Hongera Ngeleja; Hiyo ni Moja...

Hongera Ngeleja; Hiyo ni Moja...

Mkuu;
Nadhani miongoni mwa wale ma GT weye nawe umo. Sasa nauliza; Kama Ngeleja hakujichotea humo yeye mwenyewe, ili aisaidie sheria alikuwa arudishe wapi hiyo hela?? Kwa haki kamili, na kutusaidia kumpata ushahidi JR, nadhani Ngeleja alitakiwa azirudishe kwa aliyempa mgawo wala sio serekalini. Kwani JR alikuwa amemwomba azipeleke serekalini?? Tuseme, kwa mfano, wote waliogawiwa na JR wakizirudisha, naye JR akazirudisha zilizobaki. Mtamsamehe JR?
Jamani, tusijifanye wehu. Ngeleja arudishe ile fedha ya aibu aliyopewa na JR. Hiyo aliyopeleka TRA ni malipo ya miamala yake mingine aliyokuwa anadaiwa na TRA asiseme ati ni zile za JR. Barua ikimkosa mwenyewe hurudishwa kwa mtumaji sio kwa posta. Ngeleja hujatenda haki. Umemdhulumu JR aliyekufadhili. Mrudishie hela yake uliyoigundua ni ya aibu, kama kweli una moyo safi.
 
unaposema hivyo ujiulize nani alisema si za umma. Msiendekeze siasa kiasi cha kujitoa ufahamu. Aliyesema si za umma anajulikana na inajulikana kwanini alisema. Leo hii mnataka kuamini kuwa alisema kweli kwa hiyo mnaanza kuzittetea kuwa zilikuwa kweli za umma?
Rais hakusema kweli ndio unamaanisha?
 
Unampongeza mtu aliyetakiwa sasa hivi kuwa na pingu mkononi?

Kwa nini asimrudishie pesa yule aliyempa?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Na. M. M. Mwanakijiji

Tangu mapambano dhidi ya ufisadi yaanze hadi leo hii, hakuna kitendo ambacho tunaweza kukisema kimefanyika, kufanyika, au kufanywa na mtu yeyote aliyetajwa kuhusika au kuhusishwa na ufisadi ambacho kimetupa matumaini kama kilichofanywa na Ngeleja leo. Na hapo sijaweka chumvi bado.

Tulikuwa na mtuhumiwa mmoja wa ufisadi mambo yalipokuwa ya moto aliamua kutorokea Marekani hadi mauti kumkuta huko. Mwingine kelele za ufisadi zilipozidi sana yeye aliamua kujivua nafasi zote za uongozi wa chama chake na kuamua kuendelea na biashara zake. Wengine wawili waligangamana hadi kufikishwa mahakamani na kesi ikaenda kwa miaka wee hadi nusura tukasahau; mwisho wa siku wakapewa jukumu la kusafisha bustani huku wakiimbiwa na kwaya ya matarumbeta (hii chumvi sasa). Mmoja yeye aliitwa kila majina ya ufisadi lakini akagangamala hadi kutaka kugombea Urais hadi jina lake likakatwa lakini hakukata tamaa akarukie meli nyingine kujaribu nia hiyo hiyo. Wengine wengi waliamua kufa na tai zao shingoni. Hakuna kati yao aliyekuwa hata na uthubutu wa kusema "mmh hii kashfa sina cha kujificha kama ni hela basi chukueni hela yenu". Ngeleja kavunja mwiko.

Wale wa EPA wao walibembelezwa hadi tume ikaundwa ili warudishe fedha na hatujui nani alirudisha nini kwani wengine waligoma kabisa kurudisha fedha hizo (KAGODA hao) na hadi leo tumewakubalia kuwa kilichoenda kwa mganga ndio hicho tena! Sijui hata wale ambao walikuwa wanaamriwa na mahakama kurudisha fedha (restitution) kama wanarudisha hata asilimia 50 ya kilichodaiwa kwao au wengi wanakimbilia kujitangaza kufilisika.

