Minister belittles link with JK's son

Minister belittles link with JK's son

JK anaweka safu mpya katika utumishi wa umma, ukiangalia karibu wabunge wote wa ccm waliochini ya miaka 45 walioenda shule kidogo wamepata uwaziri mfano ngereja, maige, dr.devid, malima, dr.mwinyi, dr.nchimbi, hawa ghasia, dr.buriani, masha.

Itakuwa upunguwani watu kumuamria JK cha kufanya katika baraza lake la mawaziri na so far sijaona hili hapa. Kikwete anaweza kuweka yeyote anayefaa na so far anaweka wezi kwenye serikali na katika hilo hakuna chochote kinachoweza kufanyika.

mh.Masha kuwa waziri sio issue ya kujadiri ni stahiki yake, dr.matayo david ni mtaalamu wa kilimo na ndiko aliko. Ukitizama vizuri JK amechukua mawaziri wawili kila mkoa, sasa mwanza ukimtoa ngereja, masha na Diallo mbunge gani anafaa kuwa waziri?

Ni lini katiba ya serikali ilibadilishwa ili kumlazimisha Raisi wa nchi awe na mawaziri wawili kutoka kila mkoa? JK anaweza kuwa na mawaziri 10 (bila manaibu mawaziri) na hiyo nchi ikaendeshwa vizuri na kwa ufanisi. Mambo mengine hayaitaji PhD au sijui hiyo degree gani ya Matayo na Nchimbi kuyajua haya!

Suala la mtoto wa JK nidogo sana kuzungumzwa na waziri wa mambo ya ndani. Hii issue angeweza kuisemea Stella Ndikimi tu, isitoshe huyu kijana ana shahada ya sheria mlitaka akaajiriwe wapi?

Hakuna anayetaka mtoto wa Kikwete akaajiriwe kokote zaidi ya kwenye kampuni la kifisadi la IMMA ambalo limehusika kwenye wizi wa BoT kupitia makampuni ya kifisadi ya Deep Green na Tangold.
 
Watu mmezoea sana kushikwa mikono na ndo shida hiyo lazima umfagilie mtu ili akupe ulaji, kaza buti, piga marufuku ufisadi, inua watanzania wote, ulaji utakuja tu, sio kwa kutumia njia za Kifisadi, fisadi tu

Mkuu hoja kwanza, hajashikwa mtu hapa, unless wewe ndie ulioyezoea kushikwa sasa umeachwa, wote wanaume hapa watu wazima tunaongea siasa kwa ufahamu tulionao, hakuna fisadi hapa wala kushika mkono, wanaoshikwa mikono ni wale wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kujishika mikono wenyewe mkuu, sio mimi you know that, weka hoja mkuu acha hizi, kumbuka wewe ndiye mtoa topic sasa ukianza hizi utaiharibu topic yako mwenyewe, mimi M-Sailor, Baharia bro sio lelemama hapa ni real deal sio ya kushikwa mikono, hajashikwa mtu mkono hapa na haitakuja kutokea, kama hilo ndilo linakukera unataka kushikwa mkono say it, usizunguke mbuyu, omba ushikwe mkono!

Kama una dataz za Masha kuwa fisadi ziweke hapa, so far sijaziona, niliichoona ni yeye kuteleza na kuizungumzia IMMA, wakati yeye sasa ni waziri, na hilo la kuteleza hali-amount into a CRIME au UFISADI, kama una hoja ziweke lakini ukitaka personal be ready maana this time I am ready for you mkuu, sio kama zile last two times nilizokupa free ride! Hapa sio mahali pa kuharibu majina ya viongozi bila sababu za msingi, ni lazima tuwe fair na truthful kwenye analysis zetu ili tuwe treated fairly pia na wananchi wengine including viongozi.
 
Siku nyingi sana niliwahi kusoma hotuba ya Masha kwa wanafunzi waliokuwa wanaenda kusoma USA. Wakati huo alikuwa sio mbunge ila ndio alikuwa mbioni kugombea.

