Kujikwaa kisiki mara mbili

Kujikwaa kisiki mara mbili

Mkuu Radiriki, rodrick alexander , hivyo ndivyo katiba yetu inavyosema, tume ikiisha tangaza mshindi wa urais, tangazo hilo ni final and conclusive, hata kama amepatikana kwa ushindi batili, bao la mkono, uchaguzi usio huru na wa haki, tangazo hilo linatumia kanuni ya the end justify the means kwa kuhalalisha chochote kilichofanyika!.

P
Kuna katiba na uhalisia, binafsi sikupiga kura ila nilikuwa karibu na kituo cha kura wasimamizi walikimbia na kura zilikaa wiki mbili lakini matokeo yalishatangazwa.
Kwa nafasi yako kama mwandishi mkongwe una taarifa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa.
Hata waangalizi kuanzia Sadc, AU na wengineo ripoti zao zilionyesha kasoro kubwa za uchaguzi.
 
Swali lako linajijibu hapo hapo kwamba kilichofelisha maridhiano ya kwanza ni utapeli wa Samia na chama chake hivyo CHADEMAA walikua tayari kwa maridhiano hiyo 2022 mpaka muafaka ulipovunjika 2023.

Kuanzia pale tumeona wanachama na wafuasi wa CHADEMA wakitekwa na kuuwawa kama Mdude Nyagali, Deus Soka , Ali Kibao, Dioniz Kipanya, Twaha Mwaipaya .

Na wengine wengi waliobaki wamefunguliwa kesi feki za uhaini na ugaidi.

CCM haifai kufanya nayo maridhiano sababu haiko tayari kuwajibika hata kwa yale aliyoachiwa mtangulizi wake 2021 alitakiwa kuyazika ila yeye amezidisha mara tatu yake ikiwemo mauaji ya kutisha kuwahi kutokea October 29 mwaka jana.

Kwa hali iliyofikia tulihitaji msuluhishi anayeheshimika kutoka nje ya nchi na wao waje na mapendekezo kuunda tume huru isiyo na mafungamano na upande wowote na tume hiyo ichunguze kwa uhuru matukio yote yaliyojaza chuki nchi na itoe ripoti ya wazi bila kupepesa macho[sio yale ya hii ripoti ni mali yangu].

Jinamizi la October 29 litatesa sana watu halitawahi kuisha kirahisi hili litadumu vizazi na vizazi ninaona chuki itakayodumu kuna watu wataanza kumalizwa majukwaani na hata kwenye magari na kuna familia zikienda uhamishoni siku za usoni bila kutarajia.

Muda ni hakimu mzuri.
 
Wekeni mizani sawa leteni hoja mezani za maridhiano kati ya chadema na ccm

wekeni hoja zote tuzijadili kwa mapana!
 
Hao wanaotaka maridhiano watoke hadharani waeleze jamii lengo kuunla maridhiano ni nini?, cdm wana haki yakukataa malidhiano kwasabu hawakushiriki uchaguzi hivyo inawezekana sababu zao zikawa nje ya uchaguzi.
 
Kuna katiba na uhalisia, binafsi sikupiga kura ila nilikuwa karibu na kituo cha kura wasimamizi walikimbia na kura zilikaa wiki mbili lakini matokeo yalishatangazwa.
Kwa nafasi yako kama mwandishi mkongwe una taarifa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa.
Hata waangalizi kuanzia Sadc, AU na wengineo ripoti zao zilionyesha kasoro kubwa za uchaguzi.
Let the bygones be bygones, yaliyopita sii ndwele, tugange yaliyopo na yajayo, nimewashauri rafiki zangu Ushauri CHADEMA: Mchawi Mpe Mwanao Akulelee!, Barua Mliyopokea, Msisuse!, Jibuni!. Je, CHADEMA Wapeleke Jina la Tundu Lissu na Jingine au Wasuse ?
P
 
huyo mediator wanaemtaja chadema obvious ni mtu wao,let say ni Amsterndam au jamaa zake,akishamaliza ku mediate,repirt atampa nani kwa utekekezaji?,au atampa heche?🤔
Kuna kusoma ili mtu aelewe na kuna kusoma ili mtu ajibu. Nina uhakika unasoma kujibu
CHADEMA hawajataja mediator! wamesema atafutwe mtu neutral. Report ikiwa wazi kila mtu atajua jukumu lake
 
amaeamua kwamba huyu ni neutral,huyu siyo neutral,atakua nani?
 
