CHAUMMA yaionya CHADEMA, wasituletee migogoro

Sio lazima. Majadiliano yanapaswa kuwa ya hiari. Chama kisichotaka kukaa mezani hakiwezi kulazimishwa kukaa mezani. Hivyo hivyo hamna chama chenye haki ya kulazimisha chama kingine kisishiriki katika majadiliano kwa sababu yeyote ile. Kushiriki au kutoshiriki ni uamuzi wa kila chama.
Amandla...
Ni mwendawazimu pekee ndiye anaweza kueleza kuwa kinachoendelea eti ni maridhiano.
Uliona wapi mtuhumiwa mkuu wa uovu anajigeuza kuwa msimamiz8 wa maridhiano!
Anatakiwa mtu neutral anayeaminika ndiye awe msimamiz8 mkuu wa maxungumzo yanayolenga maridhiano. Kwa sasa kinachoendelea ni upuuzi mtupu ambao yeyote anayetaka haki na ukweli hawezi kuungana nao. Hao CHAUMAwanafahamika kwa utapel8 wa kisiasa, hakuna chochote wanachosimamia zaidi ya matumbo yao.
 
..kama ni madaraja kuvunjika kati ya Cdm na vyama vingine itakuwa ni kipindi cha Mbowe.
Mbowe hayuko innocent kwenye hili. Daraja lilianza kuvunjika wakati wa Ukawa ambapo Chadema iliwachezea rafu wenzao. Na tabia ya kuwaita wenzao CCM B ikaanza.
..Lissu hajaongoza Cdm zaidi ya miezi mitatu kusema amevunja madaraja na vyama vingine ni kumuonea.
Lissu alikuwa Makamu Mwenyekiti wakati wa Mbowe kwa hiyo alihusika kikamilifu katika uvunjaji wa madaraja ulioanza chini ya Mbowe. Ni kama vile hauwezi kumuondoa Heche katika yanayo endelea sasa hivi.

Lissu alianza destruction alipoamua kwenda scorched earth dhidi ya Mbowe hata kabla ya kutangaza kugombea Uenyekiti. Alionyesha dhahiri kuwa hana imani nae na kuwa anamdharau. In public.

Kufanya vile ni lazima kuliwafanya viongozi wa vyama vingine wajiulize kuwa kama anaweza kumfanyia hivi Mbowe, sisi itakuwaje! Na baada ya ushindi ndio akaharibu kabisa. Badala ya kufuata ushauri wa kaka yake kuwa "magnanimous in victory" akakaza screws. Badala ya kutibu majeraha yaliyotokana na uchaguzi yeye akawa vindictive na vicious dhidi ya wale aliohisi walikuwa upande wa Mbowe. Hakuwa na sababu ya kum engua Catherine Ruge kwa kupitia sms. Alimshambulia yule dada wa Katavi kwa sababu tu alisimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bawacha ambapo his preferred candidate lost. Na aliyowafanyia waliounda kundi la G55 was deplorable. Hasa ukifikiria kuwa wengi wao walikuwa viongozi wenzake Chadema! Katika muda mfupi alioongoza alikuwa kama Musk na Doge.

Na aliwaachia surrogates wake watukane na waseme ovyo dhidi ya viongozi waliopita. Mtu makini angewafunga speed governor watu kama Hilda Newton lakini hakufanya hivyo. Hiyo ni dalili kuwa alikubaliana na maneno ya shombo yaliyokuwa yakitumiwa dhidi ya waliokuwa wenzake.

Lissu alitumia nyundo kuua mbu aliyetua usoni mwake.
Sasa hivi Chadema ni ya Lissu ndio maana wanahofia asipokuwepo nani atawaongoza. Wakati wa Mbowe viongozi wenye uwezo walikuwa wengi pamoja na Lissu. Amekiharibu sana chama chake.
..Mbowe alishindwa kusoma mood ya wanachama wake. Kwanza hakuwa muwazi kuhusu maridhiano. Pili alishindwa kupata matokeo ambayo wanachama waliyatarajia.
Mbowe alisoma vizuri mood ya wanachama na wananchi wake. Mbowe alikuwa muwazi mno kwa chama chake kuhusu majadiliano ya maridhiano. Na sehemu kubwa ya matakwa yake yalifanikiwa. Hayo ni pamoja na kuwezesha viongozi wenzake waliokuwa wamekimbia nchi kurudi. Pamoja na mikutano ya hadhara iliyokuwa imezuiwa kinyume cha Katiba kuruhusiwa. Pamoja na kuachiwa wanachama na wafuasi wa Chadema kibao waliokuwa mahabusu.

