TANZIA Mpiga picha mzoefu Silvan Kiwale afariki Dunia

TANZIA Mpiga picha mzoefu Silvan Kiwale afariki Dunia

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
26,036
Reaction score
47,746
Aliyekuwa mpiga picha wa New Habari (2006) Ltd iliyokuwa ikizalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba, Silvan Kiwale, amefariki dunia Jumatatu, Novemba 16, 2026, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata ajali ya bajaji.

Kiwale, aliyewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Mwananchi na alikuwa miongoni mwa wapiga picha waliotoa mchango mkubwa katika tasnia ya habari nchini kabla ya kujiunga na kampuni ya New Habari (2006) Ltd.

Kifo chake kimeacha simanzi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzake waliomfahamu na kufanya naye kazi.

Aliyekuwa Mhariri Mkuu Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda, amemwelezea marehemu kuwa mtu muungwana na mtulivu.

“Pumzika kwa amani Silvan. Ulikuwa mtu muungwana na mtulivu usiye na makuu,” amesema Kibanda.

Kwa upande wake, Sarah Mosi, aliyewahi kufanya kazi kwa karibu na Kiwale, amesema alikuwa mchapa kazi, mwenye moyo wa kusaidia wengine na aliyekuwa tayari kutoa mawazo ya kuboresha kazi.

Kifo cha Kiwale ni pigo kwa tasnia ya habari iliyopoteza mmoja wa wataalamu wake waliotumia kamera kuhabarisha jamii.

Tunatoa pole kwa familia na wote walioguswa na msiba huo. Mwenyezi Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Kwenye picha hii,Silvan Kiwale ni huyo mweupe Shati jeusi wa pili aliesimama nyuma ya Mh Kikwete.

IMG-20261117-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom