Mkuu,
Unaelewa kwamba kuna watu ni tofauti kifalsafa, kisaikolojia, kiutamaduni?
Nakubali tumetofautiana ukweli.
Wengine hata Tanzania hapohapo hawataki hata kutoka mikoani mwao kuja Dar?
Nimeishi mikoa zaidi ya 20 hapa Tz, nimeongea ma watu aina tofauti tofauti na pia nimesikiliza mawazo yao.
Nimekutana na mtu, amezaliwa njombe, amekulia njombe, amesoma njombe, ameolea njombe tena ni nyumba ya pili na kwao, na watoto wake pia wanaishi kama yeye. Hivyo unachosema ni sahihi.
Lakini swali moja nilimuuliza? Je! Hutamani maisha mengine nje ya hapa ulipokulia na kuishi muda wote?
Jibu lake lilikua ni hivi, kwamba maisha ni Yale yale tuu, hata nikienda sehemu nyingine haitakuwa tofauti na hapa labda mazingira na watu ndio vitakua tofauti.
Hivyo kwa swali lako hili nitakujibu kwamba hawa wote wanaokubali kuishi sehemu Moja na wengine wanaotaka kuhama ni kwamba wote wapo sahihi ila kusema kwamba unaondoka sehemu kwasababu ya changamoto fulani hapo ndio nakataa.
Huyu jamaa niliemtolea mfano kwakweli hakuweza kuniambia shida zao pale kijijini lakini binafsi nilivyofika pale niliona changamoto nyingi sana, Yaani kukaa pale wiki tatu unaweza ukapata presha kwa mawazo😂😂😂. But for them it was like heaven.
Wengine hawataki hata kuoa kabila tofauti na kabila lao hapohapo Tanzania?
Ndio, nakubali na hata sababu zao nazikubali pia.
Nimekaa na wasukuma wao hawawezi kuoa kabila jingine na hata wakioa Hilo kabila na mahari pia inakua ndogo. Yaani kabila tofauti na wasukuma mahali mnaweza kupewa ng'ombe mbili😂😂😂😂🙌
Na hata Ulaya na Marekani kuna watu hawataki kukaa nchi zao, wanasafiri kuishi nchi za mbali?
Sijawashuhudia watu wa namna hii, na endapo wanatoka kwenda nchi zingine ni kwamba wao hawakimbii changamoto kama sisi waafrika. Nafikiri wao hufuata passion zao tuu.
Unaelewa kuna sehemu ya hili jambo inaweza kuwa ni falsafa, utamaduni na saikolojia ya mtu tu si lazima iwe utumwa na ulimbukeni kama unavyosema?
As adventure nakubali, ila unataka kuondoka nnchini kwako ili ukatafute maisha bora sehemu nyingine huu ni upumbavu kwasababu hata huko unakokwenda bado utakutana na changamoto sasa je! Umejipangaje kuzikabili changamoto za huko?? Na kama unaweza kuzikabili changamoto za huko unashindwa Nini kuzikabili changamoto za hapa????
Wazungu wanasema INTELLIGENT IS HOW YOU ADAPT TO CHANGES, Sasa kama mtu ni intelligent enough huwezi kukimbia changamoto.
Na hata ikiwa utumwa na ulimbukeni bado ni haki ya mtu kuamua anataka kuishi wapi?
Ni kweli na sahihi kabisa huwezi kumpangia mtu aishi wapi. Lakini pia ni vyema usipaseme vibaya pale ulipokua/unapokua.
What I mean ni kwamba kama umeona kuna nchi unapendezwa nayo bhasi ni haki Yako kwenda huko pasipo kupasema vibaya hapa ulipo au wengine wanapoishi.
Nakwambia dunia Leo ipo hivi ilivyo kutokana na baadhi ya nchi kuzisema vibaya nchi zingine. Imagine North Korea waishi maisha yao pasipo kuambiwa wapo chini ya udikteta si wataenjoy tuu maisha yao?
Unaelewa kuwa mambo yale yale ambayo yanaweza kukufanya wewe uone Tanzania kuna raha sana, mfano watu kuwa overly social, kupandiana sana, kuchangamana sana, kusalimiana sana bila hata ratiba, kujuana sana, kuzoeana sana, yanaweza kumfanya mtu mwingine asiipende Tanzania kama sehemu ya kuishi kwa kuona ina utamaduni usiothamini faragha, ukimya na uhuru wa mtu binafsi?
Mimi mwenyewe naishi hapa Tz kuna mambo mengi tuu ambayo yananikera, kwa yale ambayo naweza kuyabadilisha huwa napambana kuyabadilisha na yale ambayo siwezi huwa nayaacha tuu yanipite hata siwezi kuangaika nayo.
Watu wengi wanalalamikia siasa zetu, na ni kweli siasa zetu ni mbaya na ni chafu sana. Lakini je! Kila tatizo ni tatizo la kisiasa???
