uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. The Watchman

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 ACT Wazalendo: Tunaenda kwenye uchaguzi tukiwa hatuna matumaini makubwa ya haki na msingi ya demokrasia kuzingatiwa

    Akizungumza katika uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025-2026 uliofanywa na ACT Wazalendo, Mwenyekiti wa chama hicho Dorothy Semu amesema, "Kwa mwaka mwengine tena tunaenda kwenye uchaguzi tukiwa hatuna matumaini makubwa ya haki na msingi ya demokrasia kuzingatiwa. Tumeamua kuingia kwenye...
  2. E

    JamiiForums Tanzania Kikwete atetea marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani

    Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametetea marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 akihoji, "Hivi ni kweli kwamba, sheria zetu zinazohusu uchaguzi ni mbaya sana kiasi kwamba haziwezi kusimamia mchakato wa uchaguzi mwaka huu?" Ameyasema hayo leo Juni 21 katika...
  3. M

    JamiiForums Tanzania Picha: Mmoja wa mabalozi wa shina wa CCM akiwa na V 8 alilopewa kwa ajili ya uchaguzi

    Wazee wa Mavi eite 👇
  4. The Humble Dreamer

    JamiiForums Tanzania Special Thread: Yanayojiri Uchaguzi TFF 2025

    Salaam Members: June mwaka huu TFF walitoa tangazo la kuwepo kwa uchaguzi kwa nafasi ya Urais na nafasi za Wajumbe 6 wa kamati ya utendaji. Hapa utazipata updates za hatua zote za awali hadi uchaguzi mkuu utakaofanyika Tanga tarehe 16/08/2025. Pia kama una updates zozote unaweza share nasi...
  5. kavulata

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi TFF, usichukue fomu ya kugombea kabla ya kuwa na waungaji mkono, rushwa.

    Uchaguzi wa TFF una viashiria vya rushwa kwenye upande wa kupata endorsements kutoka kwa wajumbe. Mwenye fedha nyingi anaweza kununua endorsements zote na wengine kukosa hata moja. Uchaguzi umeharibika kabla haujafanyika. Ili mtu kugombea nafasi ya TFF mashariti ni kulipa TZS 500,000 na kupata...
  6. X_INTELLIGENCE

    JamiiForums Tanzania Yatakayotokea Tanzania kabla na baada ya Uchaguzi

    Awali ya yote niwapongeze watanzania kwa busara na uvumilivu wa hali ya juu tulio nao...juzi nilikutana na wazee fulani huko porini wazee hao miongoni mwao waliwahi KUFA kabla mission zao hazijatimia na wengine walitimiza huku wengine wakiwa wametimiza nusu ya mission iliyo waleta duniani...
  7. B

    JamiiForums Tanzania 🇹🇿Je, Tanzania inaweza kufungiwa na FIFA kutokana na sakata la derby (Yanga vs Simba) na uchaguzi wa TFF?

    Habari.... 1. Sakata la Derby Mechi ya watani wa jadi (Yanga na Simba) imekuwa na mvutano mkubwa. Yanga wamepinga maamuzi ya Bodi ya Ligi (TPLB) na TFF, wakidai kuna upendeleo na hujuma. Waligoma kucheza baadhi ya mechi, na waliwasilisha malalamiko yao hadi kwa viongozi wa serikali. Hii...
  8. Genius Man

    JamiiForums Tanzania Bila chama cha upinzani chenye nguvu kushiriki uchaguzi hakuna uchaguzi bali maigizo na udanganyifu

    Bila chama cha upinzani chenye nguvu kushiriki uchaguzi hakuna uchaguzi bali maigizo na udanganyifu ambao haukubariki. Chama cha upinzani kipo sahihi kuhamasisha mazingira ya uwazi na kidemokrasia kwenye uchaguzi ili uchaguzi wetu usiwe wa maigizo na udanganyifu.
  9. N

    JamiiForums Tanzania Hakuna Shamra shamra za uchaguzi mwaka huu hapa mtaani kama miaka mingine kulikoni

    Wakuu nimeshuhudia miaka mingi ya uchaguzi miezi kama hìi kunakuwa na shamra shamra za uchaguzi! Mwaka huu kulikoni au kwa sababu mshindi alishapatikana???
  10. Metronidazole 400mg

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi huu lazima aliyekalia kiti ashinde tu, tena kirahisi sanaa

    Na akishinda tegemeeni hali ya maisha yenu yataendelea kuwa magumu mno, kuanzia hela ya kula na hata matumizi madogo madogo ya kifamilia haitawezekana. Maisha yatazidi kuwa magumu na hali ya uhalifu itashika kasi hapa nchini, watu wa kawaida watauana wao kwa wao Uchumi wa nchi utaendelea kuwa...
  11. G

    JamiiForums Tanzania Ziara ya kanda ya ziwa ametuthibitishia kuwa hakuna uchaguzi huru tena