Unajua mnapojibu hoja upande mmoja tu, mimi naweka walakini juu yake. Sasa ili mjadala uwe mpana zaidi, vema tusiegemee upande mmoja. Nilitegemea japo mtu mmoja aje na msimamo wa Serikali nae nimuulize lakini nashangaa kila anayeandika ni kuhusu kuitetea Chadema.
Haipendezi ionekane tunabishana juu ya hili bali tujadili kwa kutazama mawazo ya pande zote mbili ndio Ukweli utajitenga.

Anyway sitochoka kuhoji msimamo wa Chadema maana siuelewi mpaka leo hii. Na nakumbuka vema Chadema walipokataa kuendelea na Maridhiano yale walisema Mbowe kalamba Asali hawataki tena kuendelea na Maridhiano na rais Samia.

Alotaka Maridhiano ya Kitaifa kabla ya Uchaguzi Mkuu alikuwa Polepole na alisema wazi tusikubali Maridhiano baada ya Uchaguzi, sikuwahi wasikia Chadema wakisema watarudi mezani kuendelea na maridhiano. Sijawahi niseme kweli yangu najua walikataa kabisa kuendelea na maridhiano.

Na nadhani msimamo huu wa kukataa kuendelea na maridhiano na Samia ndio ilikuwa SABABU kubwa ilomwangusha Mbowe kwenye Uchaguzi Mkuu wakisema walimwambia watoke yeye bado alikuwa anakazania waendelee..

Sikumbuki kabisa wakati wowote wa Tundu Lissu akiwa Mwenyekiti wa Chama toka January 30, 2025 hadi April 09, 2025 siku Tundu Lissu anakamatwa, Chadema walikuwa wapo tayari kurudi mezani na Serikali au Samia.

Isitoshe Wananchi hawajui ama hatujui katika Makubaliano yale walikubaliana nini, marekebisho gani yalifanyika kulingana na makubaliano na yapi yalikwamisha makubaliano yale zaidi ya Wananchi kusikia Viongozi pande zote mbuli wakilaumiana.

Itapendeza zaidi kama Tungesikia pia Upande wa Serikali wao walikataa nini na kwa nini rais anayetamba kwa 4R akatae kuridhia makubaliano kwa maandishi?

Ndio maana nimekuja na hoja hii kwetu sisi tuchambue nani mwenye kusema ama kuficha UKWELI.
Ingia YouTube, tafuta Video ya Mkutano wa CHADEMA na Wahariri. Sikiliza sehemu ya Mnyika na Heche wameeleza kwa kina kilichotokea. Ni CCM ndio hawajawahi kutoa maelezo yao.
 
Neutral Referee.
CCM wanamtaka au hawamtaki?
Nadhani watu bado hamunielewi, pengine wanatkiwa watu wenye IQ kubwa kupembua mada hii. Ni hivi - CCM haitaki maridhiano yoyote na Chadema baada ya wao kujitoa katika Maridhiano ya kwanza. Kwa nini nasema haya

Kwanza Hakuna Kiongozi yeyote wa CCM ambae amewahi kasema ama kuomba maridhiano na Chadema isipokuea ninwatu walonje ya Uongozi. Kwao vikao vile vilikwisha wakati Chadema.imejitoa, hivi sasa wamefungua Ukurasa mpya wa maridhiano ya Kitaifa na ndio maana wanataka vyama vyote na wadau wengineo.

Lakini kitu kimoja wanachokosea ni kwamba tumefika hapa tulipo ni kutokana na matukio mengi mabaya kwa Viongozi na Wanachama wa Chadema. Hata tukisema Katiba Mpya waathirika wakubwa walikuwa Chadema iwe katika Utawala bora ama Siasa Safi.

Nimetumia maneno haya mawili kwa sababu yanabeba maswala mengi ikiwa ni pamoja na Haki za Binadamu, Usawa, mamlaka ya rais, Tume huru, Usimamizi wa kura, Utekaji, Mauaji na kadhalika.

Kitendo cha Chadema kutaka Maridhiano kwa sharti la kuachiwa Tubdu Lissu na sijui Mediator kutoka nje haiwezi kutokea maana hakuna mjadala huo.

CCM haina tena mpango wa Maridhiano ya faragha na Chadema isipokuwa sasa hivi ni SERIKALI ya Samia sio Chama ndio inayotaka maridhiano na Waalikwa wote na Chadema ni miongozi mwa Waalikwa.

Maridhiano haya hayahitaji Moderator kwa sababu yanapangwa na rais kufuatia reports zatume mbili alizoziteua kufanya Uchuguzi na matokeo yake ndio zitapelekea Uundwaji wa Agenda za mikutano ya Maridhiano.

