Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

High expectations ndio tatizo na kutegemea ripoti ingejumuisha kila kitu tathimini nzuri ni adidu rejea ya kamati vinginevyo ni ngumu to accommodate feelings za kila mtu. Tupokee yakwao kwanza na tujifunze kuwa proactive kuliko kusubiri kila kitu kuletewa na kuacha maafa yatokee.

As matter of fact polisi wana bifu na vyama, marehemu Mwangosi katika mkutano wa waandishi wa habari aliuliza swali kwa Dr. Slaa,kuhusu bifu la polisi la Chadema, majibu yake Channel Ten wana documentary iliyoonesha hilo swali la marehemu muda mchache kabla ya kifo chake na msimamo wa Dr. Slaa ulikuwa liwalo na liwe mkutano uko pale pale. Tuache kabisa kutengeneza untouchables, yeyote anapokosa tumwambie ili ajifunze na kuwa bora zaidi.

Ingekuwa enzi za skonga wote wanaenda chini kula stiki, Polisi na Dr. Slaa wote wanayo dhima ya mauaji ya Mwangosi kwa kutokuchukua hatua ya kuzuia maafa ilihali maafa yalikuwa yanaonekana na marehemu alikuwa ameona hivyo na very unfortunately yeye na familia yake ndio wahanga namba moja. Mie nafsi ilitua baada ya Dr. Slaa kuchukua dhima ya kusomesha watoto wa marehemu na nikaona uungwa wa hali ya juu na fika msukumo wa lile swali la Mwangosi kwake kuhusu maafa hayo lilimgusa namna fulani.

Mzee Mwanakijiji wakati mwingine mahaba na ushabiki ukae kushoto, ukilinganisha polisi na vyama vya siasa. Mie naona vyama viko well equiped kwa maana ya skilled na competent personnel's kuliko polisi na vyama vikiamua na kuleta ubunifu vinaweza epuka maafa mengine bila kuumiza watu wasio na hatia na vigezo vya kupigania haki havitoshi kusababisha mauaji kwa watu wanyonge kuuawa. Kama ni sinema basi viongozi wa vyama ndio mastaa na wao ndio wanapaswa kufa kwanza ili uhuru upatikane kwa watu wote, sio wanakichafua na msala wanawaachia wanyonge wakati polisi wetu wenyewe hawajua hata wajibu wao wakiwa kazini, sio tu kwenye mikutano ya kisiasa bali hata wakiwa uwanja wa Taifa tu wao ni Majanga kuendelea kushindana nao ni kupoteza muda watatuumiza na wala hawajutii, yaani wameua polisi lakini jukumu la kulea familia wameenda kujitwisha watu wengine tukianza kuwapa majumu wao kama jeshi na katika bajeti zao wakaona kuna fund inaenda kutokana na maafa waliyosababisha wao wataacha tu na wajane na mayatima wakae pia katika ballacks zao wataacha lakini tunawaangalia, tunanung'unika na tunajaza thread na makala na wengine ndio wang'ara kama waandishi wazuri wa kuchambua ripoti za kamati kesho wataua tena.
wewe unajua maana ya utawala wa haki na sheria? kwanini mwiko kwa CHADEMA iwe mazoea kwa CCM? Je CCM hawahusiki na kufuata sheria?
 
Hivi kile kitufe cha THUMB DOWN kwa nini kilitolewa, kuna post zinakera sana kile kilisaidia kupunguza hasira
 
