Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Wajinga hawa, tuliwatuma watuletee majibu ya maswali yetu, badala yake wameleta maswali na mambo mengine ya ovyo ovyo. Hadi ninapoingia kaburini sitakuheshimu ihema na mjinga mwenzio wa mwananchi. Sitanunua gazeti la mwananchi na ntahamasisha wengine wasilinunue gazeti linalonunulika kupotosha ukweli.
 
Kamati iliundwa KIJINGA, ripoti yake lazima ingekuwa ya kijinga.

Serikali ikamkimbiza haraka yule Police Constable mahakamani ili kumaliza kabisa makali ya ripoti hii. Mtindo huu wa kukimbiza vitu mahakamani serikali imeutumia mara kadhaa hata kule Bungeni kuzima hoja na mijadala mbalimbali ambayo ilionekana dhahiri ingeielemea serikali.

Kamati hii ya Nchimbi/Ihema ingesitisha tu shughuli zake jibu likawa moja tu: kesi iko mahakamani. Tujikite tu kwenye namna ya kuzuia haya yasiendelee kutokea nchi hii. Kuna mapungufu makubwa kwenye kuajiri, kufundisha na kuelekeza polisi wetu kwa sasa. Kijana aliyemmaliza Mwangosi huenda hata hakujua silaha alookuwa akitumia inatumikaje.
 
Haya mambo yanasikitisha sana sasa hiyo kamati ya akina nchimbi kama walijua shauri lipo mahakamani tume aliunda ya nini.

Tuondoe ushabiki tuseme ukweli hizi tume huwa zinatufanya watz wazuzu sana eti polisi hawakuhusika sasa huyo askari walie mfungulia mashtaka amekosa nini, jamani na Mungu kawaumbua picha zimepigwa mwangosi kazingilwa na askari leo tume inakuja na mipasho inaboa sana.

Sasa wanavyosema shuguli za kisiasa zifanyike bungeni kisa mikutano inawafanya wananchi washindwe kufanya kazi kweli jamani haya ni mapendekezo ya wasomi au ndo vyeti vya kufoji.
 
Kamati iliundwa KIJINGA, ripoti yake lazima ingekuwa ya kijinga.

Serikali ikamkimbiza haraka yule Police Constable mahakamani ili kumaliza kabisa makali ya ripoti hii. Mtindo huu wa kukimbiza vitu mahakamani serikali imeutumia mara kadhaa hata kule Bungeni kuzima hoja na mijadala mbalimbali ambayo ilionekana dhahiri ingeielemea serikali.

Kamati hii ya Nchimbi/Ihema ingesitisha tu shughuli zake jibu likawa moja tu: kesi iko mahakamani. Tujikite tu kwenye namna ya kuzuia haya yasiendelee kutokea nchi hii. Kuna mapungufu makubwa kwenye kuajiri, kufundisha na kuelekeza polisi wetu kwa sasa. Kijana aliyemmaliza Mwangosi huenda hata hakujua silaha alookuwa akitumia inatumikaje.
Mimi sishangazwi na Polisi bali kuna watu wawili ndio wananiacha na mshangao, huyu Jaji Mstaafu na Teophil Makunga, hapa nashindwa kuelewa kama niko ndotoni au ni kweli nchi imefikia hapo?

Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwapongeza Chadema kwa kutangaza mapema kwamba hawatatoa ushirikiano wowote kwa kamati ambayo tofauti na kamati ya Harusi. Tunahitaji tume huru ya kimahakama yenye nguvu za kisheria.
 
Msingi wa haya yote ni dharau dhidi ya wananchi (contempt of the people). Watawala wanaamini wanaweza kusema lolote, vyovyote, kwa yeyote bila kujali matokeo yake. Hawataki kuulizwa na wakiulizwa wanaona unaleta vurugu.

The corrupt and unjust system can not discredit itself! Hiyo haiwezi kutokea.
 
Mimi sishangazwi na Polisi bali kuna watu wawili ndio wananiacha na mshangao, huyu Jaji Mstaafu na Teophil Makunga, hapa nashindwa kuelewa kama niko ndotoni au ni kweli nchi imefikia hapo?

Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwapongeza Chadema kwa kutangaza mapema kwamba hawatatoa ushirikiano wowote kwa kamati ambayo tofauti na kamati ya Harusi. Tunahitaji tume huru ya kimahakama yenye nguvu za kisheria.
Makunga anasubiri U-DC kama waandishi wenzake akina Muhingo, Makunga, Beti Mkwasa, Kipozi, Dumba, Kihemba,...

