Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Ni ripoti ya Kijinga: I really mean it...

Mwanakijiji,

Mi nina jambo moja tu, wanahabari wa nchi hii wana sehemu kubwa sana ya kulaumiwa katika uendeshaji na siasa za nchi hii. Wao ndio wapambe wakubwa sana wa wanasiasa. Lakini kubwa zaidi hasa katika ripoti hii kuna mtu anaitwa Theophile Makunga kwenye ripoti hiyo, kama naye pia ameweza kushiriki kupika ripoti hiyo iliyomhusu mwandishi mwenzake basi tena!

Ndio sababu unaweza kuona kina Muhingo Rweyemamu, Novatus Makunga, Betty Mkwasa, etc. wanaingia katika ukuu wa wilaya!
 
Makunga anasubiri U-DC kama waandishi wenzake akina Muhingo, Makunga, Beti Mkwasa, Kipozi, Dumba, Kihemba,...

Jaji Ihema anaona kabisa anaona kabisa kuna uwezekano wa yeye kuwemo kwenye tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Teuzi za siku hizi ni kuonyesha UTIIFU kidogo tu,
Sikuwa na imani na kamati hiyo wala matokeo ya kamati.Lakini kikubwa zaidi nikasema ngoja nisubiri hotuba ya JK ya mwisho wa mwezi.Pale ndiyo nikaconclude moja kwa moja kuwa wala sitojisumbua na matokeo ya uchunguzi wa hiyo kamati.Tutawalaumu wajumbe wake,lakini the bucks stops with JK.Aliwasafisha watuhumiwa wote kwenye ile hotuba yake.Kama anapita humu,anafurahia sana,maana we're just beating around the bushes,tunawataja hawa individuals bila kujuwa wanamfanyia kazi rais.Kama ya mwabwepande yenyewe yamepita,nani atathubutu kwenda kinyume na JK?Nilisema ile siku ya hotuba yake kuwa kawasafisha na lawama aliwatupia chadema,sasa ni kipi cha kutufanya tutegemee matokeo tofauti?Toka lini?
 
Nimepitia ripoti nimesoma maneno ya Jaji Mstaafu Steven Iheme, anasema Chadema ndio chanzo cha vurugu na uvujifu wa amani kijijini Nyololo, hasa kutokana na uamuzi wa kunga'ang'ania kukusanyika isivyo halali eneo hilo.
 
hiyo heading umeitengeneza mwenyewe au umeikuta hivyo hivyo!?
Kwa maana kwangu mimi kama wangeandika 'manufaa' kwa hako kakisima bado ningekataa japo kwa shingo upande ningelikubali lakini kusema "MANUFAA MAKUBWA" tena kwa taifa ambalo zaidi ya 70% fresh water inatiririkia baharini ni aibu.
Sasa hao wanaoingia jikoni, bafuni, bustanini, chooni na kuyakuta maji huko yakitiririka watasema ni mafanikio ya aina gani!? Watz inabidi tujiangalie upya akyamungu!

 
Nimepitia ripoti nimesoma maneno ya Jaji Mstaafu Steven Iheme, anasema Chadema ndio chanzo cha vurugu na uvujifu wa amani kijijini Nyololo, hasa kutokana na uamuzi wa kunga'ang'ania kukusanyika isivyo halali eneo hilo.
Tangu lini wewe ukawa na akili za kusoma? wewe hapa ni behewa tu, fanya kazi ya Nape jioni kachukuwe buku mbili yako mchezo umekwisha.
 
hiyo heading umeitengeneza mwenyewe au umeikuta hivyo hivyo!?
Kwa maana kwangu mimi kama wangeandika 'manufaa' kwa hako kakisima bado ningekataa japo kwa shingo upande ningelikubali lakini kusema "MANUFAA MAKUBWA" tena kwa taifa ambalo zaidi ya 70% fresh water inatiririkia baharini ni aibu.
Sasa hao wanaoingia jikoni, bafuni, bustanini, chooni na kuyakuta maji huko yakitiririka watasema ni mafanikio ya aina gani!? Watz inabidi tujiangalie upya akyamungu!