Hao wanachama unaosema kuwa aliwa disappoint walishindwa kusimama nae alipoitisha maandamano dhidi ya kupotea na kuuawa kwa wananchi! Wao na hawa mashujaa wa sasa walijificha na kumuachia Mbowe
,binti yake na wakina mama wachache. Shida ya wanachama na wananchi ni kuwa wanategemea viongozi wao wawafanyie kila kitu.

Ndicho kinacho endelea sasa hivi kwenye Chadema ya Lissu ambayo nje ya presa na mikutano michache ya hadhara ya Heche hamna kinacho endelea.
..Kilichomtokea Mbowe kinaweza kumtokea kiongozi yeyote yule aliyeshindwa kusoma alama za nyakati. Mbowe alipaswa kustaafu, na sio kusubiri ashindwe kwenye uchaguzi.
Kilichotokea kwa Mbowe ni betrayal ya hali ya juu ya watu aliyowaamini. Mbowe angestaafu angewapa nafasi watu kama Lissu kumchafua kwa namna walivyotaka. Ingekuwa coronation ya mfalme Lissu na sio uchaguzi wa kidemokrasia. Mbowe ameifanyia favor kubwa Chadema kwa kuwaonyesha jinsi uchaguzi wa wazi unavyopaswa kuwa na maana ya uadilifu unavyopaswa kuwa. Mtamkumbuka mtakavyofanya uchaguzi chini ya regime iliyopo. Natabiri kuwa wale wote watakaodiriki kugombea dhidi yao wataona cha mtema kuni. Yetu macho. Msiseme hamkutahadharishwa.

Amandla...
 
Ni mwendawazimu pekee ndiye anaweza kueleza kuwa kinachoendelea eti ni maridhiano.
Uliona wapi mtuhumiwa mkuu wa uovu anajigeuza kuwa msimamiz8 wa maridhiano!
Anatakiwa mtu neutral anayeaminika ndiye awe msimamiz8 mkuu wa maxungumzo yanayolenga maridhiano. Kwa sasa kinachoendelea ni upuuzi mtupu ambao yeyote anayetaka haki na ukweli hawezi kuungana nao. Hao CHAUMAwanafahamika kwa utapel8 wa kisiasa, hakuna chochote wanachosimamia zaidi ya matumbo yao.
Kwa vile umeniita mwenda wazimu sikujibu na nakuweka kwenye ignore list yangu ili usinipotezee wakati kusoma unacho andika. Kwa hali hiyo usijisumbue kunijibu maana sitaona.

Amandla...
 
Chadema itashiriki ila kwa condition waliyoweka, na kutoitisha maandamano pekee hakuwezi kuwa kigezo cha kuifanya isionekane ni chama kikuu cha siasa, hayo ni mambo yanayowezekana muda wowote.
Bado mnaamini kuwa serikali itakubali condition za Chadema? Serikali ambayo ilikiondoa kwenye uchaguzi baada ya kukataa kukubaliana na miongozi yao kuhusu ushiriki kwenye uchaguzi? Serikali ambayo badala ya kumuachia Lissu kama ambavyo Chadema inadai, imekata rufani katika kesi yake ya uhaini?
Uthibitisho wa kuwa chama kikuu cha upinzani ni uwezo wa chama hicho ku mobilize watu. Mpaka sasa hivi Chadema imeonyesha umahiri huo kwenye social media tu. Kujaza watu kwenye mikutano ya hadhara sio ishara inayotosha maana wanaohudhuria wanakuwa passive. Kuweza kuwaongoza katika kufanya maandamano ya amani ni ishara kubwa sana. Sasa chama kinachoogopa hata kuitisha maandamano kinakuwaje chama kikuu cha upinzani? Mbowe angalau aliitisha na alishiriki hata pale yalipokatazwa.

Amandla...
 
