moja kwenye mada kutokana na wimbi la vijana wasio. Na ajira kua kubwa, ili kujikimu na changamoto za kimaisha yao kila siku nashauri walipwe posho iwe kama kifuta jasho uku wakingojea kuajiriwa.
Naomba kuwasilisha.
Raisi wa Lebanon na waziri wake mkuu wote wamekuwa wakali dhidi ya nja za Marekani na Israel kuwalazimisha kufanya mambo ambayo hayana maslahi na taifa.
Kwanza ni kuhadaiwa kurejesha uhusiano na Israel na pili ni kuwanyang'anya silaha kundi la wapiganaji wa Hizbullah.
Viongozi hao wamelalamika...
NI ALMOST HAKUNAGA mtu, mwanasiasa, bilionea, mwanaharakati, askofu, shehe, mtu wa system mstaafu, ambae huwa anaweza kusimama hadharani na kuiambia serikali:
1. Nina shughuli yangu sitaki kiongozi wa serikali aje !
2. Nina hela yangu ya mfukoni nitatumia in one day kulisha wananchi ( ng'ombe...
Habari wakuu
Kwako mama Samia Suluhu na waziri wa ardhi wa JMT
Dar es salaam imekuwa ni kijiji ambacho kimezungukwa na Bar kila kona, Kelele na kumbi za sherehe huku beach zetu nazo ni chafu sana
Sisi tusiopenda vitu vya namna hiyo, tunakosa mahali pa kwenda kupumzika na kupeleka watoto. Si...
ili nchi iweze kupata mabadiliko makubwa yanoyohitajika, kupata katiba mpya pekee kama suluhisho la mambo yote kwenye nchi haitoshi kama kitu cha kuleta usawa, haki na uwajibikaji bali lazima pia na mamlaka ziache uchawa ili kuruhusu sheria iweze kufanya kazi ipasavyo.
Uchawa kwenye mamlaka...
Ni muhimu kwa serikali ikafanya maboresho kwenye kuajiri wafanyakazi wa TRA hii itaongeza ufanisi
Wapewe mikataba ya miaka 15 baada ya hapo waajiriwe wengine
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Elia Juma Kidavile, ametoa wito kwa vijana wa kuwanenea viongozi wao mazuri kutokana na juhudi kubwa wanazozifanya katika kuleta maendeleo kwa wananchi. akiongeza kuwa viongozi hao wamekuwa mstari wa mbele...
CHADEMA wanasema " no election" na wanasikilizwa na watu wengi na hii inaleta taharuki,kwa sababu hawa wana haki gani ya kuhamasisha wananchi wasipige kura. Saa ya Uchaguzi imefika, Uchaguzi unafanyika kufuatana na Katiba,kwa hiyo mtu akisema" no election" haitakii mema hii nchi.
Hii ni nchi...
Wanabodi,
Suala la serikali mbalimbali kukopa fedha kwenye taasisi za fedha kama vile benki ya dunia au IMF halijaanza leo na wala halitaisha hivi karibuni. Katika dunia ya sasa, inaaminika kwamba mikopo ni njia mojawapo inayoweza kutumiwa na serikali yoyote katika kuendeleza miradi yake na...
Niambieni Tunaongeza budget gan kwene huduma zenu!!…..
Huko mbeleni taasisi binafsi zikiwezeshwa serikalini hakutakua na mteja hata mmoja.
NB: Nawaza kwa sauti
Mfano hako ka bundeji na kimfuko cha kuchukulia sample.
Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira kwa vijana wenye elimu ya juu, hasa wale waliomaliza degree katika vyuo vikuu. Wakati huo huo, nafasi za watendaji wa vijiji na mitaa mara nyingi hupewa wahitimu wa vyeti badala ya wahitimu wa shahada. Hii ni hali inayoshusha thamani...
Mkuu wa Mkoa ni kiongozi wa watu wote, taasisi zote na vikundi vyote. Anapokuwa anatumia pesa ya watu wote kuwapa Tabora United inayoshiriki ligi kuu sawa na timu nyingine sio sawa. Hii ni tofauti na goli la mama ambalo linatolewa kwa timu yoyote inayoshiriki mashindano makubwa. Mkuu wa mkoa...
Nimepitia maoni ya watu wengi kuhusiana na hawa wasemaji wa vilabu. Wengi wao hawana weledi. Angalia namna msemaji wa Simba alivyokua akimuongelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, juzi Kamwe kamtolea maneno ya hovyo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, kashfa na kumshambulia binafsi. Wasemaji sasa wanaweza kuwatweza...
Suala la lishe ni muhimu sana, lakini naona mpango wa chakula cha mchana kutolewa kwa wanafunzi inaendelea kubaki kuwa changamoto. Mtoto anatoka nyumbani saa 12/1 asubuhi anarudi saa 10/11 jioni ndio anapata chakula cha mchana, kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwamba; watoto wa shule huwa wako...
TAARIFA KWA UMMA
(Tunaitaka Serikali kuunda tume huru kuchunguza matukio yote ya Mauwaji, Vipigo na Utekaji, Zanzibar)
ACT-Wazalendo, tumepokea kwa mshituko taarifa ya kutekwa, ndugu Fakih Ali Salim, mwenye umri wa miaka 40 na mkazi wa Kijiji cha Chozi, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba...
Nimeona hili suala mtaani twitter na nimseoma comments zinasema ni MBET, nimesikitika sana, yani wafanyakazi wanaibia kampuni mpaka mtu anafunga kampuni na kuondoka? Nikikumbuka hivi ndivyo imalaseko, nakumatt na game na shoprite ilivyofunga, ukiwauliza wengi wanasema hawaoni faida ila bidhaa...
WATASHA walisema Maisha ni mipango hili ni sahihi kwa 100%, yawekana tumeshindwa kutoboa kwa kukosa mipango sahihi na kuwa na Nidhamu hafifu ya Fedha.
Muda wa kustaafu kwa mtumishi wa umma ni miaka 60 kisheria, lakini kwa hiari ni kuanzia miaka 55 hadi 59.
Sasa kwa mtu mwenye umri wa Miaka...
Kama wewe uko ndani ya CCM na unategemea kupata vyeo au kuwa mkubwa huko mbeleni eti kwa kuwasifia Viongozi wako na kuwatukana Viongozi wa upinzani,basi sahau,maana utakuwa kama Lucas Mwamshamba,
Njia rahisi wewe nenda upinzani,hasa Chama Cha Chadema,vumilia kule hata miaka mitano halafu anzisha...
Mara nyingi ukihoji kuhusu utendaji kazi wa serikali huwa wanatokea wazarendo uchwara na wapigaji wakubwa, utasikia anakuambia "unataka serikali ikuletee maendeleo mlangoni kwako?" Wengi wao ukiwatizama huwa ni watu ambao huwa wamegawanyika kwenye makundi mawili, kundi la kwanza ni watu flani...
Kwa Hali ya shilingi yetu Kwa sasa ni mbovu na mikakati dhabiti inahitajika kukumaza fedha yetu. Moja ya maono ya JPM ilikua kuwezesha viwanda vya ndani kupitia kuwanyanyua wazalishaji wadogo na kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji Kwa viwanda vikubwa.
Sabuni hata ghetto inatengenezwa...