Hakuna hata chembe ya editing hapo, huo mzigo nimeupakuwa kama ulivyo na kuushusha hapa, ndio mjuwe ni jinsi gani Serikali hii inatudharau.
 
Mimi sishangazwi na Polisi bali kuna watu wawili ndio wananiacha na mshangao, huyu Jaji Mstaafu na Teophil Makunga, hapa nashindwa kuelewa kama niko ndotoni au ni kweli nchi imefikia hapo?

Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwapongeza Chadema kwa kutangaza mapema kwamba hawatatoa ushirikiano wowote kwa kamati ambayo tofauti na kamati ya Harusi. Tunahitaji tume huru ya kimahakama yenye nguvu za kisheria.
Chadema ni chama makini sana, hawakurupuki kufanya jambo, kila wanalolifanya wanajua mantiki yake. Ndiyo maana Tundu Lissu alitamka hadharani kuwa huyo Jaji Ihema, hana sifa ya kuwa Jaji, kama madai ya Tundu Lissu ingekuwa haina mashiko tungeona heka heka ambazo angezipata, lakini kwa kuwa mamlaka husika zinajua madai yake ni ya msingi wanashindwa kumgusa! Na huyo mhariri wa gazeti makini la Mwananchi, inashangaza imekuwaje akaingia mkenge na kusaini ripoti ya kijinga kama hiyo!
 
Jaji Ihemu, anaendelea kusema ujumbe wa sms kutoka kwa Dr Slaa ulisema, "IGP nasuburi simu yako. Wajulishe Polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha, mtakuwa na karamu ya mauji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya Hague. Ni afadhali tufe kuliko manyanyaso haya"

Ujumbe huu ukiashiria umwagaji damu ni ushaidi tosha kuwepo kwa uvujifu wa amani.
 
Heri yangu nataka kubadilisha utaifa. Hata ikishindikana kuupata wa nchi za Ulaya ni aheri niende Malawi
Mambo mengine yanayofanyika katika nchi hii ni ya kusikitisha sana, nautilia shaka sana uwezo wa kufikiri wa Watanzania, ripoti ya kijinga namna ile huwezi kuileta kwa watu mpaka uwe una uhakika kwamba uwezo wao wa kufikiri ni duni sana, nawapeni pole sana Watanzania, poleni sana ndugu zangu Watanzania.
 
Kwa hili nimemdharau sana Nchimbi. ninasikitika kuporwa wazi na serikali kwa upumbavu huu.. POLENI WALIPA KODI WENZANGU
 
Jaji Ihemu, anaendelea kusema ujumbe wa sms kutoka kwa Dr Slaa ulisema, "IGP nasuburi simu yako. Wajulishe Polisi wako waandae risasi za kutosha, mabomu ya kutosha, mtakuwa na karamu ya mauji na kisha kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya Hague. Ni afadhali tufe kuliko manyanyaso haya"

Ujumbe huu ukiashiria umwagaji damu ni ushaidi tosha kuwepo kwa uvujifu wa amani.
user-offline.png
Mlyafinono

2nd September 2012 12:00
#1
Senior Member Array


Join Date : 6th April 2012
Posts : 107
Rep Power : 348
Likes Received38
Likes Given1



icon1.png
Polisi Iringa wajiandaa kuua mkutano wa Chadema Mufindi

Jeshi la polisi mkoani Irinaga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wameshindwa kufikia maafikiano kuhusu makubaliano ya awali ya kuanza kwa mikutano yao baada ya kumalizika kwa zoezi la sensa ya watu na makazi.

Wakati jeshi la polisi wakitaka chadema kusubiri hadi tarehe 8 mwezi huu baada ya muda wa sensa kungezwa chadema wanasema mkutano wao ambao umepangwa kufanyika Mafinga wilayani Mufindi upo palepale.

