Hongera Ngeleja; Hiyo ni Moja...

Hongera Ngeleja; Hiyo ni Moja...

Unampongeza Ngereja??? ...

Kweli unafiki ni sehemu ya ilani ya CCM...

Nauliza tu, ni za umma au RUGE???
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Upuuzi wa masudi, alipaswa arudishe kwa James sio serikalini maana hizo hazikua pesa za serikali(uma by Jakaya) au huko serikalini nako waligawana mgao wao hivyo amerudisha zile walizogawana serikalini ila za James bado anazo?
 
Hela ni za Ruge na Seth wala siyo za umma! Watu watafute namna ya kuinua mapato ya serikali. Hizi za akina Ruge hatufiki nazo popote jamani! Mimi nasubiri chief wetu kama atazirudisha!!
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tangu mapambano dhidi ya ufisadi yaanze hadi leo hii, hakuna kitendo ambacho tunaweza kukisema kimefanyika, kufanyika, au kufanywa na mtu yeyote aliyetajwa kuhusika au kuhusishwa na ufisadi ambacho kimetupa matumaini kama kilichofanywa na Ngeleja leo. Na hapo sijaweka chumvi bado.

Tulikuwa na mtuhumiwa mmoja wa ufisadi mambo yalipokuwa ya moto aliamua kutorokea Marekani hadi mauti kumkuta huko. Mwingine kelele za ufisadi zilipozidi sana yeye aliamua kujivua nafasi zote za uongozi wa chama chake na kuamua kuendelea na biashara zake. Wengine wawili waligangamana hadi kufikishwa mahakamani na kesi ikaenda kwa miaka wee hadi nusura tukasahau; mwisho wa siku wakapewa jukumu la kusafisha bustani huku wakiimbiwa na kwaya ya matarumbeta (hii chumvi sasa). Mmoja yeye aliitwa kila majina ya ufisadi lakini akagangamala hadi kutaka kugombea Urais hadi jina lake likakatwa lakini hakukata tamaa akarukie meli nyingine kujaribu nia hiyo hiyo. Wengine wengi waliamua kufa na tai zao shingoni. Hakuna kati yao aliyekuwa hata na uthubutu wa kusema "mmh hii kashfa sina cha kujificha kama ni hela basi chukueni hela yenu". Ngeleja kavunja mwiko.

Wale wa EPA wao walibembelezwa hadi tume ikaundwa ili warudishe fedha na hatujui nani alirudisha nini kwani wengine waligoma kabisa kurudisha fedha hizo (KAGODA hao) na hadi leo tumewakubalia kuwa kilichoenda kwa mganga ndio hicho tena! Sijui hata wale ambao walikuwa wanaamriwa na mahakama kurudisha fedha (restitution) kama wanarudisha hata asilimia 50 ya kilichodaiwa kwao au wengi wanakimbilia kujitangaza kufilisika.

Kuna uwezekano mkubwa wengi waliopokea fedha za escrow wamezila na kunawa mikono kabisa. Ni sawasawa na watu waliokuta akaunti zao zimejazwa mamilioni na walijua siyo zao wakaenda kuzitumia wakidhani walikuwa wameteremshiwa mana na kwale jangwani! Mwisho benki inaenda kuwashtaki wanashangaa - "ooh nilidhani nimebarikiwa sana".

Alichofanya Ngeleja kimechelewa bila ya shaka. Hakuna shaka kuona kuwa Ngeleja kwa kukubali kuchukua fedha hizo wakati huo kwa mtindo aliofanya nao unamfanya aonekane alikuwa anahusika moja kwa moja au kwa kiasi na racketeering ya fedha hizo. Ni wazi pia kurudisha kwake fedha hakuna maana hapaswi kusogelewa na mikono ya sheria. Hii itakuwa ni kuchezea sheria kwani tangu wakati fedha amechukua hadi leo anaweza kuwa ameenda kuzitumia kazalisha fedha nyingine nyingine na anachorudisha ni kile ambacho anadaiwa tu. Ni sawasawa na mtu aibiwe ng'ombe jike halafu baada ya mwaka mmoja aende kwa mwizi wake na kukuta ng'ombea ana ndama mapacha. Je, arudishiwe ng'ombe jike yule tu au na wale mapacha?

