Mikopo, Nchi ya Mikopo

Mikopo, Nchi ya Mikopo

TrueVoter

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2008
Posts
4,444
Reaction score
5,663
Katika mwezi huu wa Novemba, kuna mikopo 3 imeingiwa..mikopo 2 na waziri wa fedha kutoka AfDB na Exim Bank ya uturuki, mkopo mmoja na KM-wizara ya Fedha kutoka Exim Bank-korea..
Nina maswali kwa katibu wa baraza la mawaziri..
1. Hivi itawezekana kila fani mpya ikitokea ni lazima kuwepo chuo chake..? Hapo Dodoma kuna vyuo vingi ikiwemo UDOM yenye college kubwa kabisa ya mambo ya IT..hizo kozi zinazokopewa kujengewa chuo haziwezi kufundishwa UDOM? Kuna ulazima kukopa hizo pesa kwa sasa..?
2. Ndani ya mwezi mmoja mikopo 3 nani hasa wanatoa idhini ya nchi kukopa, ni bunge..? Waziri anakopa, katibu mkuu nae anakopa imekaa sawa hali ya namna hii..? Mtu akifikiri kuwa hiyo mikopo ni deal anakosea?
3. Ni sawa kuwa na wizara inayoona njia moja tu ili kutekeleza miradi ya maendeleo ni KUKOPA..! Hakuna njia zingine..?
4. Hiyo mikopo urudishwaji wake unaeleweka..?
Maoni yangu:
i) Kunahitajika mamlaka ya kutoa idhini nchi kukopa..nchi haiwezi kuishi kwa mikopo inayotokana na maamuzi ya mtu mmoja au wawili..
ii) Mikopo kwa ajili ya majengo kwa sasa isichukuliwe..
iii) Ikihitajika kukopa..PPP itumiwe.
Mwisho, kuna jambo hili la biashara ya hewa ukaa..hivi zanzibar hakuna misitu ya kufanya carbon credit, namuuliza waziri masauni..? Bara peke yake ndio kuna misitu kwa ajili ya CCT..?
Nitoe angalizo kwa serikali, hii biashara km mnataka iendelee, basi ifanyike kwa ngazi ya vijiji..hata wilaya isichukue hata senti, viacheni vijiji vinufaike na hii biashara..misitu haiko mijini, watunzaji wa misitu wako vijijini..hapa ndipo unaona uhitaji wa kuwa na wizara ya maendeleo vijijini..huko ndiko Base na backbone ya maendeleo ya nchi!
Nimetimiza wajibu wangu!
Asante kwa kusoma na kuelewa..
 
Binafsi nimekuelewa,ila naamini mikopo yote in baraka za raisi wa nchi, wizara haiwezi kukopa bila raisi, bank kuu, gavana kutoa approve.

Swali ni je, bunge linaruhusu hayakufanyika?
 
"Itafika siku hii nchi Itauzwa, mie nawaambia ukweli, nchi ina madeni, madeni, madeni" by Ndugai.

Kilochofuata dhidi yake kilionekana wazi wazi.
 
Binafsi nimekuelewa,ila naamini mikopo yote in baraka za raisi wa nchi, wizara haiwezi kukopa bila raisi, bank kuu, gavana kutoa approve.

Swali ni je, bunge linaruhusu hayakufanyika?
Ni kweli..awamu ya 3 nchi ilikuwa imelemewa na madeni kufikia kiwango cha kutokopesheka, waliopitisha na kuchukua mikopo hawakuwepo wakati huo..anayenyimwa kukopa ni yule ambaye hakukopa..ni sawa kurudisha nchi huko tena?
 
Ndugu yangu, nani atazuia mikopo katika Nchi hii? Sisi wengine wote ni kama mateka. Mihimili na Taasisi za serikali vingekuwa huru wangekuwa wanazuia mikopo isiyo na tija.

Siku ukipatikana UKOMBOZI kamili wa Nchi hii, tutalazimika kufanya maboresho makubwa sana ya kimfumo. Ni aibu kubwa sana.
Ebu fikiri, tuna ziwa Victoria, nyasa, Tanganyika, Bahari ya Hindi na mito, lakini hadi leo hii Watanzania wana shida ya maji. Maji yanatoka ziwa Victoria yanapita Uganda, Sudan na hatimaye yanafika Misri. Sisi kutoa maji kutoka ziwa Victoria kwenda sehemu mbalimbali za Nchi kwa ajili ya matumizi tunashindwa.
Kuna hata chambe ya akili hapo?
Hadi Sisimizi na kunguni wanatushangaa.
 
..inasikitisha, kukera na kuudhi pia..waziri wa fedha anaonekana ni mtu mzima anayeweza kupima mambo kwa umbali mrefu..km hili lifanyike au lisifanyike, hata yeye binafsi akiulizwa..ndani ya familia yake kukiwa na matatizo atakubali kuingia mikopo 3 tofauti kwa siku moja?
Suala la mikopo lazima lifanyike baada ya majadiliano na mapitio ya kina kutoka mamlaka tofauti..kwa sasa wizara ya fedha ni mzigo kwa nchi ina watu wanaoipeleka nchi kusikostahili kabisa!
 
Wanataka kujenga chuo Gani tena ?
Ni Bora wajenge karakana or kiwanda watengeneze bidhas
 
Wanataka kujenga chuo Gani tena ?
Ni Bora wajenge karakana or kiwanda watengeneze bidhas
 
Katika mwezi huu wa Novemba, kuna mikopo 3 imeingiwa..mikopo 2 na waziri wa fedha kutoka AfDB na Exim Bank ya uturuki, mkopo mmoja na KM-wizara ya Fedha kutoka Exim Bank-korea..
Nina maswali kwa katibu wa baraza la mawaziri..
Haya ndio mabandiko ya kizalendo na huu ndio uzalendo.
CAG Prof Assad alitoa ushauri mzuri sana kuhusu deni la taifa, yule Blaza wangu akammind, akataka kumuadhibu akajikuta hawezi, ndio akamtuma yule andunje wa kule wamsusie. CAG, Prof. Mussa Assad, Atoa Dawa ya Kutibu Ugonjwa Hatari wa Deni la Taifa, ni Nidhamu ya Matumizi kwa Kubudget Kutumia Kile tuu Tutachokipata

Prof. Assad alishauri, kabla hatujakopa, Bunge lielezwe tunataka mkopo wa nini?, kwa terms zipi?.
Mikataba yote ya deni la taifa ipite bungeni kuwa scrutinized ili kuithibiti serikali sio tuu inajikopea tuu!.

Jamaa alishughulikiwa na kuondolewa!.

P
 
"Itafika siku hii nchi Itauzwa, mie nawaambia ukweli, nchi ina madeni, madeni, madeni" by Ndugai.

Kilochofuata dhidi yake kilionekana wazi wazi.
Itafika tena !!!! ????? Ndiyo tayari kama alivyosema Job Ndugai.

Tanganyika imeuzwa rasmi.

Yaani haya mashetani Mazanzibar yameamua na Wala sio utani, kuifilisi Tanganyika kiuchumi na kuwauwa kwa risasi na sumu yeyote anayesimamia ukweli na utetezi wa rasilimali na haki.
 
Hao , wataalum kutoka DIT hawawezeshi kujiari, wanajenga chuo ,kingine kutengeneza (jobless)matatizo zaidi,

Kwa mkopo huo huo wangezitumia kujenga batteries za umeme row materials tunazo, serikali ingezalisha ,Ajira na fedha za kigeni.
 
Back
Top Bottom