Kitendo cha Heche kutaka Maridhiano na CCM na wakiweka masharti yao, jlo wasahau CCM haiwezi jikwaa kisikini mara mbili, CCM wanajua Chadema inataka mambo yake zaidi ya Maridhiano na CCM.

Lakini lazima Serikali ielewe kwamba Chadema ndio ilopelekea kuwepo Madai mengi na kwa Ushahidi. Nje ya Chadema sioni Maridhiano yanayoandaliwa yatawahusu Waathirika wa makundi gani na kwa vigezo gani!

Maasalaam.
 
Serikali haina nia ya dhati ya kutafuta maridhiano na yeyote, inachofanya ni 'Usanii' tu kama ule waliomfanyia Mbowe.
Huu ndio ukweli.
Pia CCM na serekali wanao uwezo wa kusawazisha mambo bila kuwahitaji Chadema wala yoyote yule kama wataamua kwa dhati kuwajibishana.
 
Wewe bwana Mkandara unazungumzia habari za maridhiano wakati Mtu unayempenda na kumkubali sana bwana Mbowe hatimaye alikiri mwenyewe kuwa CCM hawana mpango wa maridhiano ya kweli na akasema kuwa "INABIDI SASA TUWE TAYARI KWA MAPAMBANO, NA TUWE TAYARI KWA LOLOTE". Hebu msikilize hapa chini/

View: https://www.youtube.com/watch?v=gnjeZxElMMo&t=13s

Nikisema nampenda sana, sii kweli kwa sababu Mbowe alifanya makosa mengi kama kiongozi kukaribisha majokeli toka vyama vingine ambao walikuja kiharibu Chama kilichopata Wanachama wengi toka Uchaguzi wa 2005 hasa Wanafunzi wa vyuo vikuu. Chadema hii inaharibiwa na Wakuja..

Ila kweli namkubali Mbowe kama Kiongozi wa Chama kuliko Tundu Lissu kwa sababu Tundu Lissu sio Mwanasiasa, Mbowe ni Mwanasiasa ana ana Leadership.Values.

Tundu Lissu hana Sifa za kuwa Kiongozi ni mjuaji sana hashauriki, anajua kubishana haambiliki na above all, he is all about himself.

Nishasema sana hili. Na labda niongezee kusema hata CCM rais Samia ni Mwanasiasa ndio, lakini hana Sifa na uwezo wa Kuongoza. Ana mapungufu mengi na udhaifu wa kike(Huruma ya Mama) Both Lissu na Samia - lack Leadership values.

Ndio maana tunashuhudia mmomonyoko ndani ya Chadema na CCM, Udini, Ukanda na matukio ya fukuza fukuza kila anayepingana naye ama akiwa tishio la kiti chake. Yaani ni Miungu watu katika Ufalme walionao.

Nikutaarifu tu kwamba mara ya kwanza nasikia Chadema wamejitoa katika Maridhiano ni Hotuba hii, ila ilikuja nishangaza wakati wa Uchaguzi wakisema Mbowe kalamba Asali kwa nini aliibukia Ikulu? Hilo lilinitia shaka sana kuona watu walokuwa pamoja kwenye vikao vyote, mara gjafla wamemgeuka.

Iweje wasikatae toka mwanzo kumwekea Shaka wasikubali kwenda Ikulu lakini walihudhilia vikao vyotr vya Maridhiano na Samia kama wakati ule wa JK walipoemda.kunywa Chai!

Ebu wewe nambie kama Samia amteua Kiongozi yeyote wa Chadema kuwa Mbunge, halafu aende Bungeni bila ridhaa yao unadhani Chadema hii wangekaa na mtu huyo hata meza moja?

Narudia kusema, sikuunga mkono kabisa Ziito na Kitila walipotimuliwa 2013, sikuwaunga mkono Chadema ilipompokea Lowassa (lebelled Fisadi) kupitia Gwajima (Opportunist) 2015 hata kama waliahidiwa Ushindi!. Kwa hiyo Mbowe hakuwa Malaika ama nampenda sana lakini katika Uongozi wake niliona positive results nyingi kuliko Mapungufu. Kama Magufuli wa CCM nilimkubali kwa sababu alikuja na Udiketa Uchwara ambao ulitupa Positive results kitaifa na Chama chake. Kwa.mara ya Kwanza Tanzania tulitoka katika nchi maskini achana na mabaya yake lakini alipambana na Ufisadi. Aliweza kutekeleza maono (vision) ya Mwalimu katika mfumo wa Uchumi wa leo. Aliweza kuirudisha CCM katika Upendonwa Wananchi.

