JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Huu ndio mwaka wangu wa mwisho kuishi maisha haya ya u bachelor..

Ni mateso ya hali ya juu, by next year najilipua Naoa kabisa...

Hakuna muda sahihi, ni kheri kuwa na mwanamke ambaye nikitoa job aniliwaze sio maisha haya ya stress za maisha na bado niwe bachelor Noo wayy.. 😔
 
Screenshot_20261121-090749_WhatsApp.jpg
 
Kila mtu unayemuona amepiga hatua kwenye maisha yake kuna siku aliwahi kukata tamaa.

Kuna watu leo ukiwaona unaweza kudhani kuwa kila siku wao wanashinda tu au hawapitii changamoto kabisa katika maisha yao.

Ila ukiwakaribia ndio unagundua kuwa kuna wakati hata wao walitamani waishie njiani na wasiendelee mbele kabisa

Hali yoyote unayopitia leo,hata kama inakupa maumivu makali kiasi gani...

Usikubali kuhitimisha kuwa umefika mwisho na hakuna tumaini tena🤷

Kabla hujakataa tamaa kaa chini jiulize ni wangapi wanakutegemea?

Usikubali kukata tamaa amini kuwa changamoto ni sehemu ni ya maisha na zitapita tu.

Usisahau kuwa Mungu akitaka kukufanya kuwa mtu mkubwa.

Wakati mwingine hukupitisha kwenye njia ngumu ili kukuandaa kuwa mshindi🏆

Usikate tamaa inawezekana umebakiza hatua chache tu ili kuufikia ushindi wako.

Thamani ya ndoto yako ni kubwa mno kuliko changamoto unazopitia leo.
-The Power Is Within You-
✨🫵
 
Nyakati ngumu hufichua watu halisi:
-Kuna ukweli ambao huwezi kuujua mpaka pale maisha yanapokupa wakati mgumu.

-Wakati kila kitu kinakwenda vizuri, ni rahisi kuwa na watu wengi wanaokuzunguka, wanaokuchekea na kukuambia kwamba "tuko pamoja"

-Lakini siku mambo yanapobadilika ndipo unapogundua nani anakujali kwa dhati na nani yupo kwa sababu ya faida anazopata kwako.

-Usipuuze watu waliokushika mkono wakati huna kitu cha kuwapa🫰

-Watu wa namna hiyo ni wachache sana,wakati mwingine, siku ngumu haziji tu kutuumiza bali zinakuja ili kutufungua macho na kutuimarisha zaidi.
-The Power Is Within You-
🫵 💥
 
-Miongoni mwa mambo ya msingi sana yanayoweza kukuongezea kasi ya kutimiza malengo yako ni uwezo wako wa kukaa kimya na kutomweleza kila mtu mipango yako muhimu.

-Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa unapomwambia kila mtu mipango yako unapunguza uwezo wa ubongo wako kuchukua hatua na kutekeleza kwa vitendo hali hii husababisha ujisikie kama umeshafanikiwa wakati bado hujaaanza🤷

-Unataka kuanzisha biashara? nyamaza kimya, unataka kwenda masomoni tena? nyamaza kimya,unataka kununua kiwanja kingine? nyamaza kimya.
(Waache waone matokeo tu)

-Kwasasabu sio kila mtu ana nia njema na mafanikio yako,baadhi wameshakuchorea mstari wa mafanikio yako hivyo wakisikia mipango yako mikubwa unaweza kujikuta unaibua vita na upinzani mkali😥

-Mtu mmoja mwenye busara aliwahi kusema kuwa "People can not attack what they don't know" akimaanisha kuwa "Watu hawawezi kushambulia kitu wasichokijua"

-Hivyo ni muhimu sana kuwa makini ni wakati gani na pia ni nani unamweleza mipango yako,Mungu akusaidie na akuepushe sana na watu wanaopiga vita mafanikio yako.
-The Power Is Within You-
✨ 🫵

(Yona Morice Yona)
 
Wakati mwingine nguvu yako kubwa iko kwenye uwezo wako wa kusamehe mapema waliokukosea.

