1. 1997 – Masha aanzisha IMMA baada ya kuwa mwajiriwa kwenye firm nyingine ndogo kwa chini ya miaka mine (4) 2. 1997 - 2000 Masha ateuliwa kuwa Managing Director wa TOL (with only 4yrs of legal experience on hand from a private practice and no management skill. Sijui ni experience gani aliyokuwa nayo ya uongozi mpaka akachumpa kwenye u-MD wa kampuni pekee ya O2 nchini. FMES tusaidie hapa.
Mkuu bado unaendela kuema uongo bila aibu, Masha alianza kazi kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo kule Playland, New York akiwa Executive Manager, akaitwa World Bank akakataa na kuamua kurudi bongo, akaingia Law Firm ya Warioba, ambako kwa ajili ya kutafta experiencce za kisheria, ilifikia mahali alifanya kazi bila mshahara for a long time, akateuliwa na rais kuwa mjumbe wa kamati ya kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Muungano, alipomaliza akaingia Oxygen kama Secretary wa kampuni, baadaye akapewa u-acting Director baada ya aliyekuwa kuondoka, badaye akaacha na kujiunga na IMMA, kwa hiyo mkuu hayo yote uliyosema hapo juu ni ukweli uliochanganywa na uongo kwa makusudi ili kuharibu jina la kijana ambaye wewe ni mtu wa karibu sana na familia yake, nashangaa sana mkuu jinsi unavyojaribu kuharibu jina la kijana kwa makusudi! I mean kijana aliyewahi kuwa Executive Manager US, leo eti ni kubebwa kupewa u-Director wa Oxygen bongo? are you serious?
3. Zaidi ya hayo, TOL ilikuwa ni mali ya serikali, Masha sio tu kuwa alikuwa hajawahi kufanya kazi serikalini bali pia alikuwa hana management training yoyote wala experience kabla ya kuteuliwa.
Alikuwa na experience kubwa mno, ila ulikuwa hujui sasa ni vyema kuuliza mkuu, badaa ya kuja kujiabisha hapa.
Sidhani kama hapakuwa na wabongo wengine waliokuwa bora kuliko yeye. How many BCom graduates don't get management works in TZ? Was Masha the most qualified to take TOL? I doubt.
4. Sijui pia kama hiyo position ilitangazwa kama inavyohitajika au alikuwa tu ‘anoited' kwenye hicho kiti? Kwa hiyo ukiangalia juu juu tu utaona kuwa definitely kutakuwa kuna mtu aliyembeba all the way mpaka kwenye u-MD, who was that?
5. 1997 – 2000 Zaidi ya u-MD, mtaalamu Masha pia akapewa kofia ya pili kuwa Company Secretary wa TOL, ingawa hizi zinatakiwa zikamatwe na watu tofauti, otherwise sijui ni nani atakayemwajibisha MD au kuwa independent advisor wa shareholders, board members n.k.
6. 1997 – 2000 Wakati haya yote yakiendelea bado Masha pia alikuwa ni mwajiriwa anayehangaika kuunda kampuni yake ya IMMA, sijui ipi kwake ilikuwa muhimu zaidi.
7. 1998 – TOL ikaanza kuuzwa, hii ni miezi kadhaa tu baada ya bwana Masha kuingia.
Mkuu hiyo kampuni ilikuwa under wazungu, nafikri huelewi simple unwritten rules za wazungu bongo kuwa inapotokea mbongo mwenye uzoefu wa kazi na elimu kutoka majuu, basi yeye ndiye hupewa, kwa hiyo haya yote unayosema hapo juu ni maginations zako tu na chuki nzito as of your usual!
Finaly akapewa uwaziri kwa CV hiyo hiyo fupi, makubwa haya. FMES umesema mko karibu sana hebu muulize akueleze mbinu aliyotumia ili na sisi tuijaribishe, maana kama ni kwa idadi ya digrii tunamzidi.
Mkuu Masha aligombea ubunge, akishirikiana na mtandao, ambao ndio waliishia kushinda, kwa hiyo kupewa kwake uwaziri haikuwa bahati mbaya wala upendeleo, ila ni reality mkuu of politics kwa nchi yoyote duniani sio bongo tu, wewe rudi bongo na wewe uingie kwenye makundi ya siasa, lakini usiwachukie wengine bila sababu za msingi mkuu!
Sio vibaya kwa wewe kumtetea mshikaji wako either kama alikushikwa mkono kama walivyodosoa baadhi hapa mtandaoni au kwa sababu nyingine binafsi, lakini ni vema pia ukakubaliana na yale ambayo yanaonekana wazi-wazi kuwa si ya kawaida. Wasalaam aleikhum
Mkuu maneno ya kushikwa mkono umeyasema wewe mwenyewe, sasa ungekuwa wa kwanza kuelezea jinsi alivyonishika mkono kuingia ubaharia wakati yeye akiwa Elementary School New York, mimi nikiwa melini MS. Hamburg Antwerpen, Belgium. Mkuu ukweli ni kwamba huna hoja ya kuthibitisha kuwa Masha, ni fisadi,
kwenye maisha hatufanani, kila mtu na bahati yake, sio wa-Tanzania wengi wako kama Masha, na sio wa-Tanzania wengi wako kama Freeman, knowing this two guys siku zote ninawalinganisha as far as maisha binafsi is concerned kwa sababu wote ninawajua kwa karibu, wote wameanza kufanya mambo makubwa sana wakiwa wadogo sana ku-umri, na wakafanikiwa, sasa dawa sio kuwachukia na kuwazushia maneno ya fitina ili kuharibu majina yao mbele ya jamii, kwa sababu mimi na wewe tumeshindwa kufikia level zao kimaisha, huo ni uzandiki na roho mbaya tena ya kikorosho,
Mkuu, na maneno yako mengi ya kishule, na maneno yako mengi ya chuki, not even once umeweza kuthibitisha charge yako against Masha, kuwa ni fisadi, I hope one day someone will.
Ahsante Mkuu.