Kauli za Viongozi

RPC iringa, Michael Kamuhanda.

-nina digrii ya maswala ya kipolisi, CHADEMA hawawezi kutushinda.
-wasipotii agizo letu nakufanya mkutano wao mafinga tutumia uwezo wetu wote kuhakikisha tunawadhibiti.


Benson Kigaila.........

Wamezuia mkutano wetu kwa kisingizio cha sensa, wakati bububu zanziba leo kuta uzinduzi wa kampeni za uchaguzi,je huko hakuna sensa?

-Liwalo na liwe mkutano leo lazima ufanyike mafinga.

Dk. slaa........

Kauli ya Benson ndo msimamo wa CHADEMA.

-Nilionge na IGP jana kumweleza kuwa tulikubaliana kistaarabu kwahiyo aheshimu makubaliano.
-Mkutano wetu leo Mafinga lazima ufanyike tumechoshwa na ukandamizaji wa Jeshi la poisi.


My take.........
Kama kweli mkutano utafanyika mafinga maafa huenda yakawa makubwa kuliko ilivyokuwa morogoro kwani tayari magari 8 ya polisi yameshakwenda mafinga kupambana na lolote litakalotokea
​
 
Tangu lini wewe ukawa na akili za kusoma? wewe hapa ni behewa tu, fanya kazi ya Nape jioni kachukuwe buku mbili yako mchezo umekwisha.

Naona unachafua mjadala tu huwezi vita na mie, mie sina muda wa kujibizana na mtu ambaye anakaa kwa semeji yake, tupambane kwa hoja kwa matusi mie sikuwezi, @Copy to Matola, No fear, Saigon, zomba,
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji,

Kwanza kabisa umenyoosha, pili ni imani niliyonayo kuwa siku si nyingi CCM watakuwa upande wa pili wa kiti cha hukumu wakisomewa mashitaka yao kwa ubaradhuli wanaowatendea watanzania.

Swali moja linabakia.."CCM wanatoa wapi kiburi hiki" cha kunyanyasa Watanzania namna hii kana kwamba wao ni wageni toka ng'ambo na siku Watanzania wakipata uhuru wao CCM watarudi nchini kwao?
 
haya yote yanaandikwa kwa vile sasa ukweli umeanza kujulikana wazi, kitu kilichokuwa kikitumia miaka 5 kujulikana kwa umma hapo awali hivi sasa hakichukui hata siku tano kila mtu keshajua hata nje ya mipaka.
Kama polisi wanashindwa kusoma alama za nyakati watakuja kuaibika zaidi katika historia ya nchi na dunia kwa ujumla wake kama watu waliokuwa wameachwa nyuma kifikra. Fikiria hata wakoloni walisoma alama wakaamua kuzitawala nchi hizi indirectly kwa 'kutupa uhuru' badala ya kung'ngania mfumo waliokuwa wameanza nao wa utawala.
Chukulia mfano wa jinshi jeshi hili linavyozidi kujidhalilisha: Kamanda Kova alisema ameunda TUME kuchunguza jambo la Dr. Ulimboka na hiyo ilikuwa hata kabla ya hili la Marehemu Mwandosi, lakini mpaka sasa hakuna anayeliongelea hilo! Kwa vile Watanzania wote uelewa wao sio ule wa kupewa sahani za pilau na kofia tu bali kuna baadhi ni waelewa na hawa mtake msitake watakuja kuuliza hiyo tume ya Kova iliishia wapi (na hapo atakuwa kastaafu labda).
Mwangwi wa majibu yatakayopatikana hapo unaweza kufuta mazuri yote yaliyowahi kufanywa na jeshi hili. Pamoja na njaa zetu lakini heshima ya binadamu nayo pia ni muhimu
 
Binafsi sikutegemea jipya kutoka kwenye hii kamati,hizi tume hazijawahi kufanya kazi ya maana
 
Ni lazima tutambue na kukumbuka kuwa watawala wanaweza kufanya hivi kwa sababu Watanzania hatutaki kuwapinga wazi na wajue wanapingwa. Waandishi wetu wa habari ndio wanatuangusha zaidi kwa kuwa kama vipaza sauti vya watawala. Tumewaona wakionesha hasira zaidi baada ya Mwangosi kuuawa lakini ni hasira inayotokana na maumivu siyo na tofauti ya mtazamo.