Hili linatuleta kwenye hoja ya laumu (culpability). Kwamba, ni kwa kiasi gani Ngeleja na wengine waliopokea fedha hizo wanahusika katika kubeba lawama ya kuwa sehemu ya organized crime hii? Je, laumu hii inaweza kuwa katika ngazi ngapi? Naomba kupendekeza ifuatavyo na ninaamini uchunguzi unaoendelea na mashtaka yanayoenda kuletwa dhidi ya wahusika mbalimbali utazingatia kitu kama hiki.

1. Wahusika wakuu - Wahusika wakuu wa kashfa ya escrow watakuwa ni wale ambao moja kwa moja na kwa pamoja walishirikiana kula njama ya kuchota fedha za escrow. Kwa sasa hawa wametajwa wawili lakini kuna uwezekano wa watu wa nyongeza. Seith na Ruge watakuwa kwenye kiti cha juu kabisa.

2. Wahusika Watumishi wa Umma - Hawa namaanisha wale maofisa wa serikali ambao wakijua kuwa wanashirikiana na wahusika wakuu walichukua maamuzi ya kufanikisha njama hiyo. Kama hawa walipokea fedha kiasi chochote kile hawa watakuwa sehemu ya wale ambao wameshirikiana njama ya kufisadi akaunti hiyo.

3. Wanasiasa na wananchi wenye ushawishi (influential persons) - Kuna kundi hapa la wanasiasa na watu wengine ambao kutokana na nafasi zao katika jamii waliaminiwa kuwa wana ushawishi wa aina fulani katika jamii. Hawa wanaweza wakawa wamepewa fedha bila kuambiwa ni za nini hasa au waliambiwa tu kuwa "shukrani" au "zawadi". Kundi hili lina watu wengi sana na ninaamini ni kundi ambalo Ngeleja alikuwa ni mmoja wao; lakini pia Ngeleja anaweza kuwa sehemu ya kundi la pili.

Sasa Ngeleja kwa kuangalia katika kundi la pili au kundi la tatu bado alichokifanya kinampa ahueni fulani fulani katika uchunguzi wowote ule. Anaweza kupewa adhabu ndogo kutokana na uthubutu wake wa kurudisha fedha na anaweza asipate adhabu yeyote kubwa hasa kama atakubali kuwa shahidi wa upande wa mashtaka na kutoa ushahidi mkubwa. Hili la pili ndio naamini litaamua sana jinsi gani serikali itaamua kumwadhibu Ngeleja. Na mwendesha mashtaka yeyote makini ataweza kupima faida au hasara ya hiyo.

Ngeleja ataulizwa:
- Kwanini ulifungua akaunti Mkombozi Benki
- Nani alikuambia ufungue
- Alikuahidi nini
- Mawasiliano gani ulikuwa nayo
- Nani wengine walihusishwa n.k

Majibu atakayoyatoa kwa maswali hayo na yanayoendana na hayo na ukweli wa majibu hayo utaamua kwa kiasi kikubwa atatendewa vipi na vyombo vya usimamizi wa sheria (law enforcement agencies).

Vyovyote vile ilivyo, hakuna shaka alichofanya Ngeleja kama kingefanywa na watu wote ambao wamepokea fedha za uhalifu au ambao wametajwa katika kashfa mbalimbali nina uhakika kiasi kikubwa cha fedha za umma kingerejeshwa mikononi mwa umma lakini vile vile kingefanya watu wafikirie mara mbili mbili wanapoona fedha zinaingia tu kwenye akaunti zao.

