Hongera Ngeleja; Hiyo ni Moja...

Hongera Ngeleja; Hiyo ni Moja...

Anastahili pongezi kwa kweli.
Kinachofurahisha nafsi yangu ni kwamba wewe Nyani Ngabu na wengine wote kama wewe, mna bei. Mmeshafikia bei, hivyo kila afanyalo Ngosha liwe baya au zuri, litakuwa zuri tu. Hesabu za logics zishafutika pale tu Kikwete alipoondoka madarakani. Na jana Mkapa , mwizi namba moja anatukana watanzania kuwa wapumbavu. Hili hamtaliona, maana ameongea akiwa na Ngosha! Kweli Nyerere alisema , Mayu weeee!!!
 
Tumwamini Rais yupi?

Kikwete, specifically hela za escrow sio za serikali.
ili jambo
Ina maana Magufuli kataarifiwa kuwa ni za umma?

Je taarifa hiyo imo kwenye report ya Mruma au Osoro?
upumbavu unaanzia hapa,nani Raisi? je leo hii unafata uongozi upi? na upumbavu unapitiliza zaidi unapo husisha suala la mchanga na escrow ningesema ni utoto lakini nina watoto ingawa sio wa umri wako lakini hili jambo wanaweza kulitofautisha.
ukitumia akili yako vizuri unaweza kuwa na tija kwa siasa za nchi hii
 
Hili swali linaulizwa saaana! Sijui kwanini hamlijibu.
...Sasa mnaanza kulisifia jizi lakini wapuliza filimbi ya kuwagutusheni kuwa mnaibiwa wametupwa nje ya bunge nanyi hamuandiki article za kuufahamisha kama sio kuukumbusha umma kwa habari ya ushujaa na uzalendo wao uliotukuka.
Wapuliza filimbi HAWA?
Si ndo wale tuliowashangilia na kuwaandikia articles kibao wakati wanapuliza filimbi ya LOWASA FISADI NUMBER MOJA TANZANIA?
Mkuu wewe unawaamini hao?
Mbona unaonekana kama vile unaakiliakili kidogo? vipi Mkuu na wewe ni MSUKULE?
Subiri utakaposikia 2025 RUGE agombea URAIS kwa hati ya DHARULA kupidia chama chetu.
 
upumbavu unaanzia hapa,nani Raisi? je leo hii unafata uongozi upi? na upumbavu unapitiliza zaidi unapo husisha suala la mchanga na escrow ningesema ni utoto lakini nina watoto ingawa sio wa umri wako lakini hili jambo wanaweza kulitofautisha.
ukitumia akili yako vizuri unaweza kuwa na tija kwa siasa za nchi hii
Tufanye mimi mjinga hewala, wewe mjanja wetu umeambiwa "......tuwaache wapumzike, wamefanya kazi kubwa" onyesha ujanja wako basi! Unambwelambwela tu!

Ulienda shule kusomea ujinga, thibitisha vinginevyo.
 
Wapuliza filimbi HAWA?
Si ndo wale tuliowashangilia na kuwaandikia articles kibao wakati wanapuliza filimbi ya LOWASA FISADI NUMBER MOJA TANZANIA?
Mkuu wewe unawaamini hao?
Mbona unaonekana kama vile unaakiliakili kidogo? vipi Mkuu na wewe ni MSUKULE?
Subiri utakaposikia 2025 RUGE agombea URAIS kwa hati ya DHARULA kupidia chama chetu.
Sasa unijibu:
Fedha escrow ni zetu au zio zetu?

N.B Kikwete alisema sio zetu.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tangu mapambano dhidi ya ufisadi yaanze hadi leo hii, hakuna kitendo ambacho tunaweza kukisema kimefanyika, kufanyika, au kufanywa na mtu yeyote aliyetajwa kuhusika au kuhusishwa na ufisadi ambacho kimetupa matumaini kama kilichofanywa na Ngeleja leo. Na hapo sijaweka chumvi bado.

