Usiweke maisha yako kwenye mikono ya watu wengine:
kwani kila mtu ana mipango yake, majukumu yake na matumizi yake. Usifikiri kwamba kwa sababu mtu ana uwezo wa kifedha basi ana wajibu wa kukusaidia kila unapohitaji msaada.
Kuna watu ambao wametunza maumivu ya muda mrefu kwasababu kwa namna moja au nyingine kuna mtu alishindwa kuwasaidia.
Ukweli ambao wengi hawapendi kuukubali ni kwamba hakuna mtu anayepaswa kusimamisha maisha yake ili kubeba majukumu yako.
Ni kweli kwenye maisha kuna wakati utahitaji msaada ila usisubiri mtu akuokoe,anza kujitengenezea maisha ambayo hutalazimika kuomba kila wakati.
Siku moja utaelewa kwa nini kujituma na kutegemea juhudi zako mwenyewe ni muhimu kuliko kutegemea huruma za watu.
-The Power Is Within You-
✨ 🫵