Alivyoelezea kwanini aliamua kuja kusoma first degree UDSM ilikuwa sio sahihi kabisa. Alikuwa ana SPIN wakati ilikuwa sio muhimu.

Inabidi kijana mwenzetu awe mwangalifu, siasa ni kama sheria tu, hakuna haja ya kutoa information ambayo unajua sio sahihi, wakati mwingine ni afadhali kutokusema kitu kuliko kusema kitu ambacho sio kweli.

Kwa viongozi wetu waliopo bado nampa nafasi Masha, ila tu awe mwangalifu hasa kwenye conflict of interest kati ya ile kampuni yao na serikali.

FMES, mwambie mshikaji alikuwa na nafasi ya kutengeneza mamilioni mengi tu kule IMMA, sasa kaamua kuwa mwanasiasa, inabidi aachane na kushughulikia mambo ya ile kampuni yao. Nafasi aliyopewa ni kubwa mno na sifa kwake na vijana wengine.
 
Sasa mlitaka awe ka Kibaki awape wakikuyu watupu, au habyarimana wahutu, albashir waarabu, idi amini waacholi pekee! unaona kitilya alivyoifanya TRA inawachaga na wapare watupu! wameshakuwa miungu watu, wanakadiria kodi kutizama seat belt!

kuhusu immma na deep green sasa shehe akikufungisha ndoa mama akawa malaya utasema siswali tena msikiti ule! Balali, mramba na megji ndio muwaulize sio wakili wa DG,

tz niyetu wote na mgawanyo wamadaraka haupingiki, mkoa gani hauna waziri? we vipi?
 
Mkuu hoja kwanza, hajashikwa mtu hapa, unless wewe ndie ulioyezoea kushikwa sasa umeachwa, wote wanaume hapa watu wazima tunaongea siasa kwa ufahamu tulionao, hakuna fisadi hapa wala kushika mkono, wanaoshikwa mikono ni wale wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kujishika mikono wenyewe mkuu, sio mimi you know that, weka hoja mkuu acha hizi, kumbuka wewe ndiye mtoa topic sasa ukianza hizi utaiharibu topic yako mwenyewe, mimi M-Sailor, Baharia bro sio lelemama hapa ni real deal sio ya kushikwa mikono, hajashikwa mtu mkono hapa na haitakuja kutokea, kama hilo ndilo linakukera unataka kushikwa mkono say it, usizunguke mbuyu, omba ushikwe mkono!

Mkulu FMES,

Nakutetea hapa Mkulu na kweli sidhani kama kumtetea Masha hapa ni lazima uwe umeshikwa mkono. Mimi nadhani mtoa hoja amekosea kwa lugha kali.

Kama una dataz za Masha kuwa fisadi ziweke hapa, so far sijaziona, niliichoona ni yeye kuteleza na kuizungumzia IMMA, wakati yeye sasa ni waziri, na hilo la kuteleza hali-amount into a CRIME au UFISADI, kama una hoja ziweke lakini ukitaka personal be ready maana this time I am ready for you mkuu, sio kama zile last two times nilizokupa free ride! Hapa sio mahali pa kuharibu majina ya viongozi bila sababu za msingi, ni lazima tuwe fair na trthful kwenye analysis zetu ili tuwe treated fairly pia na wananchi wengine including viongozi.

Mkulu,

Kwa Masha kujaribu kuwatetea IMMA hapa anafungua another front. Mshauri kijana maana hapa hajui mtego aliowekewa hapa. Tukirudi kwenye issues hapa, je kuna mtu anapinga kuhusika kwa IMMA na Deep Green au Tangold?
 
Hapa naona kuna haja ya kuunda kamati nyingine ya bunge kuchunguza wanasheria na makampuni ya sheria.

Kuna kila hali inayoonyeshwa kuwa wanasheria wetu ndio wameingiza nchi katika mikataba mibovu na ya kitapeli. Kuna kila hali kuwa utajiri uliyopo katika makampuni mbali mbali ya kisheria una dalili za kifisadi.

