Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,281
- 44,793
Na. M. M. Mwanakijiji
Tangu mapambano dhidi ya ufisadi yaanze hadi leo hii, hakuna kitendo ambacho tunaweza kukisema kimefanyika, kufanyika, au kufanywa na mtu yeyote aliyetajwa kuhusika au kuhusishwa na ufisadi ambacho kimetupa matumaini kama kilichofanywa na Ngeleja leo. Na hapo sijaweka chumvi bado.
Tulikuwa na mtuhumiwa mmoja wa ufisadi mambo yalipokuwa ya moto aliamua kutorokea Marekani hadi mauti kumkuta huko. Mwingine kelele za ufisadi zilipozidi sana yeye aliamua kujivua nafasi zote za uongozi wa chama chake na kuamua kuendelea na biashara zake. Wengine wawili waligangamana hadi kufikishwa mahakamani na kesi ikaenda kwa miaka wee hadi nusura tukasahau; mwisho wa siku wakapewa jukumu la kusafisha bustani huku wakiimbiwa na kwaya ya matarumbeta (hii chumvi sasa). Mmoja yeye aliitwa kila majina ya ufisadi lakini akagangamala hadi kutaka kugombea Urais hadi jina lake likakatwa lakini hakukata tamaa akarukie meli nyingine kujaribu nia hiyo hiyo. Wengine wengi waliamua kufa na tai zao shingoni. Hakuna kati yao aliyekuwa hata na uthubutu wa kusema "mmh hii kashfa sina cha kujificha kama ni hela basi chukueni hela yenu". Ngeleja kavunja mwiko.
Wale wa EPA wao walibembelezwa hadi tume ikaundwa ili warudishe fedha na hatujui nani alirudisha nini kwani wengine waligoma kabisa kurudisha fedha hizo (KAGODA hao) na hadi leo tumewakubalia kuwa kilichoenda kwa mganga ndio hicho tena! Sijui hata wale ambao walikuwa wanaamriwa na mahakama kurudisha fedha (restitution) kama wanarudisha hata asilimia 50 ya kilichodaiwa kwao au wengi wanakimbilia kujitangaza kufilisika.
Kuna uwezekano mkubwa wengi waliopokea fedha za escrow wamezila na kunawa mikono kabisa. Ni sawasawa na watu waliokuta akaunti zao zimejazwa mamilioni na walijua siyo zao wakaenda kuzitumia wakidhani walikuwa wameteremshiwa mana na kwale jangwani! Mwisho benki inaenda kuwashtaki wanashangaa - "ooh nilidhani nimebarikiwa sana".
Alichofanya Ngeleja kimechelewa bila ya shaka. Hakuna shaka kuona kuwa Ngeleja kwa kukubali kuchukua fedha hizo wakati huo kwa mtindo aliofanya nao unamfanya aonekane alikuwa anahusika moja kwa moja au kwa kiasi na racketeering ya fedha hizo. Ni wazi pia kurudisha kwake fedha hakuna maana hapaswi kusogelewa na mikono ya sheria. Hii itakuwa ni kuchezea sheria kwani tangu wakati fedha amechukua hadi leo anaweza kuwa ameenda kuzitumia kazalisha fedha nyingine nyingine na anachorudisha ni kile ambacho anadaiwa tu. Ni sawasawa na mtu aibiwe ng'ombe jike halafu baada ya mwaka mmoja aende kwa mwizi wake na kukuta ng'ombea ana ndama mapacha. Je, arudishiwe ng'ombe jike yule tu au na wale mapacha?
Hili linatuleta kwenye hoja ya laumu (culpability). Kwamba, ni kwa kiasi gani Ngeleja na wengine waliopokea fedha hizo wanahusika katika kubeba lawama ya kuwa sehemu ya organized crime hii? Je, laumu hii inaweza kuwa katika ngazi ngapi? Naomba kupendekeza ifuatavyo na ninaamini uchunguzi unaoendelea na mashtaka yanayoenda kuletwa dhidi ya wahusika mbalimbali utazingatia kitu kama hiki.