Tulikuwa na mtuhumiwa mmoja wa ufisadi mambo yalipokuwa ya moto aliamua kutorokea Marekani hadi mauti kumkuta huko. Mwingine kelele za ufisadi zilipozidi sana yeye aliamua kujivua nafasi zote za uongozi wa chama chake na kuamua kuendelea na biashara zake. Wengine wawili waligangamana hadi kufikishwa mahakamani na kesi ikaenda kwa miaka wee hadi nusura tukasahau; mwisho wa siku wakapewa jukumu la kusafisha bustani huku wakiimbiwa na kwaya ya matarumbeta (hii chumvi sasa). Mmoja yeye aliitwa kila majina ya ufisadi lakini akagangamala hadi kutaka kugombea Urais hadi jina lake likakatwa lakini hakukata tamaa akarukie meli nyingine kujaribu nia hiyo hiyo. Wengine wengi waliamua kufa na tai zao shingoni. Hakuna kati yao aliyekuwa hata na uthubutu wa kusema "mmh hii kashfa sina cha kujificha kama ni hela basi chukueni hela yenu". Ngeleja kavunja mwiko.

Wale wa EPA wao walibembelezwa hadi tume ikaundwa ili warudishe fedha na hatujui nani alirudisha nini kwani wengine waligoma kabisa kurudisha fedha hizo (KAGODA hao) na hadi leo tumewakubalia kuwa kilichoenda kwa mganga ndio hicho tena! Sijui hata wale ambao walikuwa wanaamriwa na mahakama kurudisha fedha (restitution) kama wanarudisha hata asilimia 50 ya kilichodaiwa kwao au wengi wanakimbilia kujitangaza kufilisika.

Kuna uwezekano mkubwa wengi waliopokea fedha za escrow wamezila na kunawa mikono kabisa. Ni sawasawa na watu waliokuta akaunti zao zimejazwa mamilioni na walijua siyo zao wakaenda kuzitumia wakidhani walikuwa wameteremshiwa mana na kwale jangwani! Mwisho benki inaenda kuwashtaki wanashangaa - "ooh nilidhani nimebarikiwa sana".

Alichofanya Ngeleja kimechelewa bila ya shaka. Hakuna shaka kuona kuwa Ngeleja kwa kukubali kuchukua fedha hizo wakati huo kwa mtindo aliofanya nao unamfanya aonekane alikuwa anahusika moja kwa moja au kwa kiasi na racketeering ya fedha hizo. Ni wazi pia kurudisha kwake fedha hakuna maana hapaswi kusogelewa na mikono ya sheria. Hii itakuwa ni kuchezea sheria kwani tangu wakati fedha amechukua hadi leo anaweza kuwa ameenda kuzitumia kazalisha fedha nyingine nyingine na anachorudisha ni kile ambacho anadaiwa tu. Ni sawasawa na mtu aibiwe ng'ombe jike halafu baada ya mwaka mmoja aende kwa mwizi wake na kukuta ng'ombea ana ndama mapacha. Je, arudishiwe ng'ombe jike yule tu au na wale mapacha?

Hili linatuleta kwenye hoja ya laumu (culpability). Kwamba, ni kwa kiasi gani Ngeleja na wengine waliopokea fedha hizo wanahusika katika kubeba lawama ya kuwa sehemu ya organized crime hii? Je, laumu hii inaweza kuwa katika ngazi ngapi? Naomba kupendekeza ifuatavyo na ninaamini uchunguzi unaoendelea na mashtaka yanayoenda kuletwa dhidi ya wahusika mbalimbali utazingatia kitu kama hiki.

1. Wahusika wakuu - Wahusika wakuu wa kashfa ya escrow watakuwa ni wale ambao moja kwa moja na kwa pamoja walishirikiana kula njama ya kuchota fedha za escrow. Kwa sasa hawa wametajwa wawili lakini kuna uwezekano wa watu wa nyongeza. Seith na Ruge watakuwa kwenye kiti cha juu kabisa.

2. Wahusika Watumishi wa Umma - Hawa namaanisha wale maofisa wa serikali ambao wakijua kuwa wanashirikiana na wahusika wakuu walichukua maamuzi ya kufanikisha njama hiyo. Kama hawa walipokea fedha kiasi chochote kile hawa watakuwa sehemu ya wale ambao wameshirikiana njama ya kufisadi akaunti hiyo.