Na ikimzingua hakuachi salama. Ujinga Ujinga hataki. Nae alikuwa na makosa yake lakini kwa nchi za Afrika kazi kubwa na ngumu sana ni kuwatoa Wananchi katika Umaskini.

Kama kuna Kiongozi anaweza, by all means necessary kututoa katika Umaskini basi mimi nitasimama na yeye! Iwe Kagame, Troure, Ghaddaf au Magufuli au yeyote ajae.

Adui mkubwa wa Waafrika ni UMASKINI na Adui wa Umaskini ni maskini wenyewe.
 
Unajua umesema kweli kabisa kwamba Sijui Chadema wanataka nini. Kama wewe unajua tafadhali nambie maana hata hao CCM sijui wanataka nini ila najua mmoja wao ni Mnafiki na ishara za mnafiki ni 3.

1. Kusema uongo: Huongea uongo anapozungumza.
2. Kutotimiza ahadi: Huvunja au hatekelezi ahadi anapotoa.
3. Kufanya khiyana: Hukosa uaminifu au hufanya khiyana anapoaminiwa.
Ccm inajurikana ni chama cha kihuni tu, lakini swali Chadema wasipotaka kukaa mezani mwisho wake ni nini? 2030 si mbali, ccm wanajipanga mitandao ya kumrithi Samia, hili la maridhiano haliwaumizi kichwa kivile.

Mimi nadhani mwalimu wa siasa ni Maalim Seif, hebu tuchukuwe notice kwake, huyu amedhurumiwa Urais hadharani na uchaguzi ukafutwa, mbinu ya kuwasusia Ccm haijawahi kuleta matunda, tutumie hekima za Maalim Seif.
 
Nadhani watu bado hamunielewi, pengine wanatkiwa watu wenye IQ kubwa kupembua mada hii. Ni hivi - CCM haitaki maridhiano yoyote na Chadema baada ya wao kujitoa katika Maridhiano ya kwanza. Kwa nini nasema haya

Kwanza Hakuna Kiongozi yeyote wa CCM ambae amewahi kasema ama kuomba maridhiano na Chadema isipokuea ninwatu walonje ya Uongozi. Kwao vikao vile vilikwisha wakati Chadema.imejitoa, hivi sasa wamefungua Ukurasa mpya wa maridhiano ya Kitaifa na ndio maana wanataka vyama vyote na wadau wengineo.

Lakini kitu kimoja wanachokosea ni kwamba tumefika hapa tulipo ni kutokana na matukio mengi mabaya kwa Viongozi na Wanachama wa Chadema. Hata tukisema Katiba Mpya waathirika wakubwa walikuwa Chadema iwe katika Utawala bora ama Siasa Safi.

Nimetumia maneno haya mawili kwa sababu yanabeba maswala mengi ikiwa ni pamoja na Haki za Binadamu, Usawa, mamlaka ya rais, Tume huru, Usimamizi wa kura, Utekaji, Mauaji na kadhalika.

Kitendo cha Chadema kutaka Maridhiano kwa sharti la kuachiwa Tubdu Lissu na sijui Mediator kutoka nje haiwezi kutokea maana hakuna mjadala huo.

CCM haina tena mpango wa Maridhiano ya faragha na Chadema isipokuwa sasa hivi ni SERIKALI ya Samia sio Chama ndio inayotaka maridhiano na Waalikwa wote na Chadema ni miongozi mwa Waalikwa.

Maridhiano haya hayahitaji Moderator kwa sababu yanapangwa na rais kufuatia reports zatume mbili alizoziteua kufanya Uchuguzi na matokeo yake ndio zitapelekea Uundwaji wa Agenda za mikutano ya Maridhiano.

Kitendo cha Heche kutaka Maridhiano na CCM na wakiweka masharti yao, jlo wasahau CCM haiwezi jikwaa kisikini mara mbili, CCM wanajua Chadema inataka mambo yake zaidi ya Maridhiano na CCM.

Lakini lazima Serikali ielewe kwamba Chadema ndio ilopelekea kuwepo Madai mengi na kwa Ushahidi. Nje ya Chadema sioni Maridhiano yanayoandaliwa yatawahusu Waathirika wa makundi gani na kwa vigezo gani!

Maasalaam.
Unatunga taarifa. Heche hajasema Chadema wanataka maridhiano na CCM. Kasema Chadema hawakatai maridhiano na CCM. Unaona tofauti hapo? Halafu hayo unayoyaita ni masharti ya Chadema ya maridhiano, ni sehemu ya madai yao ya jumla wanayoyasimamia siku zote kama chama, ambayo msingi wake ni HAKI. Hata hiyo kusema Tundu Lissu aachiwe ni sehemu ya madai yao ya kutaka haki dhidi ya mfumo wanaoamini hautendi haki.