Katika gazeti la mwahalisi linasema lina ushahidi wa malipo kutoka Deep Green Finance Limited kwenda IMMA ingawa haikufahamika ilikuwa kwa kazi gani, kama vile ambavyo malipo kutoka BoT kwenda Deep Green hayajapatiwa maelezo hadi sasa.

Halafu baada ya kupata neema Deep iliyo anzishwa na wakurugenzi wa IMMA wakaamua tena kuifilisi.

Nikisoma gazeti la mwanahalisi nagundua kuwa Masha ameshikwa pabaya ndio maana hata hakukumbuka kuwa walisema usichanganye uwaziri na Biashara, lakini inaonekana hakuwa na jinsi.

Tunahitaji kupata mwakyembe Mwingine katika hili.
 
Sasa mlitaka awe ka Kibaki awape wakikuyu watupu, au habyarimana wahutu, albashir waarabu, idi amini waacholi pekee! unaona kitilya alivyoifanya TRA inawachaga na wapare watupu! wameshakuwa miungu watu, wanakadiria kodi kutizama seat belt!

Unavyosema hapa mlitaka sijui unamaanisha kina nani mkuu!

kuhusu immma na deep green sasa shehe akikufungisha ndoa mama akawa malaya utasema siswali tena msikiti ule! Balali, mramba na megji ndio muwaulize sio wakili wa DG,

Sijui huu mfano unahusiana vipi na ufisadi wa IMMA!

tz niyetu wote na mgawanyo wamadaraka haupingiki, mkoa gani hauna waziri? we vipi?

Hakuna sheria inayolazimisha kuwa lazima raisi ateue mawaziri toka kila mkoa. Ni lini tumeanza ukabila? Ni lini viongozi wakichaguliwa basi tunaangalia wametoka mikoa gani?
 
Kwa mtirirko wa mambo kati ya Deep Green, ambao tayari inajulikana kuwa ni fisadi, na IMMA ambao baadhi yao walikuwa ni wamiliki wa Deep Green, inawafanya wahusika nao wawe na harufu ya ufisadi kama sio kwamba ni mafisadi tayari, mpaka hapo watakapotoa maelezo ya kueleweka yatakayowasafisha na sio kubrashi tu kama alivyofanya Bw. Masha. Kwetu sisi Masha hana tena sifa za kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani mpaka mambo ya Deep Green yatakaponyooka, just like Lowassa vs Richimonduli.

Mkuu ni wapi sheria inasema kuwa ushahidi wa kimazingara ukiwa overwhelming, basi una-qualify kuwa ni a crime ya kumfunga mtu? huu ushahidi uko wapi? hizi ulizofanya ni analysis tu kwa kuunganisha habari za magazeti, Masha hakutajwa personal kuhusika na Deep Green, isipokuwa kuna his former patners waliohusika, sasa yeye anahusishwa vipi na hizo "Overwhelming Ki-mazingara Evidence" kwani waliofanya huo uchunguzi hawakujua kuwa Masha alikuwa ni patners na hao wawili waliotajwa kwa majina, mbona hiyo ripoti haikusema kuwa ni IMMA nzima inahusika, unafikiri ni kwa nini wametajwa wawili tena kwa majina?

Mwanzoni wewe mwenyewe umesema ni only ushahidi wa kimazingira, in some few minutes umebadilika kuwa ni overwhelming evidence, mbona too fast hivyo mkuu? Off course kwako wewe kumtambua au kutotambua uwaziri wa Masha, kwa sababu ya ushaidi wako wa kimazingara ambao ni ovewhelming, ni rukhsa mkuu, lakini waziri huchaguliwa na rais wa jamhuri.

Mkuu jaribu kutafuta ukweli unaoudai dhidi ya Masha, huenda upo somewhere, lakini so far haujawekwa hapa. Ingawa ni lazima nikupe heshima kwa ku-keep a clean debate bila matusi wala nonesense, niko tayari ku-debate to the end na wewe mkuu, maana kwako ni hoja kwa hoja, I love it bring it on mkuu na heshima tena mbele!