-Dr.Frederic Luskin mwanasaikolojia na mtaalamu wa afya ya akili kutoka chuo kikuu cha Stanford university.

Baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu kusamehe na kuachilia waliokukosea alibaini kuwa, "Watu wanaosamehe mapema huishi maisha ya furaha na huwa hawabaki na hasira kwa muda mrefu".

-Aidha utafiti huu ulibainisha kuwa watu wanaosamehe wengine mapema wako salama dhidi ya tatizo la msongo wa mawazo na mfadhaiko wa kihisia (Stress and depression)😥

-Usisahau jambo hili kuwa kusamehe sio udhaifu bali ni uthibitisho kwamba wewe ni JASIRI una uimara wa kihisia na unaweza KUJITAWALA.

-Inawezekana umepitia maumivu makali ya kihisia lakini leo amua kuachilia na kumsamehe aliekukosea.

-Zungumza nae au mtumie hata ujumbe mfupi mwambie "Nimekusamehe" sio kwasababu anastahili msamaha bali kwasababu wewe unastahili AMANI ya moyo.

-Hata kama unaona ugumu jilazimishe utashangaa baada ya muda mfupi unaanza kuwa na amani na utulivu.

Kama umeipenda makala hii weka reaction kisha mtumie mtu mmoja tu unayemthamini ili kumponya maumivu ya moyo💕
-The Power Is Within You-
✨ 🫵

(Yona Morice Yona)
 
ACCOUNTANT
Industry: FMCG
Location: Mwanza

REQUIREMENTS
  • Bachelor’s Degree in Accounting, Finance, Commerce, or a related field.
  • CPA (T) is mandatory.
  • 3–5 years of relevant accounting experience, preferably in FMCG, manufacturing, trading, or distribution.
  • Strong knowledge of financial reporting, reconciliations, taxation, and statutory compliance.
  • Proficiency in accounting software/ERP systems and Microsoft Excel.
  • Strong analytical, numerical, organizational, and communication skills.
  • High level of accuracy, integrity, and attention to detail.

Share your CV via:
📧 recruitment@toptalentedrecruits.co.tz
 
Paones General trading Company , DSM. inatafta fresh graduate wa UDSM 2026 Course ya Bachelor Degree ya IT, Computer science Engineer na Telecommucation. Atume CV yake Human.Resources@paones.co.tz Deadline ni 23 Nov 2026. Andika Position IT Support (Networking) Intern. Lazima awe ametoka katika chuo tajwa tu. Kama kuna mtu ana mfahamu mtu au uanahitaji maelezo bas WhatsApp only 0762024713.
 
NAFASI ZA KAZI 68 ZA INTERNSHIP KUTOKA WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART)

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) unawaalika Watanzania wenye sifa stahiki, wenye uwezo wa juu, wanaolenga matokeo, wenye kujituma, waadilifu na wenye mtazamo wa maendeleo, ili kujaza nafasi sitini na nane (68) za mafunzo kwa vitendo (internship) kama ilivyoelezwa hapa chini:-

1) BRT OPERATIONS MONITORING ASSISTANTS - 20 POSTS

2) BRT FLEET AND MAINTENANCE MONITORING ASSISTANTS - 2 POSTS

3) BRT DATA AND PERFORMANCE MONITORING ASSISTANTS - 2 POSTS

4) CUSTOMER SERVICE OFFICER - 6 POSTS

5) PHOTOGRAPHER - 1 POST

6) VIDEOGRAPHER - 1 POST

7) GRAPHIC DESIGNER-1 POST

8) MARKETING AND BUSINESS DEVELOPMENT OFFICERS - 20 POSTS

9) CASHIERS -13 POSTS

10) LEGAL OFFICERS - 2 POSTS

Age Limit: The applicant should be between 18 and 35 years of age.

INTERNSHIP TENURE: Internship tenure will be 12 months with the possibility of extension to 24 months.

Remuneration: As per Government Internship Guidelines.

Deadline for submitting application is 02th December 2026;

All applications which will be sent in any other means apart from the DART Recruitment Management System (RMS) will not be accepted.

Applications should be sent to: https://ajira.dart.go.tz/
 
Back
Top Bottom