JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Amani imekuwa kitu adimu sana,watu wengi usoni wanaonekana wana furaha.

Ila mioyo yao haina amani kabisa😰,ukipata sehemu yenye AMANI hata kama hakuna kiti wewe kaa hata chini.

Mwenyezi Mungu akusaidie sana akupe hekima na uvumilivu wa kuvuka katika kipindi kigumu unachopitia leo.
-The Power Is Within You-
✨🫵
 
Ni wazazi wako pekee ndio wanaotaka kukuona umepiga hatua kubwa katika maisha na kufanikiwa kuliko wao.

Mungu akikuinua na kukupa mafanikio kuwa makini sana ni watu gani unawambia mipango yako muhimu ya maisha.

Robert Greene, mwandishi na mtaalamu nguli wa mambo ya uongozi katika kitabu chake cha "The 48 Laws of Power" katika ile Sheria ya tatu ya nguvu anaeleza kuwa "Ficha nia yako"

Usiwahi kuwaonyesha watu unakoelekea waache tu waone ukiwa tayari umefika.

Watu wengi hawafurahii kuona ukifanikiwa kuliko wao wanataka uendelee kubaki chini yao...

Au uendelee kubaki kwenye level sawa na wao, ukishawaambia mipango yako kabla haijakamilika...

Wapo watakao kukatisha tamaa, kukucheka,kukuonea wivu, na wengine watajitahidi kukuwekea vikwazo bila hata wewe kujua.

Sio kila anaye kuchekea na kukupongeza anakutakia mema.

Wapo watu walio waamini watu kwa kuwaambia mipango yao muhimu baada ya hapo wakajikuta kila kitu kimeharibika.

Inawezekana umefanya kosa hili kwa muda mrefu lakini leo chukua hatua..

Na uanze upya kwani mafanikio ya kweli hayahitaji kelele yanahitaji vitendo "Hustle and win in Silence🤫"

-The Power Is Within You-
🫵✨
 
Katika hili nimeliona kabisa kwa ndugu yangu mmoja,baada ya kiwanja chao kuuzwa na kugawana hela

Wenzake wote walifanya mambo yao kimya kimya kana kwamba hawana hela,waliojenga walijenga na walio fanya mambo mengine walifanya

Guess yeye alifanya nini?

Everything was in the internet, nyumba iko kwenye msingi hiyo picha facebook,mara pagale limepanda level fulani hiyo mtandaoni

Kilichofuatia ni masikitiko matupu,watu ni wabaya aisee,unataka kujua kilichotea we kausha tu! Ujumbe hapa fanya mambo yako kimya kimya period
 
MALIZA UNACHOKIANZA:

Profesa Cal Newport, mwandishi na mkufunzi wa chuo kikuu cha Georgetown kilichopo nchini Marekani šŸ‡ŗšŸ‡ø

Katika kitabu chake cha "Deep Work" alieleza jambo la msingi sana katika maisha kuwa.

"Mafanikio makubwa hayatokani na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja"

"Bali yanatokana na uwezo wa kuweka umakini wako wote kwenye jambo moja muhimu hadi ulimalize."

Newport, anasisitiza kuwa ili kutimiza malengo yako ni muhimu sana kuondoa usumbufu (distractions),

Kupanga muda maalum wa kufanya kazi ya kina, na kujenga NIDHAMU ya kufanya kazi bila kukatizwa na simu,

Mitandao ya kijamii au kelele za nje,Dunia ya leo imejaa vishawishi vinavyotaka kukutoa kwenye mstari.

Lakini mtu anayejua kulinda umakini wake ndie anayefanikiwa katika kile anachokifanya.

Siku zote kumbuka jambo hili...
Unapoanza jambo fulani na kuishia njiani kisha ukaanza lingine jipya, unatapanya nguvu, rasilimali muda ā° n.k

Kuwa kama Simba weka focus kwenye jambo moja hadi ulitimize.

Simba anapomkimbiza swala, huwa habadili MWELEKEO hata kama swala mwingine atakatiza mbele yake.

Ataendelea kumkimbiza swala aliyemkusudia mpaka amkamatešŸŽÆ

Hivi ndivyo ilivyo katika maisha, ukiamua kuanza jambo fulani...

iwe ni biashara,kazi au ndoto fulani IAMINI NDOTO YAKO kisha ipambanie bila kuchoka hadi itimie.

Inawezekana hata wewe umeshatumia muda mwingi kwa kuanza na kuishia njiani.

Lakini leo kumbuka kuwa ikiwa bado unapumua BADO HUJACHELEWA

Nakutakia safari njema kuelekea kwenye kilele cha mafanikio yakošŸ„‡
-The Power Is Within You-
āœØšŸ’Ŗ

(Yona Morice Yona)
 
Screenshot_20261124-140715_WhatsApp.jpg
 
Usitoe msaada unaozidi uwezo wako:
-Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard University kuhusu tabia ya kusaidia wengine unaonyesha kuwa.

"Kusaidia wengine ni jambo jema na lenye faida lakini kuweka mipaka ni muhimu sana ili usifaidishe zaidi wengine huku wewe ukibaki katika hali duni"

-Msaada au usaidizi unaokufanya ubaki katika hali duni ya kushindwa kumudu mahitaji yako muhimu sio msaada ni mateso ya kujitakia🤷

-Mwandishi na mtaalamu wa mambo ya maendeleo binafsi Stephen R.Covey katika kitabu chake cha "The 7 Habits of Highly Effective People" (Tabia 7 za watu wenye ufanisi) anasisitiza umuhimu wa kuweka vipaumbele na kutunza kile kilicho muhimu kwako.

-Covey anasema kuwa "huwezi kuwasaidia wengine kwa ufanisi ikiwa unajimaliza mwenyewe unahitaji kwanza kuwa na nguvu na uwezo ili uweze kutoa msaada wenye maana".

-Saidia watu kwa moyo na hekima ila kumbuka kujiwekea mipaka kwani dunia haichoki kupokea.
-The Power Is Within You-
šŸ†šŸ«µāœØ

(Yona Morice Yona)
 
TANGAZO LA KAZI

DEREVA
Tunatafuta dereva mwenye sifa zifuatazo
  • Mwaminifu,
  • Mchapakazi na muadilifu
  • Mwenye leseni hai class E

FORKLIFT OPARETA
Tunahitaji forklift opareta
  • Mwenye uzoefu
  • Mwaminifu na mchapakazi
  • Mwenye leseni hai

FUNDI UMEME & FITTER MECHANICS
  • Awe anacheti kinachotambulika na serikali
  • Awe mwaminifu na mchapakazi

MENEJA RASILIMALI WATU (HR)
  • Awe mwaminifu
  • Mchapakazi na mwenye kujituma
  • Uwezo wa kusimamia wafanyakazi

Jinsi ya kutuma
tuma kwenye namba 0677088098
 
Back
Top Bottom