Jaji Ihema anaona kabisa anaona kabisa kuna uwezekano wa yeye kuwemo kwenye tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Teuzi za siku hizi ni kuonyesha UTIIFU kidogo tu,
 
Kuna m2 kanitumia ujumbe huu-:
Angalia watoto wa vigogo walio pita UVCCM ngazi ya taifa

  • DICKSON MEMBE
  • FREDY LOWASA
  • RIDHIWANI KIKWETE
  • ASHURA HUSSEIN MWINYI
  • BENY SAMWELI 6
  • DEBORAMWANDOSYA
  • IREN PINDA
  • FELISTER NDUNGAI
  • CHRISTOFER NDEJEMBI
  • SHARIFA BILALY
  • JUDITH MUKAMA NA
  • JALOME MSEKWA.
My take-: Tunategemea nini katika hali hii, hii nchi imekuwa mali ya ssm na wale wanao tetea ssm wajipime kama akili zao sio masabuli. Tuchuke hatua kwa wale ambao hawajaamka, hatua chetu.


Hatushangai CCM kujikabidhi nchi, toka kwa baba/mama hadi mtoto na wajukuu....Ila tukumbuke Wale Waana wa Gadhafi na Hosni Mubarak, ni kati ya waliojaa uhodari, ukubwa na mihela....sasa wanatafuta 'pa kujisaidia' hawapati!..Hawa wa hapa kwetu, wote watakuwa 'warembo' siku raia watakapoamua kujikabidhi taifa lao! Ni jambo la muda tuu! Halipingiki hilo!
 
Mzee Mwanakijiji,
Toka unaijua nchi hii ya Ubepari kuna kesi yoyote ya Uhujumu Uchumi ama mauaji toka mkono wa serikali ambayo unakumbuka mtuhumiwa amewahi kushindwa kesi...Tumeshindwa ya Richmond, ushahidi wote unajionyesha wazi leo mnategemea kweli waajiriwa wa chombo cha serikali wakubali makosa ya mauaji wakati harakati za Chadema ni lazima zipigwe vita.

Wanaposema wao watatumia nguvu ya Dola against raia wake hapo ujue ya kwamba nchi hii imekosa kabisa mwelekeo na hivyo tusitegemee maamuzi yenye haki. Kuna watu above the law, majuzi nimecheka sana kusoma ati rais Mstaafu Mwinyi alikuwa mahakamani kutoa ushahidi watu wakasema aaah Tanzania hakuna mtu above the law.. What?... mtu kwenda mahakamani kutoa ushahidi imekuwa ndio tafsiri ya - No one is above the law!... Kazi kweli kweli....
 
Nikisha soma ripoti nitarudi kusema.
Hata hivyo naendelea kupingana na wale wanaokataa matumizi ya nguvu kuiondoa ccm madarakani. Najua siku moja tutalazimika kufanya hivyo tupende tusipende kwa faida ya vizazi vyetu vijavyo.
 
Watu walienda kutalii Iringa,ripoti imetungwa hapa hapa Dar

Nakumbuka iliripotiwa hawa wana kamati kuibiwa BAADHI YA VITENDEA kazi-IPad; hela na makbrasha mengine! walipoanza tuu kazi! Labda baada ya hapo ndio waliamua kufanya UTALII WA NDANI....

Kweli Tz kuna vitu haviwezekani kufanyika/kutokea katika DUNIA nyingine inayojitapa kutawaliwa KIDEMOKRASIA na KUJALI UTAWALA WA SHERIA......
 
hii ni habari au makala maalum na wala sio ripoti
 
Siku moja itafika,
Ninasema kwa hakika,
Siku, siku itafika,
Tutasema tumechoka,
Hata nao vibaraka,
Hakika watateseka.

Siku moja ninasema,
Fungua macho tazama,
Wala usibaki nyuma,
Kwa pamoja kujituma,
Itakuwa siku njema,
Kwa wenye mapenzi mema.

Washatudharau sana,
Kwamba hatuna maana,
Wametufanya watwana,
Thamani yetu hakuna,
Huku wao wajichana,
Mifuko yao kutuna.

Tuling'oa ukoloni,
Tukidhani tumewini,
Kumbe tunao nguoni,
Adui nambari wani,
Waso huruma myoyoni,
Kwa wetu umasikini.

Kila kitu wanauza,
Hakuna wanachosaza,
Ni dhambi kuwauliza,
Uchumi ‘napouchakaza,
Ipo siku tutaweza,
Nasi kuwateketeza.

Nchi ni ya kwetu sote,
Hatukupewa tusote,
Ili wachache wapate,
Na wanyonge tuufyate,
Haikwandikwa tusote,
Haikwandikwa wapate.

Dini ya uwekezaji,
Waja umasikinishaji,
Zao ukandamizaji,
Na kupoteza mitaji,
Wao utajirikaji,
Na marufuku kuhoji!