Ahsante mkuu.
 
Hapa naona kuna haja ya kuunda kamati nyingine ya bunge kuchunguza wanasheria na makampuni ya sheria.

Kuna kila hali inayoonyeshwa kuwa wanasheria wetu ndio wameingiza nchi katika mikataba mibovu na ya kitapeli. Kuna kila hali kuwa utajiri uliyopo katika makampuni mbali mbali ya kisheria una dalili za kifisadi.

Kaika gazeti la mwahalisi linasema lina ushahidi wa malipo kutoka Deep Green Finance Limited kwenda IMMA ingawa haikufahamika ilikuwa kwa kazi gani, kama vile ambavyo malipo kutoka BoT kwenda Deep Green hayajapatiwa maelezo hadi sasa.

Halafu baada ya kupata neema Deep iliyo anzishwa na wakurugenzi wa IMMA wakaamua tena kufilisi.

Nikisoma gazeti la mwanahalisi nagundua kuwa Masha ameshikwa pabaya ndio maana hata hakukumbuka kuwa walisema usichanganye uwaziri na Biashara, lakini inaonekana hakuwa na jinsi.

Tunahitaji kupata mwakyembe Mwingine katika hili.

Hii issue ya Deep Green inalindwa kama Raisi wa nchi mwenyewe. Jaribu kufuatilia uone usalama wa taifa wanavyokuja all over kuifunika. Ikiundiwa kamati huru basi nakuhakikishi Kikwete mwenyewe anaweza kuwa matatani. Usishangae kuwa Masha anaita mkutano wa hadhara katika hili.
 
Kwa wale walio karibu nae kama Mzee/Komandoo/FMES wanatakiwa wampe ushauri ili asije akajizamisha kwenye matope. Zama hizi ni chafu na hazifai hata kidogo, watu wanawindana usiku na mchana ili kutia mchanga kitumbua. Dirty politics anazifahamu sana na si ajabu alikuwa kwenye mtandao, zama za mtandao zimeisha maana mtandao wenyewe umesambaratika, sasa hivi kila mtu ni adui yako maana hujui atakugeuka saa ngapi!

Very strong mkuu, nimekusikia na ni exactly nilivyomwambia jana na nitarudia kumfikishia ujumbe kama huu, anahitaji kuwa careful na media na pia kama alivyosema Mkuu Kitila, kuelewa namna ya kutofautisha IMMA na SERIKALI.
 
Mkuu ni wapi sheria inasema kuwa ushahidi wa kimazingara ukiwa overwhelming, basi una-qualify kuwa ni a crime ya kumfunga mtu? huu ushahidi uko wapi? hizi ulizofanya ni analysis tu kwa kuunganisha habari za magazeti, Masha hakutajwa personal kuhusika na Deep Green, isipokuwa kuna his former patners waliohusika, sasa yeye anahusishwa vipi na hizo "Overwhelming Ki-mazingara Evidence" kwani waliofanya huo uchunguzi hawakujua kuwa Masha alikuwa ni patners na hao wawili waliotajwa kwa majina, mbona hiyo ripoti haikusema kuwa ni IMMA nzima inahusika, unafikiri ni kwa nini wametajwa wawili tena kwa majina?

.....

Mkulu kinachoulizwa hapa ni nini Masha anajua kuhusu ufisadi wa IMMA? Kumbuka kuwa hata Richmond hakuna chochote ambacho kimethibitishwa mahakamani kuwa Lowasa amehusika. Uchunguzi mwingi duniani wa wanasiasa huwa unaanza na swali rahisi la kuhusu kuhusika kwao katika skendo.

Kukiwa na probable course basi inaundwa tume au kesi inafunguliwa. So far tuko kwenye hii first step lakini wakuu wa usalama hawataki chochote kinachohusu Deep Green au Tangold kijadiliwe.

Kama Masha au Kikwete ni wasafi katika hili kwa nini wasiache uchunguzi huru ufanyike?
 
FMES na wengine tuwapeni moyo hawa mawaziri under40, kuwa waziri katika nchi kama tz kuna changamoto nyingi.