Waandishi wetu wanapokuwa mbele ya watawala wananyenyekea kwa woga; wanaogopa kuwabana na kukataa taarifa za kijinga kama hizi kwa kuogopa kuonekana wako kimbelembele au hawana heshima. Binafsi naweza kusema tuliona kazi ya uandishi pale Iringa kabla ya tukio pale ambapo waandishi (akiwemo marehemu Mwangosi) walipoweza kuwabana maafisa wa polisi na kuwaonesha kuwa hoja zao hazina akili. Leo hii Nchimbi mbele ya waandishi anasema kuwa kuna ushahiidi ambao serikali inao unaweza kumtoa hatiani mtuhumiwa na waandishi wanakubali!!

Wakati mwingine ujinga siyo vile tunavyofanyiwa bali vile tunavyofanya echoing Forest Gumps' 'stupid is as stupid does'..
 
High expectations ndio tatizo na kutegemea ripoti ingejumuisha kila kitu tathimini nzuri ni adidu rejea ya kamati vinginevyo ni ngumu to accommodate feelings za kila mtu. Tupokee yakwao kwanza na tujifunze kuwa proactive kuliko kusubiri kila kitu kuletewa na kuacha maafa yatokee.

As matter of fact polisi wana bifu na vyama, marehemu Mwangosi katika mkutano wa waandishi wa habari aliuliza swali kwa Dr. Slaa,kuhusu bifu la polisi la Chadema, majibu yake Channel Ten wana documentary iliyoonesha hilo swali la marehemu muda mchache kabla ya kifo chake na msimamo wa Dr. Slaa ulikuwa liwalo na liwe mkutano uko pale pale. Tuache kabisa kutengeneza untouchables, yeyote anapokosa tumwambie ili ajifunze na kuwa bora zaidi.

Ingekuwa enzi za skonga wote wanaenda chini kula stiki, Polisi na Dr. Slaa wote wanayo dhima ya mauaji ya Mwangosi kwa kutokuchukua hatua ya kuzuia maafa ilihali maafa yalikuwa yanaonekana na marehemu alikuwa ameona hivyo na very unfortunately yeye na familia yake ndio wahanga namba moja. Mie nafsi ilitua baada ya Dr. Slaa kuchukua dhima ya kusomesha watoto wa marehemu na nikaona uungwa wa hali ya juu na fika msukumo wa lile swali la Mwangosi kwake kuhusu maafa hayo lilimgusa namna fulani.

Mzee Mwanakijiji wakati mwingine mahaba na ushabiki ukae kushoto, ukilinganisha polisi na vyama vya siasa. Mie naona vyama viko well equiped kwa maana ya skilled na competent personnel's kuliko polisi na vyama vikiamua na kuleta ubunifu vinaweza epuka maafa mengine bila kuumiza watu wasio na hatia na vigezo vya kupigania haki havitoshi kusababisha mauaji kwa watu wanyonge kuuawa. Kama ni sinema basi viongozi wa vyama ndio mastaa na wao ndio wanapaswa kufa kwanza ili uhuru upatikane kwa watu wote, sio wanakichafua na msala wanawaachia wanyonge wakati polisi wetu wenyewe hawajua hata wajibu wao wakiwa kazini, sio tu kwenye mikutano ya kisiasa bali hata wakiwa uwanja wa Taifa tu wao ni Majanga kuendelea kushindana nao ni kupoteza muda watatuumiza na wala hawajutii, yaani wameua polisi lakini jukumu la kulea familia wameenda kujitwisha watu wengine tukianza kuwapa majumu wao kama jeshi na katika bajeti zao wakaona kuna fund inaenda kutokana na maafa waliyosababisha wao wataacha tu na wajane na mayatima wakae pia katika ballacks zao wataacha lakini tunawaangalia, tunanung'unika na tunajaza thread na makala na wengine ndio wang'ara kama waandishi wazuri wa kuchambua ripoti za kamati kesho wataua tena.
 