..mimi nadhani sio sawa vyama vya upinzani kubeba hoja za Ccm dhidi ya Chadema.
Hata kama mtazamo wako ni sahihi, tujiuze pamoja "unabebaje hoja za asiyetambua uwepo wako?' Kama ccm inaweza kuteka vyama 17 na kuviweka mfukoni na vikatii kuwa vikaragosi mimi najiuliza ushawishi na uwezo wa chadema kupambana na ccm bado ni wa mashaka na hautakiwi kukuzwa kwa viwango tunavyoaminishwa kwa maneno.
 
Bado mnaamini kuwa serikali itakubali condition za Chadema? Serikali ambayo ilikiondoa kwenye uchaguzi baada ya kukataa kukubaliana na miongozi yao kuhusu ushiriki kwenye uchaguzi? Serikali ambayo badala ya kumuachia Lissu kama ambavyo Chadema inadai, imekata rufani katika kesi yake ya uhaini?
Uthibitisho wa kuwa chama kikuu cha upinzani ni uwezo wa chama hicho ku mobilize watu. Mpaka sasa hivi Chadema imeonyesha umahiri huo kwenye social media tu. Kujaza watu kwenye mikutano ya hadhara sio ishara inayotosha maana wanaohudhuria wanakuwa passive. Kuweza kuwaongoza katika kufanya maandamano ya amani ni ishara kubwa sana. Sasa chama kinachoogopa hata kuitisha maandamano kinakuwaje chama kikuu cha upinzani? Mbowe angalau aliitisha na alishiriki hata pale yalipokatazwa.

Amandla...
Kule ambapo vyama vya upinzani huitisha maandamano huwa kuna haki za binadamu zinaheshimiwa, hapa kwetu ukiitisha maandamno unaitwa mhaini na waandamanaji wanaweza kuuliwa.

Sasa wewe ukiwa kama kiongozi wa chama cha upinzani kama Chadema utakubali kupeleka watu wako barabarani wakauliwe?!

Kama ukiamua kuwalinda ili wasiuliwe, huo sio udhaifu wala sababu ya kufanya Chadema kionekane dhaifu, bado ni chama kikuu cha siasa Tanzania, na sio chama kikuu cha upinzani kama ulivyoandika.

Ni chama kikuu cha siasa Tanzania kwasababu kina uungwaji mkono mkubwa kuzidi vyama vyote vya siasa vilivyopo.

Bado naamini pia, iko namna Chadema watafanya kukabialiana vizuri na CCM, kwasababu hata wakiendelea kususa au kuitegemea jumuia ya kimataifa inaonekana maisha bado yanaendelea kwa uoande wao.
 
Sio kweli. Hata Iran waliitisha maandamano. Afghanistan wanawake wanaandamana. Hata Mbowe aliitisha maandamano.

Hivi waandamanaji wangapi waliuawa kabla ya tarehe 29 2025? Chadema ilisema kuwa moja ya sababu za kutoshiriki kwenye uchaguzi ni kuepuka watu wake kuumizwa na hata kuuawa. Kwa kinajiitaje chama cha upinzani wakati hakishiriki kwenye uchaguzi na hakitaki kuandamana?

Ni udhaifu kuhofia chama kingine. Chadema kinaweza kujiita chochote kinachotaka lakini mpaka kitakapothibitisha uwanjani zitabaki ni tambo tu. Watabaki kuwa paper tigers.

Hamna uthibitisho wa hilo. Watu kuhudhuria mikutano sio uthibitisho. Ingekuwa hivyo basi Mwamposa amewazidi wakatoliki kwa kukubalika Tanzania.

Unajidanganya. Chadema ya leo imeshindwa kuchangisha milioni 300 hata baada ya miezi kupita. Chadema ya Mbowe ilichangiwa milioni 300 ndani ya siku mbili. Chadema ya sasa imeshindwa kufanya Mkutano Mkuu wakati ya Mbowe sio tu iliweza kufanya mikutano mikuu ya kwake na jumuia zake bali iliweza kuendesha uchaguzi mkuu ambao umekuwa kigezo kwa taifa wa namna ya kuendesha uchaguzi ulio huru, wazi na wa haki.
Chadema ya sasa inatembelea nyota na msingi wa Chadema ya Mbowe. Bahati mbaya wameshindwa kuiendeleza na wamebaki kwenye majigambo.