Anaesema mawaziri fisadi, sindo wabunge waliochaguliwa, hawa wote wameingia bungeni kwa kura. mie niko mwalugesha na udiwani wangu unanitosha.

Namshauri masha anahitaji kuwa na assistant mzuri na aandae press zake kwa umakini, akumbuke yeye sasa ni Home Minister.
 
Mkulu kinachoulizwa hapa ni nini Masha anajua kuhusu ufisadi wa IMMA?

mkuu wangu ndio maana ninasema kuwa Masha ameteleza, kwa sababu hata IMMA yeye hakuwa na nafasi kubwa hivyo ya kuweza hata kuizungumzia au kuiwakilisha, ndio kuteleza kwake ninaamini alitumia emmotions zaidi ya busara,

kilichoniingiza hii topic ni pale mkuu mmoja alipomshambulia bila sababu za msingi, lakini kama kichwa cha habari kingekuwa unavyosema sasa, wala usingeniona nikimsimamia mkuu, kma swali ni hilo unalouliza sasa, basi ni valid question, lakini sidhani kama yeye ndiye wa kujibu kwa sababu kule IMMA hakuwa na hiyo position ya kuweza kujibia kwenye media.

Halfu ufisadi wa IMMA, bado haujsemwa isipokuwa umesemwa wa patners wawili waliotajwa kwa majina, labda hawa ndio waseme wanachojua kuhusu kuhusika kwao, na IMMA kama ilihusika.
 
Very strong mkuu, nimekusikia na ni exactly nilivyomwambia jana na nitarudia kumfikishia ujumbe kama huu, anahitaji kuwa careful na media na pia kama alivyosema Mkuu Kitila, kuelewa namna ya kutofautisha IMMA na SERIKALI.

Haya ndiyo yanayokuingiza matatani Mkuu. Name dropping!!! Mtonye kimya kimya bila ya sisi wengine kujua.
 
FMES na wengine tuwapeni moyo hawa mawaziri under40, kuwa waziri katika nchi kama tz kuna changamoto nyingi.

Kuwa waziri under 40 peke yake sio tiketi ya kupata support hapa JF. UKifanya kazi yako vizuri utapata support ya kumwaga hapa JF (kama hujui hili muulize Mama Malecela). Ukifanya mambo kama Nchimbi usitegemee kupata pass hapa.

Anaesema mawaziri fisadi, sindo wabunge waliochaguliwa, hawa wote wameingia bungeni kwa kura. mie niko mwalugesha na udiwani wangu unanitosha.

Hata Lowasa alichaguliwa kuingia bungeni kwa hiyo hii sio issue hapa mkuu. Kuchaguliwa hakumaanishi kuwa wewe ni safi kwani hata Kibaki na Michuki kule Kenya nao wanachaguliwa na wapiga kura.

Namshauri masha anahitaji kuwa na assistant mzuri na aandae press zake kwa umakini, akumbuke yeye sasa ni Home Minister.

Naona Masha anataka file lake la AFGEM lifunguliwe hapa ili kusafisha au kuonyesha ufisadi wake na kampuni zake. Huu ni mwanzo tu ila kilio changu kiko kwa Kikwete na Masha kuwa waruhusu uchunguzi huru ufanyike dhidi ya Deep Green na Tangold kama kweli wao ni wasafi na watanzania wajue ukweli kuhusu nchi yao.
 
