John Mason, mwandishi na mtaalamu nguli wa mambo ya uongozi aliwahi kusema kuwa "Only fools wait for the good luck"
Akimaanisha kuwa...
"Ni wapumbavu pekee ndio wanaosubiri bahati njema ili wafanikiwe"
Maisha hayakupi kile unachokitaka bali yanakupa kile unachokitafuta.
Watu wengi sana wana ndoto kubwa lakini hawako tayari kuzipambania.
Ukweli mchungu ni kwamba hakuna MUUJIZA utakaotokea kwenye maisha yako kila kitu kuwa sawa bila juhudi yoyote.
Siku zote kumbuka jambo hili kuwa, ndoto bila JUHUDI hubaki kuwa MATAMANIO tu.
Mafanikio sio TUKIO la ghafla ni MCHAKATO🧠,usisubiri mambo yatokee YAFANYE yatokee🎯
Bila kujali ni muda gani umeshaupoteza kwa kusubiri mambo yatokee yenyewe.
Leo amua kuwa mtu mpya,jenga mtazamo mpya na uchukue hatua thabiti ili kuwa mtu bora kesho.
-The Power Is Within You-
✨ 🫵
(Yona Morice Yona)