Minister belittles link with JK's son

Minister belittles link with JK's son

Kinyambis,

Heshima mbele mkuu, unazozisema ni mbinu za capitalism, sio ujanja wa mjini wajanja wa mjini huwa hawaendi shule na kuwa wanasheria, na kufungua ofisi nzito ya kuheshimiwa na taifa zima, I mean sema tuhuma lakini usiwashuhse hadhi watu wazima kiasi hicho mkuu.

so far siioni chrge kwenye maneno yako,

baadaye!
 
Mkuu ustaafu ni marupu rupu sio maneno matupu, hata Maalim Seif ni mstaafu mkuu, huyo AG wa ZNZB haelewi anachosema, ninajibu kwa kuwa Mheshimiwa Mwafrika Wa Kike, ameniomba, yeyote aliyewahi kuwa waziri mkuu hupewa hata kama amefukuzwa, ,ni bunge tu linaweza kuamua tofauti.

Location yangu haijawahi kuhusika na mawazo yangu, ninajua ulipo lakini siwezi kusema hapa maana ni against the rules.

Hii hoja ni Masha na Ridhiwani, ukitaka mengine yafungulie topic,

naona umeanza kubadili majina yako mkuu, see yah!

Mkuu umesoma pale juu hoja ya Kinyambiss ?
 
haya naona mapya sana na hadi naona nami niingie niseme jambo ambalo nafikiri nalifahamu na ningependa wana jf tuchangie mawazo.ninazungumzia kuhusika kwa huyu ridhiwani maana ni muendelezo ambao leo tunao.

kwanza niwape pole watanzania kwa haya wanayoyaona ya ufisaidi ambao magazeti na vijiwe vyetu vimeamua kuweka wazi huku tukisubiri report za ukweli toka kwa wale tuwaitao wasema ukweli. mie sijui kama ni waandishi wa magazeti, kamati za bunge au mwanangu mwakyembe.

jambo langu , ni kwanza nimuweke sawa huyu aliyepost thread hii. inaonyesha kwa upande wake hajafurahishwa na ridhiwani kupata kazi hapo immma na yeye kuachwa. lakini nataka nijue je kwani ni lazima kuajiriwa wewe na yeye aachwe na pengine nani mwenye maamuzi ya kuajiri katika sekta binafsi?

la pili ambalo nataka mnisaidie kimawazo, inakuwaje tunazungumza ufisaid kwa kuhisi. mie nataka nijue , ni wakati gani mtu anaweza itwa fisadi na ni vipi iwe fisadi bila kuwa na vigezo na kama vigezo vipo ni kwa vipi ridhiwani anahusiana navyo.

mie nachukia sana uharamia lakini pia ninasimama katika misingi ya haki, ambayo siku zote inasisitiza kuwa ..........hukumu mtu baada ya kuridhika na ushaidi wa kutosha uliotolewa kwamba amefanya kosa fulani.....! inakuwaje leo hii tunasema fisadi na ushahidi hatuna.kama munao ni upi ambo unamuunganisha kijana huyu ,naomba tuuweke wazi.

(nazungumzia kipande hapo juu).....mfano ndg johnson lukaza tulipomuhusisha na ufisadi , nafikiri ni kwa sababu yeye ndiye mmiliki wa kampuni ya proin na kwamba anahusika moja kwa moja na shughuli zote za kila siku za kampuni yake na kiasi kama kile cha fedha kinapoingia ni nlazima hajue.leo hii inakuwaje kwa kijana huyu.

jengine ambalo linanitatiza ni kuhusiana na haki za msingi ambazo mtu anakuwa nazo katika jamhuri hii ya tanzania. ninaanza kuona kwamba tunaweza kuwa na mambo ambayo sio ya kawaida. ukiukwaji wa wazi wa ibara za katiba yetu ya jamhuri ya muungano unaanza.yawezekana vipi mtu asiwe na haki ya kufanya kazi kama inavyopingwa na ibara ya 11 ya katiba yetu?

mh. waziri ameeleza kwamba huyu bwana aliingia kama intern na baadae wakamuajiri. sasa nini tatizo wakati unaambiwa kwamba ni sera ya kampuni kuajiri huku kipaumbele kikitolewa kwa wale intern .nashindwa elewa kwamba watu wana lalamika kuwa kaajiriwa pale...nyie mlitaka nini?

ni vigumu kuwaelewa au kuwaeleza lakini wengi mnajua tunao uhuru wa kutoa mawazo lakini sio kuhukumu moja kwa moja au kutoa tafsiri ya jambo.ukweli ni kwamba ridhiwani anafanya kazi immma kama muajiriwa na immma ni kampuni ambayo inawaajiriwa wengi zaidi ya 20 na maboss zao ni wako wanne. hakuna shaka katika ili kwamba anafanya kazi lakini sidhani kama kufanya kazi pale kunaweza mfanya naye fisadi. kama hii ni maana basi tuangalie BOT,Wizara ya maliasili na utalii, wizara ya miundo mbinu,n.k.waajiriwa wote pale ni mafisadi.

hivi huyu kijana anatakiwa afanye nini?maana akifanya jambo lolote mtasema. hadi lini.basi tumsaidieni mawazo nini afanye?

kweli inasikitisha ndg zangu maana sasa itabidi watu tuanze angalia kampuni ambazo hazina historia ya ufisadi bila kuangalia namna kazi inavyo fanyika. vigumu kutambua lakini inawezekana kabisa.

mwisho nisingependa kwenda kwenye sheria maana mie sio mwanasheria ila nataka sema kitu kimoja. ninavyojua mimi,moja ya kazi ya wanasheria ni kusajiri kampuni na pia kulipwa gharama fulani za kazi baada ya usajiri. mh. waziri amezungumza wazi na kwamba sidhani kama kuna tatizo.kama lipo nafikiri tumtafute yule mwengine alisemwa kuwa ni msimamizi au muongeaji wa kampuni, atayasema. vipi kuhusu kuhusika kwao.

ninavyofikiri au kushauri mimi haipendezi kufanya personal attack kwa mtu.ukweli wa mambo utajulikana.

lakini pia tusisahau kuna usemi wa wahenga unasema......chokochoko uzaa jambo.tusikilize nini kinakuja.

nakaribisha mawazo .aksante sana.

Mhhh, regarding this....Only TIME will tell.
 
Sasa naona JF inapoteza mwelekeo wake. Hivi mtoto wa rais akiendesha BMW X5 ni swala la ajabu?... hivi mlitaka aendeshe gari gani ikiwa baba yake ni rais achana na yeye kuwa na kazi. Nina hakika kila gari ataklalo endesha litazua hoja iwe VW watasema mtoto wa rais kachoka, kabuntas na hana maana.

Kabla hamjamuhkumu Masha kwanza tazameni sheria ya nchi kama inapingana na yote anayoyafanya. Hadi sasa hivi sijaona mahala Masha akitia tobo pakacha letu la Uchumi na kisheria Conflict of interest ndani ya serikali sio kitendo haramu..imeruhusiwa na Azimio la Zanzibar, nje ya hapo tuonyesheni ni wapi Masha katumia madaraka yake vibaya.
Kuhusu Ajira hilo wazi iwe Bongo hata Ulaya, watu huvutana ikiwa una qualification zinazotakiwa.
Ridhwan pamoja na kwamba yawezekana hana kichwa cha darasani lakini ni mchapa kazi mzuri na pia kama mtoto wa rais huwezi shindana naye unless utakuwa ktk dunia ya Wagagagigikoko.

Ndugu zangu kuna wakati ni lazima tukubali reality kwani dunia hii haimsubiri mtu. Zipo madamuhimu sana kwa maslahi yetu sote lakini uchambuzi wa mtu kutokana na influence zaye hapo mkuu utakuwa wataka kunambia matumizi mabaya ya Binadamu wote sawa, the fact is hatuko sawa.
 
nimetizama autorec bei ya x5 ni us$4500 fob, sidhani kama inaweza kufika 70m baada ya kuisajiri bongo, labda kama nayeye walitizama seat belt, ingekuwa hammar sawa.

sasa naamini dar kunawatu wanaroho mbaya, kuongea na simu inakuathiri nini? kama kalipia tigo extrime siajimwaye tu. yaani kuendesha mtumba inakuwa issue, mnunulieni bajaj roho zenu zisuuzike, dt dobie kuna used benz s-series 12m tu.

kuwa ofisi moja hakumaanishi namaisha mlingane, kama dogo anaweka kadhia yake vizuri anaweza kuukwaa huo mchuma bila kutegemea baba yake.
 
Wakuu,

Kwa faida ya mjadala, naomba tuongezee na mengine. Masha alipoingia UDSM alikuwa na miaka kama 16, je alikuwa na qualifications zipi mpaka kumfanya ajiunge na sheria UDSM?

Inasemekana angebaki USA ingebidi atumie miaka mingine mitatu kabla ya kusoma sheria university, hivyo kuja Dar ilikuwa ni kutafuta njia za mkato. Je kwa wenye ujuzi na elimu za USA uvumi huo ni kweli?

Mimi namfahamu Masha toka mlimani na mwanzoni nilikuwa namjua kama Mmarekani, wakati sisi tunatoka jeshini tukiwa hoi bin taabani, tulimkuta yeye na Wamarekani wenzake wametulia na kunawiri tayari kuanza masomo.

Je Masha alikuja kusoma UDSM kama Mmarekani au kama Mtanzania? Kama alisoma kama Mtanzania, aliwezaje kuingia UDSM bila ya kupita JKT? Wakati huo ilikuwa lazima uonyeshe vyeti vya JKT. Hata waliosoma nje nao ilikuwa lazima wapitie JKT kabla ya kuingia mlimani.

Nimesema haya kwasababu katika hotuba zake huwa anasema ni uzalendo ndio ulimfanya aje asome bachelor mlimani, wakati ukweli huenda ni tofauti kabisa. Kama ni uzalendo, ni nini kilimzuia kwenda JKT?

Inatakiwa Masha awe mkweli, vinginevyo kutka kuhalalisha uwongo kunaweza kumwingiza matatizoni zaidi.

Binafsi naona ni nafuu yeye kuliko hao wengine, lakini pia asianze kujikanyaga kanyaga kwa nia kujisafisha hata mahali ambapo mambo yanaonyesha wazi kuna tatizo. Hili suala angewaachia jamaa wa IMMA wahangaike nalo na sio yeye kuingiza kichwa chake.
 
1. Mkuu Mugi, karibu tena baada ya kupotea sana na hili jina.

3. Masha, kuzungumzia IMMA, akiwa waziri hilo ameteleza period, angewaachia IMMA wenyewe wajibu, kwenye hilo nimezungumza naye jana ni off the line, lakini haimfanyi awe fisadi au un-qualified kuwa waziri, lakini ni makosa.

4. Mimi sio fisadi na wala sina urafiki na mafisadi, lakini siko hapa kuwahukumu tu viongozi bila ukweli, Masha sio fisadi, amekuwa amekuwa director Oxygen akiwa na miaka 28, ambapo angeweza kufanya mambo mengi ya ajabu kama kweli ni fisadi, Masha sio mmiliki wa IMMA, the matter of fact yeye ni mmoja wa wale waliokuwa chini kwa kipato pale IMMA, kulinganisha na wenziwe, lakini kama kuna wenye ukweli wauweke hapa uchambuliwe, lakini so far sijaona convincing dataz, lakini walionazo waziweke hapa.

Ahsante Mkuu.

Mkuu FMES

Fair enough!!!............kwa hayo hapo juu....

Mkuu Muggy Ndg yangu karibu tena
 
Naona hii topic imeanza kuyumba kidogo... basi ni hivi.

. Lau Masha, Mujuluzi, Ishengoma, Magai... wajanja wa mjini. Kwanza wanafahamiana na JK long time. Ilikupata vi consultancy vya serikali firm nyingi huwaweka watoto wakubwa... Pale mkono yuko mtoto wa maghembe,step daughter wa Malecela, Rex walikua na mtoto wa Kimei, wengine wanakamata watoto wa Majaji n.k. Ndio bongo ilivyo. Yule JKjr ni mtu mmoja ambae yuko very weak kielimu, hajui hata kuongea in an articulate way. He really is nothing special kama mwanasheria au mwanafunzi. Jamaa walimrecruit zamani wakijua baba yake atakua Rais. Anaendesha BMW X5, which costs on average 60-70 million(used tena) (anatabia yakujifanya anaongea na simu all the time akiwa kwenye gari... which is funny)Ameanzaje kazi na kupata hela yakununua ile gari in one year??? Nnamfahamu jamaa mwengine yuko pale kama advocate.. JOse... hana hata prado....yuko senior kuliko huyo dogo. Jamaa hajui chochote kuhusu deep green, hilo dili la watu wazima wameshirikiana na IMMMA partners,kulicheza. mimi ni lawyer, yule dogo sio partner wala nini... tena aliletwa hk UK traineeship na partner firm moja inaitwa DLA Piper Rudnick Gray Cary UK LLP.

Wamempa x5,atese, wao wawena skio la mzee. maisha yanaendelea.
Watuwengi wasiokuwa na access yakirahisi ma muungwana wanawatumia watoto na watu wengine wakaribu kumpelekea proposals za madili,lakini in this case hawa jamaa wajanja wanajiwekea uhakika na rafiki yao aliye juu sana asije akawasahau.swala zima ndio hilo.Huyu sidhani kama anahusika na deep green,and even if he did, basi ni very initial stage.. lakini i doubt it.

http://www.immma.co.tz/index.html

HILI LA KUWA RK NI KILAZA DARASANI PIA NIMELIPATA RELIABLY..HATA PALE MLIMANI WANASEMA VC WA SASA ALITUMIA INFLUENCE YAKE KU SHAPE TRANSCRIPT YAKE ILI AINGIE HULL...ANYWAY KUNA TOFAUTI YA AKILI ZA DARASANI NA UTENDAJI ..SOME ARE BEST IN CLASS AND WEAK WHEN IT COMES TO REAL LIFE.....SIDHANI KAMA BABA YAKE KWENYE CLASS YA 1975 ALIKUWA BEST STUDENT..BUT HE IS OUR PRESIDENT NOW...

JUZI ALIFANYA MTIHANI WA BARSHIP ..ILI AWEZE KUWA REG LAWYER WA MAHAKAMA ..SIDHANI IMEKUWAJE NA KAMA AMEFAULU...MAANA KULE NI ORAL NA HAWANGALII MAKUNYAZI...AMUULIZE DR HUSSEIN MWINYI..KWANINI ALIWAKIMBIA TANGANYIKA DOCTOTS BOARD WAKATI WA URAIS WA BABA YAKE...WALIKATAA KUMSAJILI KIULAINI ALIPOTOKA TURKEY .....SIJUI NAYE LIISHIA WAPI NA USAJILI WAKE....ALISOTA KAMA WENGINE!..THATS WHY I LIKE THIS PROFFESSIONAL BODIES ..HAWAPENDELEI.....

HUWEZI KUMFANANISHA TRAINEE RK NA WAKILI FATMA KARUME ...YULE DADA YUKO FITI KICHWANI..NA ANAJUA KUCHEZA NA UWAKILI..KAMA INAVYOTAKIWA...HATA MIMI NINGEKUWA NA KAMPUNI YA UWAKILI NINGEFURAHI KUMUAJIRI AU KUWA NAYE PARTNER..

LAKINI ALL IN ALL ELEWENI WATOTO WA WAKUBWA NAO WANA HAKI YA MAISHA BINAFSI IKIWEMO KUJIPATIA RIZKI KWA JASHO LAO BILA KUDHANIWA KUWA KILA WAKIPATACHO LAZIMA KIWE NI KWA AJILI YA MAJINA YA BABA ZAO.....THEY CAN BE THEMSELVES!!!!
 
Mtanzania huyu jamaa mbona mnazidi kumfunua, duh imebaki nanihi tu kila kitu kitakuwa nje, mama yangu, nilikuwa siyajui haya yote!

Mkandara: issue hapa nafikiri sio kumuonea wivu mtoto wa Rais kuendesha gari nzuri, hii sio issue hata kidogo. Watu wanahoji ushiriki wa mtoto huyu wa Rais wetu katika makampuni ambayo yamekuda mahela ya walipa kodi kule BOT, upo hapo ndugu yangu? Hayo mambo ya magari mbona watu siku hizi walishapita huko, tena wabongo siku hizi hawana kabisa huo wivu, unaweza hata ukatembelea ndege katikati ya mji na watu wataendelea na hamsini zao wala msukuma mkokoteni hatageuki kupoteza muda wake. Tatizo linakuja pale watakapogundua umeiba hela zao kununua hiyo ndege. Sasa wakulaumiwa hapa sio JF; wamlaumu Dr Slaa aliyewafundisha watu kuchukia ufisadi!
 


LAKINI ALL IN ALL ELEWENI WATOTO WA WAKUBWA NAO WANA HAKI YA MAISHA BINAFSI IKIWEMO KUJIPATIA RIZKI KWA JASHO LAO BILA KUDHANIWA KUWA KILA WAKIPATACHO LAZIMA KIWE NI KWA AJILI YA MAJINA YA BABA ZAO.....THEY CAN BE THEMSELVES!!!!

Kwani mzee kuna mtu amekataa hili, hii ni sawa kabisa. Ndio tunachotaka, yaani hatutaki mtu apate au akose kwa sababu ya kuzaliwa na mtu fulani. Tunataka nafasi ya maisha ya kila mtu itokane na uwezo na potential alizopewa na Mungu na bidii yake. Kinachogomba ni pale ambapo hali haiwi hivi na usitake kuniambia kwamba hujui kwamba watoto wa wakubwa katika nchi yetu wanapata mteremko kuliko akina sisi. Haya hebu tupe maelezo ya kwa nini wale watoto 13 wa wakubwa wote wamejikuta wanafanya kazi BoT? Unataka kuniambia watoto wa wakubwa wana genes za kuwawezesha kufanya kazi za mahela tu tena BoT na sio ualimu, upolisi, n.k.?
 
Haya mafisadi mie najichekea tu,maana mambo yanavyoumbuka humu.Na hii nayo kali,nakumbuka kitabu kimoja sijui mtunzi ni nani yule kinaitwa "shetani msalabani"Hebu angalia hizo attachment.LOWASSA MSALABANI,NA KINGUNGE NA WIMBO WAKE
 

Attachments

  • Golgota%21[1].jpg
    Golgota%21[1].jpg
    16.2 KB · Views: 62
Nadhani watu wameshinda kuunganisha yanayosemwa kwa kuangalia suala la Ridhwani na Masha. Ukienda kwenye original story na kurudi mbele kuna kitu ambacho unaweza kukisoma katikati ya mistari. Hebu kwa dakika chache tumtoe Ridhwani kwenye mjadala na tuangalie baadhi ya Facts:


DEEP GREEN FINANCE COMPANY:

Wamiliki wake wa kwanza ni watu wa Afrika ya Kusini na kutoka Bongo wana hisa wa kwanza ni:

Protase Ishengoma na Stella Ndikimi ambao ni mawakili wa IMMA

Kampuni hii imejitaja kuwa ni kampuni ya "Finance" lakini haikuwa kwenye orodha ya makampuni ya fedha ya Benki Kuu.

MwanaHisa mwingine ni Aloysius Mujulizi ambaye ameteuliwa na Rais Kikwete kuwa Jaji

Mwanahisa mwingine na Lawrence Masha ambaye siyo tu anachaguliwa kuwa Waziri bali anapewa Wizara ya Mambo ya Ndani (yenye kusimamia jeshi la polisi na magereza)..

TANGOLD

IMMA Advocates ni mawakili wa TANGOLD (by default Ishengoma na Ndikimi pia)

Wakurugenzi humo ni pamoja na Andrew Chenge, Gray Mgonja, Patrick Rutabanzibwa,


Sasa angalia hapa: (toka mkutano wa ushirikiano wa vyama vya upinzani)

Mnamo tarehe 18 Machi 2004 ilianzishwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. kwa madhumuni ya, pamoja na mengine, kufanya biashara kama ‘mabepari’ na wakopeshaji fedha! Kufuatana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakurugenzi wa Deep Green Finance walikuwa ni mabwana Mark Ross Weston wa New Zealand; Anton Taljaard wa Afrika Kusini; na Rudolph van Schalkwyk pia wa Afrika Kusini. Wote watatu ni wakazi wa Afrika Kusini na wanaelekea kuwa ni maafisa na/au wafanyakazi wa Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini. Kufuatana na taarifa za BRELA, wanahisa wa awali wa Deep Green Finance walikuwa ni mawakili Protase R.G. Ishengoma na Stella Ndikimi wa kampuni ya mawakili ya IMMMA Advocates; Nedbank Ltd., Nedbank Africa Investments Ltd. na SBM Nedcor Holdings Ltd. Tarehe 15 Aprili 2005 mawakili Ishengoma na Ndikimi walihamisha hisa zao kwa Nedbank Ltd. na Nedbank Africa Investments Ltd. IMMMA Advocates vile vile ni mawakili wa Tangold Ltd. ambayo imehusishwa na ufisadi tuliouelezea katika Orodha ya Mafisadi.

Taarifa za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba tarehe 1 Mei 2004, Deep Green Finance ilifungua Akaunti Na. 011103024840 katika tawi la Corporate la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Dar es Salaam. Kitu cha kwanza cha kushangaza ni kwamba siku hiyo ilikuwa ni Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) na ilikuwa siku ya mapumziko. Kitu cha pili cha kushangaza ni kwamba kampuni hii iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti hiyo bila ya kuingiza wala kutoa fedha yoyote kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzia tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 31 Julai 2005. Kitu cha tatu cha kushangaza ni kwamba pamoja jina la Deep Green ‘Finance’ kuashiria kwamba kampuni hii ni taasisi ya kifedha, orodha ya taasisi za kifedha iliyotolewa na BOT tarehe 21 Agosti 2007 haionyeshi kwamba kampuni hii imewahi kusajiliwa na BOT kama taasisi ya kifedha!

Hata hivyo, kwa kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 1, 2005 kampuni hii ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka Wizara ya Fedha na/au BOT. Fedha hizo zilitolewa kwa utaratibu ufuatao:

(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 241740, ilihamisha dola za Marekani 1,354,167.26 au shilingi za Tanzania 1,546,778,770.92 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku hiyo hiyo fedha hizo zote zilichukuliwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa utaratibu maalum wa haraka (special clearance) na kupelekwa mahali kusikojulikana na kwa madhumuni yasiyofahamika;

(b) Tarehe 1 Septemba 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 015558, ilihamisha dola za Marekani 1,827,137.44 au shilingi za Tanzania 2,083,255,881.60 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku hiyo hiyo jumla ya shilingi 2,083,333,333.33 zilichukuliwa kwa mara nyingine tena kwa kutumia utaratibu huo huo maalum wa haraka na kupelekwa kusikojulikana;

(c) Tarehe 8 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha dola za Marekani 100,256.62 au shilingi za Tanzania 114,611,746.80 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Itakumbukwa kwamba Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni iliyoandikishwa nchini Mauritius tarehe 5 Aprili 2005 na kupewa Cheti cha Kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006. Hata hivyo, mawaziri kadhaa wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wameendelea kudai kuwa kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Tanzania. Wakurugenzi wa Tangold Ltd. ni Gavana Daudi Balali, Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, Katibu Mkuu (Fedha) Gray Mgonja, Katibu Mkuu (Maji) Patrick Rutabanzibwa na Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu) Vincent Mrisho. Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa BOT ya tarehe 21 Desemba 2006, Tangold Ltd. ililipwa na BOT dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kupitia akaunti isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini na kwa madhumuni yasiyojulikana;

(d) Tarehe 16 Septemba 2005 jumla ya shilingi 129,000,000.00 zilitolewa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance na kuwekwa kwenye akaunti ya muda maalum (FDR);

(e) Tarehe 3 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 2,083,333,333.33 za Wizara ya Fedha zililipwa kwa utaratibu maalum wa haraka kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Inaelekea fedha hizo zililipwa kabla BOT haijaingiza fedha yoyote kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa vile tarehe 4 Oktoba 2005 BOT ilihamisha dola za Marekani 1,789,075.89 au shilingi 2,083,891,765.35 kwenda kwenye akaunti hiyo;

(f) Tarehe 8 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 39,761,397.98 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda Tangold Ltd.;

(g) Tarehe 31 Oktoba 2005 jumla ya shilingi za Tanzania 2,083,333,333.33 fedha za Wizara ya Fedha zilihamishiwa kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(h) Tarehe 2 Novemba 2005 dola za Marekani 1,821,095.57 au shilingi za Tanzania 2,083,653,279.68 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(i) Tarehe 30 Novemba 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 2,083,333,333.33 zikiwa fedha za Wizara ya Fedha kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku moja baadaye, dola za Marekani 1,817,199.52 au shilingi za Tanzania 2,184,610,383.04 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(j) Tarehe 10 Desemba 2005 shilingi 100,940,489.71 zilihamishwa kutoka Tangold Ltd. kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Hii ilikuwa ni siku nne tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 14, 2005 kufanyika nchini kote;

(k) Tarehe 19 Desemba 2005, siku tano baada ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, dola za Marekani 88,722.17 au shilingi za Tanzania 104,755,554.09 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(l) Tarehe 9 Februari 2006 shilingi 3,836,800.00 zilihamishwa kwenda akaunti ya mawakili wa Deep Green Finance, IMMMA Advocates, iliyoko benki ya Standard Chartered. Haijulikani kama fedha hizi zilikuwa ni kwa ajili ya malipo ya mawakili hao au la;

(m) Malipo ya mwisho kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance yalifanywa tarehe 22 Novemba 2006 ambapo jumla ya shilingi 14,465,000.00 zilihamishiwa katika akaunti isiyojulikana ya benki ya Standard Chartered na kwa matumizi yasiyojulikana;

Kutokana na rekodi za kibenki zilizoonyeshwa hapo juu, jumla ya shilingi 10,484,005.39 ziliingizwa katika akaunti ya Deep Green Finance katika kipindi cha miezi minne tu kati ya tarehe 1 Agosti na 10 Desemba 2005. Hiki kilikuwa ni kipindi cha mchakato na/au kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 14 Desemba 2005. Aidha, kuanzia tarehe 11 Desemba 2005 hakuna fedha yoyote iliyoingizwa katika akaunti hiyo hadi tarehe 27 Februari 2007 kampuni hiyo ilipovunjwa ‘kwa hiari’ ya wanahisa wake. Ni muhimu kurudia kwamba, kwa ushahidi huu wa nyaraka za kibenki, kampuni ya Deep Green Finance haikuwa na hata senti moja kabla ya tarehe 1 Agosti 2005 na wala haikupokea hata thumni mara baada ya tarehe 10 Desemba 2005 na mara baada ya Uchaguzi Mkuu.

Kwa taarifa za sasa hivi, inafahamika kwamba faili la Deep Green Finance lililotakiwa kuwa BRELA limetoweka. Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hii ilikuwa ni kampuni hewa (shell company) iliyoundwa kwa ajili tu ya kupitishia fedha za umma kutoka Benki Kuu kwenda kusikojulikana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2005. Ndio maana kampuni hiyo haikuwa na fedha zozote benki kutokea tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 1 Agosti 2005, wiki tatu kabla ya kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu. Na ndio maana mabilioni iliyolipwa na Benki Kuu yalilipwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na mara baada ya Uchaguzi Mkuu kupita malipo hayo ya fedha za umma yalikoma.

2. TANGOLD LIMITED

Kama Orodha ya Mafisadi inavyoonyesha, Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni inayomilikiwa na baadhi ya Mafisadi tuliowataja katika Orodha hiyo. Kuna utata mkubwa zaidi ambao umeigubika kampuni ya Tangold Ltd. Kwanza, licha ya nyaraka kuonyesha kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006, nyaraka za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba Tangold Ltd. ilifungua akaunti ya shilingi Na. 011103024852 NBC Corporate Branch tarehe 1 Januari 2003. Kama ilivyokuwa kwa Deep Green Finance, siku ya Tangold Ltd. kufungua akaunti yake NBC ilikuwa ni Siku ya Mwaka Mpya na siku ya mapumziko kote nchini! Aidha taratibu za kibenki za ufunguaji wa akaunti za makampuni zinalazimu kampuni husika kuwasilisha benki nakala ya usajili wa kampuni, Katiba yake, leseni ya biashara na hati ya mlipa kodi ya TRA (TIN Registration Certificate) kabla ya kuruhusiwa kufungua akaunti. Swali la kujibiwa na NBC pamoja na Serikali ni je, ilikuwaje Tangold Ltd. iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti ya benki kabla hata haijaandikishwa nchini Mauritius achilia mbali kupata hati ya kutimiza masharti ya Tanzania?

Pili, kampuni ya Tangold Ltd. iliendesha akaunti hiyo bila kuweka au kutoa fedha yoyote ile kati ya tarehe 1 Januari 2003 hadi tarehe 1 Agosti 2005 ilipoanza kunyeshewa mvua ya neema ya mabilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania kutoka BOT! Mvua hiyo ni nje ya mvua ya dola za Marekani 13,340,168.37 zilizohojiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na iliinyeshea Tangold Ltd. kama ifuatavyo:

(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 4,703,221,229.08 kwenda kwenye akaunti ya Tangold Ltd. Tarehe hii ni muhimu sana kwani ndiyo siku ambayo BOT ilifanya pia malipo ya kwanza kwa Deep Green Finance kama ilivyoelezewa katika Taarifa hii;

(b) Tarehe 2 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 244,428,386.15 kutoka akaunti yake hiyo kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Kama tuliyoelezea katika Taarifa hii, tarehe 1 Septemba 2005 Deep Green Finance ililipwa pia shilingi 2,083,255,881.60 na BOT;
(c) Tarehe 8 Oktoba 2005 shilingi za Tanzania 39,761,397.98 zilihamishiwa kwenye akaunti ya Tangold Ltd. kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(d) Tarehe 12 Oktoba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 1,690,500,000.00 kwenda Meremeta Limited;

(e) Tarehe 23 Novemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 555,300,048.00 kwenda Meremeta Ltd.;

(f) Tarehe 10 Desemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 100,940,489.71 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(g) Tarehe 12 Desemba 2005, siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu, Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 551,060,000.00 kwenda kwenye akaunti ya Meremeta Ltd.

Baada ya hapo Tangold Ltd. haikupokea wala kuingiza fedha zozote kwenye akaunti yake hadi tarehe 6 Juni 2006 ilipohamisha shilingi za Tanzania 220,980,370.00 kwenda ‘TISS.’ TISS ni kifupi cha Tanzania Intelligence and Security Service ambalo ni jina la Kiingereza la Idara ya Usalama wa Taifa! Tangu tarehe hiyo hadi leo hii Tangold Ltd. haijaweka wala kutoa fedha nyingine yoyote katika akaunti hiyo. Kwa maana hiyo, katika kipindi cha miezi minne Tangold Ltd. iliingiziwa na BOT jumla ya shilingi za Tanzania 4,742,982,627.06 na ilifanya malipo kwa Deep Green Finance na Meremeta Ltd. ya jumla ya shilingi za Tanzania 3,363,531,259.67.

Maswali muhimu ya kujiuliza kuhusiana na Tangold Ltd. ni haya yafuatayo. Kwanza, ilikuwaje kampuni ambayo haikuwa hata imeandikishwa kisheria ikalipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi na/au ya umma na bila maelezo yoyote? Pili, ilikuwaje Serikali, kwa kupitia Waziri Karamagi, itoe taarifa ya uongo Bungeni kwamba Tangold Ltd. ni kampuni mpya na imeanzishwa ili kurithi mali na madeni ya Meremeta Ltd. wakati makampuni yote mawili yalikuwa yakipeana mabilioni ya fedha za umma wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu katika mazingira ya kutatanisha? Tatu, kwa nini malipo ya mabilioni haya yalikoma mara baada ya Uchaguzi Mkuu? Nne, kama Tangold Ltd. ni kampuni inayomilikiwa na Serikali je ofisi zake ziko wapi? Watendaji wake wakuu ni kina nani? Fedha za kigeni dola za Marekani 13,340,168.37 zilizolipwa na BOT tarehe 29 Desemba 2005 zilikuwa ni kwa ajili gani na kwa nini zimeendelea kuwa katika akaunti ya Tangold Ltd. hadi wakati huu?

Hivi karibuni baadhi ya wanachama wa CCM wameanza kuhoji matumizi makubwa ya fedha wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Kama mnavyokumbuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku ametoa hadharani barua aliyomwandikia Mwenyekiti wa CCM aliyepita Bwana Benjamin Mkapa akidai kuwepo kwa ushahidi kuwa “fedha nyingi zinatumiwa katika uchaguzi huu.” Na kama alivyohoji Mzee Butiku katika barua yake kwamba “fedha hizo zinatoka wapi na ni za nani”, nasi tunawaomba wananchi wa Tanzania waidai Serikali iwaeleze mabilioni haya ya fedha za umma yalilipwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2005 kwa ajili gani.

Ili kupata majibu sahihi ya maswali yote haya, Serikali haina budi kuridhia kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi wa tuhuma zote hizi na zile zilizotolewa katika Orodha ya Mafisadi. Ni tume huru pekee itakayoweza kuchunguza ufisadi huu bila woga, upendeleo au hila. Na ni ripoti ya tume huru pekee ndiyo itakayotumika kuwawajibisha wale wote watakaobainika kushiriki kulisababishia taifa letu hasara kubwa namna hii.

Tunatambua kwamba Serikali imeteua wakaguzi wa mahesabu kutoka kampuni ya Ernst Young LLP ili kufanya uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma katika akaunti ya malipo ya nje inayoendeshwa na BOT (EPA) kwa niaba ya Serikali. Tunaomba kuweka wazi msimamo wetu kuhusiana na uchunguzi huo kuwa hauhusu ubadhirifu, wizi na/au ufisadi ndani ya BOT tuliouelezea katika Orodha ya Mafisadi na katika Taarifa hii. Vile vile uchunguzi huo hauhusu ufisadi unaohusu kusainiwa kwa mikataba mibovu na ambayo imeliingizia na italiingizia taifa letu hasara ya mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa maana hiyo, tunatoa taarifa mapema kwamba ripoti ya wakaguzi wa Ernst Young LLP haiwezi na isije ikachukuliwa kuwa ndio majibu ya Serikali kwa tuhuma za ufisadi, wizi na/au ubadhirifu wa fedha za umma zilizotolewa katika Orodha ya Mafisadi na katika Taarifa hii. Tunapenda kusisitiza kwamba tuhuma hizi zinaweza kujibiwa tu na tume huru ya uchunguzi.

Kutokana na uzito wa masuala tuliyoyaeleza katika Taarifa hii, tunapenda kuwataarifu wananchi wa Tanzania kwamba iwapo Serikali itashindwa na/au kukataa kuridhia kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi wa tuhuma hizi hadi kufikia 25 Novemba mwaka huu, vyama vyetu vitatoa maelekezo kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla juu ya hatua za kuchukuliwa nao ili kuondokana na ufisadi, wizi na/au ubadhirifu wa mali ya wananchi tuliouelezea katika Taarifa hii na katika Orodha ya Mafisadi.
 
Wakuu,

Kwa faida ya mjadala, naomba tuongezee na mengine. Masha alipoingia UDSM alikuwa na miaka kama 16, je alikuwa na qualifications zipi mpaka kumfanya ajiunge na sheria UDSM?
Inasemekana angebaki USA ingebidi atumie miaka mingine mitatu kabla ya kusoma sheria university, hivyo kuja Dar ilikuwa ni kutafuta njia za mkato. Je kwa wenye ujuzi na elimu za USA uvumi huo ni kweli?

Mkuu wangu Mtanzania,

1. Masha alizaliwa bongo na kukulia USA, ambako baba yake alikuwa mkurugenzi wa Information wa UN, takribani miaka karibu 30, Masha alipomaliza high school pale Rye Special School, huko Westchester USA, alitaka kusoma degree ya sheria, kwa bahati mbaya sheria za elimu za USA, then zilikuwa haziruhusu a foreigner, kusoma degree ya kwanza ya sheria huko, ndio yeye mwenyewe akaamua kurudi kusoma bongo kwa kusota, na kuiacha familia yake kule USA, ambako angeweza kusoma degree ya kitu kingine chochote katika mazingara ya kifahari, kama alivyosoma High School, now ndugu yangu Mtanzania, kweli unweza kuu-question uzalendo wa Masha na u-Tanzania wake?

2. I understand JKT, lakini sio kweli kuwa uzalendo wetu ni lazima upimwe na JKT, ninawafahmu wabongo wengi ambao hawakwenda JKT na ni wazalendo imara sana kuliko hata tuliokwenda huko.

Kwa kumaliza ni kwamba hata kama hizi juu hapo zingekuwa ni proven charges, bado hazi-amount kwa yeye kuwa fisadi, na Ridhiwani, kuajiriwa na IMMA au kampuni yoyote ya binafsi bila qualifications, bado sio crime ya ufisadi, kwa yeye muajiriwa au aliyemuajiri. Masha, is doing great sasa labda tuanze kuangalia yeye one day kuwa rais wetu, au?

Ahsante
 
topic ilikuwa hii "Re: Minister belittles link with JK's son" sasa haya mengine ni porojo tu, naona hakuna critical reasoning hapa zaidi ya roho za korosho.
 
Sasa naona JF inapoteza mwelekeo wake. Hivi mtoto wa rais akiendesha BMW X5 ni swala la ajabu?... hivi mlitaka aendeshe gari gani ikiwa baba yake ni rais achana na yeye kuwa na kazi. Nina hakika kila gari ataklalo endesha litazua hoja iwe VW watasema mtoto wa rais kachoka, kabuntas na hana maana.

Kabla hamjamuhkumu Masha kwanza tazameni sheria ya nchi kama inapingana na yote anayoyafanya. Hadi sasa hivi sijaona mahala Masha akitia tobo pakacha letu la Uchumi na kisheria Conflict of interest ndani ya serikali sio kitendo haramu..imeruhusiwa na Azimio la Zanzibar, nje ya hapo tuonyesheni ni wapi Masha katumia madaraka yake vibaya.
Kuhusu Ajira hilo wazi iwe Bongo hata Ulaya, watu huvutana ikiwa una qualification zinazotakiwa.
Ridhwan pamoja na kwamba yawezekana hana kichwa cha darasani lakini ni mchapa kazi mzuri na pia kama mtoto wa rais huwezi shindana naye unless utakuwa ktk dunia ya Wagagagigikoko.