Masha sio mmiliki wa IMMA
Naona unataka kupindisha ukweli soma website ya IMMMA utaona ukweli kuwa ni mmoja wa wamiliki ila kasitisha ukurugenzi yuko sabbatical. Kama ulivyokiri kuwa ni rafiki yako mwambie asichanganye biashara na siasa. Kateleza ile mbaya.
Kuhusu umahiri wake katika kazi ya uwakili na biashara( Karamagi naye alisema amebobea kumbe...) siujui ila nijuacho watu wengi walipoteza pesa walizowekeza TOL walipojilist DAR Stockexchange kwani TOL ilitoa taarifa za uongo kuhusu hali yake kipesa (financial status) yeye akiwa company secretary. Malima alipoteza kazi na TOL haijatengamaa.
Kuhusu kuteuliwa kwake uwaziri ni ridhaa rais Kikwete ambaye sasa ile kauli yake ya kutenganisha siasa na biashara ndani ya serikali yake ni changa la macho kwetu.
Ni siri ya wazi kuwa Kikwete alianza kujitayarisha kugombea urais tokea 1995 baada ya kushindwa kuteuliwa. Sasa kama Masha hakuliona hilo, inatia wasiwasi uwezo wake wa kuamua mambo ya mbele katika wizara hiyo nyeti kutokana na current trends.
Vema rais akatekeleza kwa dhati anachokisema, sioni tatizo wafanyabiashara kuwa wabunge, lakini kuwepo kwenye executive arm si sahihi endapo hakuna strong balance and checks kama ilivyo hapa kwetu. Leo hii kama kuna maamuzi yatakayo athiri kampuni za madini kama Barrick, ambazo IMMMA ni washauri wao, je Masha ataacha kulinda maslahi ya kampuni yake? Mawaziri wa namna hii wanakuwa ni kama Lobbyists waliopo Capitol Hill ndani ya serikali.
Umri wake si tatizo unatosha kabisa after all life expectancy ya waTZ ni miaka 45. JKN alikuwa waziri mkuu akiwa na umri wa miaka 30 tu, tofauti mission critical anayokuwa nayo kiongozi mhusika.

<b>MASHA come clear on this!!!</b> acha danganya toto.
 
mkuu wangu ndio maana ninasema kuwa Masha ameteleza, kwa sababu hata IMMA yeye hakuwa na nafasi kubwa hivyo ya kuweza hata kuizungumzia au kuiwakilisha, ndio kuteleza kwake ninaamini alitumia emmotions zaidi ya busara,

kilichoniingiza hii topic ni pale mkuu mmoja alipomshambulia bila sababu za msingi, lakini kama kichwa cha habari kingekuwa unavyosema sasa, wala usingeniona nikimsimamia mkuu, kma swali ni hilo unalouliza sasa, basi ni valid question, lakini sidhani kama yeye ndiye wa kujibu kwa sababu kule IMMA hakuwa na hiyo position ya kuweza kujibia kwenye media.

Halfu ufisadi wa IMMA, bado haujsemwa isipokuwa umesemwa wa patners wawili waliotajwa kwa majina, labda hawa ndio waseme wanachojua kuhusu kuhusika kwao, na IMMA kama ilihusika.

Mkuu Sijaelewa hapa

Katika gazeti la mwanahalisi linasema kwamba Masha ni mwanzilishi na mmiliki wa IMMA.

Na kwamba baada ya kugundua amesema hivyo aliharakisha kusema kwamba kwa sasa amekabidhi majukumu.

Na kwamba ni Mmmojawapo wa wakurugenzi.

Sasa Mkuu unamaanisha hizi sentensi si za kweli?
 
Jamani wadau naomba na mimi niingie jamvini nichangie huu mjadala,japo nawaomba mnielewe sana kwa tafakuri jadidi ya kile nitakachoeleza.
Kwanza kabisa nakuomba mkuu kubwa jinga utoe hiyo picha hapo,yaani picha uloitumia inayomwonesha lowasa hapo kwani true reflection yake inatafsiriwa kama defamation(slander) kwa huyo jamaa,usije ieletea jf matatizo bure.Labda ukitaka kukwepa liability tafuta kikatuni chake lakini sio pseudomatic photo kama hiyo.Anyway huu ni ushauri tu.