Je! Ugumu wa maisha hapo mjini Dar ni tatizo la kisiasa??? Yaani mtu anafanya kazi ya kulipwa laki4 na anajua kabisa matumizi yake ni zaidi ya hicho kipato chake alafu anataka lawama apewe mwanasiasa kweli???
Ukienda njombe kuna madogo wanamiaka 20+ lakini wanamiliki mitaji ya milioni 50+ Sasa hapo shida ni Nini?
Ni lazima watu wajifunze kutafuta fursa, kama wanavyofikiri ulaya kuna maisha mazuri bhasi wayatafute kwanza hapa Tz, waende mikoa tofauti kwanza.
Binafsi Mimi ni mkazi wa Dar lakini ninamakazi pia Mbeya, Njombe, Iringa na Dodoma huko nalipia Kodi na sifanyi hivyo kwamba ninakipato kikubwa hapana, nafanya hivyo ili kuzitumia fursa tuu.
Unaelewa kati ya watu wawili hawa hakuna aliyepatia au kukosea, wote wako sawa kwa sababu hili ni suala la mtu binafsi kuamua anataka nini yeye mwenyewe?
Ni sahihi lakini Kuna mmoja anakosea sana kupasema vibaya sehemu ambapo Bado yupo.
Kaka tusichokielewa ni kitu kimoja, haya tunayoyaandika huku yatabaki kuwa historia na kuna wadogo zetu pia wanajifunza kutoka kwetu, Sasa tukiacha humu kumbukumbu mbaya ni lazima kizazi kijacho kitakuja kuuishi huo ubaya tunaowafundisha Leo.
Inshort kama mtu ameshindwa kuishi bongo bhasi aseme kwamba yeye ameamua kutafuta maisha upande mwingine wa nchi pasipo kutangaza ubaya wa hapa bongo.
Tunapopishana kati yetu ni kwamba kila mtu analazimisha upande wake ndio uonekane ni sahihi, na mwisho nilihitimisha kwa kusema Kila mtu abakie na anachokiona ni sahihi pasipo kusema Cha mwenzake ni kibaya.
Umewahi kufikiria privileges na biases zako ni zipi, na zinakupofusha vipi usiwaelewe watu wengine upande wao ukoje, uka wa dismiss kuwa ni malimbukeni tu?
Yaani kwa fursa zilizopo Tz ni kwamba kila mtu anaweza kuwa tajiri akitumia akili yake vizuri. Hakuna kitu kinanifumba kwamba nisione changamoto.
Kama rushwa naombwa sana, na huko barabarani ndio usiseme ni changamoto juu ya changamoto but we survive and move on.
Nilikuwa na aunt yangu mmoja, alikuwa ana maisha mazuri sana Tanzania, kipindi cha Nyerere wakati bidhaa zilikuwa za shida, yeye alijuana na watu wa serikali na kupata bidhaa, alikuwa anaenda likizo kwenye mbuga za wanyama kaskazini mwa Tanzania, kwa ndege, akitaka chochote anapiga simu kwa marafiki zake waliojaa kwenye serikaki ya Nyerere, anapata, kuanzia nyumba za National Housing zilizo sehemu nzuri, mpaka bia wakati huo bia hazipatikani.
Huyu aunt yangu alikuwa anasema yeye hawaelewi watu wanaotaka kuondoka Tanzania, nchi nzuri kama hii, wanaondoka wanaenda wapi? Kufanya nini wakati maisha nazuri yapo Tanzania?
Huyu aunt yangu hakujua matatizo mengi ya Watanzania, kwa sababu alikuwa anaishi Masaki, ana privilege kubwa sana.
Sasa, na wewe ushawahi kuzitafiti privileges zako na biasea zako, kujua kuwa pengine Tanzania yako si sawa na Tanzania ya watu wengi? Kwamba watu wengi hawana privileges kama zako?
Na pengine si privileges za mali na access to power tu, pengine una privilege ya high tolerane for bullshit, from election fraud toTANESCOS shenanigans.
Ushawahi kufikiria kuwa huenda kuna watu hawajabarikiwa kuweza kukubali ujinga kama ulivyobarikiwa wewe, na hawa unatakiwa uwaelewe na kuwaheshimu tu?
Mkuu umetolea mfano mkubwa sana, labda nikwambie tuu.
Mbeya, Chunya, Makongorosi kuku wa kienyeji anauzwa mpaka elfu 45 na ni kuku mmoja, debe la pumba ni tsh2000 mtu amekomaa kukaa Dar sehemu ambayo kipato si Cha uhakika kwanini asiende sehemu kama hizo???
Kuna mambo hayahitaji connection Wala mitaji mikubwa Yaani ni mtu tuu kuamua na kuanza safari yake ya kuutafuta utajiri. Na hapa ndipo point yangu ilipo kwamba sisi wote tunaweza kuwa matajiri na endapo kuna mtu atakuja kukuzuia kuwa tajiri wewe kufa nae tuu.
Tuache kulaumu, Bali tutafute maisha bora kwetu wenyewe. Masuala ya siasa tuwaachie wanasiasa na sisi tufanye uliowajibu wetu.