Ni lazima tutambue na kukumbuka kuwa watawala wanaweza kufanya hivi kwa sababu Watanzania hatutaki kuwapinga wazi na wajue wanapingwa. Waandishi wetu wa habari ndio wanatuangusha zaidi kwa kuwa kama vipaza sauti vya watawala. Tumewaona wakionesha hasira zaidi baada ya Mwangosi kuuawa lakini ni hasira inayotokana na maumivu siyo na tofauti ya mtazamo.

Waandishi wetu wanapokuwa mbele ya watawala wananyenyekea kwa woga; wanaogopa kuwabana na kukataa taarifa za kijinga kama hizi kwa kuogopa kuonekana wako kimbelembele au hawana heshima. Binafsi naweza kusema tuliona kazi ya uandishi pale Iringa kabla ya tukio pale ambapo waandishi (akiwemo marehemu Mwangosi) walipoweza kuwabana maafisa wa polisi na kuwaonesha kuwa hoja zao hazina akili. Leo hii Nchimbi mbele ya waandishi anasema kuwa kuna ushahiidi ambao serikali inao unaweza kumtoa hatiani mtuhumiwa na waandishi wanakubali!!

Wakati mwingine ujinga siyo vile tunavyofanyiwa bali vile tunavyofanya echoing Forest Gumps' 'stupid is as stupid does'..
Mkuu siyo kwamba namtetea huyo mpuuzi Nchimbi,bali nadhani alichomaanisha ni kwamba huo ushahidi walioamuwa kutokuuweka kwenye ripoti,alimaanisha kwamba kama ushahidi huo utaonyesha wazi kumu incriminate muuwaji,basi anaweza kuitumia sababu hiyo kwa kusema tayari alishahukumiwa kwenye public court of opinion.Kuna watu wameshawahi kuachiliwa na mahakama kwasababu kama hizo.Lakini hilo halimaanishi kwamba ripoti hii si ya kijinga.

Kwa upande wa waandishi wa habari,wenye misimamo mithili ya Mwangosi ni wachache mno!Kama ungefahamu mazingira ya uandishi wa habari Tanzania,wala usingekaa uwe na imani nao.Kwanza kilichosaidia hata tukawa na baadhi ya waandishi wenye msimamo na magazeti yenye msimamo kama mwanahalisi,ni kwasababu ya maendeleo yaliyopatikana kwenye siasa za upinzani,na hivyo tukapata baadhi ya press ambazo haziwapigii makofi watawala kila kukicha na propaganda zao kutokana na nguvu ya upinzani dhidi ya chama tawala,kwahiyo kwasababu kuna magazeti yanayotegemea wasomaji,mabadiliko ya kisiasa yamesababisha hata baadhi ya magazeti hayo yaandike habari zenye kuwatagert wapenda mabadiliko ambapo ni wengi sana miongoni mwa wananchi.Wenye kusapoti mafisadi,wanafanya hivyo kwasababu ya pesa zao hata kama magazeti yao hayauzi.

Lakini culture ya njaa za waandishi ni za kawaida sana,ni issue ambayo slowly tunaondokana nayo,lakini utaratibu uliokuwa wa waandishi wa habari kutokutoa habari yoyote bila kupata chochote,ndiyo misingi hasa ya waandishi hao kuwalamba mafisadi viatu.

Waandishi wetu wengi,hawana culture ya kutupa habari wala kuelimisha,bali wana culture ya kuganga njaa.
 
Back
Top Bottom