Mtazamo wangu ni kuwa wote waliopokea fedha hizi popote pale walipo wafikirie mara mbili kama bado wanataka kung'ang'ania kuwa 'ni zawadi' au wanataka kuziruka na kurudisha ili angalau.. kama nilivyosema "labda, tena labda" wanaweza wakaangaliwa kwa jicho la pili... lakini wale wagumu, wanaofikiria kuwa hizi ni zama zile za yule, siku si nyingi watapigishwa magoti na wataomba wakati huo warudishe na watakataliwa. Kwani hata neema ina wakati wake.

Ngeleja kasoma nyakati, kaamua kuwahi! Kati ya aliyerudisha na wale ambao wamekaza shingo zao wakiombea kuwa hawataguswa nampa pongezi huyu...

Huyu ni mmoja, wengine?

MMM
Maccm bwana hivi mtaacha lini uzuzu...watu tumeibiwa bil. 320, halaf mnashangilia kurecover mil.40 kweli? na hapa kesho mtaandamana kumpongeza Mwenyekiti wenu na Amiri jeshi Mkuu mpiga pushapu na mtunisha kifua mjini aliyeishindwa Kibiti, ujuha ulioje!
 
Kapewa special assignment huyu ya kumsafisha huyu mwizi na fisadi.

Hapa chini alipewa special assignment ya kumchafua Prof Assad Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali lakini akakutana na formidable defence ya CAG humu naona akaambiwa aachane nayo. Sasa jiulize Mkuu kati ya huyu fisadi na mwizi Ngeleja na Prof Assad ni yupi anastahili kujiuzulu na yupi anayestahili kubaki kwenye wadhifa wake.

Prof. Assad (CAG) Yampasa Kujiuzulu au Kujieleza

Unampongeza Ngereja??? ...

Kweli unafiki ni sehemu ya ilani ya CCM...

Nauliza tu, ni za umma au RUGE???
 
Maccm bwana hivi mtaacha lini uzuzu...watu tumeibiwa bil. 320, halaf mnashangilia kurecover mil.40 kweli? na hapa kesho mtaandamana kumpongeza Mwenyekiti wenu na Amiri jeshi Mkuu mpiga pushapu na mtunisha kifua mjini aliyeishindwa Kibiti, ujuha ulioje!
Unaendekeza sana "uccM" wewe; sasa ccm inahusiana nini na hoja yangu?
 
Kapewa special assignment huyu ya kumsafisha huyu mwizi na fisadi.

Hapa chini alipewa special assignment ya kumchafua Prof Assad Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali lakini akakutana na formidable defence ya CAG humu naona akaambiwa aachane nayo. Sasa jiulize Mkuu kati ya huyu fisadi na mwizi Ngeleja na Prof Assad ni yupi anastahili kujiuzulu na yupi anayestahili kubaki kwenye wadhifa wake.

Prof. Assad (CAG) Yampasa Kujiuzulu au Kujieleza

Ukitafuta mada tafuta zote; ni peke yake niliyewahi kutaka ajiuzulu? fuatilia theme zangu utaelewa...
 
Huyu mwizi anatuchezea shere. hela aliyopeleka TRA dio ilikotoka? kama ya wizi au inauchafu si angeipeleka polisi kama kizibiti?
 
Huyu ni mchapa kazi barabarani kosa lake ni kuandika kuhusu ufisadi wa Magufuli kuhusu ukwapuzi wa nyumba za Serikali, ununuzi wa kivuko hewa na upotevu wa zaidi ya 200 bilioni za ujenzi.

Ukitafuta mada tafuta zote; ni peke yake niliyewahi kutaka ajiuzulu? fuatilia theme zangu utaelewa...
 
