Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,402
- 12,795
Nilitegemea aina hii ya insha...nachelea kuuita ripoti kwa kuhofia kushusha hadhi ya ripoti!...
Ahsante mwanakijiji na watanzania poleni. Mtu akiwa mjinga anadhani na watu wengine ni kama yeye. Mambo mengi tunaona watu wamepewa madaraka lakini uwezo wao ni ovyo.
Sanasana serikali iliyoko madarakani naona ina upungufu mno wa viongozi wanao tia aibu. NILITEGEMEA TUME ISEME MAREHEMU ALIPASWA KUWEKWA PINGU MAKE KESHA JISALIMISHA. WANADIRIKI KUSEMA POLISI HAIHUSIKI! SAD!!!!!!!!!
Nyerere aliwahi kusema "mtu mwenye akili akijua kuwa na wewe una akili akakushauri jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau". Hili ni kweli pia kwenye suala hili. Mtu mwenye akili akijua na wewe una akili ahalafu akakuandikia jambo la kijinga na wewe ukalikubali atakudharau!
Hii ripoti ni ushahidi wa kile ambacho wengine tunaamini ni kweli; CCM na serikali yake ni lazima waondolewe madarakani sooner kwa sababu wanatudharau! Ni dharau ya ajabu sana hii. Fikiria mtu anaandika hivi kwenye ripoti:
Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?
Hili swali ni la msingi sana katika tukio zima.
Lakini Kamati imeshindwa kujibu swali ambalo kwa walioona iile video ya mauaji wanalikumbuka sana yaani linalohusiana na kukatazwa kufanyika kwa mikutano ya ndani ya chama. Kamati inatuambia kuwa barua ya zuio hilo inasema hivi:
Kumbe zuio lilihusu "mikutano na maandamano". Kwamba inaweza kujengwa hoja ya kuwa "mikutano" ilimaanisha "mikutano yote" ni vigumu kutetea hasa kwa vile wakati huo huo mikutano mingine ya kisiasa ilikuwa ikifanyika sehemu mbalimbali nchini bila kuzuiwa. Kamati ili kuonesha ulinganifu ingejaribu kutafuta maelezo ya Polisi Zanzibar kwanini waliruhusu CCM kufanya mkutano wake kule wakati kuna zuio. Lakini vile vile ni vigumu kusema kuwa mikutano yote ya kisiasa ya ndani haikuwa imeruhusiwa! Ni vyama vingapi ambavyo vilikuwa na mikutano ya ndani ya kamati zake mbalimbali kati ya August 26-Septemba 8?
Kamati ingeweza ili kulinganisha "utii wa sheria" kwa vyama vingine kuelezea kuwa vyama vingine havikufanya mikutano yoyote kati ya tarehe hizo na ni CHADEMA tu ambao walikuwa na mkutano Iringa. Hoja kuwa CDM hawakuwa watii ingekuwa na nguvu! Nje ya hapo ni kutuandikia ujinga.
Lakini kuthibitisha upuuzi wa kamati hii imeshindwa kuelezea kuwa kwanini katazo hilo liwe halali Iringa lakini Zanzibar lisiwe halali wakati CCM walipofanya uzinduzi wa kampeni yao ya Bububu? Hiki ndio kipimo cha upuuzi wa ripoti hii. Kama amri ambazo zilitolewa zilihusu vyama vyote kwanini Zanzibar waliendelea na mikutano ya kisiasa? Au wao hawakutakiwa kutiia sheria hiyo au kwa vile hakukutokea machafuko yoyote (na hayajawahi kutokea yakisababishwa na polisi!) huko Zanzibar?
Ikumbukwe kuwa uhalali wote wa polisi kutumia nguvu kuwatanya CHADEMA pale Nyololo unatokana na ukweli kuwa mkutano ule ulikuwa haramu. Lakini kama mkutano ulikuwa halali (kwa maana ya mkutano wa ndani ambao haukukatazwa) uhalali wa kutumia polisi unatoka wapi?
Ili kuthibitisha kuwa ilikuwa ni ripoti ya kijinga ni kuwa Kamati haikuwahoji wale polisi waliokuwa wamemzunguka Mwangosi na haijamhoji yule mtuhumiwa ili aelezee ilikuwaje yeye na wenzake wamshambulie Mwangosi na kwanini atumie nguvu zaidi. Inashangaza tu kuwa ripoti inataka wachukuliwe hatua za kisheria. Na kamati inaonekana haikuchukua muda kuangalia ile video au hata kuitisha watu waliokuwepo kuwapatia picha za video za tukio hilo zima. Na cha kushangaza Kamati hii iliyofanya mambo mengi ya uchunguzi imeshindwa kutoa jibu au hata dokezo la vilikopotelea vifaa vya kazi vya Mwangosi (kamera na laptop)!!
