Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,772
- 60,146
Utekelezaji wa maelekezo ya kisheria yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, umeanza rasmi kwa vitendo baada ya jopo la mawakili wake kuanza maandalizi ya nyaraka za maombi ya dhamana pamoja na kukamilisha hatua ya kuwasilisha notisi ya kukata rufaa mahakamani.
Akizungumza, Novemba 18, 2026, Wakili Paul Kisabo, ambaye ni miongoni mwa mawakili wa jopo la utetezi la Lissu na Mkuu wa Idara ya Utetezi katika Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema hatua hiyo inafuatia kikao kilichofanyika Jumatatu, Novemba 9, 2026, kati ya Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA, Gaston Garubindi.
Katika kikao hicho, Lissu alirejesha rasmi maelekezo (instructions) kwa jopo lake la mawakili ili liendelee na hatua mbalimbali za kisheria katika kumtetea dhidi ya shauri linalomkabili.
Kwa mujibu wa Wakili Kisabo, jopo hilo kwa sasa linaandaa nyaraka za maombi ya dhamana. Ameeleza kuwa, kwa mujibu wa utaratibu wa kisheria, mtu aliyetiwa hatiani na anayetaka kuomba dhamana wakati akisubiri rufaa yake kusikilizwa, anapaswa kwanza kuwasilisha notisi ya kukata rufaa.
Hatua hiyo ya awali tayari imekamilishwa kupitia Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA.
Wakili Kisabo ameeleza kuwa baada ya notisi ya kukata rufaa kuwasilishwa, hatua inayofuata ni Msajili wa Mahakama Kuu kuandaa kumbukumbu rasmi za mwenendo wa kesi (Records of Appeal).
Kumbukumbu hizo zinapaswa kujumuisha mwenendo mzima wa shauri, kuanzia lilipoanza hadi kutolewa kwa hukumu.
Baada ya maandalizi kukamilika, kumbukumbu hizo zitakabidhiwa kwa mrufani na jopo lake la mawakili, jambo litakalowezesha taratibu za rufaa kuendelea katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Ni muhimu kufuatilia hatua hizi kwa karibu, kwani mchakato wa rufaa na maombi ya dhamana ni hatua mbili muhimu katika harakati za kisheria zinazoendelea.