CHAUMMA yaionya CHADEMA, wasituletee migogoro

Sasa kama Chadema hakitaki kushiriki kilazimishwe? Huo uungwaji mkubwa ulitakiwa kuthibitishwa kwa vitendo. Kama ni kweli kinakubalika hivyo kingeitisha maandamano ya amani kushinikiza Mwenyekiti wao aachiwe. Chadema ya Mbowe ilikuwa active lakini hii ya Lissu ni performative zaidi. Ndio maana CCM haikijali. Ushujaa wa kwenye social media hautaleta mabadiliko hata siku moja.

Amandla...

..Vyama vya upinzani navyo viweke shinikizo kwamba mapendekezo ya Chadema yafanyiwe kazi kabla ya maridhiano.
 
..itajenga precedence kwa viongozi wa vyama vya upinzani kufungwa kihunihuni na wakaachwa bila utetezi wa vyama vingine.
Precedence hapa imewekwa na Chadema. Fundisho ni kuwa siasa za Tanzania zinahitaji ushirikiano. Uki antagonise wenzako watakuacha uumie peke yako.
..Chadema wakienda kwenye maridhiano bila Tundu Lissu, mbele ya safari hakuna chama kitaweza kuweka msimamo kama huu walionao Chadema sasa hivi.
Shida ya Chadema ya sasa hivj ni kuwa wigo lao la uongozi ni shallow sana. Hamuoni kuwa kusema kuwa ni Lissu peke yake ndio anaweza kufanya jambo fulani ni alama ya weakness wa Chadema. Pool yao ya uongozi ni very shallow. Nadhani hata kama atatoka msimamo wa Chadema utakuwa wa kwao peke yao. Hana uwezo wa kuunganisha watu kama aliokuwa nao Mbowe.
..Msuluhishi wa Kimataifa atasaidia kuweka usawa ambao ni vigumu kuupata kwa wasuluhishi wa ndani. Na hiyo ni faida kwa vyama vyote. Yeyote atakayeteuliwa toka ndani ya Tanzania, bila shaka atakuwa ni mtu aliyepata kutumikia, na kuteuliwa, hapo kabla ktk serikali ya Ccm.
Msuluhishi wa kimataifa sio panacea ya matatizo ya Tanzania. Kusema kuwa hakuna mtu Tanzania anaweza kufanya hiyo kazI ni mtu wa nje peke yake ni kujidhalilisha.
..Vyama vya upinzani navyo viweke shinikizo kwamba mapendekezo ya Chadema yafanyiwe kazi kabla ya maridhiano.
Hawawezi kwa sababu hayo mapendekezo ni ya Chadema na sio yao.
Chadema wanayalinda kwa wivu mkubwa hivyo itakuwa kupoteza muda vyama vingine kuyabeba.
Chadema haina tofauti na CCM kwa namna inavyotaka kuburuza wengine.

Amandla...
 
Precedence hapa imewekwa na Chadema. Fundisho ni kuwa siasa za Tanzania zinahitaji ushirikiano. Uki antagonise wenzako watakuacha uumie peke yako.

Shida ya Chadema ya sasa hivj ni kuwa wigo lao la uongozi ni shallow sana. Hamuoni kuwa kusema kuwa ni Lissu peke yake ndio anaweza kufanya jambo fulani ni alama ya weakness wa Chadema. Pool yao ya uongozi ni very shallow. Nadhani hata kama atatoka msimamo wa Chadema utakuwa wa kwao peke yao. Hana uwezo wa kuunganisha watu kama aliokuwa nao Mbowe.

Msuluhishi wa kimataifa sio panacea ya matatizo ya Tanzania. Kusema kuwa hakuna mtu Tanzania anaweza kufanya hiyo kazI ni mtu wa nje peke yake ni kujidhalilisha.

Hawawezi kwa sababu hayo mapendekezo ni ya Chadema na sio yao.
Chadema wanayalinda kwa wivu mkubwa hivyo itakuwa kupoteza muda vyama vingine kuyabeba.
Chadema haina tofauti na CCM kwa namna inavyotaka kuburuza wengine.

Amandla...

..Tundu Lissu anatajwa kwasababu ni Mwenyekiti wa Chadema. Hiyo ni kama kipindi kile Chadema walisema Mbowe lazima awe huru ndipo wazungumze na Ccm.

..Mapendekezo ya Chadema yanaweza kuungwa mkono na chama chochote cha upinzani kinachoitakia mema Tanzania. Manyanyaso wanayopitia Chadema sasa hivi yakiachwa yanaweza kuvikuta vyama vingine mbele ya safari.
 
..masharti ya Chadema kushiriki mazungumzo yana mantiki.

