hip hop uchwara
JF-Expert Member
- Jan 13, 2023
- 7,772
- 5,752
Yericko Nyerere matacco yenu
Kila nikikusoma naona una chuki na huu uongozi wa Lissu, hiki ndicho chanzo kikuu cha huu ubishani unaoendeleza muda wote.Itaendelea kwa kungoja hisani ya wanaotawala?
Chadema si ndio wanasema kuwa Mbowe aliwachelewasha? Wakasema huu ni wakati wa siasa za nginja nginja! Na wakaipa serikali miezi ya kubadilisha Katiba. Hilo la "suala linahitaji muda" lilikuwa wapi?
On the contrary. CCM na serikali yake hawamuogopi Lissu na Chadema yake. Ndio maana wanawafanyia wanavyotaka. Ili kuwaonyesha ubabe wao wamekata rufaa ili Lissu akae zaidi gerezani baada ya Chadema kusema wazi kuwa hawashiriki katika mazungumzo yeyote wakati Lissu akiwa kifungoni. CCM wamewasoma na wanajua hamtafanya lolote. Mimi nadhani wanawadharau.
Hauwezi kunielewa. Tuishie hapo.
CCM haikuanza kuiba au kucheza rafu kwa Chadema peke yake. CCM ilifuta uchaguzi Zanzibar walipoona Maalim ameshinda uchaguzi wa urais. Walifuta kura za Zanzibar wakaacha za Muungano. CUF iliposusa kushiriki kwenye marudio, wao waliendelea na kujitangaza kuwa wameshinda na walitawala kwa miaka mingine mitano bila ushiriki wa CUF. Mimi ndio maana nashangaa imani yenu kuwa mkikaa pembeni CCM watawabembeleza. Mwalimu wa Chaumma alikuwa sahihi aliposema kuwa "ukiisusia CCM chakula kwenye shughuli wanaondoka na sufuria kabisa". Bahati mbaya Chadema haikumuelewa.
Tunaposema Chama ni cha fulani tunazungumzia uongozi na sio milki. Ninaposema Chadema ya Lissu nina maanisha Chadema inayoongozwa na Lissu. Kama hilo hauelewi sina namna ya kujusaidia.
Lissu na Heche waliahidi kuwa wawazi kwenye mapato na matumizi ya chama chao. Ingekuwa hali yao ya kifedha ni nzuri wangetangaza ili kuonyesha kuwa wao ni ngangari. Ukimya wao katika kufanya siasa ni ushahidi mwingine kuwa hali sivyo.
Historia ya michango katika Chadema ya Lissu sio nzuri. Sio kwamba wanakwiba ila nahisi huwa haiendi kama walivyotarajia. Mpaka leo sijui kama Lissu alinunuliwa gari. Ndio maana sidhani kama wana pesa za kutayarisha Mkutano Mkuu na kutimiza majukumu yao mengine.
Mimi naona niishie hapa. Nakushukuru sana kwa mjadala mzuri lakini sitakujibu tena kwenye suala hili.
Amandla...
Chadema haina mgogoro na yeyote. Maridhiano hayahitajiki
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.
Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.
Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.
Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Taasisi za dini ukiondoa BAKWATA Zina migogoro na serikali mkubwa tu.Kwani mpango ni kila chama na taasisi kinatakiwa kiridhiane na CCM kivyake vyake? Taasisi za dini zipi zina migogoro na CCM?
Amandla...
Nimejadiliana na wewe kwa muda mrefu kwa sababu niliamini kuwa tunajadiliana in good faith. Sijakutupia aspersions zozote. Sijahoji uelewa wako kwa sababu naamini kuwa una haki ya kuwa na msimamo wako.Kila nikikusoma naona una chuki na huu uongozi wa Lissu, hiki ndicho chanzo kikuu cha huu ubishani unaoendeleza muda wote.
Until utakapojirudi uwe normal, ndipo akili yako itaanza kufikiria kwa mtazamo chanya.
Hata Mbowe licha ya kukaa madarakani zaidi ya miaka 20 bado hakuweza kuipeleka Chadema ikulu, sasa iweje kwa Lissu mwenye mwaka tena muda mwingi akiwa jela ndio umhukumu vibaya?!
Naweza kuendelea kukujibu hapa mpaka kesho, lakimi kama hutafunguka kifikra uache chuki uliyonayo kwa kina Lissu, basi nina hakika hatutaweza kufikia muafaka.
Mambo mengi unayojadili kama Mbowe kuwachelewesha hayo ni mawazo tu ya individuals ambayo sioni sababu kwanini uyabebe muda wote kichwani.
Kwa kweli...Mzee Lazarus Chakwera alipokuja kwa kutumwa na Jumuiya ya Madola, wadau wote walikubali kuzungumza naye.
..Binafsi naamini wako watu Mashuhuri Afrika na Jumuiya ya Madola ambao wanaweza kusaidia mgogoro wetu.
..Bahati mbaya Ccm, na vyama rafiki zake, wanaangalia maslahi ya Ccm, badala ya kutanguliza maslahi ya NCHI.
..Ccm bado wanaamini wana nafasi ya kufanya janjajanja kupitia maridhiano.