- Hayo maandamano ya Iran na Afghan yanaitishwa kila mara lakini hayajawahi kufikia malengo ya kuiondoa regime kwenye mataifa yao.

Kwa msingi huu sioni uthabiti wa huu mfano wako, kuitisha maandamano lazima kufikie lengo kusudiwa ili kutolewe mfano, sio kuandamana just for the sake of it mnaishia kuuwawa.

- Chadema ni chama cha siasa kinachosimamia misingi ya haki, kama ni uchaguzi uwe huru na wa haki, sio huu uchafuzi unaotaka kuubariki kwa kuuita uchaguzi.

CCM wakitaka Chadema washiriki uchaguzi sharti wawe tayari kukubali matokeo, sio kushiriki uchaguzi huku wanaegemea msaada wa vyombo vya dola ili washinde.

Hata maandamano kama yasipozuiwa na vyombo vya dola yatafanyika kwa sababu kuandamana sio vita ni haki kisheria.

- Chadema ni chama kikuu cha siasa Tanzania, hili hawahitaji kuthibitisha popote, na kwasababu hiyo, ndio maana CCM wanawaogopa kwa kuitisha chafuzi zisizo za haki, kwasababu CCM wanajua fika, kama wakiitisha uchaguzi huru na haki hawawezi kuishinda Chadema, nakushangaa hata hili tubishane pia!.

- Uthibitisho upo nimeshakuonesha hapo juu, sina sababu ya kuurudia hapa, suala la Mwamposa kuwazidi wakatoliki nalo sioni kama lina make sense hapa.

- "Chadema ya Mbowe" huu msemo unautoa wapi?

Chadema sio ya mtu binafsi, ile ni tasisi mali ya umma, iliyo chini ya wanachama na wafuasi wake, hivyo futa huo msemo wako sio sahihi.

Suala la michango nalo ni jepesi tu, Chadema inachangiwa malengo yanafikiwa. Kilichokwamisha mkutano wa baraza kuu kufanyika ni kesi ya Lissu iliyokuwa mahakamani.

Hata suala la muda wa michango kuoatikana, hili nalo kwangu silioi uzito endapo mwisho wa siku pesa zinapatikana na mipango iliyokusudiwa inafanyika.
 
Hivi unadhani mtesi wako atakupa unachotaka wakati anajua kuwa unaogopa kufungwa, kuumizwa hata kuuawa? Wakina Martin Luther King Junior waliandamana wakati wakijua thika kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufungwa, kuumizwa na hata kuuawa. Yote hayo yaliwapata lakini hayakuwakatisha tamaa na waliendelea kuandamana. Wanawake wa Iran wamenyongwa lakini hawakomi. Nyinyi mnataka mletewe mabadiliko kwenye sahani mkiwa beach. Mbowe alielewa kuna kuumizwa na hakukata tamaa. Maalim vile vile.

Kwa hiyo mnadhani mtapata huo uchaguzi mnaotaka kwa kujifungia chumbani na kuandika kwenye social media? CCM wanataka kushinda na watatumia kila mbinu ili washinde. Hilo mlipaswa kujua na kujiandaa kukabiliana nalo.

Siwezi kukubishia kama hivyo ndivyo unavyo amini. Mimi sidhani kuwa CCM inaiogopa Chadema ya Lissu maana inajua kuwa ni wababe wa majukwaani. Waliwaogopa watu kama Mbowe na Maalim maana walijua kuwa wana uwezo wa kusimamia jambo wanalotaka na kushawishi wengine kujiunga nao. Hawa wameonyesha kuwa na uwezo wa kujenga vyama vyao mpaka kuwa tishio.

Uthibitisho hauwi uthibitisho kwa sababu wewe umeuita uthibitisho. Suala la Mwamposa lina mantik kwa sababu Chadema inaamini ina wafuasi wengi kwa sababu ya mahudhurio katika mikutano yao ya hadhara. Ndio maana nikasema hata Mwamposa anapata watu wengi katika mikutano yake. Hilo halifanyi dhehebu lake kuwa kubwa Tanzania.