Kaka Msemakweli Daima, watanzania wanao uwezo wa kufikiri na ndiyo maana wanaandika humu jf kuwa taarifa hii ni ya kijinga na kipuuzi. Mpaka wanafikia kuyasema haya wamefikiri na pengine hata kuchunguza. Watanzania wenye akili wanahoji mbona huyu, yule waliotakiwa kuhojiwa hawakuhojiwa? Maswali kama haya hayawezi kutoka kwenye vichwa vya wasio na uwezo wa kufikiri
Tatizo la watanzania ni kutochukua hatua stahiki kwa matatizo husika. Wapo wanaotaka hatua stahiki zichukuliwe, lakini wanakosa kutengeneza mbinu za kuvuta jamii ili kuungwa mkono.
Tatizo la pili ni njaa. Adui muombee njaa. Sehemu kubwa ya watanzania wana njaa kali hata Polisi. Wanadhani wakijipendekza kwa wakubwa shida yao ya njaa itapungua, lakini afadhali ya jana kuliko leo.
Kifikra watanzania walio wengi hawajajikomboa, wanahitaji mtu wa kuwakomboa na sio kuwacheka au kuwalaumu kama unavyojaribu kufanya. Deal with the brain and the trunck will follow by itself. Watanzania ni watumwa wa mfumo na wala si kwa hiari yao, wamelazimika. Hakuna mtu anayependa kuwa mtumwa, bali mfumo unamwandaa mtumwa kujiona yuko salama na tajiri kuwa mikononi mwa bwana wake. Mtumwa akizinduliwa akazinduka atauchukia utumwa na bwana wake.
Upo wakati watanzania wataamuka, wataukataa mfumo wa kutumiwa kwa manufaa ya wachache.
Jaji Ihema, huwezi kusema hajasoma ila elimu aliyopata hata kama ni kidogo, hajaelimika. Itawezekanaje mtu mwenye elimu unayejua hili ni jiwe, leo unaambiwa sema huu ni mkate. Unakubali. Unasema tena kwa sauti, bila aibu, mbele za watu! Utakuwa sio mjinga bali ni mpumbavu. Katika orodha ya watu wa aina hii tunao wengi. unaweza kuwaorodhesha, mfano😀r. Nchimbi, RPC Iringa Kamhanda Said Mwema. Kikwete naye badala ya kuwakemea polisi anawaomba wasirudie kutumia nguvu kupita kiasi. Amiri jeshi, badala ya kuamrisha jeshi anawaomba kikosi chake wafuate sheria kana kwamba kuna siku aliwaruhusu kutofuata sheria. Anadhani kiongozi bora ni yule anayelibembeleza jeshi la polisi hata pale lipofanya kinyume cha sheria aliyoapa kuilinda. Anadhani atakuwa salama.
Hafanyi hivi kwa bahati mbaya. Hapana. Hata yeye ni muovu, anaogopa wasije pia wakafichua maovu yake. Ni upumbavu RAISI WA NCHI anayedhani kuficha maovu ni mafanikio. Hakuna tofauti na mtu anayeficha uozo chini ya mvungu asijue kuwa harufu itamuumbua. Ni akili ya kitoto.
 
Tutalia tuuuu hadi tutakapodhubutu kuifundisha hii serikali adabu. Waziri gani ambaye hakuona zile picha za mauwaji ya Mwangosi? Serikali gani inayojichanganya kwa uwongo mchana kweupe? Mimi nimesema mara nyingi na ninarudia tena mambo yanayofanywa na serikali ya JK ni ya kipuuzi kupita kiasi. Mzee wa matoroli ya farasi amejiwekea mawaziri wajinga kama kina Nchimbi kuendeleza dharau kwa watanzania. Cha muhimu ni kuwa tunachoka na tunaendelea kuchoka. Siku inakuja JK, Nchimbi na wenzake watauona mchanga wa kweli kwenye hivi vitumbua vinavyowapofua macho kiasi hiki.
Hivi watanzania tunafanya nini hadi dakika hii? Tunaogopa nini? Dhaifu mwenyewe amejidhihirisha kwa kila njia kuwa hakuna lolote la laama ila kwenda kumbembea, kushangaa, na kuburutwa kwenye matoroli huku na kule huku watanzania wakiendelea kutaabika na kuuawa na serikali yake. Tukimtungua dhaifu kama huyu tutakuwa tumepoteza kitu gani? Tusijisingizie amani kwani penye amani raia hawapigwi mabomu na polisi. Penye amani waumini wa dini fulani hawatoki kuwachomea wenzao nyumba, magari, na wanyama wao. Tuache unafiki tufanye kazi ya watu wazima nayo ni kuiondoa hii serikali madarakani. Kama tunashindwa kufanya hivyo mara moja basi tuiondoe kwa kuwapigia kura kina Dr. Slaa watuondolee hizi aibu kwa sasa inatosha kabisa.
 
niliposima taito tu nilijua ni mwanakijiji. Big up big man kwa kudadavua. Hiki chama na serikali yake vimetuchoka. Nasi tumewachoka.
 