..kwa mfano kutaka mazungumzo yasimamiwe na Msuluhishi toka nje asiye na upande ni hoja yenye mashiko na maslahi kwa taifa letu.
Hawakusema awe wa nje tu bali nje au ndani ya nchi. Bahati nzuri tamko limeandikwa hivyo lisomwe kwa ukamilifu.

Hata hivyo mazungumzo hayakwepeki kwani hata hayo wanayotoa kama masharti yanahitaji kuzungumzwa na kukubaliana kama anatoka nje au ndani apatikaneje. Jambo linaloleta matumaini kwamba watafikia wakati wa kuzungumza ni kuona hata masharti waliyoanza nayo yamepungua sana na sasa wamebaki na mawili.

"Talks about talks" haikwepeki.
 
Bado swali linabaki pale pale. Huyo msuluhishi atapatikanaje bila pande zote kukaa na kukubaliana utaratibu wa kumpata anaekubalika na wote?

Amandla...
Rahisi kabisa. Vyama vinavyoshiriki kwenye mchakato wa maridhiano kupiga kura. Kila chama kitakuwa na kura moja tu. Jina litakalopata kura nyingi ndiye atakuwa msuluhishi. Huo ndio utaratibu wa kiungwana na kidemokrasia.
 
Hawakusema awe wa nje tu bali nje au ndani ya nchi. Bahati nzuri tamko limeandikwa hivyo lisomwe kwa ukamilifu.

Hata hivyo mazungumzo hayakwepeki kwani hata hayo wanayotoa kama masharti yanahitaji kuzungumzwa na kukubaliana kama anatoka nje au ndani apatikaneje. Jambo linaloleta matumaini kwamba watafikia wakati wa kuzungumza ni kuona hata masharti waliyoanza nayo yamepungua sana na sasa wamebaki na mawili.

"Talks about talks" haikwepeki.

..Masharti yao yanatekelezeka.

..Wadau wengi zaidi wanatakiwa washinikize Lissu aachiwe.

..Vyama vya upinzani viungane na taasisi kama TLS kupaza sauti Lissu aachiwe.

..Huu ni muda wa vyama vya upinzani kuwa na sauti moja.
 
Vyama vya upinzani viungane au viunganishwe na CHADEMA? Unaona hili linawezekana wakati CHADEMA inaamini yenyewe ndiyo upinzani katika nchi hii?

Hata katika mambo ya kawaida tunatafutana ili kuongeza nguvu na si anayejiona kuwa na nguvu kujitenga huku akitaka wadogo waungane naye.

Tuisaide CHADEMA kwa kuwapa ushauri wa kweli. Wanawaita wenzao vyama vya mfukoni, wewe unasema vyama vyote vya upinzani viungane na CHADEMA!!!!
 
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.

Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.

Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Kigaila yuko sahihi 100%,
malalamiko ya teki kupitia chadema yasichanganywe na mambo mengine ya kitaifa.

shida zao wazitatue kivyao nje ya waTanzania wote walioamua kusonga mbele kujenga taifa lao kwa umoja 🐒
 
Rahisi kabisa. Vyama vinavyoshiriki kwenye mchakato wa maridhiano kupiga kura. Kila chama kitakuwa na kura moja tu. Jina litakalopata kura nyingi ndiye atakuwa msuluhishi. Huo ndio utaratibu wa kiungwana na kidemokrasia.
Mazungumzo yanayolenga kuzaa maridhiano si ya vyama vya siasa pekee.
 
..Tundu Lissu anatajwa kwasababu ni Mwenyekiti wa Chadema. Hiyo ni kama kipindi kile Chadema walisema Mbowe lazima awe huru ndipo wazungumze na Ccm.
Mbowe alizungumziwa na wengi. Hata wakina Zitto walimzungumzia. Mbowe aliishajenga haiba ya kukubalika na vyama vingine vya upinzani.
Lissu ni tofauti. Yeye na chama chake wamevunja madaraja yote ambayo Mbowe alijenga. Hakuna kiongozi wa chama cha upinzani atakuwa na imani na Chadema baada ya kuona walivyomtendea kiongozi wao aliyepita pamoja na viongozi wengine waandamizi waliodiriki kutofautiana na fikra sahihi za uongozi mpya. Heche aliangalia tu wakati kiongozi wa Bawacha anafanyiwa fujo katika mkutano wake. Heche huyo huyo alisimama jukwaani na kumsemea ovyo Suzan Kiwanga ambae alitumia Chadema kwa muda mrefu katika Kamati Kuu yao. Wanaangali jinsi uongozi wa Chadema unawaangalia tu baadhi ya viongozi wake wanapomzulia kafya Mwenyekiti wake aliyepita. Unadhani Zitto na Dorothy wataingia kirahisi kushirikiana na chama kama hicho?
..Mapendekezo ya Chadema yanaweza kuungwa mkono na chama chochote cha upinzani kinachoitakia mema Tanzania. Manyanyaso wanayopitia Chadema sasa hivi yakiachwa yanaweza kuvikuta vyama vingine mbele ya safari.