Kuna uwezekano mkubwa wengi waliopokea fedha za escrow wamezila na kunawa mikono kabisa. Ni sawasawa na watu waliokuta akaunti zao zimejazwa mamilioni na walijua siyo zao wakaenda kuzitumia wakidhani walikuwa wameteremshiwa mana na kwale jangwani! Mwisho benki inaenda kuwashtaki wanashangaa - "ooh nilidhani nimebarikiwa sana".

Alichofanya Ngeleja kimechelewa bila ya shaka. Hakuna shaka kuona kuwa Ngeleja kwa kukubali kuchukua fedha hizo wakati huo kwa mtindo aliofanya nao unamfanya aonekane alikuwa anahusika moja kwa moja au kwa kiasi na racketeering ya fedha hizo. Ni wazi pia kurudisha kwake fedha hakuna maana hapaswi kusogelewa na mikono ya sheria. Hii itakuwa ni kuchezea sheria kwani tangu wakati fedha amechukua hadi leo anaweza kuwa ameenda kuzitumia kazalisha fedha nyingine nyingine na anachorudisha ni kile ambacho anadaiwa tu. Ni sawasawa na mtu aibiwe ng'ombe jike halafu baada ya mwaka mmoja aende kwa mwizi wake na kukuta ng'ombea ana ndama mapacha. Je, arudishiwe ng'ombe jike yule tu au na wale mapacha?

Hili linatuleta kwenye hoja ya laumu (culpability). Kwamba, ni kwa kiasi gani Ngeleja na wengine waliopokea fedha hizo wanahusika katika kubeba lawama ya kuwa sehemu ya organized crime hii? Je, laumu hii inaweza kuwa katika ngazi ngapi? Naomba kupendekeza ifuatavyo na ninaamini uchunguzi unaoendelea na mashtaka yanayoenda kuletwa dhidi ya wahusika mbalimbali utazingatia kitu kama hiki.

1. Wahusika wakuu - Wahusika wakuu wa kashfa ya escrow watakuwa ni wale ambao moja kwa moja na kwa pamoja walishirikiana kula njama ya kuchota fedha za escrow. Kwa sasa hawa wametajwa wawili lakini kuna uwezekano wa watu wa nyongeza. Seith na Ruge watakuwa kwenye kiti cha juu kabisa.

2. Wahusika Watumishi wa Umma - Hawa namaanisha wale maofisa wa serikali ambao wakijua kuwa wanashirikiana na wahusika wakuu walichukua maamuzi ya kufanikisha njama hiyo. Kama hawa walipokea fedha kiasi chochote kile hawa watakuwa sehemu ya wale ambao wameshirikiana njama ya kufisadi akaunti hiyo.

3. Wanasiasa na wananchi wenye ushawishi (influential persons) - Kuna kundi hapa la wanasiasa na watu wengine ambao kutokana na nafasi zao katika jamii waliaminiwa kuwa wana ushawishi wa aina fulani katika jamii. Hawa wanaweza wakawa wamepewa fedha bila kuambiwa ni za nini hasa au waliambiwa tu kuwa "shukrani" au "zawadi". Kundi hili lina watu wengi sana na ninaamini ni kundi ambalo Ngeleja alikuwa ni mmoja wao; lakini pia Ngeleja anaweza kuwa sehemu ya kundi la pili.

Sasa Ngeleja kwa kuangalia katika kundi la pili au kundi la tatu bado alichokifanya kinampa ahueni fulani fulani katika uchunguzi wowote ule. Anaweza kupewa adhabu ndogo kutokana na uthubutu wake wa kurudisha fedha na anaweza asipate adhabu yeyote kubwa hasa kama atakubali kuwa shahidi wa upande wa mashtaka na kutoa ushahidi mkubwa. Hili la pili ndio naamini litaamua sana jinsi gani serikali itaamua kumwadhibu Ngeleja. Na mwendesha mashtaka yeyote makini ataweza kupima faida au hasara ya hiyo.

