Mchungaji awatimua wanawake waliovaa ovyo

Mchungaji awatimua wanawake waliovaa ovyo

MBOKA NA BISO

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
687
Reaction score
790
Ni Wanawake kutoka Halmashauri ya Mji ya Makambako Mkoani Njombe wakilalamikia kitendo kilichofanywa na Mchungaji wa Kanisa la TAG Kivavi kuwafukuza eneo la Kanisa akiwataka kwenda kubadilisha Mavazi waliyovaa wakati wa Harusi ya rafiki yao.

Wanasema walifika katika Kanisa hilo lililotumika kama Ukumbi baada ya Misa lakini muda mfupi alifika Mchungaji na kuwazuia kuingia kwa madai ya kuwa Mavazi yao hayakuwa ya Staha.

Akizungumza kwa njia ya simu Mchungaji Raphael Migodela amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema sio kweli kwamba aliwafukuza kuhudhuria Sherehe ya rafiki yao bali aliwashauri kwenda kubadili Mavazi ndipo waweze kujumuika na wenzao Kanisani.
 

Attachments

  • Mavazi ya ovyo.mp4
    10 MB
Back
Top Bottom