Tunasema ya Mbowe kwa sababu ni yeye alikuwa anaiongoza wakati tunaouzungumzia. Hii inatofautisha Chadema ya wakati ule na ya sasa. Sasa hivi tunasema CCM ya Samia kutofautishaza JPM, Kikwete Mwinyi na Nyerere.

Kisingizio tu. Usanii usio na maana. Kwani walivyotangaza hawakujua kuwa Lissu ana kesi Mahakamani? Hawana pesa lakini hawataki kusema. Ndio maana hatusikii lolote kuhusu Tonetone.

Zitapatikana lini? Na vipi?

- Ndio maana nikasema suala la kupigania haki ni endelevu, limeshaanza na litaendelea mpakahaki zitakapopatikana, kutoandamana kwao leo, haina maana hawataandamana milele.

- Naendelea kusisitiza, mabadiliko yoyote ni mchakato, ni suala linalohitaji muda na sio hivi unavyofanya kuhukukumu kama vile dunia imeshafika mwisho leo!.

- Kama CCM hawamuogopi Lissu wasingemfunga jela kwa kosa la uongo ambalo hakushtakiwa nalo. Hii pekee ni sababu moja kunwa kuonesha vile CCM wanataka Lissu asiwepo uraiani ili asiwasumbue.

- Suala la Mwamposa nakwambia tena huo mfano hauendani na hiki tunachojadili hapa, Mwamposa yuko madhabahuni sio mwanasiasa, hajawahi kupigiwa kura popote.

Chadema wamepigiwa kura mara nyingi sehemu nyingi ndio maana CCM ikaona dawa ya kuwapoteza ni kuwaibia kura zao, sijui kwanini unakataa vitu simple kama hivi!.

- Mtu binafsi hawezi kumiliki chama cha siasa ambacho ni mali ya umma, huo msemo popote unapotumika sio sahihi, hakuna Chadema ya Mbowe, wala CCM ya Samia.. CCM ina wenyewe wafuasi na wanachama na Chadema hivyo hivyo.

- Suala la michango unavyosema kisingizio tu sijui una ushahidi gani zaidi ya ukimya wao kuuchukulia kama kigezo cha kuwahukumu.

Nachokumbuka ile michango ilikuwa inaenda vizuri tu, lakini mpaka sasa bado wapo kimya na sababu ya ukimya wao siijui, tusubiri muda utatoa majibu.
 
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.

Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.

Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Hiki wanacholilia leo CDM ikiwaambia kabla ya uchaguzi tuwaukize mlikua mnaharakisha nini kwa faida ya nani? Na baada ya uchaguzi wote mlikubaliana kua kila kitu kilikua sawa sasa mnataka mkubaliane kitu gani ambacho hamjayofautiana wakati wowote,nani analeta matatizo ni nyie au CDM?
 
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.

Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.

Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Tawi la ccm kazini
 
Vyama vyetu vya kisiasa vinaongopa sana, Tena kwa kiwango ambacho huwezi hata sema.
Hawa viongozi nao ni malaika na hawajawahi hata kumuona shetani.
Nadhani umalaika wao wanatakiwa wajipime na historia zao kule walikotoka na hapo walipo ndo wawe na ujasiri wa kuchambana wenyewe na vyama vyao
 
..masharti ya Chadema kushiriki mazungumzo yana mantiki.

..kwa mfano kutaka mazungumzo yasimamiwe na Msuluhishi toka nje asiye na upande ni hoja yenye mashiko na maslahi kwa taifa letu.
Na napendekeza awe Rais Mastaafu wa Nigeria Mh Goodluck Ebele Jonathan.
 