Watarudisha tu inshaallah, ila ufisadi ni imani, inawezekana hata sisi ni mafisadi kiimani sema tu hatujapata mwanya wa kufisidi, kwa hiyo tunachopambana nacho ni kwa nini afaidi fulani na si mimi. Ikiwa ndivyo, nasi ni mafisadi Tarajali Inshaallah.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
Love this!
 
Huyu ni mchapa kazi barabarani kosa lake ni kuandika kuhusu ufisadi wa Magufuli kuhusu ukwapuzi wa nyumba za Serikali, ununuzi wa kivuko hewa na upotevu wa zaidi ya 200 bilioni za ujenzi.
Ulisoma niliandika kwanini ajiuluzu; au umekuwa kama wengine wanaofikiria nimesema nini kwa kusoma kichwa cha habari tu?
 
Watarudisha tu inshaallah, ila ufisadi ni imani, inawezekana hata sisi ni mafisadi kiimani sema tu hatujapata mwanya wa kufisidi, kwa hiyo tunachopambana nacho ni kwa nini afaidi fulani na si mimi. Ikiwa ndivyo, nasi ni mafisadi Tarajali Inshaallah.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno

Umesema ukweli mwingi sana.

Hata mtu ukiwa kazini na ndani ya muda wako wa kazi ukaanza kuingia JF na kuanza kuchangia mada na kupiga soga, nao ni ufisadi tu.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tangu mapambano dhidi ya ufisadi yaanze hadi leo hii, hakuna kitendo ambacho tunaweza kukisema kimefanyika, kufanyika, au kufanywa na mtu yeyote aliyetajwa kuhusika au kuhusishwa na ufisadi ambacho kimetupa matumaini kama kilichofanywa na Ngeleja leo. Na hapo sijaweka chumvi bado.

Tulikuwa na mtuhumiwa mmoja wa ufisadi mambo yalipokuwa ya moto aliamua kutorokea Marekani hadi mauti kumkuta huko. Mwingine kelele za ufisadi zilipozidi sana yeye aliamua kujivua nafasi zote za uongozi wa chama chake na kuamua kuendelea na biashara zake. Wengine wawili waligangamana hadi kufikishwa mahakamani na kesi ikaenda kwa miaka wee hadi nusura tukasahau; mwisho wa siku wakapewa jukumu la kusafisha bustani huku wakiimbiwa na kwaya ya matarumbeta (hii chumvi sasa). Mmoja yeye aliitwa kila majina ya ufisadi lakini akagangamala hadi kutaka kugombea Urais hadi jina lake likakatwa lakini hakukata tamaa akarukie meli nyingine kujaribu nia hiyo hiyo. Wengine wengi waliamua kufa na tai zao shingoni. Hakuna kati yao aliyekuwa hata na uthubutu wa kusema "mmh hii kashfa sina cha kujificha kama ni hela basi chukueni hela yenu". Ngeleja kavunja mwiko.

Wale wa EPA wao walibembelezwa hadi tume ikaundwa ili warudishe fedha na hatujui nani alirudisha nini kwani wengine waligoma kabisa kurudisha fedha hizo (KAGODA hao) na hadi leo tumewakubalia kuwa kilichoenda kwa mganga ndio hicho tena! Sijui hata wale ambao walikuwa wanaamriwa na mahakama kurudisha fedha (restitution) kama wanarudisha hata asilimia 50 ya kilichodaiwa kwao au wengi wanakimbilia kujitangaza kufilisika.

Kuna uwezekano mkubwa wengi waliopokea fedha za escrow wamezila na kunawa mikono kabisa. Ni sawasawa na watu waliokuta akaunti zao zimejazwa mamilioni na walijua siyo zao wakaenda kuzitumia wakidhani walikuwa wameteremshiwa mana na kwale jangwani! Mwisho benki inaenda kuwashtaki wanashangaa - "ooh nilidhani nimebarikiwa sana".

