JIFANYE UPYA KAMA NDEGE TAI:
Siku moja jioni tulivu baada ya kusoma kitabu cha Dr. Myles Munroe kinachoitwa "The Principles and Power of Vision", nilijifunza sifa saba za ajabu kuhusu ndege Tai 🦅.
Lakini leo nataka nikushirikishe sifa moja tu, ambayo ni "Kujifanya Upya."(Renewal)
Tai anapokuwa amechoka na manyoya yake yamechakaa,huwa anajitenga na kupaa juu mlimani mbali na kelele za ndege wengine.
Huko anajitoa manyoya, makucha na mdomo uliochakaa, mchakato huu huleta maumivu makali na upweke.
Lakini baada ya siku 150 tai hurudi akiwa mpya kabisa na nguvu za ajabu za kupaa juu zaidi🔥
Hivi ndivyo ilivyo hata katika maisha yetu, ili uweze kufika viwango vya juu zaidi katika maisha yako.
Lazima ukubali kujifanya upya kama tai,hakuna mafanikio yanayokuja bila kujitoa.
Tatizo kubwa linalo wachelewesha watu wengi ni KUOGOPA mabadiliko🤷
Wanataka wafanikiwe pasipo kubadili tabia zinazo wachelewesha.
Wamebeba makosa ya zamani,majeraha, hofu,visasi.
Na mitazamo hasi inayowazuia kuchukua hatua mpya kwenye maisha.
Kujifanya upya kunahitaji ujasiri wa kujitenga na kuachana na yaliyopita.
Siku zote kumbuka jambo hili...
Maumivu ya kuchukua hatua mpya ni makali, lakini kubaki kama ulivyo ni HATARI zaidi.
Leo bila kujali kuwa umeshafanya makosa mengi kiasi gani, amua kujifanya upya.
ili uongeze kasi kuelekea kwenye kilele cha mafanikio yako makubwa🥇
-Kama umeipenda makala hii weka reaction kisha mtumie mtu mmoja tu unayemthamini🫡
-The Power Is Within You-
💥 🫵
(Yona Morice Yona)