Ngoja ni lale zangu!
Kiingereza kimekuwa kigumu mno.
Sawa!
Walikuacha bila kutoa taarifa yoyote. Hawakutaka kusikia chochote. Hawakutaka kutafuta suluhu au kurekebisha uhusiano mliokuwa nao. Na sasa, wameondoka.
Basi, utafanya nini ili wajutie kukupoteza?
Jambo la kwanza: Potea kabisa.
Rafiki yangu, ukimya ndio nguvu yako. Katika hali hii, hakuna kutuma ujumbe, hakuna kupiga simu, hakuna kuweka machapisho kwenye WhatsApp (stories), au chochote cha namna hiyo. Waache wahisi pengo lako.
Jambo la pili: Jiboreshe.
Baada ya kuondoka, jiboreshe. Fanya hivyo kwa ukimya. Jirekebishe. Inua kiwango chako cha kufikiri. Soma vitabu na ujipatie maarifa.
Jiboreshe kimwili, kiroho, na kiakili. Jiboreshe, lakini usitangaze. Waache wasikie habari zako kutoka vyanzo vingine.
Jambo la tatu: Usipatikane kwa urahisi.
Yule mtu wa zamani waliyemjua hayupo tena. Hawawezi kukuona au kuhisi uwepo wako. Hakuna tena mazungumzo ya usiku sana. Hakuna tena nafasi ya pili. Wewe tulia tu. Hakuna tena hifadhi ya kihisia kwa ajili yao. Haki hizo zote zimeondolewa.
Kwa sababu umejiboresha, na kila mtu anatamani kuwa na mtu anayepiga hatua maishani.
Jambo la nne: Waache wakuone ukifanikiwa.
Anza kufanikiwa. Anza kufanikiwa! Kufanikiwa ndilo jambo bora zaidi unaloweza kujifanyia. Huhitaji kujigamba.
Acha kung'aa kwako, amani yako, maendeleo yako, na mabadiliko uliyopata yazungumze kwa nguvu zaidi kuliko maneno.
Waache wakuone ukigeuka kuwa mtu ambaye hawakuweza kumudu au kumkabili. Nenda kafanye mambo ambayo siku zote ulitamani kuyafanya. Kuwa mtu yule ambaye siku zote ulitamani kuwa. Kuwa wewe mwenyewe.
Pale unapokuwa wewe mwenyewe, unashinda mchezo huo.
Na mwisho, jambo la tano: Usioneshe kinyongo.
Namaanisha nini? Walitarajia uwe na uchungu, lakini wewe onesha kutojali kabisa. Unaelewa? Hakuna kitu kinachoweza kumsumbua mtu zaidi ya kugundua kuwa mwenzake amesonga mbele na wala hajali tena.
Huna hasira nao. Wala hufurahii uwepo wao. Uko katikati tu—hujali kama wapo au hawapo.
Hivyo ndivyo unavyoweza kumfanya mtu ajutie kukupoteza.