Siku moja inakuja,
Hatuhitaji kungoja,
Sie sote kwa pamoja,
Tutaikata mirija,
Watabaki kubwabwaja,
Kwa ubwana ulochuja.

Siku hiyo imefika,
Tunapaswa kuamka,
Na kusema tumechoka,
Na kwa kweli watang'oka,
Kwa mizizi waloweka,
Ni kweli tumechoka.
 
Siku moja itafika,
Ninasema kwa hakika,
Siku, siku itafika,
Tutasema tumechoka,
Hata nao vibaraka,
Hakika watateseka.

Siku moja ninasema,
Fungua macho tazama,
Wala usibaki nyuma,
Kwa pamoja kujituma,
Itakuwa siku njema,
Kwa wenye mapenzi mema.

Washatudharau sana,
Kwamba hatuna maana,
Wametufanya watwana,
Thamani yetu hakuna,
Huku wao wajichana,
Mifuko yao kutuna.

Tulingoa ukoloni,
Tukidhani tumewini,
Kumbe tunao nguoni,
Adui nambari wani,
Waso huruma myoyoni,
Kwa wetu umasikini.

Kila kitu wanauza,
Hakuna wanachosaza,
Ni dhambi kuwauliza,
Uchumi napouchakaza,
Ipo siku tutaweza,
Nasi kuwateketeza.

Nchi ni ya kwetu sote,
Hatukupewa tusote,
Ili wachache wapate,
Na wanyonge tuufyate,
Haikwandikwa tusote,
Haikwandikwa wapate.

Dini ya uwekezaji,
Waja umasikinishaji,
Zao ukandamizaji,
Na kupoteza mitaji,
Wao utajirikaji,
Na marufuku kuhoji!

Siku moja inakuja,
Hatuhitaji kungoja,
Sie sote kwa pamoja,
Tutaikata mirija,
Watabaki kubwabwaja,
Kwa ubwana ulochuja.

Siku hiyo imefika,
Tunapaswa kuamka,
Na kusema tumechoka,
Na kwa kweli watangoka,
Kwa mizizi waloweka,
Ni kweli tumechoka.

Siku hizo umekuwa mwana Kwaya.
 
Siku hizo umekuwa mwana Kwaya.
Sitaraji jambo jema,
Kama hujawa makini,
Singoje yao huruma,
Jiulize ni ya nini?
Wala usijidanganye,
Ukadhani umefika,
Tena usijichanganye,
Pamoja nao vibaka.

Wao siyo watu wema,
Ni vema kujihadhari,
Kwao wala si salama,
Kumejaa nayo shari.
Tunataka nani aseme,
Ndipo wao wasikie?
Ama hadi twandamane,
Ndipo wakatufyatue?
 
Inatakiwa nguvu itumike kuondoa utawala huu wa kidhalimu,kigaidi na kifisadi,Tumwombe sana MUNGU atuteulie mtumishi wake na kumtuma kwetu,tumechoka na utawala huu ambao ni zaidi ya ukoloni.eee MWENYEZI MUNGU JIBU MAOMBI YETU Watanzania tunanyanyasika kwenye nchi yetu wenyewe.

Dai haki yako kabla hujafa.
 
Kuitegemea serikali hii kuja na maelezo ya maana katika tukio hilo ni kutarajia muujiza. Ni picha tu zimewaumbua. Mauaji ni muendelezo wa mkakati wa serikali wa kutisha na kutia hofu wale wote wasiokubaliana na jinsi serikali hii inavyoendesha mambo yake. Baada ya picha kutoka wote wako kimya; si rais, makamu wala waziri mkuu. Hata IGP analigusa suala hilo kwa kificho. Sasa hata wapayukaji akina chagonja & co. nao kauli zimeisha wanasukuma muda tu wakijua siku si nyingi waswahili watachoka na kelele zitaisha. Kwao, mtanzania wa kawaida, hana ujasiri, hana uwezo wa kufikiri wala kuona mbali, umasikini unamsumbua, kitu kidogo tu kinamweka sawa. Tushadharauliwa kabisaaa!

Jaji mzima anathubutu kusema kamati imeona nguvu kubwa iliyotumiwa na polisi si sababu ya kifo cha Mwangosi? Halafu waziri anajaribu kupoza kwa kusema kilichomuua kiko ndani ya ripoti hakiwezi kusemwa kwa kuchelea kuingilia uhuru wa mahakama! Sasa kwa nini muwahishe hadharani hii kauli ya kuwaondolea mzigo polisi? Nayo si ingeachwa "ndani ya ripoti"?

Well, let them continue with their murderous spree maybe one day it will wake the people up to the reality that evil guys are never appeased. Once you choose the path of murder as a strategy/solution to your woes, there is no return.
 
Back
Top Bottom