Alichofanya Ngeleja kimechelewa bila ya shaka. Hakuna shaka kuona kuwa Ngeleja kwa kukubali kuchukua fedha hizo wakati huo kwa mtindo aliofanya nao unamfanya aonekane alikuwa anahusika moja kwa moja au kwa kiasi na racketeering ya fedha hizo. Ni wazi pia kurudisha kwake fedha hakuna maana hapaswi kusogelewa na mikono ya sheria. Hii itakuwa ni kuchezea sheria kwani tangu wakati fedha amechukua hadi leo anaweza kuwa ameenda kuzitumia kazalisha fedha nyingine nyingine na anachorudisha ni kile ambacho anadaiwa tu. Ni sawasawa na mtu aibiwe ng'ombe jike halafu baada ya mwaka mmoja aende kwa mwizi wake na kukuta ng'ombea ana ndama mapacha. Je, arudishiwe ng'ombe jike yule tu au na wale mapacha?

Hili linatuleta kwenye hoja ya laumu (culpability). Kwamba, ni kwa kiasi gani Ngeleja na wengine waliopokea fedha hizo wanahusika katika kubeba lawama ya kuwa sehemu ya organized crime hii? Je, laumu hii inaweza kuwa katika ngazi ngapi? Naomba kupendekeza ifuatavyo na ninaamini uchunguzi unaoendelea na mashtaka yanayoenda kuletwa dhidi ya wahusika mbalimbali utazingatia kitu kama hiki.

1. Wahusika wakuu - Wahusika wakuu wa kashfa ya escrow watakuwa ni wale ambao moja kwa moja na kwa pamoja walishirikiana kula njama ya kuchota fedha za escrow. Kwa sasa hawa wametajwa wawili lakini kuna uwezekano wa watu wa nyongeza. Seith na Ruge watakuwa kwenye kiti cha juu kabisa.

2. Wahusika Watumishi wa Umma - Hawa namaanisha wale maofisa wa serikali ambao wakijua kuwa wanashirikiana na wahusika wakuu walichukua maamuzi ya kufanikisha njama hiyo. Kama hawa walipokea fedha kiasi chochote kile hawa watakuwa sehemu ya wale ambao wameshirikiana njama ya kufisadi akaunti hiyo.

3. Wanasiasa na wananchi wenye ushawishi (influential persons) - Kuna kundi hapa la wanasiasa na watu wengine ambao kutokana na nafasi zao katika jamii waliaminiwa kuwa wana ushawishi wa aina fulani katika jamii. Hawa wanaweza wakawa wamepewa fedha bila kuambiwa ni za nini hasa au waliambiwa tu kuwa "shukrani" au "zawadi". Kundi hili lina watu wengi sana na ninaamini ni kundi ambalo Ngeleja alikuwa ni mmoja wao; lakini pia Ngeleja anaweza kuwa sehemu ya kundi la pili.

Sasa Ngeleja kwa kuangalia katika kundi la pili au kundi la tatu bado alichokifanya kinampa ahueni fulani fulani katika uchunguzi wowote ule. Anaweza kupewa adhabu ndogo kutokana na uthubutu wake wa kurudisha fedha na anaweza asipate adhabu yeyote kubwa hasa kama atakubali kuwa shahidi wa upande wa mashtaka na kutoa ushahidi mkubwa. Hili la pili ndio naamini litaamua sana jinsi gani serikali itaamua kumwadhibu Ngeleja. Na mwendesha mashtaka yeyote makini ataweza kupima faida au hasara ya hiyo.

Ngeleja ataulizwa:
- Kwanini ulifungua akaunti Mkombozi Benki
- Nani alikuambia ufungue
- Alikuahidi nini
- Mawasiliano gani ulikuwa nayo
- Nani wengine walihusishwa n.k

Majibu atakayoyatoa kwa maswali hayo na yanayoendana na hayo na ukweli wa majibu hayo utaamua kwa kiasi kikubwa atatendewa vipi na vyombo vya usimamizi wa sheria (law enforcement agencies).