By the way msimamo wa Heche na Lissu, ndo huohuo ulikuwa msimamo wa hadhara wa Mbowe. Tofauti ni kwamba Mbowe aliendekeza backdoor politics, kitu ambacho kilipelekea anguko lake.
 
kitu cha kwanza alíchofanya lisu aliporudi toka uhamishoni baada ya Rais kutaka maridhiano,ni lisu kuyakataa,akisema ni mapendano,akadai mbowe karamba asali,chadema wakasubiri wiki chache kabla ya uchaguzi,ndo wakaanza kudai maridhiano,eti uchaguzi uahirishwe kwanza yaganyike maridhiano...sasa hicho kilikua kisiki cha kwanza,kisiki cha pili,chadema sasa hawataki maridhiano,watasubiri mpaka uchaguzi wa 2029 ukaribie,kisha ndo wadai maridhiano,uchaguzi usogezwe mbere😂😂,HICHO NI KISIKI CHA PILI,WATAJIKWAA,maana uchaguzi hautaajirishwa kamwe,na chàdema watasusa tena
 
Nikisema nampenda sana, sii kweli kwa sababu Mbowe alifanya makosa mengi kama kiongozi kukaribisha majokeli toka vyama vingine ambao walikuja kiharibu Chama kilichopata Wanachama wengi toka Uchaguzi wa 2005 hasa Wanafunzi wa vyuo vikuu. Chadema hii inaharibiwa na Wakuja..

Ila kweli namkubali Mbowe kama Kiongozi wa Chama kuliko Tundu Lissu kwa sababu Tundu Lissu sio Mwanasiasa, Mbowe ni Mwanasiasa ana ana Leadership.Values.

Tundu Lissu hana Sifa za kuwa Kiongozi ni mjuaji sana hashauriki, anajua kubishana haambiliki na above all, he is all about himself.

Nishasema sana hili. Na labda niongezee kusema hata CCM rais Samia ni Mwanasiasa ndio, lakini hana Sifa na uwezo wa Kuongoza. Ana mapungufu mengi na udhaifu wa kike(Huruma ya Mama) Both Lissu na Samia - lack Leadership values.

Ndio maana tunashuhudia mmomonyoko ndani ya Chadema na CCM, Udini, Ukanda na matukio ya fukuza fukuza kila anayepingana naye ama akiwa tishio la kiti chake. Yaani ni Miungu watu katika Ufalme walionao.

Nikutaarifu tu kwamba mara ya kwanza nasikia Chadema wamejitoa katika Maridhiano ni Hotuba hii, ila ilikuja nishangaza wakati wa Uchaguzi wakisema Mbowe kalamba Asali kwa nini aliibukia Ikulu? Hilo lilinitia shaka sana kuona watu walokuwa pamoja kwenye vikao vyote, mara gjafla wamemgeuka.

Iweje wasikatae toka mwanzo kumwekea Shaka wasikubali kwenda Ikulu lakini walihudhilia vikao vyotr vya Maridhiano na Samia kama wakati ule wa JK walipoemda.kunywa Chai!

Ebu wewe nambie kama Samia amteua Kiongozi yeyote wa Chadema kuwa Mbunge, halafu aende Bungeni bila ridhaa yao unadhani Chadema hii wangekaa na mtu huyo hata meza moja?

Narudia kusema, sikuunga mkono kabisa Ziito na Kitila walipotimuliwa 2013, sikuwaunga mkono Chadema ilipompokea Lowassa (lebelled Fisadi) kupitia Gwajima (Opportunist) 2015 hata kama waliahidiwa Ushindi!. Kwa hiyo Mbowe hakuwa Malaika ama nampenda sana lakini katika Uongozi wake niliona positive results nyingi kuliko Mapungufu. Kama Magufuli wa CCM nilimkubali kwa sababu alikuja na Udiketa Uchwara ambao ulitupa Positive results kitaifa na Chama chake. Kwa.mara ya Kwanza Tanzania tulitoka katika nchi maskini achana na mabaya yake lakini alipambana na Ufisadi. Aliweza kutekeleza maono (vision) ya Mwalimu katika mfumo wa Uchumi wa leo. Aliweza kuirudisha CCM katika Upendonwa Wananchi.

Na ikimzingua hakuachi salama. Ujinga Ujinga hataki. Nae alikuwa na makosa yake lakini kwa nchi za Afrika kazi kubwa na ngumu sana ni kuwatoa Wananchi katika Umaskini.

