Nimewahi kumsikia Makamu Mwenyekiti wa Chadema John Heche akisema Chadema haiwezi kwenda katika Maridhiano pasipo Kiongozi wao TAL kuachiwa huru bila masharti.
Na kuna baadhi ya.Wanachama wanakataa kabisa maridhaliano ya Serikali pasipo Uwajibikaji wa Serikali kufuatia matukio kadhaa yalowahi tokea, ilihali Serikali nayo inadai Chadema wamekuwa wakitumia wanaharakati na taasisi za nje kuvuruga Amani nchini. Msema kweli nani hata sielewi..
Sasa, katika tafakari zangu nimejikuta najiuliza maswali kadhaa kulingana mazingira ya hoja hii ya Heche na baadhi ya watu kwa sababu zifuatazo
Waingereza husema "Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me” na ingine yasema. " Once bitten, twice Shy" ni katika Maudhui hayo hayo nayotaka kuyajadili.
Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu akiwa matibabu kule Ubelgiji alikutana na rais Samia wakakubaliana kufanya mazungumzo kulenga maridhiano baina ya Utawala wake na Chadema kwa masharti ambayo Tundu Lissu yaliyainisha ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi Mwenyekiti wa Chadema wakati huo Nd. Freeman Mbowe pamoja na masharti mengineyo sitoyataja yote.
Mbowe aliachiwa huru, wakaanza mchakato na vikao vya Maridhiano ambayo kufikia hatua za mwisho mwisho l, Chadema walijitoa kwa madai ya kwamba Rais Samia akikataa kuweka makubaliano yao katika maandishi na kuyasaini. Tunaambiwa Chadema Hawakutaka maridhainao ya maneno matupu pasipo Maandishi.
Kufuatia matokeo yale najiuliza maswali yafuatayo.
Maasalaam

- Je, Chadema wanaweza kukubali kuingia katika maridhiano na rais ambaye alikataa kusaini makubaliano ya awali iweje leo atakuwa mkweli?
- Je, rais Samia anaweza kubali maridhiano na Chadema ambao anajua yawezekana ni mtegilo kama ule wa awali walojitoa katika maridhiano yale kwa sababu ambazo Yeye na majumbe wake waliona hazina msingi?
Maasalaam