Vyovyote vile ilivyo, hakuna shaka alichofanya Ngeleja kama kingefanywa na watu wote ambao wamepokea fedha za uhalifu au ambao wametajwa katika kashfa mbalimbali nina uhakika kiasi kikubwa cha fedha za umma kingerejeshwa mikononi mwa umma lakini vile vile kingefanya watu wafikirie mara mbili mbili wanapoona fedha zinaingia tu kwenye akaunti zao.

Mtazamo wangu ni kuwa wote waliopokea fedha hizi popote pale walipo wafikirie mara mbili kama bado wanataka kung'ang'ania kuwa 'ni zawadi' au wanataka kuziruka na kurudisha ili angalau.. kama nilivyosema "labda, tena labda" wanaweza wakaangaliwa kwa jicho la pili... lakini wale wagumu, wanaofikiria kuwa hizi ni zama zile za yule, siku si nyingi watapigishwa magoti na wataomba wakati huo warudishe na watakataliwa. Kwani hata neema ina wakati wake.

Ngeleja kasoma nyakati, kaamua kuwahi! Kati ya aliyerudisha na wale ambao wamekaza shingo zao wakiombea kuwa hawataguswa nampa pongezi huyu...

Huyu ni mmoja, wengine?

MMM
Akili yako ndipo ilipofikia.

Suluhu ya hawa waizi ndiyo umetoa hitimisho lao kama ulivyozoeshwa na akili yako ikareflect hukohuko.

Idiot
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakuna sababu yoyote ile ya CAG kujiuzulu ni upikwaji wa zengwe tu ili kumchafua huyu ikiwa ni special assignment yako kama hii ya kumsafisha huyu mwizi na fisadi Ngeleja eti kwa kurudisha pesa ya wizi aliyodai "inamsononesha" sijui ni lini hii pesa aliyokaa nayo kwa miezi 19 ilipoanza kumsononesha ni baso anatakiwa arudishe made riba ambayo pesa hii ingeingiza kama ingewekwa bank kwa miezi 19.

TRA ukiwa na deni wanacharge na riba ukichelewa kulipa na huyu alipe na riba husika.

Ulisoma niliandika kwanini ajiuluzu; au umekuwa kama wengine wanaofikiria nimesema nini kwa kusoma kichwa cha habari tu?
 
Only in tz Mwz anarudisha Mali aliyoipata kimagumashi na inaonekana sawa tu

OvA

Mkuu hata mimi nashangaa sana, yaani watu bila aibu wanataka kumsafisha/pigia debe/takasa Ngeleja as if hajafanya kosa!! Yeye kama former Waziri/kiongozi hapaswi kupokea zawadi of anyshape or form kutoka kwa mfanya biashara ambaye anauzia umeme Wizara aliyo kuwa anaiongoza Ngeleja, kimaadili hilo ni kosa - hatujui Rugemalira na Seth watasema nini kuhusu sakata zima la ESCROW, binafsi naona ni mapema mno kwa watu kujaribu kujisafisha at the eleventh hour - binafsi sikuona mantiki ya Mweshimiwa kujaribu ku pre-empty anything.
 
Nchi ina mambo Ya ajabu sana!

Ova
 
Hili swali linaulizwa saaana! Sijui kwanini hamlijibu.

Fedha alipewa zawadi na Rugemalila, naye alitetea kwa nguvu zake zote kuwa zilikuwa safi, kama anaona hazina usafi kaambiwa na nani kuwa hizo fedha ni serikali?
Kwanini hakumrudishia aliyempa ili apambane na kidhibiti chake?

Akamatwaye na ngozi ndiye alokula nyama!

Hata sheria ya ushahidi itaweza kumletea utata kwakuwa yeye alikuwa waziri mwenye dhamana wizara ya madini na nishati, ni wazi kuwa baraka za waziri kwenye ruhusa ya kutoa zile hela ilihusika.

