CHAUMMA yaionya CHADEMA, wasituletee migogoro

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.

Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.

Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Chaumma Wana shida gani na chadema?
 
Aisee hayajawapata kama wenzio. tafakari
 
CHAUMMA mlionywa mapema sana mkaambiwa Hela za Abdul hamtaziweza masharti yake na usipoyatimiza lazima uchague moja UFIRW**** au Wakuue sasa naona Mzee wangu hapo Kigaila anawaza hizo Hela za Abdul alizokula anazirudishaje na misheni zao kuhusu CDM zinafeli tu🚮
 
Attachments

  • FB_IMG_1794148138861.jpg
    FB_IMG_1794148138861.jpg
    20.4 KB · Views: 5

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimesema kuwa ili ukweli ujulikane na haki itendeke, ni muhimu kufanyika kwa mazungumzo yatakayowezesha pande husika kuwasilisha hoja zao na kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 25, 2026 mkoani Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa CHAUMMA, Benson Kigaila, amesema chama hicho hakioni sababu ya CHADEMA kutaka ukweli ujulikane bila kuwa tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Kigaila amesema kuwa iwapo CHADEMA wana hoja binafsi au malalamiko yanayohusu chama chao, wanapaswa kutafuta njia za kuyatatua badala ya kuyachanganya na masuala mengine.

Ameongeza kuwa masuala yanayohusu maslahi ya kitaifa yanapaswa kujadiliwa kwa pamoja kwa kukaa mezani ili kila upande uweze kutoa hoja zake na kusikilizana.

Amesema ni vyema pande husika zikashiriki katika mazungumzo hayo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Nyokooooo nyokoo CHAUMA WOTEE nyokooo
 
Kukubali matokeo kunaweza kusababishwa na vitu vingi. Al Gore alikubali matokeo ya Florida ingawa alijua thika kuwa mdogo wake George W amemchezea mchezo mbaya.

Chaumma kinaweza kuamua kukubali matokea kwa nia ya kuepusha balaa ambayo ingeweza kutokea.

Amandla...
Balaa gani hiki chama cha wapiga deal? Hii CCM B hainaushawishi wowote na watanzania wengi wala hawajui kama kuna chama kama hiki. Ujinga wenu kuna siku utawaangamiza.
 
..hiyo Rufaa ambayo Dpp amekata kuhusu Tundu Lissu inapaswa kuwa alert / taa nyekundu kwa vyama vyote kuhusu nia ya serikali kuleta maridhiano.
Inawezekana uko sahihi.
..chama kimoja cha upinzani kikiumizwa vyama vyote vya upinzani vinapaswa kuchukulia kuwa navyo vimeumizwa.
Inapaswa kuwa hivyo. Tatizo ni kwamba Chadema imejitenga na vyama vingine na kujiona peke yao ndio wapinzani. Hivyo si ajabu vyama vingine kuiacha Chadema ipambane yenyewe. Si
..Kwa maoni yangu, ushiriki wa Chadema unaongeza nguvu ktk hoja na madai ya upinzani kwa ujumla.
Ingekuwa vizuri sana lakini Chadema haina mpango wa kushirikiana na wenzake na hawezi kulazimishwa.
..Ingependeza kama vyama vyote vya upinzani vingetoa msimamo kwamba hoja za Chadema za kuachiwa kwa Mwenyekiti wao na uwepo wa Msuluhishi huru zizingatiwe.
Chadema ingewashirikisha ingekuwa rahisi kufanya hivyo. Sasa hivi vyama vingine vitasita kuunga mkono hoja hizo kwa sababu Chadema imeisha wahukumu kuwa wao ni mamluki wa CCM. Unashiriki vipi na mtu ambae hana imani na wewe?
..Madai ya Chadema kwa maoni yangu ni kwa faida ya vyama vyote vya upinzani, na yamelenga kuleta maridhiano ya kweli ktk nchi yetu.
Madai haya kwa jinsi yalivyo ni kwa faida ya Chadema. Kwa mfano kuachiliwa Lissu kutawasaidia vipi Chaumma na ACT-WAZALENDO? Maridhiano wanayotaka Chadema ni kati yao na CCM na sio vyama vingine au hata taifa kwa ujumla.

Amandla...
 
Huwezi kuja na kauli kama hii huku ukijua fika maridhiano yanalenga kuliunganisha taifa, kisha ukakiacha nje chama chenye uungwaji mkono mkubwa zaidi ya vingine vyote, hayo maridhiano yatakuwa sawa na maigizo tu na tatizo litabaki palepale.
Sasa kama Chadema hakitaki kushiriki kilazimishwe? Huo uungwaji mkubwa ulitakiwa kuthibitishwa kwa vitendo. Kama ni kweli kinakubalika hivyo kingeitisha maandamano ya amani kushinikiza Mwenyekiti wao aachiwe. Chadema ya Mbowe ilikuwa active lakini hii ya Lissu ni performative zaidi. Ndio maana CCM haikijali. Ushujaa wa kwenye social media hautaleta mabadiliko hata siku moja.

Amandla...
 
Mbona simple tu.Akipatikana kwenye nchi zenye mawazo positive ukiondoa Uganda,Rwanda,Sudani,Mali,Sudani Kusini,Msumbiji,Eritrea,Djibout,Ethiopia na DRC mbona maridhiano yanawezekana???Pia kuna nchi kama Urusi hawastahili hata kidogo kuwa wasuluhishi wa mogogoro yetu.
Mnajua mno kurahisisha mambo. Ingekuwa hivyo arbitration ingekuwa rahisi sana.

Amandla...
 
Inawezekana uko sahihi.

Inapaswa kuwa hivyo. Tatizo ni kwamba Chadema imejitenga na vyama vingine na kujiona peke yao ndio wapinzani. Hivyo si ajabu vyama vingine kuiacha Chadema ipambane yenyewe. Si

Ingekuwa vizuri sana lakini Chadema haina mpango wa kushirikiana na wenzake na hawezi kulazimishwa.

Chadema ingewashirikisha ingekuwa rahisi kufanya hivyo. Sasa hivi vyama vingine vitasita kuunga mkono hoja hizo kwa sababu Chadema imeisha wahukumu kuwa wao ni mamluki wa CCM. Unashiriki vipi na mtu ambae hana imani na wewe?

Madai haya kwa jinsi yalivyo ni kwa faida ya Chadema. Kwa mfano kuachiliwa Lissu kutawasaidia vipi Chaumma na ACT-WAZALENDO? Maridhiano wanayotaka Chadema ni kati yao na CCM na sio vyama vingine au hata taifa kwa ujumla.

Amandla...

..itajenga precedence kwa viongozi wa vyama vya upinzani kufungwa kihunihuni na wakaachwa bila utetezi wa vyama vingine.

..Chadema wakienda kwenye maridhiano bila Tundu Lissu, mbele ya safari hakuna chama kitaweza kuweka msimamo kama huu walionao Chadema sasa hivi.

..Msuluhishi wa Kimataifa atasaidia kuweka usawa ambao ni vigumu kuupata kwa wasuluhishi wa ndani. Na hiyo ni faida kwa vyama vyote. Yeyote atakayeteuliwa toka ndani ya Tanzania, bila shaka atakuwa ni mtu aliyepata kutumikia, na kuteuliwa, hapo kabla ktk serikali ya Ccm.
 
Back
Top Bottom