Kama kuna Kiongozi anaweza, by all means necessary kututoa katika Umaskini basi mimi nitasimama na yeye! Iwe Kagame, Troure, Ghaddaf au Magufuli au yeyote ajae.

Adui mkubwa wa Waafrika ni UMASKINI na Adui wa Umaskini ni maskini wenyewe.
Hayo ya Lissu mjuaji, sijui kitu gani ni irrelevant ni mipasho, hata Nyerere aliitwa Haambiliki. By the way, Lissu alikuwa hana hata mpango wa kuwa Mwenyekiti wa chama, ni baada ya kuona Mbowe anamkumbatia huyu mama, hainvoke peoples power wakati watu kama Soka, Mzee Kibao etc wanatekwa na hachukui hatua kali za kisiasa kuweka pressure kwa serikali ya CCM, na hata akatone down madai ya katiba mpya tofauti na kabla hajaenda Jela.
Pia Mbowe alianza kuwa life support ya kisiasa ya Samia kwa kumpa subtle shade ya kisiasa, kumbuka hotuba yake yake ya kisiasa kule mwanza.

Mbowe alikuja kujionea mwenyewe kuwa CCM haina mpango wa maridhiano ya kweli, wanafanya political gaming tu ili kuconsolidate power zaidi na kujinasua kutoka ktk.kikaango cha kisiasa ambacho ni cha moto.

Na ushahidi kuwa CCM na Samia wao hawana mpango wa maridhiano ya kweli ni kuwa kwa barua waliiandikia CHADEMA kukataa nukta zote za msingi zavway forward, na hicho ndo kiliua hayo mazungumzo ya maridhiano feki.

Na ili kuthibitisha kuwa Samia siyo wa kumuamini, Majuzi hapa kwenye Ilani ya CCM walizungumzia kuhusu kuleta katiba mpya, sasa hivi wanazungumzia MABADILIKO YA KATIBA. Sasa kama kitu kikubea kama katiba wanafanya tofauti na hitajio la wananchi na tena kinyume cha Ilani yao, What do you expect kwa watu hawa?.

Uliona CCM walichokifanya ktk uchaguzi wa serikali za mitaa 2024?. Je ukosefu wa maridhiano ndo ulisababisha hayo, au ni boldness ya kihuni ya kisiasa iliyopitiliza ambayo haiwezi kutatuliwa kwa mazungumzo feki.

Kosa kubwa la kisiasa unaloweza kulifanya kama mwanasiasa wa leo ni kumuamini Samia na chama chake, unfortunately Mbowe alijionea mwenyewe baadae, kuwa sweet talk na tabasamu la mama ain't nothing ni political tactic yake tu ya kuendeleza siasa feki.

Kiufupi iko hivi, CCM wanapozungumzia maridhiano wanamaanisha Cost effective strstegy ya kuminimize pressure ya kisiasa kwao, kwa kuwaita viongozi kwwnye vikao feki, wanywe juisi, wapewe bahasha, kisha watoe statement mfu za kuwapa watu matumaini bila kuwepo kwa changes zozote za msingi ili wahuni waendelee kutawala nchi kiubwete.
 
Hayo ya Lissu mjuaji, sijui kitu gani ni irrelevant ni mipasho, hata Nyerere aliitwa Haambiliki. By the way, Lissu alikuwa hana hata mpango wa kuwa Mwenyekiti wa chama, ni baada ya kuona Mbowe anamkumbatia huyu mama, hainvoke peoples power wakati watu kama Soka, Mzee Kibao etc wanatekwa na hachukui hatua kali za kisiasa kuweka pressure kwa serikali ya CCM, na hata akatone down madai ya katiba mpya tofauti na alipokuwa Jela.
Pia Mbowe alianza kuwa life support ya kisiasa ya Samia kwa kumpa subtle shade ya kisiasa, kumbuka hotuba yake yake ya kisiasa kule mwanza.

Mbowe alikuja kujionea mwenyewe kuwa CCM haina mpango wa maridhiano ya kweli, wanafanya political gaming tu ili kuconsolidate power zaidi na kujinasua kutoka ktk.kikaango cha kisiasa ambacho ni cha moto.

Na ushahidi kuwa CCM na Samia wao hawana mpango wa maridhiano ya kweli ni kuwa kwa barua waliiandikia CHADEMA kukataa nukta zote za msingi zavway forward, na hicho ndo kiliua hayo mazungumzo ya maridhiano feki.

Na ili kuthibitisha kuwa Samia siyo wa kumuamini, Majuzi hapa kwenye Ilani ya CCM walizungumzia kuhusu kuleta katiba mpya, sasa hivi wanazungumzia MABADILIKO YA KATIBA. Sasa kama kitu kikubea kama katiba wanafanya tofauti na hitajio la wananchi na tena kinyume cha Ilani yao, What do you expect kwa watu hawa?.