Pili,mimi nimebahatika kusoma na huyu bwana Ridhwani high school na pia university kwenye faculty moja huku tukifukuzana madarasa.Kuhusu ufisadi naomba niiri wazi kwamba kwa huyu kijana siujui,ila nachofahamu kwake ni kwamba ni mtu asiye na makuu anayeweza kuinteract na mtu yeyote yule.Hata alipokuwa mkwwa ni watu wachache sana waliojua ni mtoto wa jk waziri wa mambo ya nchi za nje.Tulijua tu kwa kuwa alikuwa anafanana naye na jina la ubini wake.Sote tulikula DH na hakutumia cheo chake.Ila cha ajabu wale waliojua ukweli kuhusu yeye walikuwa wanajitahidi kujipendekeza sana wakati yeye hana mpango.Sawa navyomjua wakati huo labda sio sasa kwani watu wanabadilika.

Vivyo hivyo alipokuja mlimani kitivo cha sheria hakubadilika bado aliendelea kuwa social na mtu asiye mjivuni,kila mtu alimahamu na hadi alipewa ungozi kuwa mwenyekiti wa kitivo cha sheria kwa tiketi ya daruso.Kama kawaida cha ajbu hapa kuna watu walijikomba sana na kujitafutia sifa toka kwake lakini yeye hakujali,akiwamo rais wa daruso wa wakati huo aliyeamua kumpa uwaziri wa mambo ya nchi za nje wa daruso ili afanane na baba yake.Wakina beno malisa wanajua jinsi walivyohusiana na ridhwani.

Kuhusu uwezo wake kimasomo,si kweli kwamba alikuwa na uwezo mkubwa sana kama masha anavyodai.Alikuwa na uwezo wa kawaida tena naweza kusema ni wa chini,kwani supp alikuwa nazo kadhaa hivyo kufanya GPA yake isiwe ya kutisha sana.Hata hivyo kuefli mitihani au kuwa na uwezo fulani ni kitu cha kawaida tu kwa mwanafunzi kwani uwezo wa mtu hautegemei yeye ni mtoto wa nani.Nachojua mimi IMMA huchukua watu cream sana.Tena ukiomba internship pale mnapigwa hadi pepa ikiwa ni pamoja na wao kuomba matokeo toka kitivo cha sheria.Bahati nzuri niliwahi kuwa mjumbe wa bodi ya faculty inayopitisha matokeo hivyo suala la matokeo si geni kwangu.IMMA mara nyingi huchukua watu wenye first class na wakiwakosa sana sana watawachukua wenye upper second ya point 3.7 mwisho.Na wakikosa kabisa huchukua waganda kwani wao kiingereza kinawasaidia kuwaondosha watanzania kwenye kinyang'anyiro.Ridhwani hakuwa na first wala second class upper na wala kiingereza hajui sana tena alikuwa anababaisha tu hadi tunacheka kwenye vikao vya bodi.Hili nalo si tatizo kwani wengi pia hatujui,tunabwabwaja tu,lakini alichukuliwa IMMA.Vigezo walivyomchukulia wao wenyewe wanavijua na havikofixed wanaweza kuvubadili hivyo sitawaingilia sana huko.Sasa kama navyosema aliyejipendekeza hapa huenda ni hao jamaa lakini sio bwana mdogo,kwani wao huenda azma ya baba yake walikuwa wakiijua mapemaaaaaaa.
Kuhusu wanasheria jamaani,hapa mtajadili wee lakini tutajadili kitu ambacho hatukifahamu.Mwanasheria anaruhusiwa kumtetea mtu yeyote hata kama amekiri mbele yake kwamba kweli aliua na hata kama alimwona akiua ili mradi mwanasheria huyo hakuitwa kama shahidi mahakamani.Vilevile hata kama kampuni ni ya kifisadi au vinginevyo,bado ina haki ya kutetewa kisheria na kupata egal services zote,kwani izo huwa ni tuhuma zisizothibitishwa.Na kwa tanzania hatuna sheria inayomkataza wakili kumtetea au kuisajili kampuni yeyote ile,kwani kanuni ya kisheria inayotawala biashara inasema "buyer be ware" caveat emptor hivyo wewe unayeingia makataba na mwizi ndio unatakiwa kuwa makini,kwani kampuni kama richmond inapokuja tanzania,ni vigumu mwanasheria kujua itakuwa ya kitapeli au la,yeye anaisaidia usajili anapokea mkwanja wake basi mkataba na hiyo kampuni inaisha.Ni kazi ya wanasheria wa serikali kuchunguza mtu wanayeingia naye mkataba.

