Wako wapi washabiki wa Kikwete?

Wako wapi washabiki wa Kikwete?

Sisi daima tunaongea ukweli,tumekulia shida.Hivyo tulisema JK ameshindwa watu wakatukana.sasa wameanza kuona kwamba JK alipwaya.Nchi hii watu ni waongo na wanajikomba ili wapate madaraka.Tutasimama katika haki hata Magufuli akikosea tutasema tu! Sasa anatekeleza ilani yetu.Mungu mpe hekima Magufuli aendelee hivihivi kwa faida yetu wanyonge.Amen
 
Nashangaa ccm hii hii ilikuwa inatetea safari za nje wakati wa kikwete, alipoondoka tu madarakani wanamponda. Ccm hii hii ilikuwa inatetea mbio za mwenge sijui mwakani itafutwa nayo?

Ndugu,wanaccm ni sawa na mchwa!Akili yao inaongozwa na aliye mbele,akisema twende kushoto wote hukohuko!sasa Magu tekeleza ilani za upinzani,chapa kazi,twataka maendeleo
 
Akina Sumaye wako sahihi, ukiangalia yaliyofanyika tangu 2005 ni sawa na hakuna, umasikini umerudi kwa kasi ya hali yajuu, uchumi hoi, nchi imefirisika. Zimejengwa barabara lakini ziko chini ya deni. Ni sawa na kujengwa nyumba kwa milioni 20, baada ya ujenzi ukabaki inadaiwa shilingi Milioni 25. Wakati wa Kikwete nchi haiukuwa na Rais, tunaemuita Rais 56% ya maisha yake yote alikuwa nje ya nchi. worse

Haha! Unasema Umaskini ulirudi kwa kasi wakati wa jk, tukumbushe basi uliondoka wakati wa nani hadi ikabidi urudi wakati wa jk!!
 
Jk alikuwa chaguo LA Mungu, mashekhe na maaskofu walithibitisha hilo, kwann msiilaumu CCM au Mpaka badala yake lowassa??

Acheni chuki binafsi kwa huyu mzee mlishamtukana na kumdhalilisha vya kutosha,
No one abusing ukipewa nchi unatakiwa uwe tofauti na wale ambao hawakupata hiyo fursa.
 
Nashangaa ccm hii hii ilikuwa inatetea safari za nje wakati wa kikwete, alipoondoka tu madarakani wanamponda. Ccm hii hii ilikuwa inatetea mbio za mwenge sijui mwakani itafutwa nayo?

Mi pia nashangaa Mgombea Urais wa Chadema 2015 ni mmoja kati ya mafisadi Papa 11 waliotangazwa hadharani na chama hicho kwenye List of shame kwenye viwanja vya Mwembe yanga! We jwa nn hili halikushangazi pia!
 
Wakati wa Kikwete wale wenye kipaji cha kujipendekeza ndio walionekana intelligent, mfano Makonda
 
Magufuli anacheza na akili za watu vema saana.vile vipaumbele vya ukawa ndo anavifanyia kaz.siamin kama atakuwa na kipaumbele cha kununua magar ya kuwasha.
 
Umeshaelezwa kuwa akili ya kuambiwa changanya na yako! Magufuli anawaongoza watanzania wote bila kujali matabaka. Kwahiyo, anaweza kuchukuwa zuri lolote kutoka Chama chochote ili watanzania wote wafaidike. Yeye haongozi wana CCM pekee. Ndiyo maana siku ya kutangazwa mshindi, ACT walimpa Ilani yao ili achukue mazuri yaliyomo!


Kikwazo tu ni chama chake,akifanya mazuri kwa kasi hii mpaka mwisho utashangaa anahujumiwa na wanaccm baada ya miaka 5 hapitishwi!Tuliona sitta alichofanyiwa baada ya kuongoza bunge la 9 kwa uwezo na weledi mkubwa kwa maslahi ya nchi!Akachukiwa na wanaccm,akafanyiwa hujuma akakosa uspika!Ukifanya mambo kwa maslahi ya wananchi huwezi kuwa rafiki wa ccm
 
Ndugu,wanaccm ni sawa na mchwa!Akili yao inaongozwa na aliye mbele,akisema twende kushoto wote hukohuko!sasa Magu tekeleza ilani za upinzani,chapa kazi,twataka maendeleo
Mchwa ni wale waliokula matapishi yao wakamteua Mwizi waliekuwa wakisema anaemkubali Lowassa akapimwe akili halafu wao wenyewe wakaanza kumkampenia anafaa kuwa Rais!. Mlichemka sana mwaka huu, mngejipanga vizuri ilikuwa ?cm inaondoka kwa kuwa tangu 1954 mwaka huu chama kilikuwa dhaifu zaidi kwa migogoro lakin nanyi mkaamua kupokea sehemu ya mgogoro huo! Mbowe kawakosesha penalt ya dakika 90
 