Nimepitia ripoti nimesoma maneno ya Jaji Mstaafu Steven Iheme, anasema Chadema ndio chanzo cha vurugu na uvujifu wa amani kijijini Nyololo, hasa kutokana na uamuzi wa kunga'ang'ania kukusanyika isivyo halali eneo hilo.

Je nawewe unakubaliana na majibu hayo?
 
Jaji Ihemu, anaendelea kusema ujumbe wa sms kutoka kwa Dr Slaa ulisema, "IGP nasuburi simu yako. Wajulishe Polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha, mtakuwa na karamu ya mauji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya Hague. Ni afadhali tufe kuliko manyanyaso haya"

Ujumbe huu ukiashiria umwagaji damu ni ushaidi tosha kuwepo kwa uvujifu wa amani.

Kwahiyo huo ujumbe aliwatumia wananchi au?
 
Nimepitia ripoti nimesoma maneno ya Jaji Mstaafu Steven Iheme, anasema Chadema ndio chanzo cha vurugu na uvujifu wa amani kijijini Nyololo, hasa kutokana na uamuzi wa kunga'ang'ania kukusanyika isivyo halali eneo hilo.

Uhalali wa kusanyiko nani anaupima? CCM au Polisi? Kama ni Polisi waliwezaje kwa sababu ileile ya sensa kuruhusu kusanyiko la CCM Jimbo la Bububu na kuharamisha kusanyiko la CDM Nyololo? Wewe unalinda na kutetea upuuzi kwa kutumia mdomo wakati akili na ubongo wako unajua ni upuuzi.
 
Ni lazima tutambue na kukumbuka kuwa watawala wanaweza kufanya hivi kwa sababu Watanzania hatutaki kuwapinga wazi na wajue wanapingwa. Waandishi wetu wa habari ndio wanatuangusha zaidi kwa kuwa kama vipaza sauti vya watawala. Tumewaona wakionesha hasira zaidi baada ya Mwangosi kuuawa lakini ni hasira inayotokana na maumivu siyo na tofauti ya mtazamo.

Waandishi wetu wanapokuwa mbele ya watawala wananyenyekea kwa woga; wanaogopa kuwabana na kukataa taarifa za kijinga kama hizi kwa kuogopa kuonekana wako kimbelembele au hawana heshima. Binafsi naweza kusema tuliona kazi ya uandishi pale Iringa kabla ya tukio pale ambapo waandishi (akiwemo marehemu Mwangosi) walipoweza kuwabana maafisa wa polisi na kuwaonesha kuwa hoja zao hazina akili. Leo hii Nchimbi mbele ya waandishi anasema kuwa kuna ushahiidi ambao serikali inao unaweza kumtoa hatiani mtuhumiwa na waandishi wanakubali!!

Wakati mwingine ujinga siyo vile tunavyofanyiwa bali vile tunavyofanya echoing Forest Gumps' 'stupid is as stupid does'..
Mzee Mwanakijiji ni waandishi wepi unaotegemea wawe na akili timamu? ni hawa ambao mmiliki wa Dowans alifanya nao Press Conference na akawakataza wasimpige picha na wote wakanywea?

Samahani tu nadiriki kusema Tanzania huitaji kusoma hata short course kama unataka kufanya kazi ya uandishi wa Habari, ni taaluma iliyovamiwa na watu wenye zaidi ya njaa yaani ni kinyaa kitupu.

Hiyo yote tisa kumi kutana na waandishi wa Habari za Michezo ndio utachoka kabisa wala hakuna haja ya kuwa na vyuo vya uandishi wa habari

431618_424417584286608_938257837_n.jpg
 
:ballchain:Hizi ndizo kamati uchwara na ripoti uchwara.Lakini mwisho wa haya yote umekalibia
 
Uhalali wa kusanyiko nani anaupima? CCM au Polisi? Kama ni Polisi waliwezaje kwa sababu ileile ya sensa kuruhusu kusanyiko la CCM Jimbo la Bububu na kuharamisha kusanyiko la CDM Nyololo? Wewe unalinda na kutetea upuuzi kwa kutumia mdomo wakati akili na ubongo wako unajua ni upuuzi.