Ndugu zangu kuna wakati ni lazima tukubali reality kwani dunia hii haimsubiri mtu. Zipo madamuhimu sana kwa maslahi yetu sote lakini uchambuzi wa mtu kutokana na influence zaye hapo mkuu utakuwa wataka kunambia matumizi mabaya ya Binadamu wote sawa, the fact is hatuko sawa.

Komredi Mkandara:

Hicho ndicho nakiona sasa. Ikiwa kila kitu unataka kuunganisha ABC unaweza kupoteza maana.

Hata mimi mbeba mabokisi nikirudi freshi watu wataunganisha stori kwa sababu kuna siku mtu alinivuta au kwa sababu baba yangu ni katibu kata.

Mada na points zipo jingi za kujenga taifa, hila udaku umeshamili samtimz.
 
DEEP GREEN FINANCE COMPANY:

1. Wamiliki wake wa kwanza ni watu wa Afrika ya Kusini na kutoka Bongo wana hisa wa kwanza ni: Protase Ishengoma na Stella Ndikimi ambao ni mawakili wa IMMA Kampuni hii imejitaja kuwa ni kampuni ya "Finance" lakini haikuwa kwenye orodha ya makampuni ya fedha ya Benki Kuu.

2. MwanaHisa mwingine ni Aloysius Mujulizi ambaye ameteuliwa na Rais Kikwete kuwa Jaji

3. Mwanahisa mwingine na Lawrence Masha ambaye siyo tu anachaguliwa kuwa Waziri bali anapewa Wizara ya Mambo ya Ndani (yenye kusimamia jeshi la polisi na magereza)..

TANGOLD

IMMA Advocates ni mawakili wa TANGOLD (by default Ishengoma na Ndikimi pia) Wakurugenzi humo ni pamoja na Andrew Chenge, Gray Mgonja, Patrick Rutabanzibwa

Mkuu wangu MMJ,

Exactly, kinachomfanya Masha, awe fisadi hapo juu ni kipi hasa? Mbona wananchi wa Nyamagana, walimchagua kuwa mbunge wao huku wakijua kuwa ni patner wa IMMA, maana kama dhambi yake hapa labda ni hiyo tu, kuwa "former IMMA patner" otherwise siioni tatizo, as the subjet of this topic?
 
Kaazi kwelikweli,maana huu mjadala unazidi kunoga na FMES halali.Nadhani kesho labda tutapata majibu.
 
Mkuu FM,

Huwa ninakuaminia kuwa ni kichwa, ila ninashangaa wewe kutoa hii kauli, mkuu kinachotufanya JF tuwe tofauti na forum zingine zote duniani, ni wanachama tulioko hapa, kwa kawaida hapa huwezi kumzungumzia kiongozi au mwananchi, halafu ikatokea hakuna asiyemfahamu hapa JF, na watu husema their first hand experience na the subject which makes the topic more interesting kwa wasomaji, na ndio maan huwa sina wasi wasi na kusema anytime ninachokijua first hand na siku zote huwa ninawaomba wengine waige, maana ndio hasa utamu wa mjadala mkuu,

Sasa nashangaa unaanza kunifundisha tabia ya uoga, yaani niogope kusema kwa sababu ya nini mkuu? Kuogopa maneno kutoka kwa nisiowajua na wasionijua ila wananihisi? OOH come on man, yaani wewe unaogopa wananchi wenzio kiasi hicho? Sasa kweli utaweza kumkoma nyani mkuu?

Sasa nisipokuambia nitamtonya utajuaje kuwa zimefika mkuu? Acha uoga mkuu, hapa ni taifa hatuogopi mtu wala watu, hoja hujibiwa kwa hoja, unachaojua unajua, unayemjua unamjua, hakuna anayeweza kuibadili hiyo hata kwa matusi kiasi gani mkuu, kwa hiyo ndio maana siogopi kusema mkuu, samahani kama imekukwaza kuwa nitamfikishia ujumbe, lakini hapa JF ni kawaida hiyo, acha uoga mkuu simamia taifa na unaowafahamu hapa bila kuogopa watu usiowajua na wasiokujua mkuu. Hebu pitia threads humu JF utaona watu wakikata ishus kwa kutumia first hand experience, majuzi tu Mkulu Mtanzania, alitupa elimu kuhusu siasa za Mbeya, anazozijua first hand hakuna ubishi wala hoja, Kiula alitajwa hapa, mkulu Kitla akatupa first hand anavyomjua toka jimbo lake kuwa ni bomu la kutupwa boom hakuna ubishi, ndio utamu wa mjadala mkuu, usiogope watu hapa, hakuuwi mtu, hapa ni hoja tu mkuu, kama una access na kiongozi sema mkuu unaweza kuwasaidia wengi hapa, kuliko kuogopa.

My point ilikuwa ni kuweka wazi kuwa Masha ni binadamu kama wewe na mimi, zile enzi za viongozi wetu kuwa kama alliens, kina Kingunge hakuna anayewajua au aliyesoma nao, wala kuishi nao na anayeweza kuwaongelea personal ziliisha, siku hizi viongozi ni sisi mkuu, yaani walalahoi, leo uko hapa kesho waziri, hakuna noma.

Ahsante mkuu.

Nashukuru kwa kunipa sifa ambayo sidhani naistahili. Mimi Mkuu niliukacha umande!