Lakini vile vile ripoti hii ambayo nina uhakika imetumia fedha ya kutosha tu (sijui nani atauliza Bungeni tuambiwe) imeshindwa kumhoji au hata kutuambia maoni ya shahidi muhimu sana katika sakata hili. Ripoti inatutajia kitu muhimu kumhusu:
Huyu Godrey Mushi ni mzima? kwanini alipigwa? Kwanini alikamatwa baada ya kupigwa? Hivi hawa watu hawakuona kuwa kulikuwa na kashfa mbili pale? ile ya Mwangosi na ile ya Mushi? Hivi ingekuwa Mwangosi hajafa pale hii kamati ingechunguza nini kama siyo kupigwa na polisi kwa Mushi?
Hata hivyo kuna ujinga mwingine katika ripoti hii. Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Nchimbi akiokoa jahazi alisema kuwa kuna taarifa ambazo kamati yake (ya serikali) imeweka kibindoni kwa sababu za kimahakama. Ameeleza kuwa mambo hayo yamefichwa ili kuzuia mtu aliyeshtakiwa asije kuitumia kujinusuru. Kwa maneno yake amesema hivi:
Sasa mwenyewe Nchimbi hapa inawezekana aliamini kuwa amezungumza "pointi" sana. Katika mawazo yake haki ya adui yake siyo haki. Kumbe yule mtuhumiwa anayo haki ndio maana mahakamani kwenye kesi hizi wale wa upande wa mashtaka wanatakiwa waweke wazi ushahidi wote ambao wanao hata ule unaoweza kutumiwa kumtoa mtuhumiwa hatiani katika kile kinachoitwa "discovery" kabla ya kesi kuanza. Lengo ni kuhakikisha kuwa ushahidi wowote - wa kumtia mtu hatiani au kumtoa - unawekwa wazi kwa upande mwingine ili kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapewa nafasi ya haki.
Kwa maneno ya Nchimbi serikali inao ushahidi wenye kuonesha kuwa yule mtuhumiwa wa polisi inawezekana asiwe na hatia (hata kama picha zinaonesha kashika bunduki au kweli aliua) na serikali iko tayari kuficha ushahidi huo ili mtuhumiwa yule atiwe hatiani. Sijui wanasheria wetu wanaweza kusema vipi kuhusu haki ya yule mtuhumiwa kuweza kumuita Waziri Nchimbi, Mwenyekiti wa Kamati pamoja na ripoti kamili kama sehemu ya utetezi wake ili waweze kuona kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kumsaidia. Haki ni haki hata kama ni ya adui yako. Si ndio wanasema "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni"? Kama kuna ushahidi unaoweza kumtoa yule kijana Polisi hatiani kwanini Nchimbi na Kamati wauweke pembeni?
Si ndio uvunjaji mkubwa zaidi wa haki kwenda kumhukumu mtu kwa sababu hatutaki aachiwe hata kama sababu ya kumwachia ipo?
Simply put, Ni ripoti ya kijinga.
Huu ujinga ndio tunaoukataa hapa kila siku, unaquote uzi mrefu halafu wewe unareply kwa mstari mmoja tu, ni kwa nini uku mention Mzee Mwanakijiji? au hujui kama kuna wanaotumia simu?nimechelewa but i understand what you mean.Kamati nzima ni janga la Taifa.
Tatizo la Polisi wa Tanzania:
1.ILLITERACY
2.POVERTY
3.INADEQUATE MOBILISATION
sishangai kusikia ripoti ya kuwatetea
"MAPENDEKEZO
.Mauaji ya mwandishi wa habari Daud Mwangosi yalitokea baada ya
operesheni kumalizika, na amri ya kuondoka kwa askari eneo la tukio
kutolewa na Viongozi wa operesheni hiyo"
Nimesikitishwa SANA na hawa wajumbe wawili wa hii KAMATI: Teophil Makunga & Jaji Ihema...! Sikutegemea kama wanaweza kuwa na bei nafuu...!
wajinga wa kwanza Tanzania ni WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA!serikali hii imeshaona watanzania ni wapole,wajinga na wasiojua chochote,kila kitu ni ndio mzee ndo maana wanathubutu kutoa ripoti ya ovyo kiasi hiki,jaman tuamke kutetea haki zetu.
Kamuhanda namfahamu vizuri tangu akiwa mganga katika zahanati za polisi na kabla ya kuwa RPC, sio tarehe yake ya kustaafu imekaribia bali ilishafika na kupita na sasa yuko kwa mkataba. Si ajabu ni mkataba wa kuua wapinzani wote wa ccmNa bado, kinachofuatia ni kila atakaetaka kuzungumza ataambiwa "unaingilia uhuru wa mahakama, kaa chini."
Hapa analindwa Kamuhanda pia, unakumbuka alivyosema kuhusu tarehe yake ya kustaafu imekaribia! Hakutaka kuwakera wakubwa kwa kutotii amri zao.
kuanzia jana, nimeamini tanzania ni nchi ya ajabu na kijinga. Ihema kaleta ripoti ya kijinga. Ihema=mjinga, hajaelimika.
Uwongo dhahiri hapa ukitaka post idumu kuwa pro chadema hakuna lazaidi; hii haiwezi kudumu mdau anasema ripoti ni ya kijinga lakini haonyeshi ujinga wenyewe, kwa mantiki itakuwa ni ujinga kujadili ujinga