-Watu wengi sana wanataka mafanikio lakini hawako tayari kuchukua hatua muhimu zitakazo wafanya wafike kwenye kiwango cha mafanikio wanayoyataka.
-Moja ya changamoto kubwa sana ambayo inawakabili watu (hasa vijana wengi) ni kukosa uvumilivu na kutoamini kwenye mchakato♻️
-Yani mtu anahitimu chuo 🎓 leo anataka apate kazi nzuri leo,ajenge nyumba nzuri leo azae watoto awe na familia bora leo amiliki gari leo🚗
-Mwingine anaanzisha biashara leo anataka mwaka huo huo apate faida kubwa,akipata changamoto kidogo tu anakata tamaa haraka
-Anataka kila kitu anachofanya basi kifanikiwe na kumpa matokeo makubwa haraka sana (Are you normal?)😁
-Ukweli ni kwamba
Unapopitia kwenye mchakato wa kujijenga na kutengeneza mifumo thabiti 🎯 ya maisha yako kila shilingi inayopita kwenye mikono yako utaithamini na utakuwa na nidhamu nayo sana💯
-Kijana yeyote yule anayetaka kufika juu zaidi kwenye kilele cha mafanikio yake lazima awe tayari kukubali na kuheshimu mchakato utakao mfanya kuwa mtu bora kesho.
Siku zote jikubali,pambana kwa bidii,amini kuwa wewe ni mshindi muda wako upo ni suala la muda tu⌚✨
-Kama umeipenda makala hii weka reaction kisha mtumie kijana mmoja tu unayemthamini ili kumuongezea kasi ya kutimiza malengo yake.
-The Power Is Within You-
✨ 👊 🫵
(Yona Morice Yona)