Upo Bongo bahati mbaya?

Upo Bongo bahati mbaya?

Nakuelewa sana dada.

Ujue kuna wenzetu ambao walishawahi kukaa nje, halafu ama wakashindwa kwenda na maisha ya huku, ama hawakuyapenda, wakarudishwa au kurudi wenyewe nyumbani.

Kati ya hawa, na sisemi huyu mwamba ni mmoja wao nevessarily, lakini napanua muktadha tu vitu vya kufikiria, kati ya hawa, kuna watu ambao suala la kukaa Tanzania au nje linakuwa suala very oersonal na ideological kwao, kwa namna ambayo favts don't matter, it is a philosophical, ideological, passionately emotional issue.

Yani ukiisema vibaya Tanzania na kutaka kwenda kuishi nje, which is your human right, kwao hawa, whether wanajua consciously au wanafanya kwa kutokujua subconsciously, unawatonesha kidonda cha siku zao walivyoishi nje na kushindwa au kutopapenda.

Wanakuwa si tu hawakuelewi, which is alright, lakini wanaona huna haki ya kufikiri hivyo, which is not alright.

Kwa hiyo mjadala unakuwa si wa kutazama objective facts, mjadala unakuwa wa kujadili identity politics.

Ndiyo maana unaweza kuona mtu anashindwa kujadili facts, anakuja na hoja ya "mimi nishakaa nje miaka hii na hii na nimeamua kurudi Tanzania etc". That is irrelevant, this is not about you.

Lakini wao wanaifanya inakuwa about them, na hapo ndioo facts wasizozioenda zinakuwa ngumu kumeza wanataka mpaka kufanya censorhsip msiseme mnavuofikiri.

Jambo hili linanipa swali, inakuwaje mtu ameishi nje kama anavyosema halafu haonintabu kufanya censorship kiwazi hivi? Maana angekuwa hajatoka Tanzania tungeweza jusema labda ni ushamba wa Kitanzania tu, watu wanafanya censorship kwa sababu hata hawajui censorship ni nini. Lakini, huyu je?

Mimi kuna cousin wangu yuko hivyo kwa hiyo naelewa. Yeye alikuja US kabla yangu, lakini alikuwa na mapepe sana ya kurudi Tanzania every summer ajioneshe kwa waja kwamba na yeye anakaa Marekani. Wakati papers zake hazijakaa sawa alihitaji ku renew student visa yake. Kipindi cha 9/11 walivyoanza kufuatilia watu wenye visa za wanafunzi kama kweli wanaenda vyuoni, alivyorudi Tanzania kuongeza visa wakamkatalia. Wakasema wewe mbona hata chuoni kwenyewe hujafika?

Akabaki bongo, uzuri kuna network ndefu ya kifamikia ikambeba akaendelea na kazi huko. Lakini na yeye alipitia hii cognitive dissonance ya "maisha popote, una adjust tu". Hayo ni maneno ambayo ilikuwa lazima aseme ili kujifariji. Ila mwishoni unaona kabisa mambo si mazuri huko, mizinga mingi. Tunasaidiana lakini, that is no biggie.

My point is, kuna baadhi ya watu wanaorudi Tanzania kiukweli kabisa wao wanaona kuishi nje tabu. I know friends of mine who are like this. Kuna mmoja anasema hata likizo atazunguka Africa tu sasa. Na kuna wanaorudi au kurudishwa Tanzania kwa sababu wameshindwa kuishi nje. Na kati ya hawa, wengi kufanya nao maongezi objective ni vigumu, kwa sababu hili si suala la hoja za kimantiki kwao, hiki ni suala la identity politics.

Ndiyo maana unaona mtu anakuambia ujinga wa usiiseme vibaya Tanzania, wewe adapt na mazingira tu.

Wakati hata hajui uwezo wako wa ku adapt na mazingira ukoje.
Kaka, nashukuru kwa kunielewa
Ukweli ni kama moshi.hauwezi kufichika wakati unafuka

Hao walioshindwa kukaa Ulaya haimaanishi kwamba Ulaya haikuwa rafiki kwao huenda wao ndio walishindwa kuwa marafiki na Ulaya

Ila Tanzania haina urafiki kwa mtu yeyote hasa mpenda maendeleo na zaidi mtu asie mbinafisi

Wote tunatamani kua marafiki wa 🇹🇿 na wenye mapenzi ya dhati yasio na cheating lakin
Mazingira yenyewe yanakataa kuwa rafiki
Mimi, hata kama ningekuwa na uwezo wa kumiliki ma billion ya pesa bado kwa jinsi nilivyo ningeumia kuona watu wakijazwa kwenye daladala kama ng'ombe wanaopelekwa mnadani

Nisingefurahia hii nchii

Wanasema tusikimbie, tubaki tujenge taifa letu
Swali langu je tunapewa hiyo room ya kujenga taifa letu?

Ni kama hivi tunapokosoa badala ya kuchukuliwa kama watu wanaotoa changamoto na mawazo ya kujenga, tunaitwa si wazalendo

Sasa tutalijengaje taifa kama kukosoa na kuhoji mambo yanayotuzunguka kunatafsiriwa kama kukosa uzalendo?
 
Back
Top Bottom