    Kajitangaza kawa ni mshindi tiyari wa urais, ni yeye anayeamua nani awe au asiwe mbunge, tiyari keshaanza kugawa nafasi zake 10 za ubunge. Je kuna haja tena ya kupoteza mabilioni ya kodi zetu kwenye uchaguzi fake?
  12. DogoWaNjombe

    JamiiForums Tanzania Wakili Msomi Aloyce Komba: Uchaguzi wa TFF hauwezi kuwa huru, kunahitajika reforms

    Wakati zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania [TFF] linaendelea, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Msomi Aloyce Komba anasema kuna namna Kamati ya Uchaguzi inaweza isiwe huru na kuainisha sababu...
  13. Y

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Ushauri binafsi : Mpina agombee tena kwa maslahi ya uchaguzi 2025

    Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. kwenye mada..... Hivi karibuni kumeibuka mjadala mkali juu ya kilichotokea jimboni kisesa ilipokuwapo ziara ya Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi. Watu wengi, pengine ni uelewa mdogo, wanauliza kwanini Mhe, Raisi alimjibu vile...
  14. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Tazama Luhaga Mpina akiondoka Uwanjani, Meatu baada ya mkutano wa Rais Samia

    Mbunge wa jimbo la Kisesa, Mkoani Simiyu, Luhaga Mpina akiondoka uwanja maarufu kama stendi ya Mabasi Meatu, baada yakumalizika kwa mkutano wa Rais Samia na wananchi. Pia, Soma: Rais Samia amchana Mpina: Mbunge wa Kisesa ni kuruka ruka kwamba Kisesa tunakudai, Kisesa iko kama mwanamke aliyesuka...
  15. The Father of All

    JamiiForums Tanzania Kama uchaguzi ujao ungekuwa halali bifu za Samia na wenzake zingesaidia au kuiumiza CCM?

    Tangu aingie madarakani, rais Samia Suluhu Hassan amekuwa na bifu na baadhi ya wanachama wenzake. Alianza na Job Ndugai spika wa zamani wa bunge letu. Baadaye, akafuatia Dk Bashiru Ally akiwakilisha kile kilichokuja kujulikana kama Sukuma gang. Juzi alianza bifu na Josephat Gwajima kidhabu...
  16. C

    JamiiForums Tanzania Tume 'huru' ya Uchaguzi pokeeni simu, niwape makavu!

    Mara kadhaa nimejaribu kuwapigia kwa simu mlizoandika kwenye website yenu. Ila hapokei simu, why? Pokeeni mle za uso
  17. Dogoli kinyamkela

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Utabiri uchaguzi Mkuu 2025

    Ufunuo wa Rohoni (Tazama kwa Macho ya Kiroho): Nilipouliza rohoni, ikaja picha ifuatayo: "Ninaona mti mkubwa wa kijani wenye mizizi nene katikati ya nchi, juu yake kuna mama aliyeshika taa, nyuma yake kuna upepo mkali wa manyunyu ya mvua, lakini taa yake haizimiki. Pembeni, kuna kundi la...
  18. The Burning Spear

    JamiiForums Tanzania Kama kweli haya ni mapokezi halali ya Samia Simiyu CCM inaogopa nini kuicha Tume ya uchaguzi kuwa huru?

    GT Katika mitandoa kunaonekana mafuriko ya watanzania Ngosha na bakima huko Simiyu. Tafasiri ya haraka haraka ni kwamba S100 na CCM Wanakubalika 100%. Kwa Sisi wadaidisi tunaamini huu mkusanyiko ni wa kupangwa na umetumia pesa na nguvu nyingi sana kuihadaa dunia juu ya uungwaji mkono wa sa100...
  19. Idugunde

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Tunapata picha gani Viongozi wa CHADEMA ambayo haitashiriki uchaguzi kukubalika kwa wananchi kuliko vyama ambavyo vitashiriki uchaguzi

    Fanya utafiti kwenye vijiwe vya kila namna kuanzia bodaboda, wauza mkaa, walimu na Watanzania wote. Utasikia wanaropoka bila kumug'unya maneno. Kuwa hii ndio CHADEMA ambayo ipo kwa maslahi ya umma. Kulinda na kutetea maslahi ya umma. CCM ,CHAUMMA na wenzao ni mafisadi na wapo kwa ajiri ya...
  20. mshale21

    JamiiForums Tanzania Oktoba linda kura ni kauli mbiu inayoashiria uchochezi na uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi, waliotoa kauli hii wadhibitiwe haraka

    Ni wazi kabisa ACT wazalendo walisaini maadili ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu 2025 mwezi October kuonesha kuwa walilidhia kanuni hizo, wanajua kanuni hizo ziliwaelekeza kuwaelimisha wafuasi wao kuwa hawataruhusiwa kuwa na simu eneo la uchaguzi wakat uchaguzi ukiendelea, pia wanajua wazi kuwa...
Back
Top Bottom