Ujumbe wangu ulikuwa ni kuwa ungeweza kumtetea Mheshimiwa vyema tu bila maelezo ya ziada ya uhusiano wako wa karibu naye. Haya ndiyo yaliyofanya watu waone kuwa pengine unachotetea ni urafiki bila kuangalia ishu yenyewe. Kwa mawazo yangu bila kutuambia uliongea naye jana ungeweza kusimamia hoja. Si kuwa nataka kukufundisha uoga, la hasha. Kwa kufanya hivyo bila shaka umeshamfanya Mheshimiwa ajue wewe ni nani na kwa hiyo kuna uwezekano wa kukuzuia kuwa neutral katika masuala yanayomhusu. Wengine humu naamini ni watu wa karibu kabisa na hawa tunaowajadili ( pengine wengine ni marafiki wa hao wakina Kingunge na pengine hata JK mwenyewe)na wanajificha nyuma ya hizi pseudonyms ili wawe huru kusema wanalotaka. Isingekuwa hivi basi hata wewe ungejiandika jina lako ili wote tukujue na tutambue uhusiano wako na hawa wakubwa bila matatizo! Mimi binafsi nisingependa ufanye hivyo kwa maana michango yako ingeanza kuonekana ina bias. With all due respects, Mkuu, hii ni www, nitajuaje kuwa umemtonya kama ulivyotuambia? Inawezekana kweli unawajua hawa waheshimiwa ( sina jinsi ya kuhakikisha hilo and in all honesty I could not care less). Inawezekana hauwajui na unajifanya tu ( again in all honesty I could not care less). Inawezekana wewe ndiye hawa tunaowazungumza ( again in all honesty I could not care less). First hand experience uliyoizungumzia, kwa mawazo yangu, haina mchango kwenye mada. Ulishare apartment na Mheshimiwa. Kwa hiyo unataka kusema hiyo inatuthibitishia unajua siri zake zote? Mnatembeleana nyumbani, kwa hiyo vilevile inathibitisha nini kuwa hawezi kuwa huyu wanayemzungumzia. First hand experience ambayo ingetusaidia ni wewe kutuambia umekuwa naye partner IMMA kwa hiyo unajua hausiki katika dili yeyote. Ungetuambia ulikuwa personal assistant wake wizara ya nishati kwa hiyo unajua hakuhusika vyovyote. Na nyingine kama hizi. Hizi ulizozitoa kwa bahati mbaya si katika hizo.


Wote tunamjua Mnyika na tunafahamu nafasi yake kwa hiyo tunamwelewa anapoelemea upande mmoja. Wengi kwa vile hatumjui Mzee Mwanakijiji tunaamini kuwa huwa anajitahidi kuwa neutral katika michango yake. Ana uhuru wa kumkemea yeyote bila kuonekana msaliti. Ndiyo maana nilikushauri upunguze kudondosha haya majina. Yanakupunguzia kuonekana objective. Ni ushauri wa nia njema tu kutoka kwangu nisie kichwa. Vichwa ni hao maprofesa. Samahani kama nimekuudhi lakini. Si nia yangu.
 
Kuhusu wanasheria jamaani,hapa mtajadili wee lakini tutajadili kitu ambacho hatukifahamu.Mwanasheria anaruhusiwa kumtetea mtu yeyote hata kama amekiri mbele yake kwamba kweli aliua na hata kama alimwona akiua ili mradi mwanasheria huyo hakuitwa kama shahidi mahakamani.Vilevile hata kama kampuni ni ya kifisadi au vinginevyo,bado ina haki ya kutetewa kisheria na kupata egal services zote,kwani izo huwa ni tuhuma zisizothibitishwa.Na kwa tanzania hatuna sheria inayomkataza wakili kumtetea au kuisajili kampuni yeyote ile,kwani kanuni ya kisheria inayotawala biashara inasema "buyer be ware" caveat emptor hivyo wewe unayeingia makataba na mwizi ndio unatakiwa kuwa makini,kwani kampuni kama richmond inapokuja tanzania,ni vigumu mwanasheria kujua itakuwa ya kitapeli au la,yeye anaisaidia usajili anapokea mkwanja wake basi mkataba na hiyo kampuni inaisha.Ni kazi ya wanasheria wa serikali kuchunguza mtu wanayeingia naye mkataba.

Mimi sio wakili lakini sidhani kama sheria inamruhusu wakili ashirikiane na mshitakiwa katika kujaribu kuficha ukweli. Kuna wakili mmoja yuko matatani New Jersey kwa sababu alikuwa akiwafahamisha wateja wake nani ni shahidi wa hatari kwao na wateja wakewalikuwa wakimuondoa. Attorney/ Client privilege sio carte blanche kuficha maovu. Mteja wako akikiri kwako kuwa ameua wewe kama wakili hauwezi kusimama na kusema hakuua bali unajaribu kupunguza makali ya tendo lenyewe. Ikijulikana kuwa wewe wakili ulishirikiana nae kuficha bastola ili asipatikane na kosa, wote mtakwenda na maji. Swali hapa si kuwa hawa ndugu kuwa na wateja wa aina hii, bali ni jee walishirikiana nao katika kufanya maovu ( kama kweli yalifanyika) beyond obligations zao kama mawakili wao. Hili la wao kuwa apointed kutokena na uhusiano wao na Mkuu si hoja. Nchi zote wanafanya hivyo. Yule aliyechangia katika ushindi anazawadiwa. Wamarekani wanatumia sana nafasi za ubalozi kulipa fadhila. Mimi nisichokielewa ni kwa nini watu waone aibu kwenye hili?
 
Ndiyo maana nilikushauri upunguze kudondosha haya majina. Yanakupunguzia kuonekana objective. Ni ushauri wa nia njema tu kutoka kwangu nisie kichwa. Vichwa ni hao maprofesa. Samahani kama nimekuudhi lakini. Si nia yangu.

Mkuu FM,

1. I am not sorry kwamba nimekukwaza kwa kumtetea Masha kuwa sio fisadi kwa sababu hakuna ushaidi wa kutosha kwa wale waliotuhumu.

2. Sijawahi kuwa na tatizo la objectiveness kwa kiongozi yoyote wala wananchi yoyote ambaye imethibitishwa hapa kwa ushahidi mzito kuwa ni fisadi, na ninamfahamu, Mama Mongella ninamfahamu sana lakini haikunipa taabu kuusema uhusiano wangu na yeye na kumtwanga, kwa hiyo kwenye hilo la objectiveness sihitaji shule mkuu.

3. Ni lazima kusema wazi uhusiano wangu na ninayemtetea na kwa nini ninamtetea, yes it makes a difference kwa wenye akili, as opposed na asiyemfahamu anayemtetea. Ahsante kwa ushauri wako, lakini siiuhitaji mkuu you can keep it, mimi sio Mwanakijiji na wala sio wewe, wewe uandike unavyoweza na mimi niandike ninavyoweza, hatuwezi kuandika uniformity hapa kutakuwa hakuna utamu wa mijadala.

4. Wale wanao-care less kama ulivyosema, huwa hawasemi, ukiona mtu anasema ujue panapofuka moshi, lazima chini kuna moto, yaani kumbe una-care mkuu, halafu please ninaomba usinitoe kwenye topic ya ufisadi wa Masha, maana ndio the subject ya topic, otherwise ukitaka unaweza kuanzisha topic ya style za uandishi wa post hapa JF.

Na by the way, huna chochote cha kuchangia kuhusu ufisadi wa Masha? Nanona umenililia mimi tu vipi mkuu mimi sio Masha, vipi una hoja kuhusu Masha?

Ahsante Mkuu!
 
Back
Top Bottom