- Ndio maana nikasema suala la kupigania haki ni endelevu, limeshaanza na litaendelea mpakahaki zitakapopatikana, kutoandamana kwao leo, haina maana hawataandamana milele.
Itaendelea kwa kungoja hisani ya wanaotawala?
- Naendelea kusisitiza, mabadiliko yoyote ni mchakato, ni suala linalohitaji muda na sio hivi unavyofanya kuhukukumu kama vile dunia imeshafika mwisho leo!.
Chadema si ndio wanasema kuwa Mbowe aliwachelewasha? Wakasema huu ni wakati wa siasa za nginja nginja! Na wakaipa serikali miezi ya kubadilisha Katiba. Hilo la "suala linahitaji muda" lilikuwa wapi?
- Kama CCM hawamuogopi Lissu wasingemfunga jela kwa kosa la uongo ambalo hakushtakiwa nalo. Hii pekee ni sababu moja kunwa kuonesha vile CCM wanataka Lissu asiwepo uraiani ili asiwasumbue.
On the contrary. CCM na serikali yake hawamuogopi Lissu na Chadema yake. Ndio maana wanawafanyia wanavyotaka. Ili kuwaonyesha ubabe wao wamekata rufaa ili Lissu akae zaidi gerezani baada ya Chadema kusema wazi kuwa hawashiriki katika mazungumzo yeyote wakati Lissu akiwa kifungoni. CCM wamewasoma na wanajua hamtafanya lolote. Mimi nadhani wanawadharau.
- Suala la Mwamposa nakwambia tena huo mfano hauendani na hiki tunachojadili hapa, Mwamposa yuko madhabahuni sio mwanasiasa, hajawahi kupigiwa kura popote.
Hauwezi kunielewa. Tuishie hapo.
Chadema wamepigiwa kura mara nyingi sehemu nyingi ndio maana CCM ikaona dawa ya kuwapoteza ni kuwaibia kura zao, sijui kwanini unakataa vitu simple kama hivi
CCM haikuanza kuiba au kucheza rafu kwa Chadema peke yake. CCM ilifuta uchaguzi Zanzibar walipoona Maalim ameshinda uchaguzi wa urais. Walifuta kura za Zanzibar wakaacha za Muungano. CUF iliposusa kushiriki kwenye marudio, wao waliendelea na kujitangaza kuwa wameshinda na walitawala kwa miaka mingine mitano bila ushiriki wa CUF. Mimi ndio maana nashangaa imani yenu kuwa mkikaa pembeni CCM watawabembeleza. Mwalimu wa Chaumma alikuwa sahihi aliposema kuwa "ukiisusia CCM chakula kwenye shughuli wanaondoka na sufuria kabisa". Bahati mbaya Chadema haikumuelewa.
- Mtu binafsi hawezi kumiliki chama cha siasa ambacho ni mali ya umma, huo msemo popote unapotumika sio sahihi, hakuna Chadema ya Mbowe, wala CCM ya Samia.. CCM ina wenyewe wafuasi na wanachama na Chadema hivyo hivyo.
Tunaposema Chama ni cha fulani tunazungumzia uongozi na sio milki. Ninaposema Chadema ya Lissu nina maanisha Chadema inayoongozwa na Lissu. Kama hilo hauelewi sina namna ya kujusaidia.
- Suala la michango unavyosema kisingizio tu sijui una ushahidi gani zaidi ya ukimya wao kuuchukulia kama kigezo cha kuwahukumu.
Lissu na Heche waliahidi kuwa wawazi kwenye mapato na matumizi ya chama chao. Ingekuwa hali yao ya kifedha ni nzuri wangetangaza ili kuonyesha kuwa wao ni ngangari. Ukimya wao katika kufanya siasa ni ushahidi mwingine kuwa hali sivyo.
Nachokumbuka ile michango ilikuwa inaenda vizuri tu, lakini mpaka sasa bado wapo kimya na sababu ya ukimya wao siijui, tusubiri muda utatoa majibu.
Historia ya michango katika Chadema ya Lissu sio nzuri. Sio kwamba wanakwiba ila nahisi huwa haiendi kama walivyotarajia. Mpaka leo sijui kama Lissu alinunuliwa gari. Ndio maana sidhani kama wana pesa za kutayarisha Mkutano Mkuu na kutimiza majukumu yao mengine.

Mimi naona niishie hapa. Nakushukuru sana kwa mjadala mzuri lakini sitakujibu tena kwenye suala hili.

Amandla...
 
Sio lazima. Majadiliano yanapaswa kuwa ya hiari. Chama kisichotaka kukaa mezani hakiwezi kulazimishwa kukaa mezani. Hivyo hivyo hamna chama chenye haki ya kulazimisha chama kingine kisishiriki katika majadiliano kwa sababu yeyote ile. Kushiriki au kutoshiriki ni uamuzi wa kila chama.
Amandla...
Sasa kwanini mnapiga kelele na Chadema,si mkae mzungumze wenyewe.
 
Back
Top Bottom