Wako wapi washabiki wa Kikwete?

Wako wapi washabiki wa Kikwete?

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,232
Reaction score
3,334
Katika maisha kama hujapata nafasi ya kuona jinsi wenzako wanavyofanya mambo, kama unakosa taarifa, unaweza kudhani uko sahihi kwa sababu akili yako inakuwa imefungwa. Watoto wadogo ambao hawajaanza shule huwa wanadhani dunia nzima ni pale walipo, mfano mtoto anaeishi Shinyanga anadhani dunia nzima ni Shinyanga.

Wako wale waliokuwa mashabiki wa Kikwete, sasa Magufuli ndani ya wiki mbili kamuonesha Kikwete jinsi amabavyo mambo yanavyotakiwa kupelekwa (doing things in different ways), kamuumbua Kikwete. Ndani ya hizi wiki 2 tayari milioni takribani 700 zimeokolewa kutoka kwenye mikono ya wanyan'ganyi (Sherehe za kujipongezana bungeni, sherehe za kupasua matofali kwa vichwa na kuuza sura pale uwanja wa taifa, nk). Wapi akina FaizaFoxy watoe maelezo hapa?
 
Cc Lowassa: huyu ni shabiki wa jk 1995- July 11, 2015 ndie alieshiriki kuaminisha Umma kuwa jk ni tumaini lililorejea akiwa Bagamoyo kwny kutafuta wadhamini ccm alisema urafiki na uswahiba baina yao utatenganishwa na umauti
 
Namlamu sana Lowasa kwa kumsapport Kikwete kuingia Ikulu mwaka 2005, Kikwete ndio kafanya hii nchi kusimama kwa miaka 10 na kuwa under autopilot
 
Namlamu sana Lowasa kwa kumsapport Kikwete kuingia Ikulu mwaka 2005, Kikwete ndio kafanya hii nchi kusimama kwa miaka 10 na kuwa under autopilot

Kwa hiyo before 2005 yapo yaliyofanyika sasa kina sumaye, Lowassa na mbowe wanasemaje 54 years of independence hakuna kilichofanyika?
 
Ukawa raha tupu. Nchi inaendeshwa kwa ilani ya ukawa. Magu hadi alijiita M4C. Anapenda sana CDM ila jinsi CCM walivy mazuzu hawaoni hilo. VIVA UKAWA.
 
Cc Lowassa: huyu ni shabiki wa jk 1995- July 11, 2015 ndie alieshiriki kuaminisha Umma kuwa jk ni tumaini lililorejea akiwa Bagamoyo kwny kutafuta wadhamini ccm alisema urafiki na uswahiba baina yao utatenganishwa na umauti

Huyu mzee anakunyima usingizi eeenh,
 
Huyu mzee anakunyima usingizi eeenh,

Alieuliza mashabiki wa jk sio mimi, aliejitangaza shabiki wa jk sio mimi kazi yangu ni kutaja tu kuwa Lowassa, kingunge ndio mashabiki wa jk sasa wewe tutajie wako wapi now!
 
Kwa hiyo before 2005 yapo yaliyofanyika sasa kina sumaye, Lowassa na mbowe wanasemaje 54 years of independence hakuna kilichofanyika?

Akina Sumaye wako sahihi, ukiangalia yaliyofanyika tangu 2005 ni sawa na hakuna, umasikini umerudi kwa kasi ya hali yajuu, uchumi hoi, nchi imefirisika. Zimejengwa barabara lakini ziko chini ya deni. Ni sawa na kujengwa nyumba kwa milioni 20, baada ya ujenzi ukabaki inadaiwa shilingi Milioni 25. Wakati wa Kikwete nchi haiukuwa na Rais, tunaemuita Rais 56% ya maisha yake yote alikuwa nje ya nchi. worse
 
Hakuna kama JK, hata mkiandika vipi.
Kuna watu ambao hawakuwahi kuota japo ukuu wa wilaya acha huo ukurugenzi lakini katika wakati wake hizo ndoto zilitimia!
 
Nashangaa ccm hii hii ilikuwa inatetea safari za nje wakati wa kikwete, alipoondoka tu madarakani wanamponda. Ccm hii hii ilikuwa inatetea mbio za mwenge sijui mwakani itafutwa nayo?
 
Jk alikuwa chaguo LA Mungu, mashekhe na maaskofu walithibitisha hilo, kwann msiilaumu CCM au Mpaka badala yake lowassa??

Acheni chuki binafsi kwa huyu mzee mlishamtukana na kumdhalilisha vya kutosha,
 
Ukawa raha tupu. Nchi inaendeshwa kwa ilani ya ukawa. Magu hadi alijiita M4C. Anapenda sana CDM ila jinsi CCM walivy mazuzu hawaoni hilo. VIVA UKAWA.

Mimi ni Chadema, naona Magufuli anafanya yale ambayo Chadema tuliyalalamikia, ccm wameingiza Chadema Ikulu bila kujua. MAGUFULI akiendelea hivi UKAWA tuko nyuma yake. Wengine tumeichukia ccm kwa sababu ya mambo ya ajabu, sasa kama Magufuli anatuwakilisha kwanini tusirudi kundini?
 
Hakuna kama JK, hata mkiandika vipi.
Kuna watu ambao hawakuwahi kuota japo ukuu wa wilaya acha huo ukurugenzi lakini katika wakati wake hizo ndoto zilitimia!

Kwa hiyo haijalishi kama wali deliver almradi JK aliwapa uKuu wa wilaya?
 
Hakuna kama JK, hata mkiandika vipi.
Kuna watu ambao hawakuwahi kuota japo ukuu wa wilaya acha huo ukurugenzi lakini katika wakati wake hizo ndoto zilitimia!

Sasa huo ujinga ndio hatuutaki, unapewa ukurugenzi na ukuu wa Wilaya kuwa fadhila na kujuana. Mtu mwenye fikra sahihi atakupa ukuu wa Wilaya kwa sababu ya CV yako na uwezo wako
 
what happened in VEGAS remains in VEGAS.
 
Ukawa raha tupu. Nchi inaendeshwa kwa ilani ya ukawa. Magu hadi alijiita M4C. Anapenda sana CDM ila jinsi CCM walivy mazuzu hawaoni hilo. VIVA UKAWA.
Umeshaelezwa kuwa akili ya kuambiwa changanya na yako! Magufuli anawaongoza watanzania wote bila kujali matabaka. Kwahiyo, anaweza kuchukuwa zuri lolote kutoka Chama chochote ili watanzania wote wafaidike. Yeye haongozi wana CCM pekee. Ndiyo maana siku ya kutangazwa mshindi, ACT walimpa Ilani yao ili achukue mazuri yaliyomo!
 
Hakuna kama JK, hata mkiandika vipi.
Kuna watu ambao hawakuwahi kuota japo ukuu wa wilaya acha huo ukurugenzi lakini katika wakati wake hizo ndoto zilitimia!

Hao wakuu wa wilaya wamejuletea faida zipi?
 
Kwa hiyo haijalishi kama wali deliver almradi JK aliwapa uKuu wa wilaya?

Mkuu, haya ndio baadhi ya masalia ambayo bado hayajabadilika, bado yana ndoto za Kikwete, ujipendekeze upewe ukuu wa Wilaya
 
Back
Top Bottom