Ngeleja ataulizwa:
- Kwanini ulifungua akaunti Mkombozi Benki
- Nani alikuambia ufungue
- Alikuahidi nini
- Mawasiliano gani ulikuwa nayo
- Nani wengine walihusishwa n.k

Majibu atakayoyatoa kwa maswali hayo na yanayoendana na hayo na ukweli wa majibu hayo utaamua kwa kiasi kikubwa atatendewa vipi na vyombo vya usimamizi wa sheria (law enforcement agencies).

Vyovyote vile ilivyo, hakuna shaka alichofanya Ngeleja kama kingefanywa na watu wote ambao wamepokea fedha za uhalifu au ambao wametajwa katika kashfa mbalimbali nina uhakika kiasi kikubwa cha fedha za umma kingerejeshwa mikononi mwa umma lakini vile vile kingefanya watu wafikirie mara mbili mbili wanapoona fedha zinaingia tu kwenye akaunti zao.

Mtazamo wangu ni kuwa wote waliopokea fedha hizi popote pale walipo wafikirie mara mbili kama bado wanataka kung'ang'ania kuwa 'ni zawadi' au wanataka kuziruka na kurudisha ili angalau.. kama nilivyosema "labda, tena labda" wanaweza wakaangaliwa kwa jicho la pili... lakini wale wagumu, wanaofikiria kuwa hizi ni zama zile za yule, siku si nyingi watapigishwa magoti na wataomba wakati huo warudishe na watakataliwa. Kwani hata neema ina wakati wake.

Ngeleja kasoma nyakati, kaamua kuwahi! Kati ya aliyerudisha na wale ambao wamekaza shingo zao wakiombea kuwa hawataguswa nampa pongezi huyu...

Huyu ni mmoja, wengine?

MMM
Siwezi kurudisha pesa ya mboga (mama wa makazi) na dharau za nshomile au pesa ya ushauri(mzee wa vijisenti) sijui alishauri nini,aheri ya Ngeleja kaweza anagalau kuonyesha kujutia kwake,hawa wengine muda si mrefu watachuchumaa tu kama walivyochuchumaa Ruge na singa singa wake.Enzi za mimi unanijua zimeenda na mzee wa msoga
 
Si kila safari inaanza na hatua moja; tukiwa makini inatupasa kulilia kwanza wote waliopata hizo bilioni 321 waanze kurudisha. Haba na haba hujaza...
Kwanini tunaingia gharama kubwa ya kuendesha kesi wakati kumbe hakuna kesi na suala ni kurudisha. yaani unaunga mkono Ngeleja kutumia ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kutakatisha fedha, ili tu kuhalalisha mchezo mchafu unaofanywa na CCM kwa gharama ya kuvizia matangazo kwenye kipeperushi chako? Hebu waacheni watanzania wapumzike jamani, wanaumia sana kupitia ujanjaujanja wenu wa kupindisha maneno!
 
Ni ujuha kumpongeza mtu mzima aliyekaa na fedha miaka mitatu huku akiyajua vyema maazimio ya bunge lakini akaweka pamba masikioni mpaka " asome upepo" kwanza!. Yaani Rugemalira na Seth wasingekamatwa, Huyu mtu angeuchuna tu!!!

Hakuna cha kumpongeza, Kwanza inabidi akaisaidie polisi maana na yeye at one time alikuwa waziri wa Nishati na madini, inabidi akaeleze, ilikuwajekuwaje akapokea fedha zile kutoka kwa mtu mwenye kudili na wizara ile!! ambaye kwa fedha hizo ulizokula zina utata!!!. There is no free lunch

Mwalimu alisema, mtu mwenye akili akijua wewe una akili akakueleza kitu cha kipumbavu na ukakikubali, basi atakudharau!!

Kama unakubaliana na move ile ya kisanii na kusifu usanii ule basi ukapimwe akili wewe!!
 