Ni mjinga pekee ataamini kuwa ile hela haikuwa kifuta jasho cha uidhinishaji wa malipo yasiyostahili. Ile ni rushwa, ni wizi, ni njama ya kuiba, ni kushiriki wizi.

Sasa mnaanza kulisifia jizi lakini wapuliza filimbi ya kuwagutusheni kuwa mnaibiwa wametupwa nje ya bunge nanyi hamuandiki article za kuufahamisha kama sio kuukumbusha umma kwa habari ya ushujaa na uzalendo wao uliotukuka.
whether zimewekwa serikali au kwa aliyetoa, mwisho wa siku baada ya kesi husika kwisha zitakwenda kwa muhusi.
Rejea kauli ya Raisi hivi karibuni kwamba waliokula fedha za umma, zitawatoka, juhudi ya kwanza ya serikali makini ni kupunguza impact ya loss,kwa kurudisha hizo mali serikalini/kwa wananchi.
Infact mali zote zenye tuhuma, kwa sasa zinatakiwa kuwekwa kwenye trust na kuendeleza hizo biashara nk , mpaka pale kesi kuu zitakapo isha na mwenye mali kuzichukua.kupewa kilicho chake na faida kama ipo, iwe ni serikali au mtuhumiwa.
 
Tumwamini Rais yupi?

Kikwete, specifically hela za escrow sio za serikali.

Ina maana Magufuli kataarifiwa kuwa ni za umma?

Je taarifa hiyo imo kwenye report ya Mruma au Osoro?
 
Mkuu;
Nadhani miongoni mwa wale ma GT weye nawe umo. Sasa nauliza; Kama Ngeleja hakujichotea humo yeye mwenyewe, ili aisaidie sheria alikuwa arudishe wapi hiyo hela?? Kwa haki kamili, na kutusaidia kumpata ushahidi JR, nadhani Ngeleja alitakiwa azirudishe kwa aliyempa mgawo wala sio serekalini. Kwani JR alikuwa amemwomba azipeleke serekalini?? Tuseme, kwa mfano, wote waliogawiwa na JR wakizirudisha, naye JR akazirudisha zilizobaki. Mtamsamehe JR?
Jamani, tusijifanye wehu. Ngeleja arudishe ile fedha ya aibu aliyopewa na JR. Hiyo aliyopeleka TRA ni malipo ya miamala yake mingine aliyokuwa anadaiwa na TRA asiseme ati ni zile za JR. Barua ikimkosa mwenyewe hurudishwa kwa mtumaji sio kwa posta. Ngeleja hujatenda haki. Umemdhulumu JR aliyekufadhili. Mrudishie hela yake uliyoigundua ni ya aibu, kama kweli una moyo safi.
Mkuu hawa ni mafisadi tu, ila kitendo hiki kinawapa wakati mgumu wote waliopokea mgao. Pia kurudisha serikalini ni sawa maana ukinunua mfano gari ukangudua ni la wizi huwezi kulirudisha kwa mwenyewe inabidi ulisalimishe polisi ili alokuuzia akamatwe. Ila hii picha ni ya hatari nadhani hata kwa maisha yake maana kuna wale walikula 1.6bn.
 
Upuuzi wa masudi, alipaswa arudishe kwa James sio serikalini maana hizo hazikua pesa za serikali(uma by Jakaya) au huko serikalini nako waligawana mgao wao hivyo amerudisha zile walizogawana serikalini ila za James bado anazo?
Mkuu ukiwa nje ya tanuru la moto utakuwa unasimulia tu, walio ndani hujui kwa sasa wanaungua vipi. Huyu katapatapa ila kapata angalau kutoa kichwa nje apumue kidogo. Mpaka sasa hatujui Magu atatoa tamko gani. Ila najua litakuwa ni moto mkali kwa waliogawiwa hizo pesa.
 
Back
Top Bottom