Uliona CCM walichokifanya ktk uchaguzi wa serikali za mitaa 2024?. Je ukosefu wa maridhiano ndo ulisababisha hayo, au ni boldness ya kihuni ya kisiasa iliyopitiliza ambayo haiwezi kutatuliwa kwa mazungumzo feki.

Kosa kubwa la kisiasa unaloweza kulifanya kama mwanasiasa wa leo ni kumuamini Samia na chama chake, unfortunately Mbowe alijionea mwenyewe baadae, kuwa sweet talk na tabasamu la mama ain't nothing ni political tactic yake tu ya kuendeleza siasa feki.

Kiufupi iko hivi, CCM wanapozungumzia maridhiano wanamaanisha Cost effective strstegy ya kuminimize pressure ya kisiasa kwao, kwa kuwaita viongozi kwwnye vikao feki, wanywe juisi, wapewe bahasha, kisha watoe statement mfu za kuwapa watu matumaini bila kuwepo kwa changes zozote za msingi ili wahuni waendelee kutawala nchi kiubwete.
Inachofanya sirikali ya kimama ni uhuni tu.
 
😁😁,shida ya chadema,wala siyo hiyo katiba,shida yao ni kupata urais,yaani hawa jamaa,hawafanyi hata juhudi kupata wabunge,yaani shida yao samia ampishe Lisu kwenye cheo cha urais..😂😂🙆,hawa jamaa vichwa vyao wanajijua wenyéwe,,ooh mbowe alianza kumjenga samia kisiasa,tukaona tususie maridhiano,,😂🙆🏽‍♂️,kwani shida yenu ni katiba mpya,au shida yenu ni samia?.
tatizo la chadema kwanza ni kukataa maridhiano,kwa utetezi wa kijinga sana eti mbowe karambishwa asali,,kwani tatizo ni asali au katiba?,kwanini myilie masnani kulamba asali na mkaachana na maini point ya katiba kama kweli mnashida na katiba,?.
so chadema wakajivuta vuta,hadi wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu,wakaja tena,CHADEMA TUKO TAYARI KWA MARIDHIANO ENDAPO UCHAGUZI UTAAHIRISHWA,IUNDWE SERIKALI YA MPITO😂😂🙆🏾‍♂️,
jesuschrist on a wheelbarrow...!!,yaani tusitishe uchaguzi mkuu,then serikali ivunjwe,iundwe serikali mpya,wakina lisu ,heche,kitima,wakipata uwaziri wa bila jasho,then ndio wakae kuridhiana...?!!
ombi lilipokataliwa ndioosa kina kitima na kikundi chote wakaanzisha movement ya kuangusha serikali,wakaanza kuwashawishi baadhi ya viongozi serikali wamgeuke boss wao ,watumie hata bunge kumpigia kura ya kukosa imani,wakawaahidi hao viongozi,watapewa sakramenti na komunio,na watapatowa nafasi ya kwenda mbinguni,VIP chances,😁🙆,wale viongozi wakaingia mkenge na kuanza mchakato,ishu ikashitukiwa,wakajikuta wametupwa nje ya system,
Teki na chadema wakakuna vichwa,wakaona sasa hawaezi subiri huyu mama aingie uchaguzi kwani atashinda tu,maana si waliona mikutano ya kampeni,wakaamua moja,TUKIVURUGE,liwalo na liwe,lazima KINUKE
 
Hayo ya Lissu mjuaji, sijui kitu gani ni irrelevant ni mipasho, hata Nyerere aliitwa Haambiliki. By the way, Lissu alikuwa hana hata mpango wa kuwa Mwenyekiti wa chama, ni baada ya kuona Mbowe anamkumbatia huyu mama, hainvoke peoples power wakati watu kama Soka, Mzee Kibao etc wanatekwa na hachukui hatua kali za kisiasa kuweka pressure kwa serikali ya CCM, na hata akatone down madai ya katiba mpya tofauti na kabla hajaenda Jela.
Pia Mbowe alianza kuwa life support ya kisiasa ya Samia kwa kumpa subtle shade ya kisiasa, kumbuka hotuba yake yake ya kisiasa kule mwanza.

Mbowe alikuja kujionea mwenyewe kuwa CCM haina mpango wa maridhiano ya kweli, wanafanya political gaming tu ili kuconsolidate power zaidi na kujinasua kutoka ktk.kikaango cha kisiasa ambacho ni cha moto.