Mbona yaliisha wakuta wengi kama CUF, NCCR Mageuzi, DPP n.k.? Chadema walisema hii ngoma ni ya kwao na CCM wanammudu. Waonyeshe basi umahiri wao!

Ushauri wangu kwao ni wajitahidi kujenga madaraja kwa wenzao waliokosana nao ili waweze kujipanga upya kukabiliana na CCM kwa pamoja.

Amandla...
 
..Vyama vya upinzani navyo viweke shinikizo kwamba mapendekezo ya Chadema yafanyiwe kazi kabla ya maridhiano.
Kila chama kina malengo yake. Hakuna chama ambacho kipo kwa ajili ya kusaidia chama kingine kifikie mafanikio yake. Haiwezekani chama kinachojiona chenyewe ndo upinzani katika nchi hii kisaidwe na vyama vya mfukoni. Tuwe wakweli, tusiwadanganye CHADEMA. Wanasema watanzania wako pamoja nao hivyo hawahitaji msaada wa vyama vya mfukoni.
 
..mimi nadhani sio sawa vyama vya upinzani kubeba hoja za Ccm dhidi ya Chadema.
 
Mbowe alizungumziwa na wengi. Hata wakina Zitto walimzungumzia. Mbowe aliishajenga haiba ya kukubalika na vyama vingine vya upinzani.
Lissu ni tofauti. Yeye na chama chake wamevunja madaraja yote ambayo Mbowe alijenga. Hakuna kiongozi wa chama cha upinzani atakuwa na imani na Chadema baada ya kuona walivyomtendea kiongozi wao aliyepita pamoja na viongozi wengine waandamizi waliodiriki kutofautiana na fikra sahihi za uongozi mpya. Heche aliangalia tu wakati kiongozi wa Bawacha anafanyiwa fujo katika mkutano wake. Heche huyo huyo alisimama jukwaani na kumsemea ovyo Suzan Kiwanga ambae alitumia Chadema kwa muda mrefu katika Kamati Kuu yao. Wanaangali jinsi uongozi wa Chadema unawaangalia tu baadhi ya viongozi wake wanapomzulia kafya Mwenyekiti wake aliyepita. Unadhani Zitto na Dorothy wataingia kirahisi kushirikiana na chama kama hicho?

Mbona yaliisha wakuta wengi kama CUF, NCCR Mageuzi, DPP n.k.? Chadema walisema hii ngoma ni ya kwao na CCM wanammudu. Waonyeshe basi umahiri wao!

Ushauri wangu kwao ni wajitahidi kujenga madaraja kwa wenzao waliokosana nao ili waweze kujipanga upya kukabiliana na CCM kwa pamoja.

Amandla...

..kama ni madaraja kuvunjika kati ya Cdm na vyama vingine itakuwa ni kipindi cha Mbowe.

..Lissu hajaongoza Cdm zaidi ya miezi mitatu kusema amevunja madaraja na vyama vingine ni kumuonea.

..Mbowe alishindwa kusoma mood ya wanachama wake. Kwanza hakuwa muwazi kuhusu maridhiano. Pili alishindwa kupata matokeo ambayo wanachama waliyatarajia.

..Kilichomtokea Mbowe kinaweza kumtokea kiongozi yeyote yule aliyeshindwa kusoma alama za nyakati. Mbowe alipaswa kustaafu, na sio kusubiri ashindwe kwenye uchaguzi.
 
Sasa kama Chadema hakitaki kushiriki kilazimishwe? Huo uungwaji mkubwa ulitakiwa kuthibitishwa kwa vitendo. Kama ni kweli kinakubalika hivyo kingeitisha maandamano ya amani kushinikiza Mwenyekiti wao aachiwe. Chadema ya Mbowe ilikuwa active lakini hii ya Lissu ni performative zaidi. Ndio maana CCM haikijali. Ushujaa wa kwenye social media hautaleta mabadiliko hata siku moja.

Amandla...
Chadema itashiriki ila kwa condition waliyoweka, na kutoitisha maandamano pekee hakuwezi kuwa kigezo cha kuifanya isionekane ni chama kikuu cha siasa, hayo ni mambo yanayowezekana muda wowote.
 
Back
Top Bottom