3. Wanasiasa na wananchi wenye ushawishi (influential persons) - Kuna kundi hapa la wanasiasa na watu wengine ambao kutokana na nafasi zao katika jamii waliaminiwa kuwa wana ushawishi wa aina fulani katika jamii. Hawa wanaweza wakawa wamepewa fedha bila kuambiwa ni za nini hasa au waliambiwa tu kuwa "shukrani" au "zawadi". Kundi hili lina watu wengi sana na ninaamini ni kundi ambalo Ngeleja alikuwa ni mmoja wao; lakini pia Ngeleja anaweza kuwa sehemu ya kundi la pili.

Sasa Ngeleja kwa kuangalia katika kundi la pili au kundi la tatu bado alichokifanya kinampa ahueni fulani fulani katika uchunguzi wowote ule. Anaweza kupewa adhabu ndogo kutokana na uthubutu wake wa kurudisha fedha na anaweza asipate adhabu yeyote kubwa hasa kama atakubali kuwa shahidi wa upande wa mashtaka na kutoa ushahidi mkubwa. Hili la pili ndio naamini litaamua sana jinsi gani serikali itaamua kumwadhibu Ngeleja. Na mwendesha mashtaka yeyote makini ataweza kupima faida au hasara ya hiyo.

Ngeleja ataulizwa:
- Kwanini ulifungua akaunti Mkombozi Benki
- Nani alikuambia ufungue
- Alikuahidi nini
- Mawasiliano gani ulikuwa nayo
- Nani wengine walihusishwa n.k

Majibu atakayoyatoa kwa maswali hayo na yanayoendana na hayo na ukweli wa majibu hayo utaamua kwa kiasi kikubwa atatendewa vipi na vyombo vya usimamizi wa sheria (law enforcement agencies).

Vyovyote vile ilivyo, hakuna shaka alichofanya Ngeleja kama kingefanywa na watu wote ambao wamepokea fedha za uhalifu au ambao wametajwa katika kashfa mbalimbali nina uhakika kiasi kikubwa cha fedha za umma kingerejeshwa mikononi mwa umma lakini vile vile kingefanya watu wafikirie mara mbili mbili wanapoona fedha zinaingia tu kwenye akaunti zao.

Mtazamo wangu ni kuwa wote waliopokea fedha hizi popote pale walipo wafikirie mara mbili kama bado wanataka kung'ang'ania kuwa 'ni zawadi' au wanataka kuziruka na kurudisha ili angalau.. kama nilivyosema "labda, tena labda" wanaweza wakaangaliwa kwa jicho la pili... lakini wale wagumu, wanaofikiria kuwa hizi ni zama zile za yule, siku si nyingi watapigishwa magoti na wataomba wakati huo warudishe na watakataliwa. Kwani hata neema ina wakati wake.

Ngeleja kasoma nyakati, kaamua kuwahi! Kati ya aliyerudisha na wale ambao wamekaza shingo zao wakiombea kuwa hawataguswa nampa pongezi huyu...

Huyu ni mmoja, wengine?

MMM
Heshima kuu MKJJ.
Kama kawaida umetiririka vilivyo na kufafanua mambo kwa utulivu mkubwa.
Najaribu kulitazama jambo hili kwa jicho jingine na kujiuliza maswali,
-Mzee Ruge hakuwa na pesa ingine zaidi ya za Escrow?
-Ni kipi kinachounganisha kuwa kila pesa aliyotoa Ruge ilitokana na billions za Esrow?
-Mnikulu wa wakti huo alichotewa 800 millions,je vyombo vyetu vina uhakika kuwa hizi ziliishia kwa Gurumo tu?

Nina wasiwasi ya kuwa kesi itaonea watu kwani kuna kila dalili ya kuwa pesa zimekwenda mbali kiasi ambacho ukifuatilia sana itakuwa kuiingiza nchi katika mzozo.
Tukumbuke kuwa Mh. pinda aliwahi kuapa ya kuwa hatawataja wamiliki wa kampuni mojawapo hata kama wabunge wangemsulubu.
Ninachokiona na bahati mbaya wengi hasa watu wa kawaida wanavutika nacho ni umaarufu unaojengwa bila kuangalia athari za muda mrefu.
 