Mkuu mbona unanishambulia mie bure hayo sio maneno yangu ni ripoti ya Tume ya Nchimbi.
 
Lisu aliisha sema...hii sio kamati ya kweli. Nchimbi hawezi kutengeneza kamati ya ukweli coz itakuja kumuondoa yeye na sio watu wadogo wa chini. Nchimbi anatakiwa kujiuzuri thats only solution. Anatapa tapa huku kule lakini watu wenye akili zao wameisha muona Nchimbi hasafishiki.

Nyani hawezi kumhukumu Kima hata siku moja.the only solution is to remove the system from the power.
 
Ni lazima tutambue na kukumbuka kuwa watawala wanaweza kufanya hivi kwa sababu Watanzania hatutaki kuwapinga wazi na wajue wanapingwa. Waandishi wetu wa habari ndio wanatuangusha zaidi kwa kuwa kama vipaza sauti vya watawala. Tumewaona wakionesha hasira zaidi baada ya Mwangosi kuuawa lakini ni hasira inayotokana na maumivu siyo na tofauti ya mtazamo.

Waandishi wetu wanapokuwa mbele ya watawala wananyenyekea kwa woga; wanaogopa kuwabana na kukataa taarifa za kijinga kama hizi kwa kuogopa kuonekana wako kimbelembele au hawana heshima. Binafsi naweza kusema tuliona kazi ya uandishi pale Iringa kabla ya tukio pale ambapo waandishi (akiwemo marehemu Mwangosi) walipoweza kuwabana maafisa wa polisi na kuwaonesha kuwa hoja zao hazina akili. Leo hii Nchimbi mbele ya waandishi anasema kuwa kuna ushahiidi ambao serikali inao unaweza kumtoa hatiani mtuhumiwa na waandishi wanakubali!!

Wakati mwingine ujinga siyo vile tunavyofanyiwa bali vile tunavyofanya echoing Forest Gumps' 'stupid is as stupid does'..

Kiwanda at Work!
 
We ni t.ko idiot.........OTE=torokoko;4784852]Yakhe andika yako utupe yao huitaki[/QUOTE]
 
Ni lazima tutambue na kukumbuka kuwa watawala wanaweza kufanya hivi kwa sababu Watanzania hatutaki kuwapinga wazi na wajue wanapingwa. Waandishi wetu wa habari ndio wanatuangusha zaidi kwa kuwa kama vipaza sauti vya watawala. Tumewaona wakionesha hasira zaidi baada ya Mwangosi kuuawa lakini ni hasira inayotokana na maumivu siyo na tofauti ya mtazamo.

Waandishi wetu wanapokuwa mbele ya watawala wananyenyekea kwa woga; wanaogopa kuwabana na kukataa taarifa za kijinga kama hizi kwa kuogopa kuonekana wako kimbelembele au hawana heshima. Binafsi naweza kusema tuliona kazi ya uandishi pale Iringa kabla ya tukio pale ambapo waandishi (akiwemo marehemu Mwangosi) walipoweza kuwabana maafisa wa polisi na kuwaonesha kuwa hoja zao hazina akili. Leo hii Nchimbi mbele ya waandishi anasema kuwa kuna ushahiidi ambao serikali inao unaweza kumtoa hatiani mtuhumiwa na waandishi wanakubali!!

Wakati mwingine ujinga siyo vile tunavyofanyiwa bali vile tunavyofanya echoing Forest Gumps' 'stupid is as stupid does'..

MM unaongea vitu ambavyo vinanifanya nitoke machozi waandishi ni wasaliti wakubwa ktk nchi hii, wapo wachache wenye kuweza kujisimamia lakini kundi kubwa ni kama vibaraka.

Binafsi niliangalia ile video nikajiuliza hivi hawa ni wakuu wa police au me sielewi hawakuwa na hoja huyo kamuhanda ndo kabisa anajibu pumba tupu kwakweli tumekuwa zaidi ya makondoo.