Na ushahidi kuwa CCM na Samia wao hawana mpango wa maridhiano ya kweli ni kuwa kwa barua waliiandikia CHADEMA kukataa nukta zote za msingi zavway forward, na hicho ndo kiliua hayo mazungumzo ya maridhiano feki.

Na ili kuthibitisha kuwa Samia siyo wa kumuamini, Majuzi hapa kwenye Ilani ya CCM walizungumzia kuhusu kuleta katiba mpya, sasa hivi wanazungumzia MABADILIKO YA KATIBA. Sasa kama kitu kikubea kama katiba wanafanya tofauti na hitajio la wananchi na tena kinyume cha Ilani yao, What do you expect kwa watu hawa?.

Uliona CCM walichokifanya ktk uchaguzi wa serikali za mitaa 2024?. Je ukosefu wa maridhiano ndo ulisababisha hayo, au ni boldness ya kihuni ya kisiasa iliyopitiliza ambayo haiwezi kutatuliwa kwa mazungumzo feki.

Kosa kubwa la kisiasa unaloweza kulifanya kama mwanasiasa wa leo ni kumuamini Samia na chama chake, unfortunately Mbowe alijionea mwenyewe baadae, kuwa sweet talk na tabasamu la mama ain't nothing ni political tactic yake tu ya kuendeleza siasa feki.

Kiufupi iko hivi, CCM wanapozungumzia maridhiano wanamaanisha Cost effective strstegy ya kuminimize pressure ya kisiasa kwao, kwa kuwaita viongozi kwwnye vikao feki, wanywe juisi, wapewe bahasha, kisha watoe statement mfu za kuwapa watu matumaini bila kuwepo kwa changes zozote za msingi ili wahuni waendelee kutawala nchi kiubwete.
Niloandika mimi kuhusu Tundu Lissu unayaona ni irrelevant ati Mipasho lakini uloandika wewe kuhusu Mbowe ndio relevant na Ukweli sio?

Nilitegemea zaidi ungemsafisha Tundu Lissu kwa kutueleza Tundu Lissu amewahi kuongoza wapi? Values au sifa zipi za Uongozi alokuwa nazo zaidi ya sasa Kukibomoa Chama, kufukuza wote walomkubali Mbowe! Hata kina Sugu wamerudi Chadema baada ya yeye kutiwa ndani. Halafu mnatazama wengine kama kwamba Chadema kuna HAKI na USAWA?

Adui Mkubwa wa Chadema leo ni Mbowe ambae walisema mzee akae pembeni apishe vijana lakini kutwa wanaulizama Mbowe yuko wapi? Amewafanyia nini kibaya saana mpaka mumchukie kiasi hiki? Mngekuwa watawala nadhani Mbowe angekuwa jela sasa hivi.

Mbona Mzee Mtei alipostaafu hatukusikia wakiuliza yuko wapi? Haya kule ACT, Zitto kajiuzuru sijasikia akibezwa, wanaendelea na kazi za Chama chao kama kawaida. Chadema ni Uadui kwa yeyote anayemkosoa ama kupingana na Tundu Lissu. Hiki Chama cha Siasa au Saccos!

Niarudia, CCM haitakuwa na Mazungumzo na Chadema tena, na hizi habari za kupigania Uhuru kama ANC sijui Mandela ndio mnazidi kujipotosha kabisa. ANC haikuwa Chama cha Siasa bali wapigania Uhuru kama TAA nje ya mfumo wa Kiutawala.

Chama chochote kikisha Sajiliwa na kutambuliwa kama Chama Cha Siasa nchinj, kinaingia moja kwa moja katika mfumo wa Utawala wa nchi hiyo, wanatambuliwa wanakuwa sehemu ya Utawala na kupewa jukwaa la kujitangaza, sio Wapigania Uhuru tena bali Chama kinachowakilisha Wananchi kwa maslahi ya Taifa. Ebu nedeni Shule mkasome SIASA.. tunakosa Siasa Safi kwa Ujinga kama huu.

Msipoelewa kwamba Chadema ni Chama cha Siasa kinachowakilisha Wananchi katika mrengo wa Kisiasa basi mtapata shida sana na sasa naelewa kwa nini CCM ina deal na watu kama nyie.

Ni sawa na Chama cha MAGAIDI kama ilivyokuwa TAA kabla ya Usajili wake kuwa Chama cha Siasa. Na kama hizi ndio Siasa zenu basi hamfai hata kuingia Uchaguzi Mkuu, Endeleeni kupigania huo Uhuru wenu sijui mtaenda msituni kule Kibiti. Mnasikitisha sana..

Maasalaam
 
Back
Top Bottom