Sasa unijibu:
Fedha escrow ni zetu au zio zetu?

N.B Kikwete alisema sio zetu.

Achana na Kikwete mkuu.
Hizi ni zama za JPM, Lazima kitajulikana tu!
bado LUGUMI tulia tu ujionee.
Ndipo utakapomuelewa LEMA kwa nini anapata HOFU ya nani atampokea MAGUFULI 2025 wakati mwanzo alimtabiria kifo.

Kwani chama chetu kinasemaje siku hizi?
Bado kinasema ni za Umma? au kimeshabadilisha mwelekeo kama kilivobadilika kwa LOWASA?
 
Maswali ya msingi hayapati majibu
siasa na porojo tu
 
Wengine wengi waliamua kufa na tai zao shingoni. Hakuna kati yao aliyekuwa hata na uthubutu wa kusema "mmh hii kashfa sina cha kujificha kama ni hela basi chukueni hela yenu". Ngeleja kavunja mwiko.
Wengine imelazimika mkuu wa kaya kuwalinda wasiishiye jela kwa kisingizio cha kufanya mambo mengi.
 
Achana na Kikwete mkuu.
Hizi ni zama za JPM, Lazima kitajulikana tu!
bado LUGUMI tulia tu ujionee.
Ndipo utakapomuelewa LEMA kwa nini anapata HOFU ya nani atampokea MAGUFULI 2025 wakati mwanzo alimtabiria kifo.

Kwani chama chetu kinasemaje siku hizi?
Bado kinasema ni za Umma? au kimeshabadilisha mwelekeo kama kilivobadilika kwa LOWASA?
Kwani mnacheza mziki gani mpaka sasa?
 
Mkuu hawa ni mafisadi tu, ila kitendo hiki kinawapa wakati mgumu wote waliopokea mgao. Pia kurudisha serikalini ni sawa maana ukinunua mfano gari ukangudua ni la wizi huwezi kulirudisha kwa mwenyewe inabidi ulisalimishe polisi ili alokuuzia akamatwe. Ila hii picha ni ya hatari nadhani hata kwa maisha yake maana kuna wale walikula 1.6bn.

mkuu;
Nakubaliana na wewe kabisa ila mfano ulio utoa si sawa na yaliyo tokea hapo jana. Ngeleja alitakiwa azirudishe zile hela ka JR kwa sababu alisha kaa nazo muda mrefu sana. Ka sivyo, basi angelizipeleka polisi ziwe kielelezo cha ushahidi.
Leo amekaa nazo, amefanyia biashara zake, halafu faida ndo anapeleka TRA!! Sio sahihi man. TRA iliziandikia ni mapato gani?? Road license?? Hotel levy?? Kodi ya vileo?? Ziliandikiwa ni nini Ngeleja kaleta?? Aungane na Singa na James kule Keko si uraiani
 
Tufanye mimi mjinga hewala, wewe mjanja wetu umeambiwa "......tuwaache wapumzike, wamefanya kazi kubwa" onyesha ujanja wako basi! Unambwelambwela tu!

Ulienda shule kusomea ujinga, thibitisha vinginevyo.
sasa mbona unajibu kwamba hewala , wewe mjinga , halafu hapo hapo unaonyesha hasira za unambwelambela tu! any way kwa kuwa mimi mstaarabu nitasema asante.
 
Naona somebody anamsifu mhalifu, kwa sababu ya tu ya mhalifu kukiri Uhalifu wake BASI Kumemfanya authibitishie Umma jinsi yule Ampendaye anavyotisha!, Jinsi mafisadi wanavyomuogopa!!!
Yaani badala ya kuombea au kutaka mafisadi kuziogopa sheria yeye anafurahia jinsi wanavyomuogopa mtu, na badala ya Kumtaka yule ampendaye saaana mwenye dhamana kuu ya kusimamia sheria azisimamie sheria kweli kweli, yeye anapongeza "Hatua dhaifu" za kisanii kama hizi za kurudisha mali ya wizi bila kuulizwa kwa nini aliiziba in the first place!. Shame shame shame!
 
Back
Top Bottom