Viongozi wa Tz bana. Sasa kaenda huko halafu kawaambia wamfuate kwake, wakati anajua mradi haujaanza. Angefanya moja wapo.
Ukawa raha tupu. Nchi inaendeshwa kwa ilani ya ukawa. Magu hadi alijiita M4C. Anapenda sana CDM ila jinsi CCM walivy mazuzu hawaoni hilo. VIVA UKAWA.
Yaani unamlaumu waziri mkuu Majaliwa kwa kutetea ilani ya Ukawa? Sasa nimeamini wewe kweli ni nyumbu.
 
Wakati wa Kikwete wale wenye kipaji cha kujipendekeza ndio walionekana intelligent, mfano Makonda
Magufuli kaagiza CV zote za maDC apelekewe sijui ndugu yangu huyu mfunga gidadi za mwana mfalme kama atasalimika.
 
Namlamu sana Lowasa kwa kumsapport Kikwete kuingia Ikulu mwaka 2005, Kikwete ndio kafanya hii nchi kusimama kwa miaka 10 na kuwa under autopilot

fuvu lako limejaa maji tu,na watoto wako wakfata akili zako itakua hasara kwa taifa kufuga viumbe wasio na faida..afadhal ya ngiri wanaleta watalii
 
Hivi UKAWA bado ipo? kike kibabu duni na kingunge sijui vimefia wapi? eti mabadiliko ujing nao kazi kwakweli
 
ustadh Ritz na ustadhat FaizaFoxy Tafadhali msipite kimya kimya ktk threads zinazo Sifia utendaji kazi wa kasi ya ajabu wa mseminari magufuli.wekeni udini pembeni.
 
Last edited by a moderator:
Mchwa ni wale waliokula matapishi yao wakamteua Mwizi waliekuwa wakisema anaemkubali Lowassa akapimwe akili halafu wao wenyewe wakaanza kumkampenia anafaa kuwa Rais!. Mlichemka sana mwaka huu, mngejipanga vizuri ilikuwa ?cm inaondoka kwa kuwa tangu 1954 mwaka huu chama kilikuwa dhaifu zaidi kwa migogoro lakin nanyi mkaamua kupokea sehemu ya mgogoro huo! Mbowe kawakosesha penalt ya dakika 90


sina hakika kama unaijua ccm vizuri,ni kwa nguvu ya pamoja kwa kushirikiana na lowassa ndio maana unaona zanzibar uchaguzi unalazimishwa kurudiwa.Ni mara ya kwanza upinzani kufikisha asilimia 40 kura za urais.Lowassa amechangia mafanikio haya,Magufuli ni karata ya mwisho kwa ccm ndio maana hata yeye ameshtuka anatembelea nyota za upinzani kwa kufanya yale yaliyopigiwa kelele kwa miaka nenda rudi na upinzani lakini mchwa wa ccm wakawa wanapinga tu bila hoja.
Waliotetea safari za Jketi leo wamejivisha koti lingine na kufagilia harakati za Magufuli zenye beat la upinzani.Sasa upinzani utashirikiana na Rais kama ataendelea na msimamo huu.
 
Katika maisha kama hujapata nafasi ya kuona jinsi wenzako wanavyofanya mambo, kama unakosa taarifa, unaweza kudhani uko sahihi kwa sababu akili yako inakuwa imefungwa. Watoto wadogo ambao hawajaanza shule huwa wanadhani dunia nzima ni pale walipo, mfano mtoto anaeishi Shinyanga anadhani dunia nzima ni Shinyanga.

Wako wale waliokuwa mashabiki wa Kikwete, sasa Magufuli ndani ya wiki mbili kamuonesha Kikwete jinsi amabavyo mambo yanavyotakiwa kupelekwa (doing things in different ways), kamuumbua Kikwete. Ndani ya hizi wiki 2 tayari milioni takribani 700 zimeokolewa kutoka kwenye mikono ya wanyan'ganyi (Sherehe za kujipongezana bungeni, sherehe za kupasua matofali kwa vichwa na kuuza sura pale uwanja wa taifa, nk). Wapi akina FaizaFoxy watoe maelezo hapa?

Kwa akili yako bila JK JPM angeenda ikulu? thubutu, this are three smart Men BWM JK and JPM.
 
Back
Top Bottom