Wanatuona Watanzania ni wapumbavu sana ndio maana wanakuja na hoja nyepesi sana. Kama alipewa kwa ajili ya Maendeleo ya jimbo, amezitoa wapi sasa? Si angeweka wazi miradi ya maendeleo au shughuli yoyote ya kimaendeleo aliofanyia Bungeni na kisha kutoa Maelezo alivyopata, kwanini alichaguliwa yeye ambae aliwahi kuwa waziri anaeisimamia sekta ya nishati ambayo ndiyo iliokumbwa na sakata?
Ngeleja anadhani Watz wajinga ,kila kitu na wakati wake ,huyu Mh aliwahi mfukuzisha askari wa Group 4 alipoambiwa anaweka msururu kwenye ATM alipokuwa akiongea na simu ndani ya ATM,yule askari aliulizwa unanijua mimi,kama hunijui kesho utakuwa huna kazi na kweli kwa roho mbaya Ngeleja akamchomea utambi mlinzi huyo kwa vibosile wa Group 4 ambao waliona isiwe taabu wamtose .
 
Mkuu umechambua vizuri, kwamba kwanini Ngereja alihamua kufungua account Mkombozi bank, nani alimwambia?, kwanini mtoa huo msaada hasimwandikie Cheque pesa zikapelekwa kwenye benki yake ya siku zote?

Hapa Majambazi ya CCM yana kitu cha kujibu
 
Ni hasira alizokuwa nazo kuona wenzake walilipwa milioni zaidi ya mia. Yeye tena aloyefika level ya uwaziri atapewa tumilioni twa mboga!
====
Ama anaanda rescue ya watu katika mambo ya kisheria?
 
Angepewa nyingi hata nusu ya chenge angerudisha?
 
Unampongeza mtu aliyetakiwa sasa hivi kuwa na pingu mkononi? Kwa nini asimrudishie pesa yule aliyempa?
Yaani kurudisha baada ya kufanyia biashara kunapongezwa!

Nina amini kwa dhati,nia njema si kurudisha tu, alipaswa kujutia makosa kwa kujua au kutojua
Kujutia ni kuachia nafasi yake ya ubunge. Kwa sasa ana poor judgement na hana public trust

Ngeleja atasimama wapi kutueleza jambo la kitaifa kwa haya ynayotokea?

Minister hakuwa na judgement ya kuhoji milioni 40 kutoka kwa mtu binafsi hazina 'conflict of interest' the least to say

Waziri hakujua ni kwanini aliambiwa afungue account Mkombozi

Waziri hakujua 'washiriki wa mkombozi' na hiyo haikutosha kuwa red flag kwake

Hata baada ya kelele za miaka mingi, waziri hakuweza kuchunguza suala hilo

Leo Ruge na Seth wametiwa kibano ndipo waziri anapata fahamu, halafu apongezwe! real
 
Shangaa nawe Mkuu jinsi baadhi ya Watanzania walivyokuwa na ZUZU BRAINS. Jamaa alipokea pesa tangu December 2014 anatakiwa pia arudishe riba ambayo pesa hizo zingeingiza kama zingekuwa bank tangu hiyo December 2014 mpaka July 2017. Ni mwizi mwingine huyu na fisadi nyumbani kwake ni lupango tu.

Walivyopokea mlishangilia na kusema sio za umma,sasa mnashangilia na kusema ni za umma.
 
Umeona eeh! Mwanakijiji huyu si yule wa miaka mitano ya nyuma ambaye alijizolea umaarufu mkubwa sana nje na ndani ya Tanzania kwa kusimamia maslahi na sheria za nchi bila kupindisha hata chembe. Huyu wa leo ni boya kabisa na ni watu wawili tofauti kabisa.

Unampongeza mtu aliyetakiwa sasa hivi kuwa na pingu mkononi?

Kwa nini asimrudishie pesa yule aliyempa?
 
PAMBANA NA HALI YAKO. Kwa sasa Makala zimebaki kufungia maandazi, raia wana Swap si kidogo siku hizi. Na hao wanaofungia maandazi ni vile bado hawajajua kuwa ni sumu inayowaua taratibu, siku wakijua basi wateja wako watabaki kuwa wapuliza rangi za magari.

"PAMBANA NA HALI YAKO"
 
Back
Top Bottom