VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,489
- 1,465
Mwamba akabiliwa na shitaka la kumnyanyasa mkewe kijinsia, kwa kilichotasiliwa kama mumpiga na kumuumiza mkewe kisa kunyimwa haki yake ya ndoa.
Baada ya kukaa ndani kwa muda wa wiki mbili sasa, mahakama imeamua akae ndani siku 30 wakati upande wa mashitaka ukikusanya vielelezo zaidi.
Nchini Rwanda, mkeo wa ndani akikushitaki kumnyanyasa kingono, ni kosa kishelia na yeye ndo mwenye ushahidi.
Mbali na hilo, mijadala kuhusu kesi kama hizi mtandaoni, hupelekea wengi kujikuta wakitafutwa na kufunguliwa mashitaka kwa kinachoitwa kueneza habari zisizo na ukweli, huku la lenyewe ni kosa kishelia.
Makosa yote haya, kifungo cha chini kabisa ni miezi sita, huku muda mrefu wa kukaa gerezani ukiwa ni miaka miwili.
Siku 30 alizopewa huyu bwana, wapo watu ambao mpaka sasa wana miaka zaidi ya 3 gerezani wakiwa bado kesi zao hazijasikilizwa, kwa kinachodaiwa kuendelea kukusanya ushahidi.
Mwisho wa siku wapo wanaopatikana kutokuwa na hatia, wengine hukumu kuwa chini ya mda waliokaa gerezani na mahakama kuamuru waachiwe mara moja.