Hivyo basi sheria zinazotawala uwakili tanzania ni moja au mbili tu, ADVOCATES ACT na Tanganyika law society Act.Wanasheria wanabanwa na professional ethics ambazo kwa ufupi zinawakataza wasijitangaze,na ndio maana huoni matangazo yao redioni,au kwenye bill boards,wasiende kusolicit biashra yaani wasijipigie debe ama kupigiwa debe(tauting) wala wasiingie njama na mteja kumdhuru mteja mwingine (champerty) na vilevile kanuni kama vile kuvaa suti,joho kuheshimu mahakama n.k ndizo zinazowabana.Na mwisho na kubwa sana ni rule agaisnt conflict of interests. Kwa mana ya kwamba mwanasheria huwezi kuwatetea wateja wawili wanaopingana,huwezi leo ukaisajili richmond afu kesho ukawa unaishtaki au unahusika katika uchunguzi wake.Wala huwezi kutengeneza mkataba fulani halafu kesho wewe mwenyewe unakuwa wakili wa upande mwingine unaopinga makataba huo huo.Au kama masha huwezi kuwa waziri wa mambo ya ndani halafu idar yako ya polisi inaichunguza deep green ambayo wewe ulihusika kuisajili.Unatakiwa uachie ngazi kumoja ili uruhusu uchunguzi huru kwingine.

Kutokana na mwanga wa maelezo haya,sasa nadhani tunaweza kuona kuna upungufunupi katika sheria za mawakili na maadili yao,suala zima la ridhwani na mambo mengine yanayohusiana na sula hili,maswali maoni welcome
 
So far so good. Ila tu tahadhari yetu ileile kwamba hakuna haja ya kuvalisha label; tujenge hoja. Sasa mtu akionekana anamtetea Masha asionekane aliwahi kushikwa mkono na Masha. Vilevile kwa yule anayempiga madongo asionekane anamchukia.

Kilichowazi hapa ni kwamba watu wengi, at least hapa JF, inaonekana wana imani na Masha na wangependa afanye kazi yake vizuri. Nami ni hivyohivyo, nafikiri kwamba katika viongozi tulio nao huyu bwana anaweza kutusaidia. Japokuwa yupo katika mazingira hatari katikati ya jalala la taka, bado ana nafasi ya kuweza kushinda majaribu na kuchapa kazi. Record yake ya huko nyuma ni clean sana: amepata elimu yake katika utaratibu sawia kabisa (sio kama wenzake walioamua kupitia shor cut), he is an intelligent chap, amefanya kazi zikaonekana, hana historia ya kuchipatia mali kwa njia ya mkato. Anachotakiwa sasa awe makini, achape kazi, acheze siasa ya kimaadili-hii itampa heshima sisi ambao tupo the other side of the political spectrum, tutampa heshima kama kiongozi wa nchi. Lakini kama mtindo wenyewe ndio utakuwa huu wa kuwatetea akina Ridhiwani unecessarily and out of context, I see tutakabana mashati.

Hope shule iliyotolewa kwenye hii thread itamfikia mheshimiwa Masha na wanasiasa wengine tunaowategemea katika CCM including Ezekiel Maige.
 
Masha hashabihiani na Lowasa hata chembe, EL kawajibika kwenye uwaziri mkuu. Ubunge wake uko palepale. Kumhusisha masha na wateja wa immma, niufinyu wa fikra, ukitizama profile za partner wake nikweli Masha hakuwa na ubavu na hakustahili kuwa msemaji. Inawezekana ulimi uliteleza tu, ndio kwanza anaanza kuwa mbele ya press. Kwani kampuni ya uwakili inawajibikaje kwa mteja wake?

Haya ya bot ni babies wa balali, mgonja, mramba na megji msitafute wachawi wapya.
 
Back
Top Bottom