Alafu ukweli unabaki kuwa hakukuwa na sababu ya mwangosi kuuwawa kwa style ile.
 
viongozi kama wakina Nchimbi ndio wanaoifanya tanzania iingie kwenye maajabu saba ya dunia... wenye akili timamu hawawezi kuelewa kama TZ kuna viongozi mmoja wao ni mimi.
 
Yakhe shakua bahau; ripoti swafi; yakhe tupe yako tusome nini kulalama kama kigori

Kwa kuwa tukio la kifo cha Daudi Mwangosi liligusa hisia za jamii, Tume imeona ni vyema kukutana na wawakilishi wa vyombo vya habari ili kutoa taarifa yake.


2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI
Katika uchunguzi wake Tume imebaini kuwa:
Tarehe 02/09/2012 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliruhusiwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi (OCD) kufanya mikutano ya ndani na kuzindua matawi mapya. Lakini jioni ya tarehe 01/09/2012 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), alizuia CHADEMA kufanya mikutano iliyoruhusiwa na OCD ambaye ni "Officer In-charge" wa polisi wa eneo husika kama sheria inavyotaka.
Viongozi wa CHADEMA walikuwa na mazungumzo na Mkuu wa Polisi Mkoa Upelelezi (RCO) na kuruhusiwa kufungua matawi yao bila ya kuwa na mikutano ya hadhara.
Msajili wa vyama vya siasa aliwaandikia barua viongozi wa vyama vya siasa kuwataka kusitisha shughuli zao kwa sababu ya sensa.
Wakati shughuli za uzinduzi wa tawi la Nyololo ukiendelea, RPC alifika katika eneo hilo na kuamuru viongozi wa CHADEMA wakamatwe; na kuwa wafuasi wa CHADEMA walipinga kukamatwa kwa viongozi wao.
RPC aliamuru kupigwa kwa mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika ofisi za tawi hilo la CHADEMA.
Baada ya mabomu ya machozi kupigwa, wananchi walitawanyika na kukimbia ovyo; na kuwa marehemu Daudi Mwangosi alizingirwa na askari, aliteswa na hatimaye inadaiwa alipigwa bomu na kufa hapo hapo.
Daudi Mwangosi aliuwawa umbali wa takriban mita 100 kutoka ilipo Ofisi ya CHADEMA tawi la Nyololo.
Katika tukio hilo wananchi kadhaa walijeruhiwa kwa mabomu, wakiwemo Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Bwana Godfrey Mushi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CHADEMA Wilaya ya Mufindi, Bibi Winnie Sanga na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mufindi, Asseli Mwampamba aliyekuwa akifanya jitihada za kumuokoa marehemu Daudi Mwangosi.


Kutokana na hayo yote, Tume imejiridhisha kuwa tukio lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi limegubikwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.


2.1 Uvunjwaji wa Haki za Binadamu
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights of 1948), Mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa (International Covenant on Civil and Political Rights of 1966) na Mkataba wa mataifa ya Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu (African Charter on Human and Peoples Rights of 1981), Tume imejiridhisha kuwa Jeshi la Polisi limevunja haki zifuatazo:
Haki ya kuishi,
Haki ya kutoteswa na kupigwa,
Haki ya usawa mbele ya sheria na
Haki ya kukusanyika na kutoa maoni.


CHADEMA ni chama cha siasa ambacho kina usajili wa kudumu. Chini ya sheria ya vyama vya siasa (Cap. 258 RE. 2002), vyama vya siasa vyenye usajili vimeruhusiwa kufanya maandamano na kuwa na mikutano ya kujitangaza baada ya kutoa taarifa kwa "Afisa wa Polisi" wa eneo husika. Baada ya taarifa kutolewa chama husika kinatakiwa kipewe ulinzi na "security agencies" (mawakala wa usalama).

2.2 Ukiukwaji wa Misingi ya Utawala Bora

Ili pawepo utawala bora mamlaka zote za serikali ni lazima zifuate utawala wa sheria. Uchunguzi umebaini kuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda tarehe 02/09/2012 katika utekelezaji wa majukumu yake alikiuka Sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) kifungu cha 11(a) na (b) na sheria ya Polisi (Sura ya 322) kwa kuingilia kazi za OCD wa Mufindi na kutoa amri ya kuzuia shughuli za CHADEMA wakati yeye hakuwa "Officer In-charge" wa polisi wa eneo husika. Kwa maana hiyo amri aliyoitoa haikuwa halali kwa kuwa ilitolewa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria kutoa amri hiyo. Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka, hivyo ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.