1. Wahusika wakuu - Wahusika wakuu wa kashfa ya escrow watakuwa ni wale ambao moja kwa moja na kwa pamoja walishirikiana kula njama ya kuchota fedha za escrow. Kwa sasa hawa wametajwa wawili lakini kuna uwezekano wa watu wa nyongeza. Seith na Ruge watakuwa kwenye kiti cha juu kabisa.
2. Wahusika Watumishi wa Umma - Hawa namaanisha wale maofisa wa serikali ambao wakijua kuwa wanashirikiana na wahusika wakuu walichukua maamuzi ya kufanikisha njama hiyo. Kama hawa walipokea fedha kiasi chochote kile hawa watakuwa sehemu ya wale ambao wameshirikiana njama ya kufisadi akaunti hiyo.
3. Wanasiasa na wananchi wenye ushawishi (influential persons) - Kuna kundi hapa la wanasiasa na watu wengine ambao kutokana na nafasi zao katika jamii waliaminiwa kuwa wana ushawishi wa aina fulani katika jamii. Hawa wanaweza wakawa wamepewa fedha bila kuambiwa ni za nini hasa au waliambiwa tu kuwa "shukrani" au "zawadi". Kundi hili lina watu wengi sana na ninaamini ni kundi ambalo Ngeleja alikuwa ni mmoja wao; lakini pia Ngeleja anaweza kuwa sehemu ya kundi la pili.
Sasa Ngeleja kwa kuangalia katika kundi la pili au kundi la tatu bado alichokifanya kinampa ahueni fulani fulani katika uchunguzi wowote ule. Anaweza kupewa adhabu ndogo kutokana na uthubutu wake wa kurudisha fedha na anaweza asipate adhabu yeyote kubwa hasa kama atakubali kuwa shahidi wa upande wa mashtaka na kutoa ushahidi mkubwa. Hili la pili ndio naamini litaamua sana jinsi gani serikali itaamua kumwadhibu Ngeleja. Na mwendesha mashtaka yeyote makini ataweza kupima faida au hasara ya hiyo.
Ngeleja ataulizwa:
- Kwanini ulifungua akaunti Mkombozi Benki
- Nani alikuambia ufungue
- Alikuahidi nini
- Mawasiliano gani ulikuwa nayo
- Nani wengine walihusishwa n.k
Majibu atakayoyatoa kwa maswali hayo na yanayoendana na hayo na ukweli wa majibu hayo utaamua kwa kiasi kikubwa atatendewa vipi na vyombo vya usimamizi wa sheria (law enforcement agencies).
Vyovyote vile ilivyo, hakuna shaka alichofanya Ngeleja kama kingefanywa na watu wote ambao wamepokea fedha za uhalifu au ambao wametajwa katika kashfa mbalimbali nina uhakika kiasi kikubwa cha fedha za umma kingerejeshwa mikononi mwa umma lakini vile vile kingefanya watu wafikirie mara mbili mbili wanapoona fedha zinaingia tu kwenye akaunti zao.
Mtazamo wangu ni kuwa wote waliopokea fedha hizi popote pale walipo wafikirie mara mbili kama bado wanataka kung'ang'ania kuwa 'ni zawadi' au wanataka kuziruka na kurudisha ili angalau.. kama nilivyosema "labda, tena labda" wanaweza wakaangaliwa kwa jicho la pili... lakini wale wagumu, wanaofikiria kuwa hizi ni zama zile za yule, siku si nyingi watapigishwa magoti na wataomba wakati huo warudishe na watakataliwa. Kwani hata neema ina wakati wake.
Ngeleja kasoma nyakati, kaamua kuwahi! Kati ya aliyerudisha na wale ambao wamekaza shingo zao wakiombea kuwa hawataguswa nampa pongezi huyu...
Huyu ni mmoja, wengine?
MMM