Aidha, hatua ya Msajili wa vyama vya siasa, Mhe. John Tendwa kuwaandikia barua viongozi wa vyama vya siasa kuwataka kusitisha shughuli zao kwa sababu ya sensa ilikiuka misingi ya utawala bora kwani maelekezo yaliyotolewa ndani ya barua hizo yanakinzana na sheria ya takwimu Na. 1 ya mwaka 2002 inayotoa fursa kwa wananchi kuendelea na kazi zao wakati wa sensa pia ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) Kifungu cha 11(a) na (b) inayotoa fursa kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa.


Ibara ya 8(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelezea kwamba Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na Haki ya Kijamii, aidha ibara 18(b) na (c) ya Katiba inaeleza kuwa kila mtu anayo haki ya kufanya mawasiliano (kutoa maoni/habari) na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake. Haki hii imekiukwa kwa kiasi kikubwa na Jeshi la Polisi katika tukio la Nyololo Mufindi kwa kuwa waandishi wa habari na wafuasi wa CHADEMA walizuiwa na Polisi kufanya shughuli zao za kupata habari na za kisiasa. Huu ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kwa kuwa hali hiyo inazorotesha au inafifisha uhuru wa habari.

3.0 MAONI NA MAPENDEKEZO

Kwa kuzingatia Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na. 7 ya mwaka 2001 Kifungu cha 15(2)(c) na 28 Tume inapendekeza yafuatayo:
Kamati za ulinzi na usalama za Mkoa na Wilaya ziwe makini na vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utalawa bora vinavyofanywa na mamlaka mbalimbali kwenye maeneo yao. Aidha, kamati hizo zihusike moja kwa moja na usalama wa wananchi na mali zao kwa kujadili masuala yote ya kiusalama kabla hatua hazijachukuliwa na vyombo vinavyotekeleza sheria.
Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao waepuke malumbano na vyombo vya dola kwa kutii maagizo yanayotolewa na vyombo hivyo bila shuruti. Pale wanapogundua kuwa pana uonevu au upendeleo ni vyema busara ikatumika ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea.
Jeshi la Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa waepuke kufanya maamuzi au matendo yanayoibua hisia za ubaguzi au upendeleo miongoni mwa jamii wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kisheria. Mfano, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya CHADEMA kwa sababu ya sensa wakati huo huo Chama cha Mapinduzi (CCM) walikuwa wakifanya uzinduzi wa Kampeni huko Zanzibar. Aidha, rai ya Msajili wa vyama vya siasa haikuzingatiwa kwa upande wa CCM Zanzibar huku CHADEMA walishurutishwa na Polisi kutii rai hiyo.
Demokrasia ya mfumo vya vyama vingi iheshimiwe na kulindwa.
Elimu ya vyama vya siasa na sheria ya Polisi kuhusu vyama vya siasa itolewe kwa askari polisi ambao wanaonekana kutozifahamu kabisa.


4.0 HITIMISHO
Jukumu la kulinda amani na utulivu ni wajibu wa kila mtanzania, mkulima na mfanyakazi, viongozi wa serikali na watumishi wa umma wote wanapaswa kuwa wazalendo wa kweli wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. Tume inatoa wito kwa watanzania wote kuheshimu haki za binadamu na kutekeleza kwa vitendo misingi ya utalawa bora. Kwa kufanya hivi Taifa letu litaendelea kuwa na amani na utulivu. Tume inatoa rai kwa jeshi la polisi kutekeleza wajibu wake mkuu wa ulinzi na usalama wa raia bila kutumia jazba.


Kuwepo kwa vyama vya siasa ionekane kuwa ni kukuwa kwa demokrasia na sio kuwa ni upinzani kwa chama tawala.


.............................. ......................
Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri R. Manento


MWENYEKITI
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA


OKTOBA 10, 2012
 
Back
Top Bottom